Urusi kukutana na makundi yote ya kipalestina kwa mashauriano. Ni mchakato wa kuundwa taifa huru la Palestina

Asiyeshindwa ni Allah peke yake na anayejaribu kuchukua sifa hiyo lazima atamfedhehesha na kama alivyofanya kwa akina Fira'aun na wengine waliotangulia.
Mkuu, usichanganye mambo, tofautisha allah na Mungu. The later is supreme
 
Hiyo ardhi ilipogawanywa na UN Israel walipewa 55% na Wapalestina wakapewa 45% wakakataa wakitaka 100% yote. Wapalestina mpaka leo kuna makundi yanataka maeneo ambayo Israel haiwezi yatoa nayo yawe sehemu ya Palestina. Au wengine wanataka kabisa Israel ifutike waende sijui wapi na ardhi nzima iwe Palestina.

Kama unadhani Israel inatishika na mikutano wewe jidanganye tu, hiyo ni mikwara mbuzi kwao. Hakuna taifa la Palestina litaanzishwa kwa maeneo yaleyale wanayodai Wapalestina. Na hakuna taifa lolote litailazimisha Israel ikubali taifa la Palestina kinyume na msimamo wao wa do or die.

Pale suluhu ilikuwa ni mataifa mawili jambo ambalo wote hawataki. Huwezi wafukuza Wapalestina sababu walipolowea hapo baada ya Waisraeli kupigwa na Babylonian empire, utawala wa Byzantine, Roman empire na Muslim crusaders walizaliana hivyo ni kwao. Waisraeli walikimbia eneo lao sababu ya kuteswa na kunyanyaswa na kila jirani na kila state, hawakuikana au kuisahau ardhi yao (rejea wimbo wao wa taifa - Hatikva). Walikuwa goigoi, leo hii huwatoi hapo bora uwaue.

Huwezi waondoa Waisraeli sababu zaidi ya miaka 1400 nyuma ile ni ardhi yao, wana historia nayo na ushahidi kama magofu ya temple ya Suleiman upo.

Kwa akili ya kawaida tu, jiulize Wayahudi kwao wapi? Walijikusanya kutoka Uingereza, Ufaransa, Marekani, Canada, Misri, Uturuki, Urusi na kote uko walikuwa na tamaduni zilezile, lugha ileile na dini ileile. Kwahiyo Myahudi wa Marekani ilitokea zari tu akafanana kilakitu na Myahudi wa Uturuki maelfu ya kilometers mbalimbali? Jibu ni lazima kuna chimbuko lao, ndio hapo Israel sasa.

Ukitaka kuunda Palestina kwa masharti ya Wapalestina hawa basi waue Waisraeli wote. Nao wamejipanga kukusubiri, wakiwa na machungu na hasira za kuzunguka dunia nzima wakinyanyaswa kisa wamekimbia kwao. Sasa jichanganye waweke pembeni sheria za kimataifa waingie kwenye death mode.
Apa Umepuyanga mzee

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Uhuru wa Palestina hauwezi kupatikana bila usuluhishi wa pande zote 2 kuhusishwa na kukubaliana. Palestina atataka baadhi ya maeneo na miji kutoka Israel ili aanzishe taifa hilo, je Israel atakubali takwa hilo? Hicho kitu haliwezekani, jambo jema ambalo lingezaa matunda ni kuundwa kwa taifa moja tu la jamuhuri ya muungano wa Israel na Palestina ili iwe jamii moja, Hamas waache misimamo yao ya kidini. Bila hivyo itazuka vita vya 3 vya dunia, Israel hatanii na wala hawezi kuogopa mikwara ya Russia, China hata USA, tusubiri vita vikali sana kati ya Israel na maarifa ya kiarabu
Wenye msimamo ni Israeli au palestina
 
