Urais wa Mama Samia Suluhu Hassan: Changamoto na fursa zilizopo

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Mjadala wetu utakuwa na sehemu SITA kama ifuatavyo:

Kufuatia utangulizi, sehemu ya kwanza itaangalia kwa kifupi historia ya nafasi ya Makamu wa Rais katika jamhuri ya muungano wa Tanzania. Katika hili tutaangazia vipindi viwili muhimu katika historia ya Jamhuri ya Muungano Tanzania:

-Kipindi cha mfumo wa chama kimoja (1965 – 1995) na

-Kipindi cha mfumo wa vyama vingi (1995 – hadi sasa).

Sehemu ya pili itajikita katika mjadala juu ya mfumo wa mgombea mwenza nchini Marekani. Hii ni kwa sababu urais wa Mama Samia Suluhu Hassan ni matokeo ya kazi ya tume ya Jaji Bomani iliyopendekeza nchi yetu iigie mfumo wa mgombea Mwenza, Marekani.

Sehemu ya Tatu itajikita katika mjadala kuhusu ushiriki wa Makamu wa Rais katika maamuzi na shughuli za kila siku za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Lengo kuu hapa ni kuangalia ushiriki wa Makamu wa Rais anayetokana na mfumo wa mgombea mwenza.

Sehemu ya nne itaangazia uzoefu wa Marekani, hasa kujifunza kuhusu ‘legacy’ inayowezwa jengwa na Rais aliyerithi kiti cha urais kilichoachwa wazi na rais aliyefariki dunia. Lengo kuu hapa pia itakuwa ni kuangalia hayo katika muktadha wa Rais ambae awali alikuwa ni mgombea mwenza.

Sehemu ya tano na itajikita katika muktadha wa uongozi wa sasa chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuangalia fursa alizonazo Rais Samia Suluhu Hassan.

Sehemu ya sita na ya mwisho itajikita katika mjadala juu ya changamoto zilizopo.
 
Utangulizi

Taifa bado lipo katika msiba mkubwa wa kuondokewa na Rais wa awamu ya Tano Dr. John Pombe Magufuli. Tukio hili la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufariki akiwa madarakani sio tu kwamba ni la kipekee bali pia ni la kwanza kutokea tangia uhuru wa Tanganyika (1964) na muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964). Kipindi cha nyuma, hasa enzi za mfumo wa chama kimoja tukio la aina hii lingeweza sababisha mkanganyiko mkubwa wa ‘transfer of power’ na ‘transition of government’. Lakini kutokana na mabadiliko ya kumi na moja ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1993) nchi imeweza kuwa na ‘smooth transfer of power’ na kumpata Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ambae kabla ya kifo cha Rais Magufuli alitumikia nchi kwenye nafasi ya uMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Sehemu ya Kwanza - Historia fupi ya Nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tanganyika huru (1961 – 1964) haikuwahi kuwa na nafasi ya Umakamu wa Rais Kikatiba. Nafasi hii ilizaliwa kwa mara ya kwanza baada ya Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar (1964). Kufuatia muungano baina ya nchi hizi mbili, mazingira mapya ya kiutawala na kiutendaji yalihitaji nafasi mbili za umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ifuatavyo:
  • Nafasi ya Makamu wa KWANZA wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Nafasi ya Makamu wa PILI wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande mmoja, mpangilio ulikuwa kwamba iwapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatokea upande wa Tanganyika, basi Makamu wa kwanza wa Rais atatokea upande wa Zanzibar na Makamu wa pili wa Rais atatokea upande wa Tanganyika. Kwa upande mwingine, mpangilio ulikuwa kwamba iwapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatokea upande wa Zanzibar, basi Makamu wa kwanza wa Rais atatokea upande wa Tanganyika na Makamu wa pili wa Rais atatokea upande wa Zanzibar. Kiongozi wa kwanza kushikia nafasi mpya ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar (1964) alikuwa ni Rais wa kwanza wa Tanganyika Julius Kambarage Nyerere. Kwa vile yeye alitokea upande wa Tanganyika, kofia ya Makamu wa Kwanza wa Rais ilivaliwa na Rais wa Zanzibar - Abeid Karume. Hali hii ilimfanya Abeid Karume avae Kofia mbili:
  • Kofia ya kwanza ilikuwa ni ya “Urais wa Zanzibar”. Chini ya kofia hii, Abeid Karume alikuwa na majukumu ya kusimamia na kuendesha mambo yote yaliyohusu Zanzibar nje ya masuala manne ambayo yalikubaliwa yawe ni ya muungano kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano (1964). Masuala haya yalikuwa ni kama ifuatavyo:
  • Ulinzi;
  • Mambo ya Ndani;
  • Fedha na;
  • Mambo ya Nje.
  • Kofia ya pili ya Abeid Karume ilikuwa ni ile ya “Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. Chini ya kofia hii, Abeid Karume alikuwa na majukumu ya kusimamia na kuendesha mambo manne yaliyokubaliwa yawe ya muungano, kwa upande wa Zanzibar – yani - Ulinzi, Mambo ya ndani, Fedha na Mambo ya Nje.
Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kama tulivyokwisha ona, mbali ya nafasi ya Makamu wa kwanza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkataba wa muungano (1964) pia ulizaa nafasi ya “Makamu wa Pili” wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiongozi wa kwanza kushika nafasi hii alikuwa ni Rashid Mfaume Kawawa. Jukumu la Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa ni kusimamia masuala manne yaliyokubaliwa yawe ya muungano kwa mujibu wa mkataba wa muungano, yani – Ulinzi, Mambo ya Ndani, Fedha na Mambo ya Nje.

