HIMARS
JF-Expert Member
- Jan 23, 2012
- 73,319
- 103,582
Afrika huchangia kutumia hiyo michango katika kuwahudumia wakimbizi, elimu, maji, magonjwa na chakula.Nataarifiwa hapa USA pekee huchangia yapata 22% ya bajeti ya UMOJA WA MATAIFA (sisi Afrika kwa umoja wetu, AU wenye nchi 54 tunachangia % ngapi huko UN?). Mhe. Trump ataendelea na formula (22%) hii? Hivi Afrika hatuwezi kujipanga tukawapelekea ng'ombe, mahindi na maharage wauze kwenye mnada wapate pesa za kujiendesha, kama mchango wetu badala ya pesa cash?
Wanatuibia kivipi wakati ufisadi tunafanya wenyewe, mikataba tunasain wenyewe tena kwa hiari na kisirisiri na udikteta tunafanya wenyewe.Wacha marekani wachangie hiyo 22% tena bado ndogo, kwa sababu hizo pesa wanazochangia sio zao wameiba kutoka Afrika. USA pamoja na Europe watawasumbua sana Waafrika hadi pale watakapopata akili.
Mmh source ya takwimu hizi ni wapi?Nchi 20 huchangia 83.7pc
Nchi 173 huchangia jumla ya 16.3pc
Sisi Tanzania ni LDC hivyo twachangia 0.01pc
HahahahaAwamu hii kilamtu anahasira zake, Tusitafutane jamani...
Hata kulalamikia viongozi tu halafu bado tunaendelea kuwaacha watawale pia ni ujinga.Sasa tusikwepe majukumu na kutaka sauti kubwa zaidi. Wanawanyonya kwa sababu viongozi wenu wanakubali aina ya mikataba mibovu kama hii ya Tz na madini. Hamlazimishwi sijui ni 10 percent?
Umejibu vizuri sana. Hakuna hoja ambayo huwa naiona mbovu kama hii ya kwamba wanatunyonya. Hivi tangu tumepata uhuru si tumeshindwa hata kuendeleza walivyotuachia, na bado tunakesha kila kukicha tukiwaita waje wachukue hata rasilimali zetu kupitia uwekezaji usio na tija. Hatujalazimishwa ila tunawaita wao waje wachukue. Kwahiyo ni ujinga usio na kifani kulalamika eti wanatunyonya. Na kuhusu UN, yaan tunataka tupate vya bure, upewe nafasi ya kuwa na sauti kubwa wakati hupendi kuchangia gharama. Jambo la ajabu sana hili