Kiranja wa jamii
JF-Expert Member
- Jan 2, 2023
- 222
- 528
Kuna mjadala wa kuletewa msaada wa mchele na nchi ya Marekani na walengwa ni vijana wetu walioko mashuleni.
Kwa bahati mbaya kizazi hiki hakina uwezo wa kuhoji na wazazi wao wamekuwa machawa wanaosifia kila kitu kinachofanywa na mabwana wakubwa bila kujali madhara ya kitu chenyewe.
Wazazi na wanafunzi wa shule hizo wanahaki ya kufahamu kama;
1.Shule hizo zilikuwa hatarini kiasi gani kufungwa sababu ya uhaba wa chakula?
2. Wakuu wa shule hizo waliandika barua wizarani kuomba msaada wa dharula wa kupatiwa chakula? Kama hawakuandika, serikali imejuaje kama wanahitaji msaada?
3. Wazazi walihusishwa kwenye majaribio ya project hiyo ya GMO? (Walijaza consent form?) ya kukubali msaada huo wa chakula? Kitu cha kupewa bila kuomba unayo haki ya kupokea au kukataa na kisheria watoto maamuzi yao hufanywa na wazazi
Kama wazazi na uongozi wa shule walishirikishwa hatua kwa hatua na wakakubali wenyewe, basi sasa ni zamu yetu kuhoji kwasababu hatukuwa na taarifa na ni haki yetu kufahamu pale maslahi ya kiafya ya watanzania wenzetu yanapokuwa mashakani.
Hata kama yote hayo yalifanyika, yatupasa kufahamu kwamba wakulima wa mchele "originale" huko mashambani wanalanguliwa na madalali mchele wao mzuri kwa bei rahisi sana na mchele wao kusafirishwa nchi za nje kwa bei ya super normal profit, halafu watoto wao wanafanyiwa majaribio kwa kulishwa mfano wa mchele uliotengenezwa maabara na viongozi wao wanachekelea mbele ya camera
Tutambue kwamba hayo mazao ya GMO ni project ya muda mrefu yenye malengo maalumu ambayo ki uhalisia wanaofahamu ni wao wenyewe.
Ni jambo la ajabu sana kuruhusu wafanye majaribio ya miradi yao kwa watoto wetu. Huu ni wenda wazimu
Kama zamani, watoto hawa walitakiwa wagome kula na waandamane kudai haki yao ya kula chakula kizuri.
Wazazi nao huku mtaani walitakiwa waifundishe serikali kwamba hawajashindwa kuwapa watoto wao chakula kizuri. Wazazi wafungashe viroba vya mchele kutoka Kyela na Kilombero na madumu ya mafuta ya alizeti kutoka Singida wawapelekee watoto wao shuleni kama ishara ya kuonyesha kwamba Tanzania hatujafikia hatua ya kupewa msaada wa chakula.
Kwanini chakula hicho kipelekwe kwa vijana? Watanzania tuamke