Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa - Lema

Status
Not open for further replies.
mkuu kamanda Ben, binafsi nakuheshimu sana,lakini kitendo cha kamanda lema sio sahihi hata kidogo, lema ni kiongozi hakupaswa kuleta kwenye media kuhusu kuwalaumu wasaliti ndani ya chama. Angetumia vikao, huo ndo ukweli. Tukitaka chama chetu kisonge mbele, lazima tuepuke double standard katika maamuzi.

kama angetajwa mtu sawa,lakini kazungumzia usaliti
 
unajuaachokifanya huyo unaemtetea ndani ya chama chetu, uliwahi kukaachini na kuhesabu watu wangapi kasha sababisha kufukuzwa ndani ya chama? mkuu ni wakati wa kungia mizizi siyo matawi..

Lini Lema amewai kutoa hoja kwenye vikao vya kamati kuu kuwa Zitto ni tatizo ajadiliwe.?

kama yeye ni mjumbe wa kamati kuu na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama, iweje anakuja kupiga poroja kuwa kuna msaliti ndani ya chama mbaya zaidi hamtaji jina?

Juzi hapa tumemlaum sana Mwigamba kwa upuuzi
 
Mkuu The Boss lema amepotoka na hakuna kiongozi atakaye tumia njia kama yake hasa kwenye mitandao lakini najua kwenye vikao vyama ndipo anapo takiwa kukemewa.

Lakini wenye nafasi ya kumkemea humu kwenye mitandao ni sisi wanachama.

Mimi nasema tena huu utoto wa lema alio ufanya una kivuruga chama kabisa.

Lema amepotoka kabisa alitakiwa akajenge hoja kwenye vikao vya chama si hapa na thread ya kuvuruga watu kama hii.
mkuu umekitendea vema chama chetu, chadema tutumie vikao, hasa viongozi wetu!
 
Last edited by a moderator:
Safari yetu ya kubadilisha utawala inaonekana kufika ukingoni na nifuraha ya kila Mtu mwenye hisia ya ukweli katika maisha na ninapotazama mbali sana ninaona jinsi ambavyo Usaliti na Unafiki unavyoangamiza Taifa ni bahati mbaya sana uwezi kuwaepuka katika harakati hizi lakini tukiwa makini tunaweza kuwathibiti .

Kama Chadema leo itashindwa kuwachukulia hatua wasaliti wa wazi wa kazi hii njema ni vipi Chadema itaweza kuitaka Serikali na Rais iwajibishe Viongozi wake katika ufisadi na wizi wa mamilioni ? Na Wananchi lazima wajue lengo kubwa na muhimu la Chadema kwanza liwe kubadilisha fikra na mitazamo na kuupa UMMA elimu na mamlaka na nguvu ya kusimamia Taifa lao katika kuhoji ,kudadisi na kukemea , kwani UMMA usipojua wajibu wake katika kusimamia rasilimali na Taifa lao , ukweli utabaki kuwa Nchi itabadilishwa na kufanikishwa na Jamii iliyoamua kuishi matendo dhahiri ya ukweli na haki na sio unafiki na usaliti .

Viongozi wote wa Siasa wanatokana na Jamii kwa hiyo jamii Thabiti inayo furahia UTU ni Nchi bora tutakayoijenga lakini Jamii yenye woga na hofu na Sifa itazaa Taifa lenye usaliti na Wanafiki . Usaliti na Unafiki unaliangamiza Taifa sana . Maombi na Dua za Watu wengi kuelekea 2015ni kutaka kuona Chadema inachukua Nchi , lakini Dua na Sala hizi zina Imani kubwa na Viongozi wa Chadema na sio rangi ya Chadema , hivyo ni muhimu Chadema kuchukua hatua sasa ya kusafisha Chama na kama hatua hiyo muhimu ya kuondoa Watu wenye rangi mbili italeta madhara katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwamba tunaweza tusishinde dola basi madhara hayo ni muhimu kwani lengo letu lisiwe tu kwenda Ikulu bali kubadilisha fikra ya utawala katika kutenda na kuamua .

“ Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani “ Chadema lazima ifanye maamuzi sasa ya kusafisha Nyumba yake la sivyo itakuja kujuta katika siku za mwisho , wasaliti wote waondolewe hasa yule Kiongozi wao kwani hakuna genge la usaliti lisilokuwa na Kiongozi , kuna Watu wengi Vijana wamekuwa wahanga na ndoto zao kupotea katika Siasa kwa sababu waliongozwa vibaya na Kiongozi mkubwa anayeratibu usaliti ndani ya Chama .

