Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Wewe unatatizo kwann ulipogundua kunajambo linaendelea kwa mwenza wako ukapiga kimya? ilikubidi u stand nakumkanya huyo binti wa kazini kwake
 
Sasa na ww kilichokupeleka kwa mtu bila taarifa ni nini acha tabia hiZo za kipuuuuI
 
Mjumbe wa amani, pole dada yangu. Lkn najiuliza, huo uchumba wa miaka mitano maana yake nini? Yaani kila mtu ana kazi yake, mnashirikiana yote hadi mnalala pamoja kwa miaka sita!

Ningekuwa mzazi wako ama ningewafungisha ndoa ya mkeka au ningewatenganisha.

Ktk uchumba wa miaka sita , mnashirikiana yote kama wanandoa halafu uhusiano unavunjika mwanamke ndiye anajeruhiwa zaidi.

Nawashauri dada zangu, msijiachie na kuwa huru kiasi hicho ktk uchumba, hakuna uchumba wa miaka mitano, hiyo ni sawa na kucheza kamari.

Vv
 
Mabibi na mabwana wa JF salam!

Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! Pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.

NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe. Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.

Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake. He was more than a generous lover. Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana. Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu. Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana. Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu (kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye. Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.

Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? Moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea. Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi. Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani nilichokiona sikuamini! Yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? Office mate wake wa kike? Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.

Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, kweli niliamua kuwauwa wote! Potelea mbali, liwalo na liwe. Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu. Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi. Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo. Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu. Nimemwambia mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?. Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo. Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote, wacha waishi ila sitarudiana naye hata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radhi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama. Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SITOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo. Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.

NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI, ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.
Hilo ni pigo Kali sana na jeraha lake haliponi hata ukisamehe mi naona ishi maisha yako tu huku ukimwomba Mungu afanye Kitu ktk maisha yako swala la mahusiano acha kwanza usikurupuke ukakutana na mwingine akakuumiza zaidi ukaamua kufanya mabaya yatakayoleta tabu ktk maisha yako yote
 
yaani toaka 2011 mtu anakugegeda si mtoto angeshaanza shule?
kweli uzinzi haulipi ebu cheki faida yake
ungetulia zako miaka yote hyo ungekuwa mbali
mlikuwa mnapanga nini miaka yote hyo? yaani mimi sikai na mwanaume hata mwezi kama hasomeki bora nionekane sina maana kuliko kuwa daraja la mtu
Hahahaaaaa we Nouma
 
Kwanza pole sana mana najua hali hiyo huwa inawakumba wengi katika mahusiano,ila ushauri wangu kwako kuwa robo tatu ya sisi wanaume mpango wa kando lazima uwepo hivyo hata huyo utakae mpata uziwekeze roho yako yote na kumweka katika diary yako mana ndo tabia yenu.Ila unaruhusiwa kumpa second chance mana binadamu hatujakamilika
Atarudia tu itakuwa kazoea kama so mzoefu asingemleta mpaka home kwake inaonyesha kazoea kuwalaghai na itakuwa ni mengi kafanya kwa siri ila Mungu kaamua kumuumbua kabla awajaingia ktk ndoa
 
Kwa nini Watu wa hivi Mpaka Leo mnapumua!??
naomba unipatie evidence zilizo simama imara kuwa hiyo sio fiction story.....ukishindwa kunipa we baas ni mwanamke kama wanawake wengine
 
Mabibi na mabwana wa JF salam!

Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! Pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.

NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe. Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.

Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake. He was more than a generous lover. Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana. Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu. Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana. Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu (kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye. Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.

Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? Moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea. Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi. Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani nilichokiona sikuamini! Yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? Office mate wake wa kike? Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.

Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, kweli niliamua kuwauwa wote! Potelea mbali, liwalo na liwe. Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu. Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi. Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo. Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu. Nimemwambia mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?. Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo. Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote, wacha waishi ila sitarudiana naye hata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radhi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama. Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SITOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo. Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.

NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI, ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.
Ww ni miongon mwa wanawake jasiri sna ila tu utakaposimamia msimamo wko..
 
duuuh.. bonge la funzoooo..... ila vp hkuchkua hta clip 2lione pcha
 
Kwa kweli sasa hivi ata akija bwana siitaji mwanaume tena.
Pole, najua unazungumza hivyo kwa kuwa una jeraha bichi. Hujaona mtu aliyewahi kujiapiza hivyo na baadaye ameingia kwenye ndoa? Usiitie nafsi yako kwenye vifungo na maapizo yasiyo na maana, subiri na umuombe Mungu akuponye na hilo jeraha.

Muhimu ni kuwa usije ukafanya makosa hayo tena- uchumba wa miaka 5. Miaka 5 ktk uchumba ni muda mrefu sana labda kama nafsi zenu zimekufa, hakuna hofu ya Mungu na hamuwastahi wazazi na jamii yenu. Labda kama mmoja yuko nchi nyingine; hata hivyo bado anaweza kurudi kufunga ndoa kisha kurudi ughaibuni.

Uguza majeraha dada, hayo maapizo achana nayo, Mungu anaweza kukukutanisha na mtu hadi ukashangaa kuwa alikuwa dunia gani.

Sawa Mkuu ila elewa maisha hayana formular, unaweza kukaa kwenye uchumba mwezi mmoja, mwaka mmoja 2,5, au kumi...wala kuwahisha uchumba na kuingia kwenye ndoa haitabiri ndoa imara.
 
naomba unipatie evidence zilizo simama imara kuwa hiyo sio fiction story.....ukishindwa kunipa we baas ni mwanamke kama wanawake wengine
Mkuu kumbuka hii siyo theory inayohitaji hypothesis, pia siyo dini inayohitaji imani, ni tukio halisi lililonitokea.Kwahiyo wacha kubishana if its a fiction or not!
 
Mjumbe wa amani, pole dada yangu. Lkn najiuliza, huo uchumba wa miaka mitano maana yake nini? Yaani kila mtu ana kazi yake, mnashirikiana yote hadi mnalala pamoja kwa miaka sita!

Ningekuwa mzazi wako ama ningewafungisha ndoa ya mkeka au ningewatenganisha.

Ktk uchumba wa miaka sita , mnashirikiana yote kama wanandoa halafu uhusiano unavunjika mwanamke ndiye anajeruhiwa zaidi.

Nawashauri dada zangu, msijiachie na kuwa huru kiasi hicho ktk uchumba, hakuna uchumba wa miaka mitano, hiyo ni sawa na kucheza kamari.

Vv
Mkuu uchumba wa miaka 5,6,au 10, siyo issue sana.Ni maamuzi ya kati ya wawili kuhusu ni lini waoane....kwenye hicho kipindi tumeshuhudia watu wakifunga ndoa na kuachana in less than 3yrs.
 
Sasa na ww kilichokupeleka kwa mtu bila taarifa ni nini acha tabia hiZo za kipuuuuI
Mkuu hujasoma hapo kwamba nilimtafuta kwenye simu bila mafanikio? Sasa kama mpenzi wake, haikuwa busara kwenda kumjulia hali ili nijue kulikoni? kama angekuwa kazidiwa hoi bin taaban na mimi nisiende, ingeleta picha gani?
 
Sawa Mkuu ila elewa maisha hayana formular, unaweza kukaa kwenye uchumba mwezi mmoja, mwaka mmoja 2,5, au kumi...wala kuwahisha uchumba na kuingia kwenye ndoa haitabiri ndoa imara.
Kwa sehemu umeelewa, kwa hivyo maapizo yako hayana maana.

La pili, muda ni factor muhimu sana mnapoanza mahusiano ya uchumba, uchumba sio uhusiano wa kudumu, umri wa mwanadamu unaenda mbele haurudi nyuma. Mwombe Mungu upone majeraha na akupe mtu mwafaka, kama unao wito wa ndoa usijaribu kuutosa.

Vv
 
Back
Top Bottom