Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Mabibi na mabwana wa JF salam!

Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! Pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.

NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe. Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.

Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake. He was more than a generous lover. Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana. Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu. Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana. Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu (kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye. Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.

Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? Moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea. Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi. Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani nilichokiona sikuamini! Yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? Office mate wake wa kike? Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.

Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, kweli niliamua kuwauwa wote! Potelea mbali, liwalo na liwe. Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu. Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi. Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo. Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu. Nimemwambia mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?. Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo. Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote, wacha waishi ila sitarudiana naye hata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radhi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama. Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SITOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo. Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.

NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI, ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.
2011-2016 you were still dating... Uwanja wa mazoezi tu
 
Dah! Mjumbe wa amani! ya nini tena kujihusisha na kutaka kujiingiza kwenye murder case Mkuu? Yakikushinda si unasepa tu badala ya kuharibu maisha yako yote hapa duniani na kubaki na majuto mjukuu? Pole sana kwa yaliyokusibu. Huyo Bata mweusi achana naye kabisa.
Kaka mapenzi yanaumiza jamani unampenda mtu kwa moyo woteee!!!mi hata simlaumu kwa kweli!
 
Geniveros simlaumu bali nilikuwa namtahadharisha tu. Ni kweli mapenzi yanaumiza sana lakini ni muhimu sana kuwa makini ukitokewa na hali kama hiyo ya kumkuta mpenzi ndani ya kumbato zito na mdada/mkaka mwingine. Je, ukiua ndiyo itafuta kile kilichotokea na kukishuhudia!? Jibu ni hapana bali utakuwa umejiharibia maisha yako yote kwa kwenda jela kwa kifungo cha maisha au adhabu ya kunyongwa.

Kaka mapenzi yanaumiza jamani unampenda mtu kwa moyo woteee!!!mi hata simlaumu kwa kweli!
 
Geniveros simlaumu bali nilikuwa namtahadharisha tu. Ni kweli mapenzi yanaumiza sana lakini ni muhimu sana kuwa makini ukitokewa na hali kama hiyo ya kumkuta mpenzi ndani ya kumbato zito mdada/mkaka mwingine. Je, ukiua ndiyo itafuta kile kilichotokea na kukishuhudia!? Jibu ni hapana bali utakuwa umejiharibia maisha yako yote kwa kwenda jela kwa kifungo cha maisha au adhabu ya kunyongwa.
akili mda huo inakua haipo kabisa yaani
dàh mapenzi bwana!!
undefined....!!unampenda mtu anakuumiza!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pole sana,ila hili tatizo liko kotekote asipofanya mwanamke atafanya mwanaume.ila huyo kaka amefanya vibaya sana ,alafu kaa na ww ujiulize kwanini amekufanyia hayo au ulikuwa unambania ile nanii...... Mpaka ndoa kwanza
 
Well.. Everyone has a story to tell.. Ni changamoto tu za kidunia. Love isn't easy. Stay strong, hiki ni kipindi cha mpito tu love never ends but its gonna shape up your attitude so be very careful with yourself.

Make a self analysis kujua ulipojikwaa and move on huku ukijaribu kutatua mapungufu yako mbele ya safari. Itakusaidia utakapo mpata mtu mwingine ili mambo kama hayo sitokee tena.
 
Mabibi na mabwana wa JF salam!

Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! Pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.

NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe. Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.

Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake. He was more than a generous lover. Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana. Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu. Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana. Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu (kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye. Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.

Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? Moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea. Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi. Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani nilichokiona sikuamini! Yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? Office mate wake wa kike? Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.

Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, kweli niliamua kuwauwa wote! Potelea mbali, liwalo na liwe. Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu. Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi. Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo. Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu. Nimemwambia mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?. Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo. Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote, wacha waishi ila sitarudiana naye hata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radhi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama. Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SITOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo. Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.

NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI, ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.

U
yaani toaka 2011 mtu anakugegeda si mtoto angeshaanza shule?
kweli uzinzi haulipi ebu cheki faida yake
ungetulia zako miaka yote hyo ungekuwa mbali
mlikuwa mnapanga nini miaka yote hyo? yaani mimi sikai na mwanaume hata mwezi kama hasomeki bora nionekane sina maana kuliko kuwa daraja la mtu
Umeongea bonge la point. Na mimi nilikuwa na mawazo kama yako. Wadada mnafanya makosa wenyewe alafu mnakuja kulia lia unapoumizwa
 
Aisee ww ni halali yako kabisa kusalitiwa yaan toka 2011 anakubanjua tu halo lazma ulikuwa umemchosha. Na kama utaendelea na tabia hyo utakuwa unabanjuliwa lakn kuolewa wanaolewa wengne huku ww ukifanya kazi ya kuhudhuria send off tu.
 
akili mda huo inakua haipo kabisa yaani
dàh mapenzi bwana!!
undefined....!!unampenda mtu anakuumiza!
Lakn mkuu ww unafikir mtoa maada alikuwa na malengo kweli na huyo mwanaume? Toka 2011 hamna kinachachoendelea zaidi ya kutoana out weekend hata kama ni kuchunguzana tabia hyo imezidi hapo kisalitiana lazma
 
Iv mwanamke unamwonea wivu mwanaume kwa kipi!
Kwani anakunjwa?! atatanuliwa maumbile?! atabebeshwa mimba aje akusingizie wewe?!
Yani huwa sielewagi kabisa, hata vitabu vya Mungu vinasema watakatifu na mitume walikua na mitala.
Hahahaaa Mzee Wa vikindu ktk ubora wako
 
Lakn mkuu ww unafikir mtoa maada alikuwa na malengo kweli na huyo mwanaume? Toka 2011 hamna kinachachoendelea zaidi ya kutoana out weekend hata kama ni kuchunguzana tabia hyo imezidi hapo kisalitiana lazma
huwezi jua labda ukute hiyo 2011 alikua shule may be secondary,mpk advance level plus chuo 3yrs na ukute mpk mama ake kamuombea msamaha yamaanisha ni mahusiano yaliyokua yanafahamika na walikua wako kwenye hatua nzuri tu!
 
Labda
 
Back
Top Bottom