Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

N hasira tu,, huwezi kusema huitaji tena mwanaume naamin ukitulia na ukawa sawa hutakumbuka tena hayo,,... Mwanamke atabaki kuwa mwanamke tu siku zote
 
huwezi jua labda ukute hiyo 2011 alikua shule may be secondary,mpk advance level plus chuo 3yrs na ukute mpk mama ake kamuombea msamaha yamaanisha ni mahusiano yaliyokua yanafahamika na walikua wako kwenye hatua nzuri tu!
Mkuu hongera kwa kuwa na ubongo fikirishi...unaangalia kitu kutokea angle mbali mbali...ni wachache sana walio na huo uwezo.
 
daah ungekuwa segerea unagonga nguna ya anko magu muda huu bahati yake mngeshagawana majengo ya anko magu mapenzi bwana! pole sana
 
Hapo sawa inapendeza kuja na story iliyofanyiwa maamuzi tayari maana haituchoshi.
 
Asante mkuu...kwa kweli kila kitu kilikuwa kwenye kumbu kumbu...lakini hakuna marefu yasiyo na ncha.
Lakn najua utasahau tu hata ukiachanaNa kutafuta mwingne ukae ukijua kwamba hakuna mwanaume ambaye hachepki labda hata mm nipo kwenye ndoa lakn mchepuko lazma hyo ni kwakila mwanaume.

Haijalishi kuwa anaridhika au haridhiki. Mwanaume anaweza akatoka kufanya tendo sasa hivi lakn baada ya lisaa anataman mwanamke mwingne..

Utambue kwamba mwanaume anavyochepka sio kwamba ww ni mbaya au ww unamapangufu au sio kwamba ww haumridhishi hapana hii ni nature yetu wanaume kitoridhika na mwanamke mmoja..

Japo ni uchungu lakn huo ndio ukweli. Sema alichokosea yeye jamaa yako ni kuingiza mchepko ndan ya geto lake wakat anajua upo naye ww ..

Ukiona mwanamke hachepki ujue anamatatizo ya kimwili au kiuchumi..
Lakn mkuu ukweli ni kwamba hakuna mwanaume asiyetoka nje hata ukiachana naye utajipotezea mda wako bure au itafika hatua ww baadae ndo utaonekana hujatulia kwasababu kila ukiona mwenzi wako amechepka utaachana naye hapo ujue idadi ya wanaume ulioachana nao inaongezeka hvyo ww ndio utaharibikiwa fungua moyo mama kuwa mpole maisha mahusiano ndivyo yalivyo
 
Pole sana dadangu na rafiki. Mahusiano mengi tunayaanza kwa kumshirikisha shetani badala ya Mungu. Ninachokushauri wala usiwaze kuwachukia wanamume wote, tafuta upendo na amani ya kweli ambayo inapatikana toka kwa Mungu na huko ndipo utamoata mume bora wa maisha yako ambaye hatakuumiza daima.
 
....Amwambie mamake atafutwe mwanamke mwingine wa kuchezea! Miaka 5 Na mnachezeana kisa eti mnapendana au mnapimana nini??? Kuweni makini vijana
 
Dah pole dada utasahau tu ni sehemu ya maisha mana binadamu wameumbiwa kusahau jpo uwezi meza mataoishi si kila kin'gaacho ni dhahabu
 
Mabibi na mabwana wa JF salam!

Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! Pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.

NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe. Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.

Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake. He was more than a generous lover. Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana. Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu. Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana. Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu (kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye. Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.

Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? Moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea. Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi. Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani nilichokiona sikuamini! Yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? Office mate wake wa kike? Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.

Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, kweli niliamua kuwauwa wote! Potelea mbali, liwalo na liwe. Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu. Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi. Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo. Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu. Nimemwambia mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?. Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo. Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote, wacha waishi ila sitarudiana naye hata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radhi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama. Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SITOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo. Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.

NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI, ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.
[emoji121]
MKUU
HAUNA PICHA JAPO YA PASSPORT SIZE UIWEKE HAPA?
 
Back
Top Bottom