US Election Coverage 2008

YN: kwamba wapiga kura wa TZ na US wanafanana, hapa inabidi nikubaliane na wewe kwa kiwango cha kutosha!

Nyani kaniambia eti tangu Obama apata ule ushindi wa NC unakunywa kishenzi?!! Nakukumbusha kuwa madaktari wanapendekeza kuwa mwanamume asizidishe 3-4 units kwa siku 🙂
 

..ushauri umefika ndugu yangu!! asante. LOL
 

Sio kwa mwanamume tu bali pia mwanamke..especially inapokuja kwenye swala la ujauzito..Hata ile wine kidogo tu wanasema haifai
 
....BHO rasmi na kwa mara ya kwanza kachukua lead miongoni mwa super delegates ambao tayari wapo commited!!! mambo hayo, jamaa yupo mbele kila kitu sasa sijui argument ya HRC kuendelea na "camp-pain" ni nini?! kaaaazi kweli.

Kaka Kitila na Best NN mnaweza kutusaidia maelezo hapo....maana tunajua nini Wolfson(HRC 'camp-pain' communication director) atachosema!!. bwahahahaha.
 
mama akiamua kurun kama independent itakuwaje?

Swali zuri ila duh haitaleta picha nzuri....itakuwa sio tena mapenzi kwa nchi bali ni tamaa na uroho wa madaraka especially baada ya kushindwa kwenye mchakato.

YNIM, hii kitu watu waliiwrap miezi miwili nyuma...sema ndio hivyo kama Dick Morris anavyosema ...apart from her stubbornness hesabu nazo zinamchanganya mama.
 

...nadhani huyu mama alikuwa kapania sana kupata nomination na baadae urais, hakuwa na option ya kwamba kuna kushindwa (kama sio yeye basi hakuna mwingine)....yaani hii kushindwa ni kama ndoto mbaya na nadhani ndio maana inakuwa taabu kwake kuukubali ukweli!!! aibu sana, mtu anapokuwa na tamaa ya madaraka kwa kiasi kama hiki.
 


So far hakuna kati yao aliyokwisha fikisha delegates 2,029 (which is a requirement). Pamoja na kwamba Obama anaongoza lakini bado hajapata, nikiazima maneno ya JK, kura za kutosha kumfanya awe nominee. Against this, sioni ni kwa nini Hillary aonekane ni kituko kwa kuendelea kupambana na kujaribu kukamilisha ndoto zake. Isitoshe kanuni za DNC zinasema kwamba superdelegates watafanya maamuzi independently kama wapiga kura wengine ikiwa na maana kwamba wapo hutu kum-support mgombea yeyote kati ya Barack Hussein Obama na Hillary Rodham Clinton. Sasa hizi kelele zinatoka wapi? Kwa nini watu wasisubiri process nzima ikamilike? Kama tumeweza kusbiri miezi 12 tunashindwaje kusibiri wiki tatu ili hiyo June 3 ifike na mambo yaeleweke? Au mshikaji ana haraka sana ya kutinga oval house hata kabla ya Januari 2009?
 

Jamani jamani, hivi ni kipi kinachomfanya Hillary aonekane ana tamaa ya madaraka kushinda wanasiasa wengine? Mlitaka afanyeje, yaani ajitoe tu ili aonekane hana tamaa ya madaraka?
 
Jamani jamani, hivi ni kipi kinachomfanya Hillary aonekane ana tamaa ya madaraka kushinda wanasiasa wengine? Mlitaka afanyeje, yaani ajitoe tu ili aonekane hana tamaa ya madaraka?

...ndio ajitoe, tena ajitoe sasa ama sivyo sie tunamwona ni spoiler na mwenye tamaa ya madaraka!!.
mahesabu jinsi yalivyo, she does not have any chance to win this thing!! yaani wanategemea kudra tu za mwenyezi mungu.....hii inanikumbusha hadithi ya Fisi mwenye njaa na mkono wa binadamu apitae njia!! LOL....its not going to happen, hivi anataka mpaka ashindwe mara ngapi hizi primaries ndio atoke?? mbona wakina Romney walijitoaga mapema kule kwa GOP? huyu mama vipi.........?
 

YN: Siasa ingekuwa inaenda hivi watu wangekuwa hata hawahangaika kugombea. Kwani hatukujua kuwa JK angeshinda 2005, sasa kwa nini akina Mbowe na wengine walihangaika kugombea na kukimbiakimbia nchi nzima wakikampeni? Siasa haiendi hivyo kaka. Politics is never static and so are politicians. A winner this minute could be a big looser in the next. Tumeyaona haya hata kwenye mchakato wa hapo US. MacCain angesikiliza kelele kama hizi leo asingekuwa nominee wa republicans.
 
... mbona wakina Romney walijitoaga mapema kule kwa GOP? huyu mama vipi.........?

Kumlinganisha Romney na Hillary ni kumuonea kwa sababu i) Romney alikuwa nyuma ya MacCain kwa kiwango cha kutisha ii) even more important, Romney alijitoa rasmi baada ya MacCain kufikisha idadi ya delegates wanaotakiwa (1900 na ushee). Sasa huyu Barack Obama ana delegates wangapi sasa hivi hadi awe declared presumprive nominee? Nyie mna haraka ya nini wakati uchaguzi ni Nov na kuapishwa ni hadi January? Hao DNC walioweka hizo tarahe za uchaguzi za nini kama mtindo wenyewe ndio huu wa kutaka watu wawe ma-quittors?
 
Nadhani huyu 'die hard" wa HRC, nadhani baada ya mama kuachia ngazi atahamia kwa babu McCain maana yeye anachotak ani uzoefu..mmh sijui Mbowe alikuwa na uzoefu gani kwenye utumishi wa uma zaidi ya ubunge wa muda mfupi tu...mama kashindwa sasa anaharibu mambo kumpa mzungu mwenzake nafasi, mcCain.Anajitahidi kuchafua ili McCain aje apate urahisi...but hatafanikiwa..White house itakuwa black house mwaka huu...kichwa kile...uzoefu wa kuzaliwa..sio wa kuolewa na rais wala kupigana vita na kula mi torture mpaka unapagawa..halafu unasema unauzoefu..mmh mtu wa 72 y.o si babu wa kukokewa moto jamani? Jaluo kichwa acha aingie white house.
 

Kweli na hii imepelekea kukidhofisha chama in terms of division kutokana na emotions ambazo ali zi stir up delibarately!

The question then becomes...WHY?...

The assumpted reason is the fact kwamba Mama alifikiri Obama atakuwa kama maji ya mto ambayo ataswim kulekea ng'ambo ya pili ambapo ni paradiso(white house)Badala yake ni wazi kuwa hakushughulika kuyapima maji kabla hajajitosa! She thought it was gonna be an easy swim kwasababu Mc Cain alikuwa yuko very low in polls na kizingiti (maji) kuwa Obama!

Kwasabau baada ya ule uchaguzi mdogo wa 2006 na polls zilizokuwa zikiendelea kuonyesha wananchi kukatishwa tamaa na job outsourcing, the slip of dollar values in the world monetary exchange, High gas prices, The war in Iraq..The list goes on and on....Kuyumba kwa Republican kulikuwa kumepelekea very low rate job approvals!

Hivyo kama Obama na yeye angesema OK Mama nenda..Ni wazi general election angepeta!

Lakini message ya Obama ili resonate zaidi na wananchi kwani wamechoshwa na okey dokeys za washington! Na inapokuja kwenye issue...Hawana tofauti kubwa wala nini na kwa hiyo mpambano unaendelea kwasababu Mama anasema we dont know this guy so lets buy time something might happen?

Hivi tumesahau kuwa file lake la passport lili uko State department la rekodi zake nyingi tu ikiwa za kusafiri zili kuwa zinachunguzwa?

Sasa wote tunasubiri kwani tunahisi kuwa kuna kitu Mama anajua na watu wanataka afanye haraka aseme ni nini siri hiyo!

Lakini kuna lots and lots of other suprising factors Mama hakuweza kuweka kwenye msamiati wake kuwa ama hata mawazoni mwake kuwa there's someone kama Obama anaweza kumletea upinzani yeye mwenye resume ya zaidi ya miaka 35 ndani ya Chama!

Yani ni sawa na Aloyce Kimaro amwangushe Kikwete kwenye uchaguzi wa uwakilishi wa CCM 2010!

Mama bado ana disbelief na ameamua kufanya yale ambayo hakuna anayeamini na hivyo kupelekea personal hate between them!

