Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

Usaliti: Nusura niue mtu hii weekend

MJUMBE WA AMANI

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
262
Reaction score
238
Mabibi na mabwana wa JF salam!

Ni imani yangu kwamba mmekuwa na weekend njema na yenye utulivu nawapongeza sana na poleni kwa mliokumbwa na dhoruba za maisha kama mimi.Binafsi hii weekend haijawa nzuri kwangu kwani ilibaki chembe kabla sijampeleka mtu kuzimu. Mungu wangu! Pengine mida hii ningekuwa nahaha kutafuta mawakili wa kunitetea kwenye murder case.

NDUGU ZANGU IPO HIVI:
Nilikuwa kwenye mahusiano na mwanaume mmoja kwanzia jun.12 2011 hadi Ijumaa iliyopita tar.2 sep 2016. Kwakweli tulipendana mno tena sana, tulijaliana na kushirikiana kwa kila jambo, Mimi nilipenda sana, nilimjali na kumheshimu kwenye kila kitu.Hakuwa mkamilifu kwa 100% ila nilitambua hakuna haja ya yeye kuwa mkamilifu hivyo nilimpenda kwa moyo wote, nilimwona ni sehemu ya mwili na maisha yangu mimi, kwahiyo nilimjali kama ninavyojali mwili na maisha yangu mwenyewe. Mapungu ya kibinadamu aliyokuwa nayo nilijisi kama vile ni ya kwangu so nilimuweka wazi kabisa ni jinsi gani nilivyompenda.

Kuhusu yeye siwezi kueleza yote, alinipenda hadi nikajihisi kwamba nina deni kwake. He was more than a generous lover. Alinijali kwanzia nje hadi chumbani nakote huko niliridhika na kujiona nimepewa kuliko nilivyostahili.
Kwa ufupi tulikuwa na mapenzi ya dhati sana. Kwa hicho kipindi cha miaka mitano na zaidi, tulipata furaha iliyosaidia kupooza changamoto za maisha tulizo kabiliana nazo, It was like a single soul living within the two separate bodies.Wote tulikuwa na imani moja, yaani kuishi pomaja milele panapo majaaliwa ya Mungu.

MKASA WENYEWE:
Kwenye mahusiano yetu tulikuwa na mazoea ya kutoka pamoja kila ijumaa ama jumamosi kwenda sehemu nzuri ya utulivu na kuongea mawili matatu juu ya maisha yetu. Juzi ijumaa nilimpigia simu mida ya saa nane hadi tisa lakini simu yake haikupatikana. Basi nikachukua uamuzi wa kwenda kwake kumjulia hali na kama mambo yangekuwa poa basi tutoke kama kawaida yetu (kila tulipotoka tulichangia gharama, kwa jinsi nilivyompenda sikukubali kabisa abebe mzigo wote wa ghara, wakati mwingine nililipa mimi au yeye. Ulikuwa ni utamaduni wetu). Nilipita sehemu nikanunua matunda mbali mbali na ya kutosha, nilipenda sana kubeba chochote pindi niendapo kwake.

Baada ya kufika nilipatwa na mshangao pale nilipoona viatu vya kike mlangoni,nikajiuliza vitakuwa vya nani? Moja ya jibu lililonijia pengine ni ndugu yake wakike kamtembelea. Nikaingia ndani nikazidi kushangaa zaidi, sebuleni hakuna mtu na mlango upo wazi. Ghafla nikasikia kicheko cha Mwanamke chumbani, Oh my God! sikuhitaji genus aniambie nini kinaendelea ndani.Nilipatwa na kizungu zungu lakini niliweza kujimudu, nikaweka mikoba yangu chini nikatoka nje kuchungulia kwa dirishani nilichokiona sikuamini! Yani mwanaume niliyempenda kwa moyo wangu wote leo kamkumbatia mwanamke mwingine? Office mate wake wa kike? Anyway iliniuma ila sikupatwa na mshituko sababu nilishajua kilichokuwa kinaendelea jamani yasikie tu, lakini maumivu niliyohisi Mungu ndiye ajuaye.

Nilichokiamua ni kuwadelete hao wasaliti wangu kwenye uso wa dunia, kweli niliamua kuwauwa wote! Potelea mbali, liwalo na liwe. Nikaingia ndani nikachukua mikoba yangu nakuondoka ili kupanga namna nitakavyotekeleza hukumu yangu. Ile nakatiza kona mara nikasikia mtu ananiita jina, alikuwa ni huyo mwanaume akiwa kavalia pensi. Sikutaka kumsikiliza, nilichapa mwendo hadi kwenye gari na kwenda zangu hadi nyumbani. Baada ya kufika nyumbani nilikwenda moja kwa moja hadi chumbani na kulia sana, nililia kama mtoto mdogo. Hadi saa tano usiku mashavu yaliniuma, macho yalivimba na muda wote mate yalikuwa machungu mdomoni nikapitiwa na usingizi hadi asubuhi.

Sasa jana katuma watu waje kumwobea msamaha, kwamba eti amekosa nimsamehe, niliwarudisha mbio bila kujali ni kina nani alimtuma hadi mama yake mzazi ila nilimwambia, mama huyo mwanao zamani alikuwa mpenzi wangu na pengine mume mtarajiwa ila kwa sasa namwona kama bata mweusi tu. Nimemwambia mama yake amwambie atafute mwanamke mwingine wa kuchezea siyo mimi siwezi kuwa kwenye mahusihano na bata asiye na utu, yaani kumbe alikuwa ni michepuko ila aliigiza maisha pindi alipokuwa na mimi?. Anywa kwa kuwa aliniona pindi naondoka kwake, nionda adhabu ya kifo. Akifa ili hali inaeleweka kwamba tupo kwenye mgogoro sintakuwa salama, laiti kama asingeniona lazima ningepanga mipango ya kwaondoa wote, wacha waishi ila sitarudiana naye hata kama Mbingu zitashuka kuja kutupatanisha.

MWISHO:
Nimekuja hapa jukwaani;
1.Kuwaomba radhi niliowakwaza jana jioni na leo asubuhi, jamani niwieni radhi, nilikuwa na hasira juu yenu pasipo sababu.
2.Kuwaasa wanawake wenzangu kuwa makini na hawa wanaume, wachache ni wanaume ila wengi wao ni wavulana walioishi miaka mingi
3.Enyi wanaume kuweni makini mnapopewa moyo wa mtu, inauma sana kusalitiwa jama. Wanawake tu dhaifu ila siyo sababu ya kutokuwa wakatili pindi unapopita kwenye 18 zetu vibaya.

Maamuzi nimeshafanya mwenyewe KAMWE SITOMRUDIA HUYO BATA MWEUSI, kwa hiyo siitaji kushauriwa juu ya hilo. Nimeshagombana na rafiki zangu wawili kisa shauri zisizo na umuhimu.

NIMEKUJA KUWAASA TU JAMANI, ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI.
 
Daah pole csteri. Ndiyo maana asubuhi chit chat ulitaka kukinukisha? Pole.. pole.. pole.. saana. BTW natamani ningeliona behind the scene ya yaliyokusibu.
 
Dah! Mjumbe wa amani! ya nini tena kujihusisha na kutaka kujiingiza kwenye murder case Mkuu? Yakikushinda si unasepa tu badala ya kuharibu maisha yako yote hapa duniani na kubaki na majuto mjukuu? Pole sana kwa yaliyokusibu. Huyo Bata mweusi achana naye kabisa.
 
Daah pole csteri. Ndiyo maana asubuhi chit chat ulitaka kukinukisha? Pole.. pole.. pole.. saana. BTW natamani ningeliona behind the scene ya yaliyokusibu.
Mkuu ndio maana nikaomba samahani Kakangu,..yaani niliingia Jf kuondoa stress, ila nikajikuta nawasababishia watu mushkeri...ndio maana nikakimbia mapema.
 
Dah! Mjumbe wa amani! ya nini tena kujihusisha na kutaka kujiingiza kwenye murder case Mkuu? Yakikushinda si unasepa tu badala ya kuharibu maisha yako yote hapa duniani na kubaki na majuto mjukuu? Pole sana kwa yaliyokusibu.
Mkuu nadhani Mungu kapita kati kati ndio maana hayajatokea,..usaliti mbaya sana Kakangu.
 
Mh baada ya kumfumania sasa jamaa amekuwa BATA tena BATA MWEUSI....mkuu ina maana nawe ni bata? Maana BATA hawezi date binadamu...au mie ndo sijui???
Itakavyokuwa na iwe tu, kwa sasa thamani yake ni kama bata, ndio maana nilitaka kumchinja.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu ndio maana nikaomba samahani Kakangu,..yaani niliingia Jf kuondoa stress, ila nikajikuta nawasababishia watu mushkeri...ndio maana nikakimbia mapema.
Haya dadangu..usirudie kuhifadhi moyo wako kwa matapeli eeh..!! Hawana hiyana wataudondosha
 
yaani toaka 2011 mtu anakugegeda si mtoto angeshaanza shule?
kweli uzinzi haulipi ebu cheki faida yake
ungetulia zako miaka yote hyo ungekuwa mbali
mlikuwa mnapanga nini miaka yote hyo? yaani mimi sikai na mwanaume hata mwezi kama hasomeki bora nionekane sina maana kuliko kuwa daraja la mtu
 
Back
Top Bottom