Kuna tofauti kati ya U.T.I=Urinary tract infection na
S.TD=Sexual transmitted disease.
Naona wewe umeandika kuwa una U.T.I lakini kama ni mwanaume kupata U.T.I ni kama haiwezekani vile kwa kuwa njia kuu ya kupata U.T.I ni bacteria kutoka njia ya haja kubwa kuhamia njia ya mkojo. Kwa wanawake ni rahisi sana kwa kuwa kuna ukaribu mkubwa sana kwa njia zote mbili.
2.U.T.I kama ilivyo S.T.D inajumuisha bacteria/virus wa aina mbali mbali. Si wote wanatibika kwa Ciprofloxacin au Tetracycline. Ushauri ni kwenda kufanya vipimo vya kitaalamu uambiwe ugonjwa ulionao kisha upate dawa badala ya kuuliza tiba za vijiweni. Uwe na siku njema.
Good professional advice!