Usafiri enzi zile Mwanza yetu


Hapo kwenye red mkuu alikuwa anaitwa Karoli! Bonge la tumbooooo, lakini mkwara wake sasa!! Alikuwa anapenda rushwa huyo jamaa wasafiri wa kwenda Sengerema walikuwa wanapata taabu na Mh. Karoli, alikuwa ananyang'anya watu mizigo yao si kidogo. Nafikri mnakumbuka jinsi serikali ilivyokuwa corrupt wakati wa mzee ruksa!! Mwanza wakati huo kulikuwa na akina Karoli wawili ambao walikuwa tishio kwa raia, huyo wa Kamanga na mwingine alikuwa askari polisi kazi zake alikuwa anazifanyia pale stand ya Tanganyika!
 
Hahaha nimekumbuka mbali dakik bus service
Hii ilikuwa inaitwa Dakik au DikDik? Hii nilikuwa napanda kutoka Kayenze kuja mjini miaka hiyo! Kayenze tunapandishwa saa 8 usiku, nilikuwa nachoka kabisa, njia nzima umesinzia tu mpaka unafika mjini. Siku moja nikashushwa home pale Nyakato saa 11 alfajiri almanusura niangukie mikononi mwa vibaka, shukrani kwa mzee Mathias mzee wa Kikurya jirani yetu aliyekuwa askari pale Mwatex!
 
Enzi hizo ukienda na demu mkali lazima Matata akupore,sasa hivi ni Mheshimiwa Diwani.
Aisee! Kumbe ugaidi huwa hauishi hata kama utazeeka yaani unazeeka nao, hili jamaa mika hiyo lilikuwa gaidi sana lakini naona mpaka leo linaendelea kuwa gaidi!
 
Shukran mkuu nimekuelewa.
 
Mimi mwenzenu nimesomea Buswelu ni mzaliwa wa kirumba. Nakumbuka wakati nasoma usafiri ulikuwa chai maharage canter.kutoka kirumba mpaka national ilikuwa unafika ukiwa umejaa vumbi. Uniform haitamaniki.
 
Mzee khalifan yule wa kiarabu au mana mi nimekulia ile nyumba ilikua na hospital hpo jirani n moonlight

Hapana alikuwa mswahili yaani alikuwa anaishi nyumba ya pili kutoka kwa Sadoti (nyumba kubwa ila ilikuwa haijaisha vizuri na walikuwa wanauza bia za jumla.. nyumba imetizamana na shimo la taka.. Moonlight niliwahi kufanya kazi hapo wakati nasubiri matokea miaka hiyo.....
 

Hpo tulihama 82 tukahamia kirumba jirani na pamba quarters,tulikua tunakaa hiyo nyumba opposite na moonlight ilikua na hospital
 
mmenikumbusha Mayeji,jina la hizi express lilikuwa la binti wa kwanza ya tajiri.
 
Enzi zile Express za Mkuyuni mwisho ilikuwa kona ya Butimba! Ha ha ha! Kwenda nyegezi jeshini lazima ukanyage!

Kwenda nyegezi ilikuwa unakanyaga na kile kimuinuko ni noma kma zali lako ukutane na land lover za jeshi upate lifti.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…