USA vs N.Korea Military Power

Source itakuwa mkura tv
 
China mwenyewe rafiki wa Korea kwenye statement yake leo 25.04.2017 anasema vita ikipiganwa NK atapata hasara sana kuliko US
 
1. Ninaamini Marekani ina silaha kali, zana nyingi na uwezo mkubwa sana wa hardware na N. Korea hawawakaribii kabisa.
2. Inaeleweka kwamba uwingi wa zana na ukali wake si guarantee ya ushindi. Ingekuwa hivyo Marekani isingeutimua Vietnam, wala vita vya Iraq visingekuwa bado mpaka leo, wala mabomu kama MOAB yasingetumika hivi leo huko Afghanistan.
3. Watu wa kawaida ndiyo wanaoumia na vita hivyo ilhali wenyewe wanapiga pesa tu.
 
 
Wabongo kwa kusikiliza propaganda hatujambo. Hawa N. Korea kwa marekani ni sawa na mgambo wa jiji. hapa duniani kwa sasa hivi hakuna nchi yenye uwezo wa kijeshi angani na majini kama marekani. sasa wewe jiulize huko korea, Japan, mashariki ya kati , Africa nk. marekani ana base zake huko. Wajinga wachache kwa ushabiki tu walisema Saddam Hussein angemshinda Marekani lakini kila mtu anajua kilichotokea. Kwani unafikiri ni kwamba China na Russia hawaoni vitendo vya marekani? Kiukweli hata kama huipendi marekani ndiyo yenye nguvu kijeshi duniani kwa sasa. Na ukae ukijua vita ikipiganwa itapiganwa N.Korea siyo marekani.
 
kinachowaweka kwenye usawa ni nuklia tu, uchumi hauna nafasi, hoja za kujadili ni je north korea anaweza kurusha nuklia ndani ya u.s.a..?
Linaweza kufika lkn litakuwa intercepted....
 
Dogo angekuwa yupo fit angeshafanya yake longtime.. Nahisi hana issue..
 
Tatizo utafikaje hapo uweze kudondosha bom. Kwanza kwa upande wa Submarine N. Korea wapo njema. Wapo na Submarine Rocket Launcher

Wanaodai majaribio yanafeli, mbona imezungumzwa vizuri sana ktk clip.
 
Bila shaka na Wewe umemezwa na ngonjera za Mrus na NK unadefend kwA nguvu zote as if ulikuwepo mradi hoja yako ipate mashiko...
iyo hoja ya kwamba mtu anadefend as if alikuwepo, ni kweli upo sawa, ila ni hoja ya wajinga. aliyekuambia kuwa newton aligundua formular fulani ya kisayansi ukaamini, ndio aliyekueleza yaliyotokea nyuma na leo unaona ushahidi wake. hivi nadefend urusi au naeleza uhalisia, swala la edward synowden unalichukulia easy kwa sababu hujui historia na hata siasa ya dunia hii. lile urusi ingekuwa nchi lelemama, linaanzisha vita kubwa, na hivyo hivyo korea kujitamba mbele ya mkubwa ni kiburi alichokipata kwa mrusi miaka hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…