USA huchangia 22% bajeti UN, Afrika huchangia ngapi huko?

USA huchangia 22% bajeti UN, Afrika huchangia ngapi huko?

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2016
Posts
7,682
Reaction score
9,564
Nataarifiwa hapa USA pekee huchangia yapata 22% ya bajeti ya UMOJA WA MATAIFA (sisi Afrika kwa umoja wetu, AU wenye nchi 54 tunachangia % ngapi huko UN?). Mhe. Trump ataendelea na formula (22%) hii? Hivi Afrika hatuwezi kujipanga tukawapelekea ng'ombe, mahindi na maharage wauze kwenye mnada wapate pesa za kujiendesha, kama mchango wetu badala ya pesa cash?
 
Kwa mtindo huu maamuzi ya mtoaji zaid ndio yatakuwa influence zaidi! africa tatizo tuna integration nyingi za kiuchumi ambazo kimsingi majukumu yanafanana!
 
Nataarifiwa hapa USA pekee huchangia yapata 22% ya bajeti ya UMOJA WA MATAIFA (sisi Afrika kwa umoja wetu, AU wenye nchi 54 tunachangia % ngapi huko UN?). Mhe. Trump ataendelea na formula (22%) hii? Hivi Afrika hatuwezi kujipanga tukawapelekea ng'ombe, mahindi na maharage wauze kwenye mnada wapate pesa za kujiendesha, kama mchango wetu badala ya pesa cash?
Afrika tunachangia 1% ambapo SA wanachangia 0.9,, jiulize Tz tunachangia ngap? Cna uhakika kama kiwango kimebadilika
 
Yani Tanzania imchangie Marekani? wtf??
Kutunyonya watunyonye na kuwachangia pia tuwachangie? WAMETUOA AU?
Sasa tusikwepe majukumu na kutaka sauti kubwa zaidi.

Wanawanyonya kwa sababu viongozi wenu wanakubali aina ya mikataba mibovu kama hii ya Tz na madini. Hamlazimishwi sijui ni 10 percent? [emoji72] [emoji72]
 
Sasa tusikwepe majukumu na kutaka sauti kubwa zaidi. Wanawanyonya kwa sababu viongozi wenu wanakubali aina ya mikataba mibovu kama hii ya Tz na madini. Hamlazimishwi sijui ni 10 percent?

Umejibu vizuri sana. Hakuna hoja ambayo huwa naiona mbovu kama hii ya kwamba wanatunyonya. Hivi tangu tumepata uhuru si tumeshindwa hata kuendeleza walivyotuachia, na bado tunakesha kila kukicha tukiwaita waje wachukue hata rasilimali zetu kupitia uwekezaji usio na tija. Hatujalazimishwa ila tunawaita wao waje wachukue. Kwahiyo ni ujinga usio na kifani kulalamika eti wanatunyonya. Na kuhusu UN, yaan tunataka tupate vya bure, upewe nafasi ya kuwa na sauti kubwa wakati hupendi kuchangia gharama. Jambo la ajabu sana hili
 
Jengo la makao makuu pale AU, Addis Ababa pamoja na furniture wametusaidia "rafiki" zetu Uchi-na.
 
Back
Top Bottom