Muungano: VP na Waziri wa Afya, hili si la Muungano. Msiliingize Kinyemela

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,410
31,397
TANGANYIKA ISIWE 'CASH COW'

Kwa hisani na shukrani kwa gazeti la The Citizen


Gazeti la la Tarehe 09/02/2024 linaripoti ufunguzi wa Mkutano wa maradhi yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa Moyo huko ' Zanzibar, mgeni ni Makamu wa Rais( VP) Dr P. Mpango.

VP Mpango akasema kuna uhitaji wa Taasisi ya moyo JKCI Muhimbili ili kurahisha upatikanaji wa huduma Tanzania na mbali. VP akaeleza utayari wa Serikali kuwekeza katika utafiti na matibabu ya maradhi ya Moyo

Akijibu hoja za VP, Waziri wa Afya wa Tanzania Bara au Tanganyika Bi Ummy Mwalimu alisema kuna eneo maalumu limetengwa Zanzibar kuanzisha huduma za JKCI .

Bi Mwalimu alisema tangu kuanzishwa JKCI, taasisi imekuwa kituo cha utafiti na mafunzo katika A.Mashariki.

Mkurugenzi wa JKCI Dr Kisenge alieleza ongezeko la uhitaji wa huduma hiyo Tanzania na nchi za Jirani
Dr akaeleza mpango wa kufungua JKCI Zanzibar ili kupunguza rufaa ikizingatiwa taasisi haina nafasi za kutosha

HOJA ZITOKANAZO.
1. VP wa Tanzania kufungua makongamano au shughuli nyingine zisizo za kiutendaji Zanzibar si si tatizo.
Majuzi , Makamu wa Zanzibar alifungua mkutano wa Vyama vya siasa, ni mambo ya kawaida.

2. Waziri wa Afya wa inayoitwa Tanzania Bara ni wa Tanganyika.
Jina Tanzania Bara si rasmi kwa nchi yoyote bali linatumiwa makusudi kufunika jina la Tanganyika.

Wizara ya Afya ya Tanganyika si jambo la Muungano, Waziri wa Tanganyika hana mamlaka ya mambo ya Afya Zanzibar. Waziri Ummy kuagiza ijengwe Taasisi ya JKCI Zanzibar si sahihi wala hana mamlaka, Zanzibar ina SMZ yenye Katiba, Wizara ikiwemo Afya, Taasisi n.k.

Kuingiza Wizara ya Afya kinyemelea katika Muungano kama alivyofanya Waziri si kuwatendea haki Wazanzibar.
Wazanzibar wamelalamika haya kwa muda mrefu, hawataki yasiyo ya Muungano kufanywa ya Muungano

Lakini pia Wazanzibar wanajukumu. Linapotokea la kero kama la Waziri wa Tanganyika kufanya maamuzi ya Wizara ya Afya Zanzibar, Wazanzbar waeleza kutoridhishwa na kuingiliwa.

Bila Wazanzibar kuzungumzia hili watathibitisha hoja ya UNAFIKI walionao katika Muungano.
Ni unafiki kwasababu unyemela wa kuongeza mambo ya muungano ni huu, wako wapi kukemea?

3. Mkurugenzi wa JKCI anasema wana mpango wa kujenga kituo Zanzibar.

Ukifuatia hotuba ya VP na Waziri Ummy, kuna ushirikiano wa kulisukuma jambo hili kwenda Zanzibar.
Si kazi ya Mkurugenzi kuingiza siasa katika tiba , pengine aliagizwa ayaseme ili kujenga hoja ya JKCI Zannzibar.

Mkurugenzi anaaminisha Umma kwamba rufaa za Wagonjwa 20 kutoka Zanzibar ni kubwa ukilinganisha na rufaa kutoka Mwanza, Kigoma, Mbeya au Ruvuma na nchi za jirani 8 ambazo ni kwa maelfu

Mkurugenzi wa JKCI akiacha siasa na kukumbatia tiba na huduma kwa mtazamo wa sayansi na uchumi, JKCI itakuwa taasisi bora duniani ikizingatiwa soko la Watu milioni 120 la nchi 8 tunazopakana nazo na si wagonjwa 30 au 200 kutoka Zanzibar. Kuna uwezekano mkurugenzi alipewa shinikizo tu na yeye kutamka tu !!!

4. Ikiwa lengo ni kupeleka huduma kwa Wananchi wengi wa Tanzania na nchi jirani kama ilivyoelezwa, JKCI haina manufaa yoyote kujengwa Zanzibar. Kwanza, Zanzibar ina idadi ndogo ya Wakazi kwa wakati mmoja ambao zi zaidi ya milioni moja.

Wazanzibar wengi wanaishi Tanganyika hivyo rufaa za Wagonjwa ni chache na ukweli ni kwamba hakuna.
Wazanzibar wanapanda boti na kutibiwa Muhimbili kama wanavyotibiwa watu wa Kigoma.

Zanzibar inapakana kwa ukaribu na Kenya kama jirani.
Tanganyika inapakana na nchi 8 na kati ya hizo yenye idadi ndogo ya Watu ni Burundi yenye Watu Milioni 12.

Kwa mantiki, kupata Wagonjwa wa nchi 8 zenye idadi ya watu zaidi ya milioni 120 ni muhimu kwa Taasisi ya JKCI kujiendesha kwa faidia ukilinganisha na Wagonjwa 30 au 200 kutoka Zanzibar.

Msukumo wa kujenga JKCI ni wa kisiasa badala ya kisayansi , kiuchumi na kisosholojia.

Ni msukumo unaolenga kufurahisha viongozi au unaosukumwa kisiasa bila kuzingatia uhalisia wa gharama za kuendesha kituo hicho Zanzibar na gharama za Wananchi. i! Hakuna mantiki ya kujenga Zanzibar

Badala ya kujenga Zanzibar, JKCI ijengwe maeneo ya kimkakatia kama Dodoma ambako Wananchi watafika kwa urahisi kutoka mikoani ikiwemo nchi jirani ikiwemo nchi ya Zanzibar.

Kituo kijengwe Kigoma ili kuhudumia Watanganyika wa Magharibi na nchi jirani ya DRC, Rwanda au Burundi ambazo pekee zina ujumla ya watu milioni 80. Hili ni soko linalohitaji JKCI si Zanzibar

Kijengwe Mbeya kuhudumia Wananchi wa kanda za kusini na nchi za Zambia , Malawi n.k. watu Milioni 40

Kudhani Wananchi watatoka Malawi, Songea, Kigoma, Musoma , DRC, Rwanda, Burundi n.k kwenda kutibiwa Zanzibar ni wazo lisilo na maana lililojengwa kwa misingi ya kisiasa isiyo na maana pia.

Haiingi akilini kwa anayefikiri sawa sawa kwamba ni rahisi Wagonjwa kusafiri kutoka Sumbawanga hadi Zbar
Hakuna mtu yoyote anayefikiria kimkakati, kiuchumi na kijimii anayeweza kuafiki wazo la kiwango duni kama hili

Ni wazo lenye taswira ya kisiasa lisilo na maana yoyote wala faida kwa jamii.
 
Sehemu ya II

JKCI ZANZIBAR ; VP na Waziri, msiwabebeshe Watanganyika mzigo wa Taasisi. Hili si la Muungano

Ujenzi wa JKCI Zanzibar ni wazo lenye taswira ya kisiasa lisilo na maana yoyote wala faida kwa jamii .

Kiuchumi ni rahisi kuleta wananchi 30 kutoka Zanzibar watibiwe Tanganyika hata kama Tanganyika itawalipia gharama lakini kupitia uwekezaji makini gharama hizo zinajilipa kwa huduma za Wageni wa nchi jirani( watu 120 Milioni). Tanganyika pekee ina watu milioni 60 kwanini huduma kama hii ipelekwe kwa watu chini ya milioni

Wazo la kujenga JKCI Zanzibar ni la kisiasa bila kujali ongezeko la mzigo wa kuendesha Taasisi kwa walipa kodi wa Tanganyika kupitia jina la Tanzania. Ikiwa ni wazo zuri, Wazanzibar wajenge na kuendesha kituo kwa gharama zao, lakini kulifanya la Muungano kinyemela ni kumtwisha Mtanganyika gharama zaidi

Kama ilivyokuwa kwa kero za Wazanzibar, VP analiangalia suala hili kisiasa ni si iuchumi, kihuduma, kijamii n.k.
Hili si la Muungano, wala halipaswi kubeba gharama za Muungano. Ni kuwatwisha Watanganyika mzigo

5. Zanzibar ina Serikali , Wizara na Taasisi zake, inapata mgao wa 9% ya Bajeti ya Tanganyika, inapata mgao wa misaada , inalipiwa madeni na hazina Tanganyika kwa jina la Tanzania, na inakusanya mapato yake yasiyoingia Hazina ya Tanzania, hivyo iendesha ''JKCI' yake yenyewe.

Ni kwanini VP awabebeshe walipa kodi wa Tanganyika mzigo wa kujenga na kuendesha JKCI Zanzibar ?

Dr Mpango na Waziri wa Afya Bi wanapaswa kuelewa Afya si jambo la Muungano, hivyo kutoa pesa za Tanganyika kwa jina la Tanzania kwenda Zanzibar si kuwatendea haki Watanganyika.

SMZ iachwe iratibu mambo yake ikiwemo kujenga Taasisi zake kama walivyofanya kwa Bandari.
Vipi leo kodi za Watanganyika zitumike katika Taasisi zisizo za Muungano kwa kisingizio cha jina Tanzania!!

Kwenye mapato kama Bandari Wazanzibar hawataki Muungano.
JKCI inahusu gharama Wazanzibar wanataka liwe jambo la Muungano.

Tunasisitiza, ujenzi na uendeshaji wa JKCI Zanzibar uachwe kwa Wazanzibar wenyewe.

VP Mpango alisimamia kuondoa kero za Wazanzibar, hili si kero.

Wazanzibar hawataki mambo yasiyo ya Muungano kuingizwa kinyemela, ni kero kwao.
Afya si jambo la Muungao, tuheshimu hoja za Wazanzibar na tuheshimu kodi za Watanganyika

Tanganyika haina mtetezi lakini isifanywe '' Cash Cow'' .

Tanganyika inahitaji uongozi wake unaowajibika kwa watu wake ili kujinusuru na kujitetea .
 
YASIYO YA MUUNGANO YAONDOLEWE, YASICHOMEKWE KINYEMELA

Wazanzibar wasikilizwe, Watanganyika wasibebeshwe mizigo.

Moja ya malalamiko ya Wazanzibar ni kutotendewa haki kwa ukiukwaji wa mambo ya Muungano.
Kwamba yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 na kwa mujibu wa VP Maosud Othman aliyekuwa AG yamefikia 32

Hoja ya Wazanzibar ya ysiokuwa ya Muungano yaachwe kwa nchi Washirika. Ni ukweli kwa mujibu wa mkataba 1964

Kwa upande mwingine hoja ya Wazanzibar ina matatizo ndani yake
1. Mshirika Zanzibar ana mfumo wa utawala na maamuzi makubwa kuliko ya Muungano.
Mshirika Tanganyika amefichwa kwa jina la Tanzania ambalo pia Zanzibar ana 'share'.

Kile cha Tanganyika kinaitwa Tanzania ni cha wote.

Katika sherehe za Uhuru wa Tanganyika , Dec 09 1964 inaitwa Uhuru wa Tanzania Bara, nchi isiyokuwepo
Rais SSH alikwepa jina Tanganyika kwa kuhofia utajwa wake utazua hoja ya usimamizi na utawala kama Zanzibar.

2. Tatizo la hoja ya Wazanzibar ni uwepo wa Unafiki. Jambo lenye manufaa Zanzibar si la Muungano.
Bandari ni miongoni mwa mambo 11 ya mkataba wa 1964 lakini Zanzibar wameondoa katika Muungano
Yes, wana uwezo huo kwasababu Tanganyika haitambuliwi kiutawala ingawa Tanzania ya sasa ndio Tanganyika.

Rais wa JMT hawezi kuitetea Tanganyika kwasababu kiutawala Tanganyika haipo. Rasilimali za Tanganyika ni za Tanzania na Rais ana uwezo wa kuzielekeza popote ikiwemo Zanzibar.
Zanzibar ina uwezo wa kuchukua maamuzi hata yanayokinzana na sheria za Muungano kwasababu wana serikali.

Mfano wa Pili, Elmu ya Juu si jambo la Muungano. Kamwe Wazanzibar hawalalamiki kuwa la muungano kwasababu wananufaika tena kwa upendeleo. Mfano, nafasi maalumu za Zanzibar kwa Vyuo vya Elimu ya juu zisizozingatia sifa za Taaluma bali Uzanzibar. kuna nafasi maalumu kwa mikopo HESLB kwa Zanzibar n..

Hutawasikia hata siku moja wakilalamika Elimu ya Juu kuwa jambo la Muungano ''in the spirit of Hypocrisy. Unafiki

Mfano , akifungua maghala ya nafaka, Waziri wa Kilimo Tanzania Mh Bashe alimweleza Rais SSH ujenzi wa Ghala kule Unguja na Pemba. Kilimo si jambo la Muungano na Waziri wa Kilimo wa Tanzania hana mamlaka Zanzibar.
Kwanini Ghala lijengwe Zanzibar kwa gharama za Tanganyika?

Kwa kuwa ni ujenzi wa maghala una manufaa kwao hutawasikia Wazanzibar wakilalamikia unyemela. Unafiki

Orodha ya yasiyo ya Muungano ambayo Zanzibar imeyakubali kwasababu yana manufaa ni ndefu sana.

Wazanzibar hawalalamiki JKCI ya Wizara ya Afya kujengwa Zanzibar ni mwendelezo wa 'double face'' au UNAFIKI.

Swali lisilojibiwa na Wazanzibar kuhusu mambo ya mwaka 1964 kuongezwa kutoka 11 hadi 32 ni hili;
Katika mambo 21 yaliyoongezwa kinyemela ni jambo gani ambalo Tanganyika inannufaika nalo!

Swali la pili, ikiwa Zanzibar inapata 9% ya Bajeti ya JMT, ikiwa inapata '' 1/3 ya misaada' na ikiwa haiwajibiki kulipa mikopo au gharama za kuendesha Muungano! ni kwavipi Tanganyika iwajibike kwa gharama za Muungano na kisha mambo yasiyo ya muungano upande wa Zanzibar?

Ni Mkoa gani wa Tanganyika unaopata 9% ya Bajeti ya Muungano?.

Ni Mkoa gani wa Tanganyika usioonekana katika taarifa ya BoT.

Zanzibar inachangia GDP kiasi gani!

Tuhitimishe kwa kusema 'mambo yasiyo ya Muungano' yaachwe , hoja za Wazanzibar za kutoingiza mambo kinyemela zizingatiwe. Na pia Zanzibar iache Unafiki wa kuchagua! Muhimu Tanganyika inatakiwa iwepo ili ijisimamie
 
NDIYO! NI UNAFIKI

Kuna hoja inajitokeza kwamba kusema 'Wazanzibar wana Unafiki' ni lugha kali au tusi.

Neno unafiki si tusi wala si lugha kali. Unafiki ni tabia ya mtu au watu kutenda tofauti na wanayoyasema au kuyaamini

Mathalani, kiongozi anaposema anachukia rushwa, halafu anatoa msamaha kwa wala rushwa huo ni UNAFIKI
Kiongozi akichukia udhalilishaji halafu wasaidizi wake wakawa wadhalilisha huo ni UNAFIKI

Tunapoongelea masuala ya Muungano, kuna unafiki kwa upande wa Wazanzibar

Kwa mfano, katika mambo 22 wanayosema yameongezwa kinyemela katika orodha ya mambo ya Muungao, tumeuliza ni yapi yananufaisha Tanganyika?

Yaani kwa kuongeza hayo mambo Tanganyika imenufaika vipi?
Hakuna Mzanzibar anayejibu wakati huo huo wanasisitiza , Tanganyika ina neemeka. Ni UNAFIKI

Wazanzibar wanaamini kuongeza mambo yasiyo ya Muungano ni kukiuka mkataba, kwanini yanapoongezwa kama hili la Wizara ya Afya au Elimu ya Juu, TAMISEMI., Ardhi au Ajira zisizo za Muungano n.k. Wazanzibar hawalalamiki au kukemea!

Kwahiyo wanaposimama majukwaani na kukemea yameongezwa kinyemela lakini hawakemei na wanayatumia kwa faida zao ni maelezo sahihi (definition) ya UNAFIKI

Tatu, Wazanzibar wanaposema hakuna mfuko wa pamoja wa FEDHA, lakini pia hawataki kuchangia mfuko huo kwa wao wenyewe kukataa ni UNAFIKI.

Orodha ya mambo ya uchumi yenye UNAFIKI ni ndefu, lakini haiishi hapo.

Katika siasa kuna UNAFIKI
Rais wa JMT akitokea Bara Wazanzibar wanalalamika kuonewa na wanataka kuvunja Muungano au uwepo wa serikali 3. Rais akiwa Mzanzibar hutawasikia wakidai tena. Huo ndio UNAFIKI

Tutalitumia neno unafiki kama lilivyo, kwamba sura mbili au double face ni UNAFIKI
 
Tanganyika Inafaidika vipi na 'Unyemela' kama wanavyodai Wazanzibar?

Baadhi ya mambo yaliyoongezwa katika idadi zaidi ya yaliyomo katika mkataba wa 1964 ni haya;

1. Utabiri wa hali ya Hewa.
swali; Kwa kulifanya jambo hili liwe la Muungano, Tanganyika imefadika na nini!

2. Takwimu
Kuna idara za Takwimu za pande mbili za Muungano. Ni haki kusema ile ya JMT ni ya Tanganyika
Watumishi na uongozi wa idara unazingatia uwiano wa Muungano kwa idara za Tanganyika
Fursa za idara zinagawanywa kwa pande mbili, lakini zile za Zanzibar ni Zanzibar tu
Swali; Tanganyika inanufaika na nini kwa utabiri wa hali ya hewa?

3. Utafiti
Uliingizwa katika Muungano mwaka 1986 kwa sheria no. 7
Swali; Tanganyika inafadika na nini kwa kufanya utafiti suala la Muungano?

4. Baraza la Mitihani
Baraza lilifanywa jambo la Muungano 1977. Zanzibar inashiriki katika uongozi wa baraza na ajira za utumishi.
Swali; Tanganyika inafadika vipi na uwepo wa Baraza la mitihani katika Muungano?

5. Elimu ya Juu
Iliingizwa katika mambo ya Muungano mwaka 1967, Tanganyika ikiwa na Chuo kikuu kimoja.
Kufikia mwaka 2000 Tanganyika ilikuwa na vyuo vikuu, na 2001 Zanzibar ikaanzisha chuo cha SUZA
Tangu muungano 1964 Wazanzibar walipata elimu ya Juu kutoka Tanganyika.
Swali: Kuongeza elimu ya juu katika mambo ya muungano, Tanganyika imefadika na kitu gani?

6. Leseni za Viwanda na Takwimu
BRELA imelalamikiwa na Wazanzibar na SMZ ina chombo chake cha kutoa leseani. Kwa maneno mengine BRELA ni chombo cha Tanganyika. Bodi ya BRELA ya Tanganyika ina Wajumbe 2 kutoka Zanzibar
Swali; Tanganyika inafadika na nini kwa kuwa na BRELA katika Muungano?

7. Ardhi na Ajira- haya ni mazito yanahitaji sehemu yake. Tutafafanua

Orodha ya mambo yaliyoongezwa ni ndefu, maswali kwa Wazanzibar, ikiwa mambo hayo yaliongezwa kinyemela kwa lengo la kuwadhulumu, ni kwa njia gani , na kwa faida gani kwa Tanganyika?

Haya ni maswali ambayo Wazanzibar hawataki kuyajibu.

Hoja ya 'unyemela' inajibika ikiwa Wazanzibar wataonyesha ni kwa vipi, mfano suala la Takwimu linanufaisha Tanganyika. Lakini pia Wazanzibar wana kila sababu ya kupaza sauti yasiyo ya Muungano yaonolewe, ukimya na kulalama unyemela ni kutimizia utamaduni wa UNAFIKI.
 
'' Unyemela unapopata Uhalali''

Hoja ya kuingiza mambo yasiyo ya Muungano inayotolewa na Wazanzibar ni kweli na ina mantiki
Moja ya hayo ni suala la Elimu ya Juu ambalo tumelieza liliingizwa lini katika bandiko lililotangulia.
Elimu ya Juu inahusisha utoaji wa nafasi na siku hizi gharama zake kupitia HESLB

Kuna nafasi maalumu za Elimu ya Juu kwa Wazanzibar. Kwamba kigezo cha kwanza ni Uzanzibar halafu sifa za taaluma
Lakini pia Wazanzibar hawakatazwi kupata nafasi hizo wakiwa Tanganyika kama Watanzania.

Kuna nafasi maalumu kwa mikopo ya Wazanzibar kupitia HESLB. Kigezo kikuu ni Uzanzibar kwanza kabla ya sifa nyingine
Lakini pia Wazanzibar wana bodi yao ya mikopo ZEHSLB ambayo ni mahususi kwa Wazanzibar tu!

SWALI; Ikiwa tunakubaliana na hoja kwamba Elimu ya Juu si suala la Muungano kama wanavyodai Wazanzibar, kwanini ziwepo nafasi '' Maalumu za kuingia vyuoni na kupata mikopo' kwa Wazanzibar kwa sifa ya Uzanzibar?
Ile 'Haramu wanayokataa Wazanzibar inageuka vipi kuwa halali kwao hata kuiombea nafasi maalumu?

Je huu si UNAFIKI !
 
ELIMU YA JUU
Tumeliangalia suala la Elimu ya Juu kwa muktadha kwamba si la Muungano. Hoja za Wazanzibar kwamba ni moja ya mambo yaliyoingizwa kinyemela ni ya kweli. Hata hivyo ukweli huo unaambatana na UNAFIKI

Elimu ya Juu inahusisha utoaji wa mikopo. Kuna nafasi maalumu zisizopungua 1,000 kwa Wazanzibar kwa takwimu za takribani miaka 5 iliyopita. Inaweza kuwa kiwango hicho kimeongezeka au kupungua lakini ukweli unabaki pale pale kuna nafasi maalumu za Wazanzibar kwa HESLB tofauti na nafasi maalumu kwa mikoa ya Tanganyika.

HESLB inapotoa mikopo hukusanya kupitia waajiri wa Tanganyika. Ikiwa kuna mwanafunzi wa Zanzibar aliyepewa HESLB na kupata ajira SMZ, ni kwa vipi HESLB kinaweza kukusanya mikopo kutoka Taasisi za SMZ?

Maswali yanayojitokeza ni haya
1. Ikiwa Zanzibar wana ZHESLB isiyotoa mikopo kwa Watanganyika , ni wazi HESLB ni chombo cha Tanganyika.
Kwanini kuna nafasi maalumu kwa Wazanzibar ?
Je, mikopo wanayopewa wanarudisha kwa utaratibu gani wakirudi SMZ?
Je, wanachopewa ni mikopo au scholarship au grant?

2. Kwanini Wazanzibar walalamike kupewa nafasi maalumu Elimu ya Juu na HESLB kwa jambo lile lile wanalosema limeingizwa kinyemela na si la Muungano?
Je, huu si UNAFIKI ?
 
ARDHI YA TANGANYIKA

Katika hoja Wazinzibar wasizotaka kuzisikia ni Ardhi. Rais Mwinyi, alitamka wazi Mtanganyika atapewa ardhi kama Mfilipino, Mnigeria , Mchina au Mmarekani. Kwamba Mtanganyika asahau umiliki ardhi visiwani.

Kwa mujibu wa sheria za Zanzibar alichosema Mh Mwinyi na Wanachoamini Wazanzibar ni Kweli
Katiba ya Zanzibar inatamka nani Mzanzibar na anamiliki vipi ardhi.
Katiba ya 2010 haimtabui Mzanzibar kama Mtanzania, kwa maana Wazanzibar si Watanzania

Katiba ya JMT inatambua kila mtu kama Mtanzania wakiwemo Wazanzibar wenye haki ya kumiliki Ardhi Tanganyika kwa mapande wanayotaka na haki ya kuwauzia Watanganyika ardhi yao.

Haki ya Wazanzibar haipatikani kwa makubaliano yoyote, wao wanatambua ndiyo maana hawataki suala la Ardhi likawa la Muungano. Haki ya Wazanzibar inapatikana kwa ukweli kila mali ya Tanganyika imebatizwa jina la Tanzania, na pili,kiini macho cha jina la Tanzania Bara hakina mamlaka wala serikali kama SMZ.

Kwa maneno machache mali za Tanganyika hazina msimamizi, kilichopo ni usimamizi wa mali za Tanzania ambao haupo.

Usimamizi wa Tanzania haupo kwasababu Tanzania inayosemwa ina mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano na ardhi ni mojawapo. Kwa mantiki Ardhi haina mwenyewe lakini Tanzania amejivisha umiliki

Yes Tanzania imejivika umiliki wa Ardhi kwa makosa. Sheria iliyounda Tanzania inasema yapo ya Muungano na yasiyo ya Muungano. Ardhi si ya Muungano. Tanzania hana haki ya umiliki wa Ardhi ya Tanganyika.

Lakini pia hakuna taasisi itakayomzuia Tanzania kumiliki ardhi kama ilivyo SMZ kwasababu mmiliki Tanganyika amefanywa 'msukule' kwa jina la Tanzania bara.

Hakuna nchi iliyoitwa Tanzania bara na hivyo hakuna ardhi ya Tanzania bara. Ardhi iliyopo ni ya Tanganyika

Swali:
Ikiwa Wazanzibar wanasema Ardhi si suala la Muungano, iweje wanapoulizwa wanamiliki vipi ardhi Tanganyika wanaolilia ubaguzi? Mbona Watanganyika wakinyamwa ardhi visiwani si ubaguzi?

Je, huu si UNAFIKI?

Tunauliza si unafiki kwasababu huwezi kudai kutendewa haki wakati unatenda dhulma!

Kumiliki ardhi isiyo ya Muungano ni dhulma, na ni dhulma zaidi Mtu kutoka Unguja au Pemba anapomiliki ekari za mashamba na kisha kuwauzia Watanganyika wenye mali yao!
 
ARDHI YA TANGANYIKA vs YA TANZANIA

Sheria ya nchi inakataza mtu asiye Raia wa Tanzania kwa maana asiye Mtanzania kumiliki ardhi.
Raia wa India, Marekani, Nigeria, Rwanda, Burundi, Kenya, Malawi , Uganda n.k. hawaruhusiwi kumiliki ardhi Tanzania

Miaka ya nyuma nchi za EAC zilitaka suala la uhamishaji mitaji na masoko uhusishe Ardhi.
Tanzania ya Rais Kikwete ilikataa Ardhi lisiwe katika mpango huo. Hicho ndicho chanzo cha kuundwa EAC (COW).
Tunajua COW ilikufa baadaye kwasababu suala la Ardhi walilotaka halikutimia

Tanzania ilifanya hivyo kulinda masilahi ya Ardhi ya nchi, lakini kwa mtazamo mwingine Tanzania haikutenda haki.

Kwanini haikutenda haki?
Ardhi ya Tanzania ni ya ( Tanganyika + Zanzibar). Kwa mantiki Tanzania ilikataa Wasio Watanzania kupewa Ardhi.

Zanzibar inasheria yake ya Ardhi, na Sheria ya Ardhi ya Tanzania haitumiki Zanzibar.

Kwa maneno mengine, ukiwa na Tanzani (Tanganyika + Zanzibar) ukaondoa Zanzibar kwasababu inasheria zake, Ardhi ya 'iliyobaki si ya Tanzania tena ni ya Tanganyika.

Inapotokea Tanzania ikawakataza Raia wa EAC kumiliki Ardhi halafu ikaruhusu Raia wa Zanzibar kumiliki hata kuuza Ardhi si kuwatendea haki watu wa EAC.

Kwa Zanzibar kuwa na sheria yao ya Ardhi, hakuna tofauti na Raia wa Rwanda , Burundi au Kenya n.k.
Kwanini tuwatenge raia wengine wa EAC kuhusu Ardhi ya Tanganyika?

Je, Zanzibar huu si Unafiki wa kukataa dhuluma lakini kukubali kudhulumu?
 
TAASISI ZINA MBADALA, IPI YA TANZANIA NA IPI YA ZANZIBAR?

Tumeeleza huko nyuma kwamba hakuna! hakuna taasisi yoyote ya ''Tanzania'' isiyo na mbadala nchini Zanzibar

Huo ndio msingi wa kusema taasisi za Tanzania ni za Tanganyika au kwa wanaoona aibu huita Tanzania Bara
Pamoja na kufichwa kwa jina Tanganyika taasisi hizo zinanyimwa haki kwa kile Wazanzibar wanachoita 'Unyemela'

Moja ya taasisi hizo ni BRELA (Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni). Taasisi haitambuliwi Zanzibar.

Kuna Taasisi mbadala wa BRELA inayosimamia shughuli za Biashara na Lesini nchini Zanzibar.
Kwa maneno mengine BRELA ya Tanzania ni ya Tanganyika na kwasiku hizi wanaita Tanzania Bara.

Bodi ya BRELA inaundwa na Wajumbe, miongoni mwao wawili (2) lazima watoke Zanzibar.

Swali la kujiuliza, Wajumbe hao wawili wanakuja kusimamia masilahi gani ya Zanzibar ikiwa BRELA haitambuliwi Zbar?
Je, Wazanzibar hao wana uchungu na BRELA kama ilivyo Watanganyika au wameletwa kwa ajili ya ajira !

Ndivyo ilivyo kwa taasisi kama ya viwango (TBS) ambako kuna ZBS lakini kuna Wajumbe wa Zanzibar ndani ya TBS
Je, huu siyo unyemela wanaouzungumzia Wazanzibar lakini kwa unafiki wanautumikia 'haramu' hiyo!

Lakini pia katika siasa hilo lipo. Rais SSH aliunda kikosi kazi cha Prof Mkandara kukusanya maoni.
Kuna kikosi kazi kingine kiliundwa Zanzibar kwa sababu hizo hizo kikiitwa kikosi kazi maalumu.

Rais SSH alinukuliwa akisema '' kwa mazingira ya siasa za Zanzibar ilibidi kiundwe kikosi kazi maalumu'
Kwa maneno mengine, kikosi kazi cha Prof Mkandara kilikuwa kwa ajili ya Tanzania au Tanganyika au Tanzania bara

Ndani ya kikosi kazi cha Prof Mkandara kulikuwa na Wajumbe kutoka Zanzibar kwasababu ya kuwakilisha upande wa Muungano. Kwamba, Wazanzibar hao walikuwa na uhalali wa kukusanya na kutathmini maoni ya Watanganyika licha ya ukweli kwamba kikosi kazi cha Mkandara ni cha Tanganyika na Zanzibar wanachao.

Kuleta au kuteua Wazanzibar kwenye Taasisi za Tanganyika zisizo na mamlaka Zanzibar ni 'unyemela' wa kuwatafutia ajira na si kwa masilahi mapana ya Tanganyika.
Ni unyemela unaolenga kutumia Taasisi za Tanganyika kwa jina la Tanzania kutoa ajira na wala si ufanisi.

Tulitegemea unyemela huo upigwe vita na Wazanzibar lakini kwenye mafao hutawasikia! UNAFIKI
 
MADINI NA NISHATI YASIINGIZWE KINYEMELA

Miaka ya karibuni kumefanyika kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu Muungano 1964
Waziri wa madini na nishati wa Tanzania alisaini makubaliano ya ushirikiano (MoU) na Waziri wa madini na nishati kutoka nchi ya Zanzibar.

Laiti Marais wangesimamia utiaji saini, ina maana Rais SSH angekuwa upande mmoja na Rais H.Mwinyi upande mwingine. Swali lingejitokeza, Rais wa JMT ipi ambaye hana mamlaka Zanzibar?

Huo ndio msingi wa MoU kutiwa saini kinyemela, walijua si jambo saihihi na limefanywa kwa mkakati maalumu

Wizara ya nishati na madini si suala la Muungano isipokuwa maeneo ya Muungano kama gesi na mafuta.

Zanzibar iliondoa gesi na mafuta licha ya kuwa ni moja ya mambo 11 ya Muungano.
Zanzibar iliondoa kwa jeuri tu kwasababu Katiba ya SMZ ya 1984 toleo 2010 inatoa mamlaka hayo

Watanganyika hawana uwezo huo, nguvu ya Kikatiba haipo wala hawana uongozi wa kusimamia jambo hilo

Kwamba Katiba ya SMZ ina ukuu dhidi ya Katiba ya JMT na kwamba gesi na mafuta ni rasilimali za Zanzibar tu

Inapotokea Zanzibar isiyo na madini hata mawe au kokoto inataka MoU na Tanganyika inafikirisha sana.

Kwanza, uwepo wa MoU kati ya Nchi ya Tanzania na Nchi ya Zanzibar haujawahi kuwepo. Kwanini leo?
Ni wazi MoU imelenga jambo jingine, hakuna sababu yoyote ya Tanganyika kuingia MoU na Zanzibar

MoU imelenga kuliingiza suala la nishati na madini katika Muungano kinyemela.
Wanaotaka MoU si Tanganyika isiyo na sababu bali Wazanzibar wale wale wanaolalamika mambo ya Muungano kuingizwa kinyemela Kwa maeno mengine MoU ni mbinu tu za kuingiza madini katika Muungano kinyemela. Ikiwa ni unyemela kwanini Zanzibar waandae MoU? Unafiki

Lakini pia kuna maswali ya kujiuliza. Ikiwa madini si suala la muungano kwanini madini ya Tanganyika yamefanywa ya Muungano? Mapato ya madini ynaingia katika bajeti na kupitia hapo Zanzibar inapata 9%

Gesi ya Mtwara na Lindi na kwingine Tanganyika inachangia Bajeti ya Tanganyika na kupitia hapo Zanzibar inapata 9%. Gesi na mafuta yatakayopatikana Zanzibar ni mali ya Wazanzibar!

Lakini si hilo, utalii pia si suala la Muungano. Gazeti moja liliripoti mwezi uliopita kwamba utalii uliingizia Taifa takribani dola 1.6 Bilioni ambazo ni takribani trilioni 5 na ushee.
Kiasi hicho kinaingia katika Bajeti ya Tanganyika kwa jina la Tanzania na 9% inakwenda Zanzibar.

Wanaopaswa kulzungumzia unyemela ni Watanganyika.
Wazanzibar wanaolalamika hawaoni haya? Unafiki
 
Hawa Wansfanya Kazi Kwa Woga Hawasomi Sheria Yaani Utaona Kifo Cha Jiwe Waliwaza Vyeo Bila Kuangalia Kanuni, Taratibu Na Sheria Wanazikiuka. Uroho Ulikuwa Vyeo Vyao
 
NISHATI INAVYOGEUZWA SUALA LA MUUNGANO
WIZARA YA NISHATI NA MADINI INAJENGA MIUNDO MBINU NCHINI ZANZIBAR

Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania bara au Tanganyika Dr. Biteko alikwenda Zanzibar kufungua Ofisi ya mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) wakati wa kuelekea kwenye sherehe za Mapinduzi.

Dr Biteko aliwashukuru Rais Samia na Rais Mwinyi kwa kutekeleza miradi ya kimkakati.

Akimkaribisha Dr Biteko, Waziri wa Nishati na Madini wa Nchi ya Zanzibar Mh Shaibu Kaduara alimshukuru Naibu Waziri Mkuu wa '' Nchi ya Tanzania Bara'' kwa ushirikiano anaoutoa kwa miradi ya umeme kama ule wa kuimarisha miundo mbinu ya umeme ya KV 220 wa Rasi Kilomoni na KV 132 kule Pemba.

Hoja: Nishati na Madini si suala la Muungano, Waziri wa Tanganyika anasimamiaje miradi ya umeme wa Zanzibar?

Zanzibar kuna shirika la Umeme ZESCO '' linalonunua'' umeme Tanesco.
Miundo mbinu ya Pemba na Kilomoni ni wajibu wa SMZ, ipo Nchini Zanzibar na yupo Waziri wa Nishati wa SMZ.

Kwanini kodi za Mtanganyika zihudumie miradi ya SMZ? Zanzibar tayari inapewa 9% ya Bajeti ya Muungano, misaada 1/3 na mikopo isiyorudisha. Kilichobaki Wizara ya Nishati na Madini ni Bajeti ya Tanganyika.
Lakini pia hili si jambo la Muungano, iweje basi fedha na kodi za Tanganyika zikatumike nchini Zanzibar?

Kwanini Tanganyika itumie kodi kuimarisha miundo mbinu Zanzibar tukijua Zanzibar ilivyosanehewa Bilioni 60! Kwamba kodi za Tanganyika zinatumika kutengeneza miundo mbinu ya Umeme ya Nchi ya Zanzibar bila Nchi hiyo kulipa bili za umeme si kuwatendea haki walipa kodi wa '' Nhci ya Tanzania Bara '' zamani Tanganyika.

Lini suala la Nishati na madini limekuwa la Muungano? Je, si hawa Wazanzibar waliondoa mafuta na gesi !
Kwanini hili halikemewi na Wazanzibar kuingizwa kinyemela katika mambo ya Muungano! Je, huu si Unafiki

Bandiko lilotangulia hili tumeeleza kiini macho na kituko cha JMT chini ya Rais SSH kusaini MoU na SMZ ya Nchi ya Zanzibar . Ukitazama kwa mantiki MoU ililenga hilo la kufanikisha miradi ya Nishati na Madini kwa mgongo wa JMT inayoitwa Tanzania Bara lakini ukweli ni Tanganyika kupitia MoU.

MoU ilitengenezwa ili kuhalalisha matumizi ya kodi za Tanzania Bara kwa mira ya SMZ kama hii.
Hakujawahi kuwa na MoU kati ya Tanzania na Zanzibar kwa awamu zote zilizopita! kulikoni sasa?
 
WAJUMBE KUTOKA ZANZIBAR WANAWAKILISHA MASILAHI YA NANI?

Hapo nyuma tumeonesha uwepo wa Taasisi za Tanzania na mbadala wa Taasisi hizo katika Nchi ya Zanzibar.
Kwamba kunakuwaje na Nchi ya Tanzania halafu Nchi ya Zanzibar, hilo tuliache kwa muda!

Hoja ni kwamba, Taasisi za Tanzania au Tanzania Bara au Tanganyika Wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa wanawakilisha masilahi mapana ya Watanganyika. Uteuzi wao hauangalii mjumbe katoka wapi.

Tofauti na hilo , Wajumbe kutoka Zanzibar wana nafasi maalum kwa maana wanatambuliwa kwa Uzanzibar.
Kwa mfano, sheria ya BRELA inasema kutakuwa na Wajumbe 2 kutoka Zanzibar.

Tumeona, Leseni za Biashara si la Muungano. Zanzibar wana sheriana Taasisi mbadala wa BRELA chini ya SMZ.
BRELA ni Taasisi chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara Tanganyika, haina mamlaka Zanzibar

Tumeona pia sheria za JMT siyo 'binding kwa Wazanzibar' kwa maana hazilamiki kutumika Zanzibar, hata inapodi lazima zipitie utaratibu mwingine wa Bunge kama Katiba ya SMZ inavyotamka.

Maswali ya kujiuliza
1. Wajumbe wa Zanzibar katika Bodi za Tanganyika wanawakilsha masilahi gani na yanahusu nini Zanzibar? Wajumbe hao wa Zanzibar wana uchungu au ukereketwa upi na mambo ya Tanganyika?

2. Ikiwa Taasisi hizo zipo chini ya Wizara zisizo za Muungano, kuteua Wajumbe kutoka Zanzibar si Unyemela?

3. Ni Bodi gani ya Wakurugenzi Zanzibar yenye Wajumbe kutoka Tanganyika?
Kama lengo ni kuleta sura ya Muungano kwanini hakuna wateuliwa kutoka Tanganyika?

Lakini pia si kwa taasisi ndogo ndogo, hata taasisi kubwa kama Bunge kuna matatizo.

Wabunge kutoka Zanzibar wapo katika kamati za Bunge za Mambo yasiyo ya Muungano.
Wabunge hao wanawezaje kusimamia mambo yasiyo ya Muungano na yasiyo na masilahi Zanzibar!

Wabunge kutoka Zanzibar wanajadili Bajeti za mambo yasiyo ya Muungano.
Bajeti za mambo yasiyo ya Muungano zinawahusu nini wao kam Wazanzibar waiotaka unyemela!

Kwanini Wabunge wa Zanzibar waijadili mambo ya Muungano kisha kuondoka kama ishara ya kutotaka mambo yasiyo ya Muungano kuingizwa kinyemela! Hili pia litawasaidia Watanganyika kuwa na fursa ya kujadili mambo yao kwa uhuru kama wanavyofanya Baraza la Wawakilishi.

Itapunguza gharama kwa walipa kodi wa Tanganyika. Ikiwa Wabunge wa Zanzibar wataendelea kukaa Bungeni kujadili yasiyo wahausu ya Tanganyika halafu wanalalamika yameongezwa kinyemela, ni UNAFIKI

Ni Wazanzibar hao hao na Wabunge wao wasiotaka mambo ya Muungano yaongezwe kinyemela, lakini wapo Dodoma na kwenye taasisi zisizo za Muungano Kinyemela . Huu si UNAFIKI?
 
RAIS WA JMT ANAPOSIMAMIA MIKATABA YA SMZ

Tarehe 13 June 2022 Rais wa JMT Alishuhudia utiaji saini wa mikataba baina ya Tanzania, Zanzibar na Oman katika Butsani iliyojulikana kama Al Bustan, Muscat , Oman

1. Mkataba wa makubailiano ya Utalii kati ya Tanzania na Oman. Waziri Pinda Chana alisaini kwa Tanzania.

Swali; Ni mkataba wa Tanganyika na Oman au Tanzania? Utatekelezwaje Zanzibar ikiwa Utalii si jambo la Muungano
Waziri husika wa Utalii atakuwa na 'mandate' gani Zanzibar ikiwa Waziri Mkuu wa Tanzania hana ''mandate'' hiyo?

2. Mkataba wa ushirikiano katika Nishati (Oil and Gas) kati ya Tanzania na Oman. Alisaini Mh J.Makamba
Swali: ''Oil na Gas'' iliondolewa na Zanzibar katika Muungano. Huu Mkataba unakuwaje wa Tanzania?

3. Mkataba wa Ushirikiano wa Elimu ya Juu
Swali : Ni Elimu ya juu ya Tanganyika au Tanzania? Zanzibar wana Wizara na mipango yao, itakuwaje ya Tanzania?

4. Mkataba wa makubaliano ya kukuza ushirikiano katika uwekezaji (ZIPA) kati ya NCHI MBILI, Zanzibar na Oman(OIA)
Maswali: Katika masuala ya Kimataifa kuna NCHI ya Zanzibar inayoweza akuingia mikataba yenyewe bila kupitia JMT? Utaratibu huo upo wapi kisheria? Umeanza lini? Tuna Wizara za mambo ya nje ngapi?

Pili, aliyesaini kwa Upande wa Nchi ya Zanzibar ni Mkurugenzi wa ZIPA na aliyeshuhudia ni Rais wa JMT.

Mkurugenzi wa ZIPA anteuliwa na Rais wa SMZ ! Rais wa JMT hana mamlaka naye kwasababu siyo ''authority''
Inakuwaje Rais SSH anasimamia mikataba ya SMZ akiwa Rais JMT bila kuwa na mamlaka kwa Watendahi wa SMZ?

5. Mkataba wa Mashirikiano kati ya watoa huduma za mafuta na Gesi (AGAS), wato huduma za mafuta Zanzibar (ZAOGAS) na Watoa huduma za mafuta Oman. Kwa upande wa Zanzibar aliyetia saini ni Mwenyekiti wa ATOG

Maswali: Rais alishuhudia mikataba ya Tanzania na kisha alishuhudia mikataba ya Nchi ya Zanzibar.

Kuna tatizo hapa, Tanzania ni ipi na Zanzibar ni ipi? Kwanini isiwe Tanganyika na Zanzibar !

Pili, Rais wa JMT ana mamlaka gani kikatiba kutekeleza mambo yasiyo ya Muungano kwa niaba ya Zanzibar?

Hoja:
Ziara hii ya Mh Rais inatuonesha mambo mengi yanayochanganya na yasiyo na utaratibu wala majibu
Inatuonesha nyufa za Muungano na jinsi ambavyo ''Yatima Tanganyika'' anavyoweza kuwa 'abused' kwa jina JMT

1. Mamlaka ya Rais JMT yamepunguzwa kwasababu alikwenda na ujumbe wa nchi Mbili, moja ikiwa Zanzibar
2. Mamlaka ya Rais wa JMT yalivuka mipaka kinyemela kwa kusimamia watendaji wa SMZ asiowateua
3. Mikataba inayohusu Tanganyika imeitwa Tanzania na ya Zanzibar imeitwa Zanzibar
4. Gharama za ujumbe wa Rais zimebebwa na Tanganyika lakini pia kuna wajumbe wa SMZ Zanzibar kinyemela
5.Ni ushahidi wa Taasisi zinavyojirudia lakini za Tanganyika ni za Tanzania , zile za Zanzibar ni zao peke yao

Rais AH.Mwinyi alipuuza suala la Zanzibar kujiunga na OIC kinyume na Katiba !
Hoja ilikuwa kwamba kuna mambo ya nje kama nchi ambayo Tanzania ilikuwa moja.

Kuruhusu Zanzibar kusaini OIC bila kuwasiliana na ''Tanzania'' ilikuwa kuvunja Katiba. G55 ilizaliwa kwa hasira za Watanganyika. G55 ililenga kusimamia masilahi mapana ya Tanganyika isiwe yatima na kutwezwa.
Ras JMT A.H.Mwinyi, kwa sababu za Uzanzibar alipuuza Katiba na kuitumbukiza nchi katika mtanziko mkubwa

Historia ina hulka ya kujirudia!
 
' NDIZI NA VIDONDA VYA TANGANYIKA'

Miaka ya 70/80 SMZ ilikuwa na sharti la Watanganyika kuingia Zanzibar kwa Passport.
Suala lilizungumzwa ndani ya Bunge na Serikali ya JK Nyerere iliwasikiliza Wananchi.
Watangnayika walitaka kuwa Passport ikihitajika Zanzibar na kuja Bara pia itumike

SMZ ilibaini takwa la Tanganyika lingeumiza. Takwimu za Biashara Zanzibar inategemea soko la Tanganyika kwa bidhaa zinazoingizwa kwa kodi ya chini au kukwepa kodi. Sharti la Passport likaondolewa mara moja na SMZ

Kuondoa sharti kukaacha kidonda cha Muungano kikivuja damu. Watanganyika walionja machungu ya kuipoteza Tanganyika ndani ya Muungano.

Miaka ya 90 Rais Mwinyi aliruhusu Zanzibar kujiunga na OIC kama NCHI kinyume na Katiba ya JMT
Suala hilo likatonesha kidonda cha Passport na kundi la G55 likaundwa kuizindua Tanganyika iliyofichwa na JMT

Tangu kundi la G55 lilipoleta hoja na kuzimwa na Nyerere, mzimu wa Tanganyika umepiga kambi
Kila Tume, Kamati iliyoundwa ilikuja na hoja ya 'kupunga mapepo' mzimu wa Tanganyika kwa kuwa na Serikali 3

Rais JK Kikwete alibaini Watanganyika hawaridhiki na Muungano. Kikwete alijua kuundwa kwa Tume ya Warioba kungekuja na mzimu wa Tanganyika lakini aliamua aliamua liwalo na liwe kwasababu kuu mbili.
1. Kikwete alijua uwezekano wa Wapinzani kushinda uchaguzi kwa agenda ya Serikali 3.
2. Alijua hata kwa msaada ''wa vyombo'' Wapinzani wasingeupata Urais lakini idadi Bungeni ingefikia 2/3 na suala la Tanganyika lingerudi. Katika 'failure' zake ni kuogopa Wahafidhina wa Unguja, akazima mchakato

Majuzi , SMZ ilipiga marufuku ndizi za Tanganyika, jambo lililowakasarisha sana Watanganyika.
Kwamba wao hawana chombo cha kutetea masilahi ya nchi yao kama ilivyo Zanzibar

Marais wa JMT na SMZ walikaa kimyaa wkaijua wazi hili ni tatizo linatonesha vidonda vya Muungano.

Walijua kwamba kinachoitwa kero za Wazanzibar husikilizwa haraka, lakini kadhia na udhia wa Watanganyika unadharauliwa kwa vile Watanganyika hawana pa kusimama, wakawapuuzwa.

Ndizi si suala kubwa kwasababu ''population' ya Zanzibar ni chini ya 700,000 kwa wakati mmoja.
Tanganyika ina amasoko makubwa ya ndani na nje yenye watu zaidi ya milioni 100
Tatizo ni chuki za Wazanzibar na kisha viongozi kukaa kimya. Mtakumbuka suala la Mh Mbowe alipotahadhrisha

Pengine Marais wa JMT na SMZ ambao ni Wazanzibar wameamua kukaa kimya kuridhia ' ubabe wa marufuku ya ndizi' au wamekaa kimya kwa kuwaogopa Wazanzibar kama ilivyo katika masuala mengine

Kimya cha SSH na H. Mwinyi kimetonesha donda la Muungano, Tanganyika inatamkika hata na wana CCM wa Tanganyika kuliko wakati mwingine.

Kwa aibu na ukimya, Zanzibar wameondoa sharti la ndizi kwa kuelewa ni tatizo kwao ikiwa Tanganyika itasimama kidete, ikiwa Wabunge na Watanganyika watasimama kidete kwa masilahi ya Taifa lao.

Kitendo cha Zanzibar kutangaza marufuku ya ndizi kwa mbwembwe na nyaraka za sheria na sasa kuondoa kimya ni Unyemela na Unafiki.

Tanganyika ya watu milioni 60 na imezungukwa na watu milioni 100, haihitaji soko la watu milioni 1, inahitaji irudishwe na kupewa heshima zake isimamie mambo yake kama ilivyo kwa Zanzibar.
 
WABUNGE WA ZANZIBAR ACHENI UNYEMELA, MUHESHIMU KAULI ZA WAZANZIBAR

Wabunge wa JMT Dodoma wapo wanaoingia kwa kofia ya Uzanzibar.
Wabunge hao huchaguliwa na watu kati ya 2,500 na 10,000 lakini wanabeba hadhi sawa na Mbunge yeyote

Katiba ya JMT inasema ''kutakuwa na Wabunge wa kuchaguliwa kutoka Zanzibar na Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi''. Wabunge wa Zanzibar, kwa mujibu wa Katiba wana kura ya 2/3 ya mambo yanayohusu Muungano.

Kura ya 2/3 ya mambo ya Muungano ni kwa masilahi ya Zanzibar siyo ''Tanzania''.
Mishahara Posho na gharama zote za Bunge zinalipwa Tanganyika kwa ukweli kwamba ;
1. Zanzibar wanapewa 9% ya Bajeti ya Muungano (siyo 4.5%) kwasababu zisizojulikana
2. Zanzibar inapewa misaada kwa Fromular ya 1/3 na si idadi ya watu kwa Formular isiyojulikana
3. Zanzibar inapewa sehemu ya mikopo kwa Formula isiyojulikana , na hakuna Formular ya kulipa mikopo hiyo
4. Zanzibar haina mchango wowote katika Bajeti au gharama za kuendesha Muungano

Kwa mantiki, ukiondoa hayo kilichobaki ni Mali ya Tanganyika inagharamania mambo mengi ikiwemo Bunge.

Swali: Kwanini Wabunge wa Zanzibar walipwe gharama zao kwa kodi za Tanganyika! tukijua Zanzibar imeshapewa 1-3 hapo juu na haina 4! na kwamba wapo kwa mambo 11 ya Muungano wakitetea Nchi yao ya Zanzibar.

Pili, Wazanzibar wanasema '' Yasiyo ya Muungano yaachwe yasiingizwe kinyemela''

Kwanini Wabunge wa Zanzibar Dodoma wakae miezi zaidi ya 3 kujadili Bajeti ya Tanganyika! ukiondoa 11 ya Muungano? Kujadili yasiyo wahusu ni Unyemela na kukaa Dodoma kuzungumza yasiyo wahusu ni UNAFIKI

Ni Unafiki kwasababu Wazanzibar hawataki mambo yasiyo ya Muungano yajadiliwe kama ya Muungano.

Ni Unafiki kwasababu wanapokwenda Dodoma na kujadili mambo yasiyo ya Muungano ni kuwatia Watanganyika gharama . Kwanini Wazanzibar wajadili bajeti ya TAMISEMI. Wizara ya Utalii na Mali asili, Wizara ya elimu, Afya, mawasiliano, Kilimo, Madini n.k. Je, hapa si kuingiza majadiliano yasiyowahusu wanayoyaita Unyemela?

Wabunge wa Zanzibar waheshimu matakwa ya Wazanzibar ya kuyaacha yasiyo ya Muungano nje.

Kukaa Dodoma wakisikiliza yasiyo wahusu ni Unyemela na kukaa kimya ni Unafiki.

Ni wakati sasa Wabunge wa Zanzibar walipwe na kugharamiwa na SMZ , lakini pia waombe ratiba ya Bunge itakayowapa fursa ya kujadili yale 11 wanayosema kisha waondoke Bungeni kuwapunguzia Watanganyika gharama.

Hoja za Unyemela za Wazanzibar ziheshimiwe! lakini pia Tanganyika ipewe hadhi ya kujisimamia
 
MWENEZI WA CCM ZANZIBAR, COMRADE MBETO APOTOSHA
MGAO WA ZANZIBAR SI HAKI KIKATIBA
MADENI YA ZANZIBAR YANALIPWA NA TANGANYIKA

Video ifuatayo ni kwa hisani ya Global Radio wakifanya mahojiano na mwenezi wa CCM Zanzibar Comrade Mbeto.

View: https://www.youtube.com/watch?v=HfO1-X2-AeI

1. Katika video sikiliza dakika 1.09: 34 mwenezi wa CCM anasema '' Serikali ya Rais Mwinyi zamani ilitegemea asilimia 40 kutoka pesa za wihasani, sasa hivi asilimia 98 bajeti ya Zanzibar ni makusanyo ya pesa za ndani, maana yake serikali ya DrMwinyin inaweza kufanya shughuli za maendeleo bila kutegemea pesa ya Mhisani aina yoyote''

2. Mbeto akajibu swali kwamba, pesa ya Jamhuri ya Muungano ni mgao wake KWA MUJIBU WA KATIBA na inakuja
kwa njia ya msaada wa kibajeti''

3. Bajeti ya SSH inakwenda takribani Trilioni 41 anasema Mwenezi

4. Hoja kuhusu Mikopo, zanzibar inakopa? inakopa kwa utaratibu gani?
Mwenezi Mbeto anasema '' 1964 tulipounganisha nchi zanzibar ilitoa sovereignty na anayeweza kukopa ni JMT.
Zanzibar inaleta mapendekezo inayotaka kukopa na ina mention italipavipi.
Tunapolipa deni, tunapofanya BAJETI TUNATENGA sehemu fulani kuleta Hazina

HOJA ZITOKANAZO
Mwenezi wa CCM Zanzibar anapaswa kuelewa 'facts' kabla hajaingia katika majadiliano.
Tunasema hivi kwasababu sehemu ya maongezi yake amepotosha sana na kusema uongo

1. Bajeti ya SMZ ya 2023/2024 ni 2.8 Trilioni, makusanyo ya kodi na ushuru pamoja na msaada wa Kibajeti kutoka JMT ambayo ni asilimia 9% kwa mujibu wa comrade Mbeto.

Pili, Bajeti ya Zanzibar haina Wizara zenye gharama kubwa kama Ulinzi, mambo ya ndani, nje, Muungano n.k.
Tatu, Bajeti ya Zanzibar haina fungu la Taasisi za Muungano.

Kwahiyo, anaposema kwa asilimia 98 Zanzibar haitegemei msaada kutoka kwa WAHISANI ni uongo, pengo la asilimia 40 hadi 98 anazosema linazibwa na pesa za Tanganyika.

Ni pesa za Tanganyika kwasababu Zanzibar imeshapewa sehemu ya misaada na mikopo na asilimia 9 na si asiliia 4.5 inayopewa (kwa mujibu wa Mbeto) ni pesa za kodi za Watanganyika na zitokazo na rasilimali za Tanganyika

2. Comrade Mbeto anasema 9% inayopewa Zanzibar ni mgao wake kwa mujibu wa Katika.ni UONGO uliokithiri.

Katiba ya JMT na ile ya Zanzibar hazielezi Zanzibar itapewa kiasi gani, hakuna kifungu hicho asilani
Mbeto atambue awamu zote Zanzibar ilikuwa inapata 4.5% , kiasi hicho kimeongezwa na Rais SSH hadi 9% kwa utashi wake na si kikatiba. Ikiwa ni suala la Kikatiba kiasi kingepitia Bungeni

3. Mbeto anasema Bajeti ya SSH inakwenda kuwa takribani Trilioni 41.
Mbeto na Wazanzibar wana haki ya kushangilia ukubwa wa BAJETI ya Tanganyika.
Mwaka 2024/2025 Zanzibar itapewa asilimia 9 takribani Trilioni 10 kutoka Bajeti ya Tanganyika.
Hii ni mara 4 ya Bajeti ya Zanzibar ya 2023/2024. Kadri Tanganyika inavyokusanya kodi na rasilimali zake kama madini, kilimo, utalii na uvuvi ndivyo mgao wa Zanzibar unavyoimarika.

4. Kuhusu Mikopo, Comrade Mbeto amethibitisha tunayosema kwamba Zanzibar inakopa kwa mgongo wa JMT.

Comrade kasema UONGO kwamba SMZ ina Bajeti ya kurudisha mikopo hiyo Hazina.
Bajeti ya SMZ 2023/2024 hakuna kipengele kinachoonyesha matumizi ya pesa kugharamia mikop

Zanzibar inakopa kupitia JMT na hairudishi mikopo.
DENI la mikopo hiyo linalipwa na kodi za Watanganyika ikiwa ni pamoja na mapato yanayotokana na rasilimali zao.

Tumkumbushe Mbeto na Wazanzibar kwa ujumla kwamba, ni vema katika bajeti ya SMZ 2023/2024 tukaona haya;
a. Mchango wa Zanzibar katika Muungano ili tujue Wizara na Taasisi zinahudumiwaje na SMZ katika Muungano
b. Bajeti ya SMZ inayotumika kulipa madeni ya mikopo HAZINA kama alivyosema Mbeto
c. Bajeti ya SMZ ionyeshe kiasi kinachokwenda kwenye Taasisi za Muungano

Ni kwa mtazamo wa hayo hapo juu, tunaona jinsi kisiwa cha watu milioni 1.5 ambao takribani nusu wanaishi Tanganyika na kutumia rasilimali zake kama Watanzania, kikipewa rasilimali nyingi kwa Trilioni kuliko eneo lolote jingine la Tanganyika.

Watanganyika wana HAKI ya kujua uwekezaji wa Matrilioni ya fedha zao Zanzibar una ''return'' gani.
Kwamba nini mchango wa Zanzibar katika maendeleo ya Tanganyika kama sehemu ya Muungano?

Ikiwa Watanganyika hawataelezwa ni kwanini eneo la watu milioni 1.5 linapewa uwekezaji mkubwa kuliko eneo kama Dar es Salaam linalochangia asilimia 80 ya pato la Taifa, au mkoa wa Mwanza unaochangia zaidi ya Trilioni 3, maswali yatazidi kujitokeza.

Na ikiwa Watanganyika hawataelezwa mchango wa Zanzibar ambayo ina uwezeo wa kulipa Wazee Pensheni, ni haki kwa Watanganyika kuhoji, kwanini Watoto wadogo wasipewe BIMA YA AFYA bure?

Hata kama Bima ya Watoto itagharimu Trilioni 1, kiasi hicho kitatoka kwa kodi za Wazazi wao na rasilimali za nchi yao na bado ni kidogo kuliko Trilioni zinazokwenda Zanzibar bila kuona mchango wake ndani ya Muungano.
 
WAZANZIBAR WALALAMIKA KUNYANYASWA BANDARINI DAR ES SALAAM

Gazeti la Mwananchi la 06/04/2024 limeandika kuhusu Mbunge wa Viti maalum (Zanzibar ) akilalamika Wazanzibar kunyanyaswa bandarini Dar es Salaam. Mh Mwanahamis Kasim Hamis anadai watu wanaosafirisha bidhaa na vyakula kutoka Zanzibar wanaulizwa VIBALI.Mbunge anatolea mfano wanaobeba kilo 10 za nyama kuulizwa vibali.

Akichangia Bajeti ya ofisi ya Waziri mkuu, Mwanahimisi anauliza watu watapata wapi Vibali?
Mh 'Mishi' anadai hata Wabunge wanasumbulia, je hali ikoje kwa Wananchi wa kawaida!

Mbunge huyo wa Viti maalum Zanzibar anamalizia hoja yake kwa kusema ''SISI SOTE NI WATANZANIA''.

HOJA
Hii si mara ya kwanza kwa Wabunge wa Zanzibar kudai 'Utanzania'.
Mwaka jana kuna Mbunge alilalamika kutozwa ushuru kwa TV zinazoingia Bara akisema sisi ni nchi Moja bidhaa kutoka Zanzibar ni sawa na za Mbeya kwenda Mwanza ambako hakuna kodi.

Miezi miwili iliyopita Mfanyabiashara kutoka Tanganyika alinyang'anywa ndizi zake kwasababu Nchi ya Zanzibar inasheria za uingizaji Ndizi. Kwamba kulikuwa na zuio kudhibiti maradhi ya migomba( siyo ndizi).

Wazanzibar walisimama kidete kutete sheria hiyo iliyotungwa na Baraza la Wawaklishi, wakidai Sheria za Zanzibar ni za nchi yao na hawatambuia sheria za Muungano. Hoja yao ni kwamba Zanzibar ni Nchi na sheria zake kamilifu

Kuna maswali,; ni wakati gani sisi tunakuwa '' Watanzania na nchi moja'?
Kwanini Wazanzibar wanapotaka fursa za Tananyika wanautaka Utanzania na sheria za 'nchi moja'!

Ikiwa sisi ni Watanzania wa nchi moja, ni kwanini ilitumika sheria kutupa Ndizi na kumtia mfanyabiasha hasara

Wazanzibar watambue kwamba mfumo wa kodi hauruhusu kodi za Zanzibar kuvuka bahari, zinabaki kwao

Tanganyika ina haki ya kuziba mianya inayotumiwa na Wafanyabiashara wa Zanzibar wasio waaminifu kuingiza bidhaa hafifu na kwa kukwepa kodi.

Ni bidhaa haifufu kwasababu Wazanzibar walikataa tathmini za Tanzania Bureau Standards (TBS) na kuanzisha ZBS ili kuweka ''viwango' vyao. Ikiwa sisi ni 'Nchi moja na sote ni Watanzania'kwanini kuna TBS na ZBS?

Utaratibu wa kuingiza bidhaa kutoka Zanzibar kwa hoja ya Nchi moja unaikosesha Tanganyika mapato, unaingiza bidhaa hafifu na unawabebesha Watanganyika mzigo wa kodi kutokana na mapato kupungua.

Uingizaji bidhaa duni kwa kodi hafifu limekuwa tatizo Tanganyika na limewaumiza Wafanyabiashara wa Tanganyika wanaopitishia bidhaa zao Bandari na Viwanja vya ndege vya Tanganyika

Hakuna sababu za Wazanzibar kulalama kunyanyaswa ili hali wana Nchi na sheria zao kama zile za Ndizi.

Bandari Dar es Salaama wanaisaidia Zanzibar kudhibiti bidhaa kutoka Bara kama ilivykuwa kwa Ndizi

Kinachotokea ni '' Chickens come home to roost' Ni kile wanachoita '' Karma is bitch''.
Matendo mabaya anayofanya mtu ipo siku yatamrudi.
 
..YA PAUL KIMITI NA MZEE WARIOBA

Wiki iliyopita Waziri wa Zamani Mh Paul Kimiti alihojiwa katika kipindi cha Dakika 45 na F. Middle
Mh Kimiti alikuwa mjumbe wa Tume ya Katiba ya Mzee Warioba. na amekiri kushawishi Bunge la Katiba likatae Serikali 3 kwasababu ilililenga kuua Muungano.

Katika mahojiano, Kimiti alitaka uwepo wa somo mashuleni kueleza Muungano ingawa hakutaja faida za Muungano wala uatatuzi, Kimiti alieleza kutatuliwa kwa kero za Wazanzibar kama sehemu ya suluhu.

HOJA:
Pamoja na kuwa mjumbe wa Tume ya Warioba , Kimiti hakuwa na ushawishi ndani ya Tume.

Kimiti si miongoni mwa 'VIjana wa Mwalimu Nyerere' kama akina Butiku, Salim Ahmed, na Mzee Warioba.
Vijana wa Mwalimu waliiona kesho ya Muungano wakaitafutia mwarobani katika Rasimu.
Kimiti alikimbilia Kamati ya Bunge na kuwasaliti wenzake hatua ya saliti.

Ni zaidi ya miaka 10 rasimu ilipofanyiwa 'uhuni' na CCM ya akina Kimiti matatizo ya Muungano yameongezeka Watanganyika wakichoshwa kubeba mzigo na mzigo wa Zanzibar kwa pamoja.

Watanganyika wana maswali kuhusu 'ukuu , umuhimu na upekee wa Zanzibar' katika Muungano ikipewa nafasi muhimu sana si kwa mchango wake bali kwa Uzanzibar tu.

Watanganyika wanahoji Zanzibar kupewa rasilimali kuliko eneo jingine la Tanzania bila mchango wake kuoenkana Hazina au BoT. Wanahoji ubaguzi na chuki iliyofuruta dhidi ya Watanganyika ikitendwa na Wazanzibar na kupata usaidizi wa viongozi kwa kukaa kimya!

Mzee Warioba
Wiki hii Mzee Warioba amenukuliwa na gazeti la Mwananchi digital akieleza mambo 4 yanayohitaji kuzungumzwa juu ya Katiba mpya. Wariona kasema suala la Muungano lipo na si leo bali kwa miaka 30.

Jaji Warioba alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, ameshiriki mambo mengi yanayohusu Muungano.
Mzee anasema suala la Muungano lina upekee akirejelea maoni ya Tume kutoka kwa Wananchi.

Warioba akasema ni lazima mjadala uendelee na Wananchi waamue ili kuleta utulivu na utengamano.

HOJA
Mzee Wariona ana uona umuhimu wa kuzungumza kuhusu Muungano.
Jaji anatambua matatizo ya Muungano hayamalizwi kwa kuwapa Wazanzibar kila wanachotaka.
Warioba anasema ni lazima Wananchi wasikilizwe akimaanisha ni suala la nchi na si sehemu ya nchi.

Kuna utamaduni umezuka kwamba Wazanzibar wana haki ya kuongelea Muungano wanavyotaka hata kuutusi na kudhalilisha. Watanganyika wakiongelea Muungano ni 'kosa la jina' na husemwa Wana chuki.

Katika nyuzi hii tunapoongelea matatizo ya Muungano nahali ilivyo inasemwa ni chuki dhidi ya Wazanzibar. Hakuna chuki bali chuki inajitokeza ukweli unapoelezwa hasa kwa wasioutaka.

Kwanini kuzunguzia kero za Wazanzibar ni heri, kuzungmzia ya Watanganyika wasio na platform ni haramu?

Kwa mfano, bandiko lijalo tutaeleza namna Zanzibar inavyopewa kodi za Wafanyakazi wa Muungano.
Kwanza, kwanini ipewe
Pili ipewe kutoka wapi
Tatu inachangia nini katika upatikanaji wa kodi hizo.

Kwanini kuyaeleza ya Watanganyika iwe chuki lakini ya Wazanzibar yaitwe kero?
 
Back
Top Bottom