Na ndio maana kule PA wakabakia kufanya vituko kama bowling na kunywa pombe!

Hii ni kwasababu sasa Mama anayatumia mahesabu yake ya tokea mwanzo kuwa the longer the fight..the lesser they will talk issues..Sasa hapo yanaanza mambo ya kipumbavu..eti hawajui wafanyakazi ngumu na hodari wa marekani wa viwandani, mashambani Sasa unamuona Obama na yeye ana enda kunyonyesha ndama nk!

Eti hata pombe hanywi kama sisi! Eti hata bowling hawezi huyu si mwenzetu!

Hivi unafikiri SD hawaoni hilo?

Hawa watu hawapendani na nafikiri ni baada ya jaluo kutoamini macho yake pale Clintons walipo cheza karata chafu ikiwa ni pamoja na ya race, gender na kuwa na roho ngumu hata ikiwa na kukigawa chama!

Delegates wamegundua mama ni shetani na nadhani kwasababu hawapendani kabisa anaweza kuutolea nje U VP akiamini kuwa Obama hatashinda na hivyo kijijengea mazingira ya kusema ..Si ni lisema? Hapo baada ya term ya Mc Cain ili na yeye a run!

Ama inabidi vikao vya siri kati yao viwekwe na wanegotiate kwa sababu U VP si kitu sana na hauna nguvu sana so wanaweza kunegotiate terms za function za Mama!

Ama pia wasaidizi wengine na wakongwe wa cahma kama vile familia ya Kennedy wanamshauri aachane na Mama na ajenge coalition safi isiyokuwa na baggage nyingi!

Kuna yule mama wa Arizona naye wanam mention sana ili kukaunta balance ile notion kuwa wakina dada wamekuwa marginalized na hivyo wataenda kwa Mc Cain!

We'll wait and see!
 
..mimi nafikiri HRC ni kama wale wakimbiaji mbio ambao humalizia ili kujua wametumia muda gani. mshindi tayari anajulikana kuwa ni Barack Obama.

..kinachonishangaza ni hawa wanaomsumbua huyu mama. wana wasiwasi gani?

..kama suala ni kuleta umoja ktk chama basi nadhani njia za kiungwana na kistaarabu zinapaswa kutumika kumshawishi Mama asitishe kampeni yake.

..nadhani HRC anapaswa kukaribishwa ktk timu ya ushindi ya Barack Obama. hii tabia ya kumfokea HRC ajitoe nadhani ndiyo inayotishia zaidi umoja wa Democratics.

NB:

..Ted Kennedy alikuwa na kura chache kuliko alizonazo HRC sasa hivi but he took his case all the way to the convention. tena he did that against a sitting President of his own party.

..nimefurahishwa na uungwana wa Senator.Mc Govern alipo-jump ship kuhamia kwa Barack Obama. hii ni tofauti na uhuni aliofanya Bill Richardson.

..I hope Obama atakuwa careful na huyu Bill Richardson. Kile kitendo chake cha ku-leak mazungumzo yake na HRC kwa waandishi wa habari kiliondoa heshima niliyokuwa nayo kwa Bill Richardson.
 
portion of news from cnn website

In an interview with USA Today, she cited an Associated Press report that, she said, "found how Sen. Obama's support among working, hard-working Americans, white Americans, is weakening again, and how whites in both states who had not completed college were supporting me."
It is difficult to overstate the negative effect this remark has had on superdelegates, party leaders and her Democratic colleagues in both houses of Congress. "That's not a way to land the plane," one of her key supporters said. "If you were a superdelegate, you'd say, 'We have to shut this down right away.' "

But others worried that her words were calculated, that by venturing into such risky, rhetorical territory about race, she might put Obama under increased pressure to take her on the ticket before more damage and loss of support from her working-class base is felt.

Former San Francisco Mayor Willie Brown, an old Clinton friend, said Friday that she had made a major mistake in suggesting "that hardworking Americans are white people." [/B]"This statement has got to be dealt with by Hillary Clinton, and Hillary Clinton alone," he said on MSNBC's "Hardball." "The sooner she does that," he said, "the sooner her ship is going to start sailing in a better direction


wazee mnaona mambo hayo?.
 

