Danisamweswa
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 453
- 154
Mmmmmmm! hoja kama hoja ina ukweli kwa mustakabali wa taifa kwa ujumla wake. kwa kuwa kuwa na msaliti katika taifa ni hatari kwa taifa hilo.
Inapokuja kwenye vyama vya siasa ni kweli usaliti ni sumu mbaya sana. Na kiukweli kuwabaini wanasiasa ambayo hawana chembe ya usaliti ni kitu kigumu sana haswa huku kwetu Africa. Kwa watu wenye akili zao ukiona mtu mwenye tabia ya kuhama hama vyama huo ni wa kuogopa sana kwani ukimfuata mtu wa namna hiyo hutajua kesho atakupeleka wapi. Kwa wenzetu wao wanasimamia wanachokiamini katika sera na imani za vyama.
Huku kwetu wengi wanaangalia upepo unakwenda upande gani. Wanasiasa wanaofuata upepo hao ndiyo watu wakuogopa sana katika ujenzi wa demokrasia ya vyama vingi. Uhuni wa namna hiyo uko kenya kwa kuwa wao huangalia maslahi yao wenyewe ndo maana walipofika bungeni walianza kudai kuongezewa mishahara watu wakaandamana wakapeleka hata nguruwe maeneo ya bunge.
Viongozi wenye tabia ya usaliti huua ndoto za wafuasi wao. Na zaidi sana huwafanya wafuasi wao wakate tamaa. Ndiyo sababu viongozi makini kama kina Wales wa Scotland walikua tayari kuuawa kuliko kuomba rehema kwa mfalme wa Uingereza akijua akifanya hivyo morali ya watu wa Scotland kudai nchi yao na uhuru wao utafifia na vita yao itakuwa ni bure.
Ni watu wangapi wamepoteza maisha yao kwa kuwa tu wanaamini kuwa CDM itakomboa nchi hii toka kwenye mikono ya CCM ambayo imepoteza dira na kuwa genge la wanyang'anyi? Kile chama kilichodai bidanadamu wote ni sawa na Afrika ni Moja na kuwa sitapokea wala kutoa rushwa kwa kuwa rushwa ni adui wahaki? Kilichojipambanua kuwa ni chama cha wakulima na wafanyakazi? ambapo wakulima wakilima wanapigwa marufuku kuuza mazao yao nje ya nchi? na ambacho kinasimamia mbuge apate posho ya siku inayolingana na mshahara wa mwezi wa mfanyakazi?
Msaliti wa juhudi za vijana wa kitanzania na wapenda maendeleo ya nchi hii wanaotaka kujikomboa kutoka kwenye kongwa la kifungo cha CCM huyo ni mtu mbaya afadhali mtu huyo asingelizaliwa katika nchi hii. Ni kwasababu anasaliti juhidi na kazi inayofanywa ya kuliomboa taifa hili.
Atakayesaliti juhudi hizo alaaniwe yeye na uzao wake. Kwa kuwa juhidi hizi zimegharimu maisha ya watu kama akina Mwangosi na wengineo.