Diva the Bawse vs Wasafi Media; Mnyukano, watoleana Siri

Diva the Bawse vs Wasafi Media; Mnyukano, watoleana Siri

Alexido jz instagram

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2026
Posts
2,360
Reaction score
5,775
Kinachoendelea kupata umbeya, pia nikujifunza mambo mbalimbali.

Kwanza chanzo cha MNYUKANO, Diva alianza kumuongelea vibaya mitandaoni, marehemu Dida aliye kuwa mtangazaji mwenzake, hapo wasafi.

Watu hawakukubaliana nae, kwanini unamuongelea marehemu sasa, kwanini usingesema kipindi kile, tena unamuongelea kipindi amabcho unataka kuacha kazi na kwenda kujitegemea, unamaanisha sio kheri ni shari hiyo!

Baada ya kumsema marehemu kumbe marehem ana watu, jamaa na ndugu zake wee, acha kinuke mzeer, wamemvaa, sasa, Miongoni mwa watu waliosimamia show ni Juma Lokole aliyekuwa swahiba wa Dida.

Baada ya Diva kuona mambo yamemfika kooni raia zime muandama, akaona isiwe KESI, akaanza kutoa siri za ofisi na WAFANYAKAZI wenzake hapo Wasafi, tuachane na umbeya, nilitaka ni share elimu niliyo ipata kwenye huu mtifuano.

1. Kabla hujatengeneza urafiki na mtu wa kuambiana shida zenu mchunguze, ana kifua?

2. Punguza kiherehere mnapomjadili mtu, boss wenu au yeyote, tulia kuwa msikilizaji.

3. Kikulacho kinguoni mwako, marafiki zetu, wana mengi ya kutusema wanasubiri tuondoke!

4. Tuache kufeki maisha, kama huna huna tu, huyu diva anajiita tajiri, sasa hivi ndio siri inafichuka, alikuwa anasaidiwa na LUGUMI, kodi na pesa ya apartment aliyokuwa anaishi.

5. Alishawahi kudai hawezi ishi Goba na kupadharau, kumbe yeye mwenyewe kitonga hana hela.

6. Tujitegemee walau kidogo, inasemekana alikuwa anamuomba Diamond hela mara kwa mara, japo anadai alikuwa anakatwa kwa mshahara. Tujifunze kujitegemea tusiwe mizigo kwa maboss wetu, nao wana majukumu ya kifamilia. Ila Diamond namuonea huruma, kila msanii au jamaa akipata shida breki kwa Mondi!

Kuna dada mmoja nilikuwa nimepanga naye NYUMBA moja, alikuwa anajifanya mwema kwangu, kumbe huwa ananiteta na mambo mengine saa zingine nikawa namuona ananichora. Huwezi amini baadaye anataka tuwe closely sana nikamkataa live, kanitukana vibaya sikumjibu hata, nikatemana naye. Basi mambo niliyokuja kuyajua kumhusu yeye inasikitisha na kuogopesha sana, wanaume na wanawake tujitahidini kuweka mipaka ya kusema na watu private issues, we ropoka tu.

Wengine wataongezea chini.

Screenshot_20260609-065837.jpg
Screenshot_20260609-072154.jpg
Screenshot_20260609-072210.jpg
Screenshot_20260609-072410.jpg
 
Somo ni lilelile mfanyakazi mwenzako sio rafiki yako

Wengi wanashindwa kutofautisha kati ya rafiki na mfanyakazi mwenzake

Kilichowakutanisha ni kazi, piga kazi epuka ukaribu nao

Piga kazi epuka vikundi vikundi wakati wa mapumziko au mlo

Kipenga cha kurudi nyumbani kikilia wahi nyumbani kwako

Kazini ni sehemu yenye majungu, unafiki, husuda, wivu na roho mbaya
 
Ukishakua sehemu yenye watu wengi mtaani au mtandaoni umbea, manyanyaso, masimango, wivu ni ngumu kuepuka.

Muhimu ni kua kwenye mstari wako sahihi na kutoyumbishwa na maneno ya watu.
Ni kweli usipuuzie sasa, watu wanaweza kula njama wakudondoshe, be care muda wote kama swala, ana kula huku ana angaza huku na huko kama Kuna wanyama wasio na huruma
 
usiku wa kuamka leo insta palikuwa pamoto watu hawajalala kabisa ila diva mwisho wa siku haiwezi hii akae tu kimya
Kaharibu alikua sawa, ila kumtumia marehemu hiyo kete, itamtafuna muda sana tena sana marehemu asemwi, tena mtu mwenye nyomi kama yule, ye ange tafuta njia nyingine ya kuondoka wasafi Kwa kheri si hii alio chagua
 
Somo ni lilelile mfanyakazi mwenzako sio rafiki yako

Wengi wanashindwa kutofautisha kati ya rafiki na mfanyakazi mwenzake

Kilichowakutanisha ni kazi, piga kazi epuka ukaribu nao

Piga kazi epuka vikundi vikundi wakati wa mapumziko au mlo

Kipenga cha kurudi nyumbani kikilia wahi nyumbani kwako

Kazini ni sehemu yenye majungu, husuda, wivu na roho mbaya
Do job, go home
 
Kaharibu alikua sawa, ila kumtumia marehemu hiyo kete, itamtafuna muda sana tena sana marehemu asemwi, tena mtu mwenye nyomi kama yule, ye ange tafuta njia nyingine ya kuondoka wasafi Kwa kheri si hii alio chagua
Atapata shida sehemu nyingine kupata kazi maana wameshamjua ni lopolopo hata alivyoondoka Clouds ulikuwa mtiti history yake sio nzuri akihama sehemu kwa hicho alichokifanya imemuharibia zaidi na alivyokuwa mjinga anahisi labda anaharibia taasisi kumbe ni mpaka yeye mwenyewe Brandi yake imechafuka kwa ujinga wake mwenyewe watu wamejua hayo maisha anayotamba insta kujifanya ni wa expensive kumbe ni fake
 
Haya mambo mnayataka , mbaya mwanamke akishakuzoea basi hawezi kukuheshima .IKitokea mkagombana , anaweza kuongea maneno makali dhidi yako kama mwanaume unaweza kupanic,

Acha mazoea na watu wa kazini , sio marafiki zako , ikiwezekana wakaushie iwe ni salamu tu . Leo watoto wa kiume hasa hawa Gen Z kama ''Mahanithi'' yaani , unakuta kidume kinaenda nyumbani kwa mfanyakazi wa kike eti kuhudhuria ''Birthday party '' ya mwanamke.

Ujinga mwingine , unakuta watu kisa wako ofisi moja , wanaanza kupostiana huko status za whtasapp huku nyuma wanalambana visogo . Unafiki ni mwingi sana , yaani mnaenda mpak vacation kwani hauna familia ? huo muda unavyokuwa available kama kidume unajichoresha ;unakuwa cheap sio hulka za kiume hizo .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom