Uchaguzi 2020 Urais wa Zanzibar siyo jambo la Muungano. Si sahihi kwa Watanganyika kushiriki kwa namna yoyote ile kumpata Rais wa Zanzibar

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Tunayo mambo mengi tu ya Muungano lakini suala la Uraisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar siyo mojawapo.

Hivi sasa Chama cha Mapinduzi kiko busy kutafuta Mgombea Uraisi wa Zanzibar, katika vitu ambavyo ni makosa ni kuwahusisha Watanganyika katika mchakato wa kumtafuta mtu ambaye atakuwa raisi wa Wazanzibari.

Hivi karibuni kutafanyika mchakato wa uteuzi wa Mgombea Uraisi wa Zanzibar ndani ya CCM, pamoja na kwamba mchakato utaanzia Zanzibar lakini bado Watanganyika waliomo kwenye kamati kuu na baadae mkutano mkuu wa CCM Taifa utahusika sana katika kuwapata wagombea wa nafasi ua Uraisi huko Zanzibar.

Hili siyo sawa kwa sababu haipaswi na haitakiwi kwa Watanganyika kushiriki kwenye kuweka serikali huko Zanzibar ambayo ni ya Wazanzibar na wala haiwajibiki kwa mambo ya Watanganyika!

Hao wana CCM akina Magufuli Basjiru Ally, Mangula na wengineo watakaoshiriki kupitisha Wagombea uraisi wa Zanzibar, wao raisi wa Zanzibar anawahusu nini?, wao ni watanganyika hawana haki ya kuingilia mambo yanayoihusu Zanzibar!

Wana haki ya kujadili wabunge wa muungano watokao huko Zanzibar lakini hawana haki hata kidogo ya kushiriki kuhusu wawakilishi wa huko Zanzibar na Raisi wa Zanzibar!

Uraisi wa Zanzibar siyo jambo la Muungano, sasa je wana CCM wa Tanganyika iweje washiriki kumpata mgombea uraisi wa Zanzibar, huyo raisi yeye anawahusu nini?
 
Siasa ni jambo la Muungano ndio maana hata makamu mwenyekiti wa Chadema Zanzibar huchaguliwa Tanzania bara kwenye mkutano mkuu wa chadema.

Hawaachiwi wazanzibari wenyewe wamchague huko huko Zanzibar. MBOWE na watu wa bara walishiriki kumchagua Makamu Mwenyekiti Chadema Zanzibar wakati sio Wazanzibari

ACT WAZALENDO pia viongozi wa zanzibar walichaguliwa mkutano mkuu uliofanyika Tanzania bara ambapo watanzania bara akina zitto kabwe nk walishiriki kuwachagua wakati sio wazanzibari
 
Beberu wa Wazanzibari ni watanganyika..
Huko waache wachukue form, wachafuane ila raisi wao atatokea kufuatia maamuzi ya Chamwino.. :D

Everyday is Saturday..........................:cool:
 
CCM hawaingilii Maamuzi ya Zanzibar bali Mgombea Urais anapigiwa kura na NEC ya CCM ambapo Uchaguzi huo hufanyika Makao Makuu ya Chama ambayo yako Dodoma, Tanganyika( nadhani hiki ndicho kinakuchanganya) baadae anaenda kupigiwa kura na Wazazibar wenyewe chini ya ZEC
 
Siasa ni jambo la muungano ndio maana hata makamu mwenyekiti wa chadema zanzibar huchaguliwa Tanzania bara kwenye mkutano mkuu wa chadema.hawaachiwi wazanzibari wenyewe wamchague huko huko Zanzibar.MBOWE na watu wa bara walishiriki kumchagua makamu mwenyekiti chadema zanzibar wakati sio wazanzibari

ACT WAZALENDO pia viongozi wa zanzibar walichaguliwa mkutano mkuu uliofanyika Tanzania bara ambapo watanzania bara akina zitto kabwe nk walishiriki kuwachagua wakati sio wazanzibari
Thread closed
 
Tunayo mambo mengi tu ya muungano lakini suala la Uraisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar siyo mojawapo.

Hivi sasa chama cha Mapinduzi kiko busy kutafuta mgombea uraisi wa Zanzibar, katika vitu ambavyo ni makosa ni kuwahusisha Watanganyika katika mchakato wa kumtafuta mtu ambaye atakuwa raisi wa Wazanzibari...
Naona Wazanzibar mnaamka taratibu , japo kwa kuchelewa
 
Zanzibar wakijitenga na Tanganyika baada ya miaka mitano , zanzibar itaanza kutoa misaada nchini Tanganyika
Sound zenu mnajiliwaza tu; kama mna bunge, serikali, jeshi, wimbo wa taifa, mahakama, na kila kitu...nini kinawashinda kuyafikia hayo maendeleo mnayoimba kila siku?!

Nyie urojo tu.
 
Back
Top Bottom