Forcus on the highlights:

Mama hajafokewa ajitoe bana we vipi?

Ni mazingira halisi ndiyo yanayofanya aonekane kama ana ka ukichaa flani hivi!

Hivi wewe unaona hii ni kawaida?

Bill Richardson ni m hispanic so alishtushwa kuona kuwa ni wazi Clintons wako radhi kukumbatia ubaguzi!

Hili lilimshtua given the fact wako together for a long period of time!

Tumejifunza mengi ndani ya mioyo ya watu ni tofauti na nje na matendo yao hufunua baadhi ya nia zao za ndani!

Richardson ni mwanamume wa kweli!

Na siku ana muendorse Obama aliwaambia umati wa waspanish waliojazana hapo kwa ki spanish kuwa... "Huyu ndiye atakayewaheshimu kiukweli kweli!"

Hivi hiyo satement we uliichukulia vipi?

Jamaa hakujali licha ya kwamba wa spanish walikuwa wanampigia kura Mama, na mama kushinda NH etc etc..

Anajua pia kuwa Clintons wali captalize on divide and rule pale walipo kuwa wakiendeleza ubaguzi na vurugu kati ya minority hawa! Divide and rule waliyokuwa wakii enjoy kina Clinton pamoja na watawala wengi tu waliopita!

Hivi hujui kulikuwa na mpango madhubuti wa kuwaingiza waspanish zaidi hapa Marekani ili waspanish wawazidi namba weusi kwenye issue ya ni nani minority mwenye nguvu!?

Kujaribu kupunguza nguvu zao za kisiasa!


Richardson alishare uchungu wa minority wa kuendelea kupewa maziwa tu!

Wamegundua wanataka mtu mwenye kuwaheshimu ki ukweli na kuwa si maziwa tu..Bali hata ng'ombe mzima na maziwa yake ni possible hence UTU!
 
gamba la nyoka,

..mimi nadhani hawa liberal wataja toana macho jinsi wanavyomgombania Barack Obama.

..yaani wanajiaibisha sana wanavyopakaziana mambo ya u-racist ili mradi waonekane they are cool and comfortable with AA and Obama.

..hii habari ya kusema Obama anakosa support ya white-blue-color workers hakuianzisha HRC. tena kama unafuatilia kila network huchambua ushindi wa Obama/HRC na kuelezea umetokana na which demographic group.

..sasa ukianza kuchambua kura kwa kutumia demography ktk nchi kama Marekani basi huwezi kuepuka comments kama za HRC. lakini comments hizohizo tumekuwa tukizisikia kila siku kwenye hizi networks.

..ppl need to be very careful here b4 race becomes the theme, and major issue, in this presidential race.

jmushi1,

..hayo mambo ya kugawa wapiga kura white,black,latino, yellow, blue-color etc etc, Barack Obama amekuwa akiyapinga siku zote.

..vilevile mambo ya kuchongeana, huyu RACIST, huyu vile, sidhani kama yanamsaidia Obama. sana sana yanaweza kuwa-galvanize weupe dhidi yake. race should not be an issue in this race.

..Obama ndiyo alikuwa mgombea wa kwanza kurusha tangazo kwamba HRC "hawaheshimu" Hispanics. Hiyo ilikuwa wakati wa primaries za Nevada.

..sikuelewa alichosema Bill Richardson wakati anamu-endorse Obama. kama hicho ndicho alichokisema basi kinaenda kinyume na kauli mbiu ya kampeni ya Obama kuwaunganisha Wamarekani wote.

..nadhani Richardson hakupima uzito wa maneno yake. je Obama akimchagua HRC kuwa running mate, Richardson atawaeleza nini Latino. Si itakuwa Obama kachagua mtu asiyeheshimu Latinos, hivyo Obama haheshimu Latinos?
 

Joka Kuu sitaki kuendeleza malumbano..Ila nakupa changamoto:
Wewe Nyoka na Nyani si mnadai issue ya race tuna ikazia mno! Then if thats the case...

1)Mama anadai jamaa hana support ya hao wewe unaowatetea kuwa ni "Blue Color White Voters!

2)Na sisi tunasema Democrats ina wanachama zaidi ya 50% ambao ni weusi..Cheza ngoma then nipe jibu!

NB:Halafu joka mbona sikuoni kwenye home politics bana!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…