Urusi baada ya kupata ushindi mnono kule Advidika dhidi ya Ukraine imejiona ina wajibu wa kushauriana na makundi yote ya kipalestina wakati ambapo vita vya Gaza navyo viko ukingoni kumalizika.
Inawezekana harakati hizo za Urusi ni kupiga hatua za mbele za mbele katika mchakato wa kuundwa kwa taifa la Palestina kuwahi kupata ushawishi mkubwa kwenye taifa hilo jipya ambalo tayari mataifa kadhaa ya Ulaya yameshatoa wito kwa Benjamin Netanyahu aondoe vikwazo vyake visivyokuwa na mashiko kuhusiana na taifa hilo.
Makundi yaliyoalikwa huko Moscow ni pamoja na Hamas wenyewe,Islamic Jihad yenye makao makuu Syria,PLO iliyoanzishwa na Yasser Arafat na makundi kadhaa mengine.kIkao hicho kinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Katika siku za karibuni viongozi wa Ufaransa,Uiengereza,Hispania na Ujerumani wamekuwa wakimshinikiza sana waziri mkuu wa Israel aache vipingamizi dhidi ya uundwajji wa taifa la Palestina.Macron wa Ufaransa amesema taarifa za kudai kuundwa kwa taifa la Palestina si siri tena na kwamba anataka ifanyike haraka.
Raisi wa Brazil kwa upande wake amepuuza sasa madai ya vifo vingi vya holocast.
Russia invites Palestinian factions to meet next week: Palestinian Authority PM

Alwaz:

Huwezi kuunda chochote hapo bila kukaa na Israel......Utaunda serikali hewani, Try to be realistic jamaa yangu! Najua una mapenzi na Hamas, sio mbaya hata kidogo....Just be realistic....Kama ni hivyo lazima Urusi ikutane na Israel....Unaona hicho kitu kinawezekana? Israel imeweza mara nyingi kwenda Kinyume na Marekani, sembuse mapendekezo ya Urusi....Usiweke kabisa mategemeo katika hilo.
 
Wayahudi wanalalamika sababu kila ikitokea fujo ambazo hata hawajaanzisha wao, wao ndio uibuka washindi au kupata hasara kidogo. Hizi lawama ni sababu Wayahudi hawashindwi, wangekuwa wanashindwa kila mapigano basi Waarabu wasingelilia hizo haki.
Marekani ameongoza dunian kwa kuuza silaha huko Israel Kila siku wanafyatua mabom ili Israel isianguke , mpaka hapo ilipofika kama sio marekan euro .nakuhakikishia hatachakula cha hao wanaheshi wangekosa
 
Vipi kama Iran isingekuwa inaipa silaha Hamas.......Umeliangalia hilo....Jaribu kila mara kuangalia pande zote.
 
waunde taifa moja ila gaza na west bank ziwe autonomous regions kama zilivyo honkong,macau,xianjin
 
Mgogoro ni complex, umebeba extremes kila upande, Israel na Palestina, Kumbuka kuanzishwa kwa Hamas ni extreme version ya Wapelestina, na Netanyahu na chama chake cha Likud kuunda serikali yake kachukua watu wa chama chenye extreme views....Ni vigumno kufikia ufumbuvi....Kama wangepatikana moderates pande zote, angalau mwelekeo wa amani ungeweza kufikiwa.
 
Watu wengi pia hawajui chuki ya Hamas dhidi ya Wapelestina wenzao, nikiwa na maana PA ( Palestine Authority) ni kubwa mno pengine hata kushinda chuki yao na Wayahudi, PA inaonekana ni kama collaborators inaposhiriki hizo Peace negotiations..... Na upande Wa Israel kuna wanaoshangaa wanaposikia kuna hata harufu ya mapatano kati ya serikali yao na Waarabu......Sio rahisi kama tunavyodhani.
 
Urusi baada ya kupata ushindi mnono kule Advidika dhidi ya Ukraine imejiona ina wajibu wa kushauriana na makundi yote ya kipalestina wakati ambapo vita vya Gaza navyo viko ukingoni kumalizika.
Inawezekana harakati hizo za Urusi ni kupiga hatua za mbele za mbele katika mchakato wa kuundwa kwa taifa la Palestina kuwahi kupata ushawishi mkubwa kwenye taifa hilo jipya ambalo tayari mataifa kadhaa ya Ulaya yameshatoa wito kwa Benjamin Netanyahu aondoe vikwazo vyake visivyokuwa na mashiko kuhusiana na taifa hilo.
Makundi yaliyoalikwa huko Moscow ni pamoja na Hamas wenyewe,Islamic Jihad yenye makao makuu Syria,PLO iliyoanzishwa na Yasser Arafat na makundi kadhaa mengine.kIkao hicho kinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Katika siku za karibuni viongozi wa Ufaransa,Uiengereza,Hispania na Ujerumani wamekuwa wakimshinikiza sana waziri mkuu wa Israel aache vipingamizi dhidi ya uundwajji wa taifa la Palestina.Macron wa Ufaransa amesema taarifa za kudai kuundwa kwa taifa la Palestina si siri tena na kwamba anataka ifanyike haraka.
Raisi wa Brazil kwa upande wake amepuuza sasa madai ya vifo vingi vya holocast.
Russia invites Palestinian factions to meet next week: Palestinian Authority PM

Ni njozi za mchana kweupe.....Waarabu wenzao imewashinda kuwapa mtazamo mmoja, ndio Mrusi.....!
 
Hakuna taifa la Palestina litakaloundwa kwa shinikizo la vikundi vya kigaidi kama Hamas na wala uingiliaji kati wa taifa la kiimla kama Russia pia hauwezi kuleta mafanikio yoyote.

Hao watu hakuna wanachofanya ni kujipotezea muda tu. Wapalestina waongee na Saudi Arabia wawagawie ardhi hilo linaweza kuwasaidia ila kinyume cha hapo, watakuwa wanasubiri mtumbwi mlimani.
 
Kama Israel hatanii basi na wengine nao hawana utani pia.Watambana mpaka ataachia taifa liundwe kwa usalala wake.

Alwaz: Hii attempt ya Hamas ya October 7 haitaki fikira nzito! Wamejaribu, Wameonya ujasiri, ni kama ule ujasiri wa waarabu wa vita vya mwaka 1973! Hatimaye Waarabu walipoteza zaidi.

Kwa kukusaidia tu Hamas wanapoteza Gaza! Sijui source ya habari ni ipi hasa, kinachozungumzwa sasa hivi ni reconstruction Gaza baada ya vita, na Hamas is not the major player! Itakuumiza, lakini ukweli ndio huo.

Hapo utaona Utengano wa Waarabu, na utaona Iran ni fundi tu wa kutumia proxy but not real war, utaona nguvu ya Marekani, hasa akiweka pressure zake za chinichini....

Kinachoumiza zaidi Rafah inaweza kuvamia kipindi cha Mfungo wa Ramadhani.....Sielewi kwa nini Israel imechagua kipindi hicho

Kwa hiyo attempt ya Hamas October 7 was very daring, lakini inaonyesha support ya Iran haikua kama walivyotarajia....Houthi haina msaada wowote....Inapoteza muda muda....Haibadili mwelekeo wowote wa Gaza.
 
Urusi baada ya kupata ushindi mnono kule Advidika dhidi ya Ukraine imejiona ina wajibu wa kushauriana na makundi yote ya kipalestina wakati ambapo vita vya Gaza navyo viko ukingoni kumalizika.
Inawezekana harakati hizo za Urusi ni kupiga hatua za mbele za mbele katika mchakato wa kuundwa kwa taifa la Palestina kuwahi kupata ushawishi mkubwa kwenye taifa hilo jipya ambalo tayari mataifa kadhaa ya Ulaya yameshatoa wito kwa Benjamin Netanyahu aondoe vikwazo vyake visivyokuwa na mashiko kuhusiana na taifa hilo.
Makundi yaliyoalikwa huko Moscow ni pamoja na Hamas wenyewe,Islamic Jihad yenye makao makuu Syria,PLO iliyoanzishwa na Yasser Arafat na makundi kadhaa mengine.kIkao hicho kinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Katika siku za karibuni viongozi wa Ufaransa,Uiengereza,Hispania na Ujerumani wamekuwa wakimshinikiza sana waziri mkuu wa Israel aache vipingamizi dhidi ya uundwajji wa taifa la Palestina.Macron wa Ufaransa amesema taarifa za kudai kuundwa kwa taifa la Palestina si siri tena na kwamba anataka ifanyike haraka.
Raisi wa Brazil kwa upande wake amepuuza sasa madai ya vifo vingi vya holocast.
Russia invites Palestinian factions to meet next week: Palestinian Authority PM
Urusi anachokitaka kwa ukraine kinatofauti gani na islael anachikifanya kwa palestina?. Wote ni wavamizi.
 
Hiyo ardhi ilipogawanywa na UN Israel walipewa 55% na Wapalestina wakapewa 45% wakakataa wakitaka 100% yote. Wapalestina mpaka leo kuna makundi yanataka maeneo ambayo Israel haiwezi yatoa nayo yawe sehemu ya Palestina. Au wengine wanataka kabisa Israel ifutike waende sijui wapi na ardhi nzima iwe Palestina.

Kama unadhani Israel inatishika na mikutano wewe jidanganye tu, hiyo ni mikwara mbuzi kwao. Hakuna taifa la Palestina litaanzishwa kwa maeneo yaleyale wanayodai Wapalestina. Na hakuna taifa lolote litailazimisha Israel ikubali taifa la Palestina kinyume na msimamo wao wa do or die.

Pale suluhu ilikuwa ni mataifa mawili jambo ambalo wote hawataki. Huwezi wafukuza Wapalestina sababu walipolowea hapo baada ya Waisraeli kupigwa na Babylonian empire, utawala wa Byzantine, Roman empire na Muslim crusaders walizaliana hivyo ni kwao. Waisraeli walikimbia eneo lao sababu ya kuteswa na kunyanyaswa na kila jirani na kila state, hawakuikana au kuisahau ardhi yao (rejea wimbo wao wa taifa - Hatikva). Walikuwa goigoi, leo hii huwatoi hapo bora uwaue.

Huwezi waondoa Waisraeli sababu zaidi ya miaka 1400 nyuma ile ni ardhi yao, wana historia nayo na ushahidi kama magofu ya temple ya Suleiman upo.

Kwa akili ya kawaida tu, jiulize Wayahudi kwao wapi? Walijikusanya kutoka Uingereza, Ufaransa, Marekani, Canada, Misri, Uturuki, Urusi na kote uko walikuwa na tamaduni zilezile, lugha ileile na dini ileile. Kwahiyo Myahudi wa Marekani ilitokea zari tu akafanana kilakitu na Myahudi wa Uturuki maelfu ya kilometers mbalimbali? Jibu ni lazima kuna chimbuko lao, ndio hapo Israel sasa.

Ukitaka kuunda Palestina kwa masharti ya Wapalestina hawa basi waue Waisraeli wote. Nao wamejipanga kukusubiri, wakiwa na machungu na hasira za kuzunguka dunia nzima wakinyanyaswa kisa wamekimbia kwao. Sasa jichanganye waweke pembeni sheria za kimataifa waingie kwenye death mode.

Mkuu HAKUNA JAMII ILIYOPEWA ARIDHI HAPA DUNIANI NA MUNGU

Binadamu ni kiumbe wa kuhama hama vinginevyo wahindi wekundi wangedai aridhi yao na kuwafukuza wahamiaji wote

Mipaka ya nchi ilijitengeneza baada ya binadamu kuzidi kustaarabika baada ya vita za kugombania maeneo

Leo hii unaambiwa Wangoni asili yao SA, Wairaki asili yao Somalia nk nk
Leo hii tunaambiwa Waarabu wote asili yao ni mashariki ya kati lakini walikuja kulowea Afrika nk nk

Ustaarabu wa mipaka ulipoanza kufanyika basi jamii iliokua inaishi sehemu husika ndio walitambulika kama eneo lakwao

Wapalestina wapo pale kwa miaka zaidi ya 600, wamezaliana vizazi kwa vizazi pale ni kwao

Tatizo kubwa la mgogoro huu ni Waisrael kuamini ile ni aridhi yao kwa mujibu wa imani yao walipewa na invincible God ambaye HAYUPO

Kwa mujibu wa taratibu za kidunia ile aridhi ni halali kwa wapalestina walioishi pale kwa miaka zaidi ya 600

Hakuna namna waarabu wa Afrika wanaweza kwenda nchi yoyote ya Mashariki ya kati na kudai ni kwao
Au haiwezekani hata kwa Black America kuja Africa kudai Afrika ni kwao..... wao ni wamarekani

Tatizo hili alilizalisha Mwingereza baada ya kuwa ignore wapalestina na kuanzisha mchakato wa taifa la waisrael kwenye aridhi yao walio ikalia miaka kwa miaka kisa imani ya dini yao inayosema ile ni aridhi walipewa na Mungu na kuna mahekalu yao
Baada ya hapo wakaanza kuokotezwa waisrael popote pale duniani na kuanza kuletwa Palestine
Na mbaya zaidi ni pale Umoja wa mataifa wa enzi hizo kukubali ombi la Waisrael kuanzisha taifa bila kushirikisha pande zote mbili na kuainisha mipaka anuai

Tatizo kubwa la mgogoro huu watu wengi hawajui Wapalestina wanadai nini?

Two states solution bado inakuwa inawapendelea zaidi Waisrael
Ilianza na 60/40 sasa hivi ipo almost 80/10

Kuna watu hata hawajui maisha ya Gaza na West Bank yakoje
Wanaona ni kama wanavyoishi kwenye nchi zao tu
Gaza ni JELA ya wazi ile
West Bank inakaliwa kibabe kuliko hata makaburu walivyo ikalia Soweto

Dunia nzima tumewa lebel wapalestina kama MAGAIDI as if jamaa ni wajinga sana kudai HAKI yao

Kwa hali ilivyo sasa hakuna pa kuwapeleka mahali Waisrael wala wapalestina

Taifa moja haitakuja kukaa iwezekane.... chuki ni kubwa mmno

Two state solution ya 50/50 ikiwemo Jerusalem angalau ikifanikiwa inaweza kuleta amani
 
Urusi baada ya kupata ushindi mnono kule Advidika dhidi ya Ukraine imejiona ina wajibu wa kushauriana na makundi yote ya kipalestina wakati ambapo vita vya Gaza navyo viko ukingoni kumalizika.
Inawezekana harakati hizo za Urusi ni kupiga hatua za mbele za mbele katika mchakato wa kuundwa kwa taifa la Palestina kuwahi kupata ushawishi mkubwa kwenye taifa hilo jipya ambalo tayari mataifa kadhaa ya Ulaya yameshatoa wito kwa Benjamin Netanyahu aondoe vikwazo vyake visivyokuwa na mashiko kuhusiana na taifa hilo.
Makundi yaliyoalikwa huko Moscow ni pamoja na Hamas wenyewe,Islamic Jihad yenye makao makuu Syria,PLO iliyoanzishwa na Yasser Arafat na makundi kadhaa mengine.kIkao hicho kinatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Katika siku za karibuni viongozi wa Ufaransa,Uiengereza,Hispania na Ujerumani wamekuwa wakimshinikiza sana waziri mkuu wa Israel aache vipingamizi dhidi ya uundwajji wa taifa la Palestina.Macron wa Ufaransa amesema taarifa za kudai kuundwa kwa taifa la Palestina si siri tena na kwamba anataka ifanyike haraka.
Raisi wa Brazil kwa upande wake amepuuza sasa madai ya vifo vingi vya holocast.
Russia invites Palestinian factions to meet next week: Palestinian Authority PM
very unfortunate, Israel ameshaweka wazi kwamba kutokana na icho kilichotokea October 7, hawaoni watakuwa salama kama kutakuwa na nchi ya palestina pembeni yao, wameapa kamba hiyo ni ndoto ya mchana. hata hivyo westbank kuna wayahudi wakazi zaidi ya 600,000 hivyo kwao bora waishi na wapalestina ndani kuliko kuwapa nchi, hilo halitakuja kutokea na urusi hana uwezo wa kumpa maelekezo yeyote Israel. hii ndio bahati mbaya kwa wapalestina. hamas kawaponza sana.mazungumzo yalishaanza na saudia na quatar kutengeneza taifa, hamas wakatibua maji.
 
Alwaz: Hii attempt ya Hamas ya October 7 haitaki fikira nzito! Wamejaribu, Wameonya ujasiri, ni kama ule ujasiri wa waarabu wa vita vya mwaka 1973! Hatimaye Waarabu walipoteza zaidi.

Kwa kukusaidia tu Hamas wanapoteza Gaza! Sijui source ya habari ni ipi hasa, kinachozungumzwa sasa hivi ni reconstruction Gaza baada ya vita, na Hamas is not the major player! Itakuumiza, lakini ukweli ndio huo.

Hapo utaona Utengano wa Waarabu, na utaona Iran ni fundi tu wa kutumia proxy but not real war, utaona nguvu ya Marekani, hasa akiweka pressure zake za chinichini....

Kinachoumiza zaidi Rafah inaweza kuvamia kipindi cha Mfungo wa Ramadhani.....Sielewi kwa nini Israel imechagua kipindi hicho

Kwa hiyo attempt ya Hamas October 7 was very daring, lakini inaonyesha support ya Iran haikua kama walivyotarajia....Houthi haina msaada wowote....Inapoteza muda muda....Haibadili mwelekeo wowote wa Gaza.

Mimi huwa sielewi kabisa kuhusu Iran

Hivi watu walitarajia Iran ifanye nini ili ionekane imei sapoti Hamas?

Vita ni gharama na RISK kubwa haswa kupigana DIRECT
Ndio maana unaona mpaka sasa ni vikundi tu kama Houth, Hezbollah vinavyo jaribu kuishambulia Israel na sio nchi kama nchi

Iran hawezi kufanya ujinga wa kuishambulia Isreal maana atakua kaipa sababu Dunia chini ya US kuishambulia
Anajua kabisa atakua anapigana na Dunia vs yeye
 
Uko sawa mkuu....wengi assumption ni kwamba Hamas walipofanya vile walijua reaction ya Israel itakuwa kubwa, sasa ni nini walitegemea kwa malipizi ya Israel? Hapo ndipo inapokuja Iran......kwa sababu ni mfaziliwa wao mkubwa in terms of Military equipment's, hivyo ilidhaniwa Hiran itaingia vitani kuwasaidia....

Uko sawa mkuu Vita ni risk kubwa mno, inaweza Marekani na Urusi....wana cushion kubwa kiuchumi ku absorbs madhara ya vita, Iran haina hiyo licha ya kelele nyingi, na politically iko fragile, suppression kwa wananchi wake ni kubwa, ukifungulia mlango wa vita itaumia within.

Swali kubwa Hamas ilitafakari madhara ya kulianzisha? Ukweli ni kwamba hakuna chochote kile, Gaza inaondoka mikononi mwao.....Hawawezi kabisa kubadili mwelekeo wa vita, na reaction ya International community haiwezi kuipush Israel ibadili mwelekeo!

Uko sawa Mkuu...
 
very unfortunate, Israel ameshaweka wazi kwamba kutokana na icho kilichotokea October 7, hawaoni watakuwa salama kama kutakuwa na nchi ya palestina pembeni yao, wameapa kamba hiyo ni ndoto ya mchana. hata hivyo westbank kuna wayahudi wakazi zaidi ya 600,000 hivyo kwao bora waishi na wapalestina ndani kuliko kuwapa nchi, hilo halitakuja kutokea na urusi hana uwezo wa kumpa maelekezo yeyote Israel. hii ndio bahati mbaya kwa wapalestina. hamas kawaponza sana.mazungumzo yalishaanza na saudia na quatar kutengeneza taifa, hamas wakatibua maji.
Ile nchi za kiarabu kuanza kurudisha uhusiano na Israel ndicho kilichowapa nguvu Hamas kufanya mipango madhubuti ya kutibua na kujitetea.
Hivy alichofanya Hamas kama utafikiria kiume na kiubindadamu ni sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom