G.Man
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 1,008
- 2,002
Salam wakuu
Nimepata nafasi ya kusikiliza Wasafi FM kwa siku kama mbili sasa baada ya kuwashwa kwenye mkoa niliopo, na nimeweza kusikiliza vipindi vya asubuhi kabisa(goodmorning) na cha jioni(mgahawa). Kwasababu natamani mfanye vizuri zaidi, binafsi nimeona dosari Kadhaa zinazotakiwa kushughulikiwa kama ifuatavyo:
Ethics za utangazaji
Watangazaji wengi wanakosa `Swags` za kutangaza, wanaongea kama wanapiga story tu kijiweni, kupishana kwenye Mic(kuongea) kwakwel naona ndo changamoto kubwa zaidi, watu hawapeani nafasi kuna wakati kelele zinakuwa nyingi utasema mnabishana, japo sio wakati wote ila ni mara nyingi
Usomaji wa matangazo na Habari
Hii ni changamoto nyingine kubwa kabisa, matangazo naona wanasimulia tu wakati mwingine wanapotelea kwenye story mpaka unaweza fikiri tangazo lilishaisha kumbe bado. Kwenye Habari kwakweli bado, hamna utulivu hasa sound track kwa mbali cjui kwanini inawekwa wakati mtu anasoma habari kamili
Segment nyingi sana ndogo ndogo kwenye kipindi kimoja
Ambavyo huwa naona ni kwamba segment hasa zinagawanya panapo badilishwa wadhamini au kuingiza kitu kipya kwenye kipindi, mfano labda muda wa magazeti, lakini naona wasafi kuna segment nyingi alaf unakuta wanaongelea kitu almost kilekile cha mwanzo(simaanishi break)
Kum-refer Diamond bila hoja ya msingi!
Kuna wakati unaweza tafsiri kama watu wanajipendekeza kwa boss wao, ni sawa. Lakini kidogo sioni kama kuna haja ya kuleta story kumuhusu ili tu uonekane mna mahusiano ya ziada nyuma ya kioo, yule ni Boss wenu hata wasikilizaji tuna expect mtakuwa na mahusiano mazuri tu nje ya kazi. Mjue tu Diamond ana kofia tofauti, sio kila msikilizaji wenu basi ni shabiki wake na haitakuwa ni jambo jema kwa media ikiwa ndivyo, Kikawaida naona watu wengi hukerwa na mtu anaesifia sana vitu vyake hata kama haiwahusu
Mrundikano wa watangazaji kwenye kipindi
Kama watangazaji wakiwa wengi alafu wakashindwa kuongea kiutaratibu inakuwa ni kero,pia kuna ambao sio wabishani basi unaweza hata usijue kama wapo kwenye kipindi.
Hayo ni baadhi tu ya nliyoweza kuyaona japo yako mengi zaidi. Nitaendelea na maoni yangu na ushauri...