
historia ya wapi hiyo mkuu, embu leta hata source tuone.
Hivi hujui vita vya Korea marekani ilipiga mabomu Pyongyang yote ile mpaka wakawa wanaripoti kwamba hakuna cha kulipua tena mji wote upo udongoni.
Marekani ilirusha mabomu tani 650,000 kwenye ile vita zaidi ya mabomu yote iliyorusha kwenye vita vya pili vya dunia ambayo yalikua tani laki nne na kitu.
Theluthi ya raia wa NK waliuawa, zaidi ya watu milioni 3 waliuawa. Marekani ilibakisha sehemu ndogo tu iichukue Korea yote ile. Huyo mchina kaja kuingilia kipindi NK kashakula kichapo cha mbwa mwizi ndo majeshi ya US yakarudishwa nyuma hadi pale mpakani (DMZ). Unadhan Kim kung'ang'ania nukes ni mjinga?!,anawajua Marekani vilivyo...
Wakati wa vita vya Korea NK ilikua ishateka Korea kusini yote ikibakiza kisehemu kidogo tu iichukue SK yote, ndipo Marekani akaingia mzima mzima kumtandika NK kuanzia SK mpaka kwake tena chumbani kabisa kuanzia Pyongyang mpaka vijijini kabisa huko. Usicheze na Marekani ww... Hata vita sasa hv vikizuka huyo mchina atakuja kuingilia baadae kipindi dogo yuko hoi taabani ili kuokoa jahazi maaana mchina mwenyewe anajua shughuli ya Marekani.