Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Kuna yoyote Kasoma Shule ya msingi GEDELI ilioko NYAKATO miaka ya 70 humu?
 
Wito studio pale mjini na Gilia studio mtaa wa rufiji


 
Aisee twende PM inaonekana umesoma mwenge na pengine tulikuwa darasa moja kabisa, Bunango alikuwa balaa yule mwalimu, usiombe akakuandikia NIONE kwenye daftari lako la hesabu utajuta kumfahamu mwenga wa kwa Sadoti.
Mwalimu bunango yupo hadi leo, hazeeki bana, anafundisha Nyanza primary siku hizi


"Mafyele" mtoto wake huyo, mume wa Mwalimu "Bunango" Mwalimu mnoko sanaaaaaaaa
 
Ndo hivyo ndg yangu maisha hayana formula, wanafunzi wa Isenga tulikuwaga tunawaona wa kijijini na wale wa kiloleli, tulikuwaga tunawakubali kwenye kwaya tu tukikutana kwenye mashindano, mlikuwa juu


 
Subisubi- Mwaloni-mjini/stand ya taxi.
Simba mtoto- Mkuyuni- stand ya Tanganyika

Eheee umenikumbusha mbali sana mkuu. Nakumbuka bus nililopanda kutoka Bukoba kwenda Mwanza mwaka 1977 lilikuwa linamilikiwa na Tanganyika bus na jina lake maarufu ilikuwa linaitwa Simba Mtoto likiwa na picha ya Simba.

Tiba
 
Wito studio pale mjini na Gilia studio mtaa wa rufiji

Yap kumbe wewe unaijua Mwanza ya enzi hizo vizuri. Halafu eti mtu anataka tuweke picha, tupate wapi kama picha zenyewe mpaka ujiapake poda na kwenda kujipanga studio!!!!

Tiba
 

Tiba

Unakumbuka enzi cha Chai Maharage?
 

Nataman niwe kama zaman,...
 
Picha zenyewe black n white, mkiingia humo studio ni famili ya watu maybe 7 au 10, hadi mpiga picha aanze kuwapanga ni leo, nakumbuka jumamosi moja tulienda kupiga picha alikuja babu kututembelea kutoa kijijini, tulifika pale gilia saa nane but tuliingia ndani kupiga picha saa kumi jioni, na mkishapiga hizo picha kwenda kuzichukua ni baada ya siku 3, tumetoka mbali jamani


Yap kumbe wewe unaijua Mwanza ya enzi hizo vizuri. Halafu eti mtu anataka tuweke picha, tupate wapi kama picha zenyewe mpaka ujiapake poda na kwenda kujipanga studio!!!!

Tiba
 
ahahahahhhh, nimecheka mie, duh nimeikumbuka hii gari, tukifika shule tunaulizana leo umekuja na gari gani aliyetokea nyegezi utamsikia nimekuja na I Love manori, mweee! i wish those days zijirudie jamani

Nyegezi,ILOVE MANORI.
 
Nyie jamaa wa zamani sana.....mi nmeanza kupanda zangu DONT PANIC.....nyakato _ town....
aaah aaaah
 
mambo ya falcon bus yenye milango miwili

Kumtoroka konda pasi kulipa nauli nje nje

..tivoli na liberty sinema...!

Disco Toto Mapokezi Club pale Mwanza Hoteli.

Mwanza ya enzi zile.
 
Jirani na kwa Sadoti pale kulikuwa kuna mwehu anaitwa mchelechele ndo alikuwa analala chini ya mti.

Duh mpaka unamkubuka jina.. Halafu kwa mzee Sadoti kulikuwa kuna mlinzi kazeeka kweli halafu anakunywa pombe ile mbaya ikifika saa mbili anafunga njia hakuna mtu kupita. Watu wote tulikuwa tunanywea jamani enzi hizo dah..
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…