Wazee 2015 ni mwaka wetu, nawaomba wadau wa M4C elekezeni nguvu vijijini. Asilimia kubwa ya wapiga kura ipo vijijini na awareness si kama mjini, mjini tumemaliza lakini tuelekeze vijijini ambako magamba hutumia umaskini na uaminifu wa ndugu zetu kuwadanganya kwa khanga, kofia, T.shirts, chumvi, unga na kadhalika. Wananchi wa vijijini waelimishwe kwamba wakija na vitu hivyo wavipokee vizuri sana lakini kwenye kura wawaadhibu vilivyo. Bila hivyo magamba watashinda kwa karne nyingi zijazo.