Tuwashukuru Wamarekani kwa msaada wa mchele wenye virutubisho mashuleni badala ya kujipiga vifua kwa kiburi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,639
46,281
Ukweli usemwe kwamba pamoja na ardhi kubwa na uzalishaji mkubwa wa chakula tunaoringia nchini kwetu Watanzania wengi bado wanakula milo duni sana, wengi hawapati milo bora (balanced diet) na wengine wengi hata kupata chakula tu ni shida kabisa. Zaidi sana bado tuna tatizo kubwa la udumavu.

Tanzania kuna shule nyingi watoto hawapati chakula shuleni , kuna shule watoto wanakunywa uji wa sembe wa sukari tu. Shule nyingi chakula ni ugali maharage, nyama kwa mbinde sana na vitu kama maziwa au mayai shuleni bado ni ndoto.

Sasa kwa Wamarekani mlo bora kwa wanafunzi ni jambo muhimu sana tena ni ajenda kubwa sana hadi kwenye siasa za nchi hiyo. Huko kutegemea na jimbo shule za umma wanafunzi wanakula kuku, nyama, mayai, maziwa, njegere, matunda n.k.

Kupewa msaada wa chakula kutoka Marekani isiwe nongwa bali ni uhalisia wa jinsi ambavyo bado tuko nyuma hata katika swala jepesi la chakula bora na kizuri mashuleni. Tuwashukuru Wamarekani hata kwa hicho kidogo.
 
Back
Top Bottom