Mtu huyu wote tunamjua ni matumaini yangu Usaliti wake sasa utafika kikomo kama Chama kitaamua kuwa na busara za kutosha katika kujenga siku njema zinazokuja . Mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya katika Chama yanayohusu usaliti na amewaponza Vijana wengi na kuangamiza ndoto zao kwa sababu ya mambo yake binafsi .

“ To me, the thing that is worse than death is betrayal. You see, I could conceive death, but I could not conceive betrayal.” Malcolm X



Lema Godbless - Mp

Usaliti uko wa namna nyingi, hata ule wa kusubiri ulipwe zaidi ndipo uhudumie na kutetea maslahi ya waliokuweka (maslahi ya wananchi) hapo ulipo. Rejea kauli yako Mhe. kwa mujibu wa ulivyonukuliwa kwenye vyombo vya habari.


“Nilisema huwezi kuzuia taasisi moja
kupewa maslahi bora eti tu kwa sababu
watumishi wengine hawalipwi vizuri, ni
haki wabunge kulipwa vizuri na wakati
huo wapiganie maslahi ya watumishi
wengine,” alisema Lema na kuongeza.
 
Nadhani wananchi wengi (hususan wanachama na wapenzi wa CHADEMA) wanakerwa na hizi siasa chafu na za kinafiki. Ndio maana kwa sisi tunaona afadhali kumwondoa huyo Mnafiki.

Nikiangalia damage alizokwishajaribu kuzifanya na hasara husika naamini there is NOTHING to lose anymore. In other words, NO LOVE LOST!
 
unajuaachokifanya huyo unaemtetea ndani ya chama chetu, uliwahi kukaachini na kuhesabu watu wangapi kasha sababisha kufukuzwa ndani ya chama? mkuu ni wakati wa kungia mizizi siyo matawi..

Lini Lema amewai kutoa hoja kwenye vikao vya kamati kuu kuwa Zitto ni tatizo ajadiliwe.?

kama yeye ni mjumbe wa kamati kuu na ni mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama, iweje anakuja kupiga poroja kuwa kuna msaliti ndani ya chama mbaya zaidi hamtaji jina?

Juzi hapa tumemlaum sana Mwigamba kwa upuuzi ambao leo anaufanya Lema. .......

Anachofanya Lema ni kujaribu kupoteza upuuzi wake kuhusu posho kwa kumvaa Zitto....Yaani hataki kukubali kuzidiwa kihoja na Zitto hata kama uwezo hana.
 
unajua maoni na malalamiko tofauti yake..

Ana hasira za Posho tu,na mbaya zaidi amejisikia aibu Zitto alivomjibu kwa kumchongea kwa wananchi.

Hapa anakaribu kutuhamisha kwenda Agenda yake ya kusaliti msimamo wa chama juu ya posho tu.
 
aisee .....cdm ni noma...hii ni kutokana na issue yeyote page zinapaaaaa
 
Nadhani wananchi wengi (hususan wanachama na wapenzi wa CHADEMA) wanakerwa na hizi siasa chafu na za kinafiki. Ndio maana kwa sisi tunaona afadhali kumwondoa huyo Mnafiki.

Nikiangalia damage alizokwishajaribu kuzifanya na hasara husika naamini there is NOTHING to lose anymore. In other words, NO LOVE LOST!

point zimeshiba mkuu.
 
Kaama hii ndio vetting ya JF mlioisema chadema, kwa Zitto imekula kwenu. Kwa utetezi alioupata humu, ni nani anaeweza kumfukuza kama mlivyomfukuza Mwigamba? Mawee.

Magwanda mnajuwa mkimfukuza Zitto na chadema ndio hata JF sijui kama itabaki, maana naona humu zaidi 80% wanamkandia Lema na kumtetea Zitto.

Zitto, namna hiyo, wewe tazama senema ya bure tu.

cc Ben Saanane
hoja sio nani yuko sahihi, bali wanachadema tunapinga mfumo wa kuwa na double standard kwenye jambo moja! Mh. Lema alipaswa kutumia vikao na sio mitandao ya kijamii kwa kutuhumu viongozi ndani ya chama.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom