Dkt. Lilian Mnabwiru: Kitaalam inashauriwa kwenda kukojoa baada ya kumaliza tendo la ndoa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Dkt. Lilian Mnabwiru, Bingwa wa Magonjwa ya Kina Mama na Masuala ya Uzazi, Muhimbili anasema Urinary tract infections (UTI) ni ugonjwa unaoathiri njia ya mkojo na moja kati ya njia au sababu zinazoweza kusababisha maambukizi ni wakati wa kujamiiana hasa kama mazingira si masafu.

Ameyasema hayo wakati akichangia mada kuhusu maambukizi ya Ugonjwa wa UTI katika mkutano ulioandaliwa na Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na kitengo hicho cha Serikali.

Anasema njia ya mkojo inaanzia kwenye mrija wa mkojo kwa Mwanaume na Mwanamke. Mrija huu unajulikana kama URETHRA na ukishapata maambukizi ugonjwa sehemu hii unaitwa URETHRITIS. Njia ya mkojo inayofuata baada ya urethra ni BLADDER yaani kibofu, Wanawake wanakuwa na urethra fupi 4cm kulinganisha na wanaume 25cm hivo kupelekea kupata UTI kwa urahisi.
Dkt.JPG

Dkt. Lilian Mnabwiru
Dkt. Lilian anasema njia nyingine zinazoweza kuchangia maambuziki ya UTI ni Wakati wa kuwekewa mpira wa mkojo, ikitokea kuna uchafu unaoweza kusababisha UTI katika mpira husika.

Mazingira ya kukojoa kisha mkojo kutoisha wote, mara nyingi hali hii huwa inawatokea watu wazima.

Mazingira ya kujisafisha hasa kwa Wanawake, unapojitawaza kutoka nyuma kwenda mbele kuna Wadudu wanaoweza kuingia, inatakiwa kujisafisha kutoka mbele kwenda nyuma.

Pia anasema Wanawake wajawazito wanakuwa katika hatari ya maambukizi zaidi kutokana na kibofu kuwa karibu na sehemu ya haja kubwa, hivyo wanapokojoa mkojo haushi wote.

Anataja baadhi ya dalili za UTI kuwa ni; Mkojo kuchoma au unaweza kuambatana maumivu ya tumbo la chini wakati wa kukojoa, kukojoa usiku mara kwa mara (ni dalili kuwa mfumo hauko sawa) hasa kama mtu hajanywa maji mengi usiku, mkojo kutoa harufu kali, homa na kusisimka mwili.
Picture1.jpg

Anaeleza kuwa sio kila ugonjwa wa UTI unatakiwa kutibiwa na dawa za Antibiotic bali ka ani katika hatua za awali inatakiwa mhusika anywe maji mengi ili kusafisha njia ya mkono na kuweza kuutoa uchafu.

Kuhusu tiba, Dkt. Lilian anaeleza kuwa sio kila UTI inasababishwa na wadudu na kuwa inashauriwa baada ya tendo la ndoa mhusika anatakiwa kukojoa ili kama kuna wadudu au vimelea ambavyo vinakuwa vimebaki sehemu ya juu vinaweza kutoka kwa njia ya mkojo.

Anaeleza kuwa elimu ya kujisafisha inatakiwa iongezwe hasa kwa wanawake wajisafishe kutoka mbele kwenda nyuma, anasema kuna bakteria ambao wapo katika njia ya haja kubwa na hawatakiwi kuingia sehemu ya mbele, hivyo mtu anapojisafisha kinyume na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua bakteria kutoka nyuma kuwahamishia mbele.
37883d3a-ef39-4964-a121-d048d93e14ff.jpeg

Maafisa wa Afya wakifuatilia mkutano.
Anashauri kuwa matumizi ya Dawa za Antibiotic yanatakiwa kutolewa kulingana na hali ya mgonjwa kwa kuwa dawa zina makundi.

Anasema “Hospitali kadhaa za binafsi zinataka kupata faida, matokeo yake zipo ambazo zimekuwa zikitoa dawa kali za bei juu kwa wagonjwa wa UTI ili wapate hela hata kama UTI sio kiwango cha dawa husika.

“Matibabu ya UTI ambayo haijakomaa yanatakiwa kuanza na dawa za chini, mwisho wake wanasababisha usugu kwa kuwa walianza na dawa kali.

“Hali hiyo imesababisha usugu, hata inapotokea mdudu amehama kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine anakuwa ni yuleyule sugu, hivyo baadaye inaleta shida kwenye matibabu."

Kushiriki kinyume cha maumbile
Akielezea uwezekano wa Wanaume wanaoshiriki ngono katika mtindo wa kinyume cha umbile, Dkt. Lilian anasema wana uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya UTI kwa kuwa wanapofanya hivyo kuna wadudu ambao huwa wanakaa sehemu ya haja kubwa na anapowachukua kuwahamishia kwenye uke nao wanahamia huko pia.

Mbali na hapo Mwanaume anaweza kupata UTI pia kwa kujisaidia katika vyoo vichafu ambavyo mkojo unaporuka ukagonga sehemu chafu kisha kumrudia unaweza kuambayana na wadudu wanaoambukiza.

Amesema “Unaweza kukuta mtu kalewa anaenda kwenye choo kichafu anashika kwa mikono kisha anashika sehemu zake za siri, hapo ni rahisi kuhamisha maambukizi pia.”
 
Back
Top Bottom