Mfumo huu mpya chini ya makubaliano ya muungano (1964) wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusaidiwa majukumu yake na makamu wawili wa Urais ulijenga uhusiano au ‘link’ ya moja kwa moja baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar hivyo ‘logic’ kwa nchi kuwa na Muungano wa Serikali Mbili. Pamoja na mfumo huu wa serikali mbili kutokuwa ‘ideal’, lakini ulikuwa ‘workable’ (ulifanya kazi) hasa kwa sababu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bado ilikuwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha Siasa – Chama Cha Mapinduzi.

Ujio wa Mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi Vya Siasa (1992)

Ujio wa mfumo wa Vyama vingi vya Siasa (1991/2) ulilazimisha uongozi wa nchi kupitia upya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kukidhi mahitaji mapya, hasa juu ya nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya mazingira mapya ya kisiasa. Haya yalikuwa ni mabadiliko ya kumi na moja ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msingi wa mabadiliko ya kumi na moja ya Katiba ya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa ni sintofahamu iliyojitokeza, nayo ni kwamba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania angeweza kutoka chama cha siasa ambacho ni tofauti na chama anachotokea Rais wa Zanzibar. Kufuatia sintofahamu hii ambayo ni matokeo ya muendelezo wa kuweka viraka Katiba ya nchi kila mara inapoonyesha uchakavu badala ya taifa kuja na Katiba mpya, Rais wa awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi aliunda tume maalum iliyoongozwa na Jaji Mark Bomani - Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tume ya Jaji Bomani ilipewa jukumu la kuja na suluhisho juu ya kilichoonekana wakati ule kuwa ni ‘mkanganyiko wa kiutawala kwa nafasi ya juu kabisa katika jamhuri ya muungano wa Taanzania. Tume ya Jaji Bomani ikaja na mapendekezo yafuatayo:
  • Pendekezo la kwanza – kufuta nafasi za Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikatiba.
  • Pendekezo la pili – Katiba ya Tanzania ifuate mfumo wa Marekani. Chini ya mfumo huu, nchi inakuwa na Makamu wa Rais Mmoja tu ambae anapatikana kupitia utaratibu wa Rais kuwa na ‘Mgombea Mwenza’.
  • Pendekezo la tatu - Rais wa Zanzibar aondolewe Kofia yake ya pili ya Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili asiwe tena na ‘link’ au uhusiano wa moja kwa moja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapa ifahamike kwamba mabadiliko hayo yakawa mwanzo wa mfumo wa serikali mbili kupoteza ‘logic’ au mantiki.
  • Pendekezo la nne – mchakato wa Kikatiba wa ‘temporary transfer of power’ pale nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano inapokuwa wazi kutokana na Rais aliyepo kujiuzulu, kufariki dunia au kushindwa kuendelea na majukumu yake ya Urais kwa sababu za kiafya.
Ni mapendekezo haya ndio yalizaa mabadiliko ya kumi na moja ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa mara ya kwanza (1995) taifa likajipatia Makamu wa Rais aliyetokana na mfumo wa Marekani – mfumo wa mgombea mwenza. Kiongozi wa kwanza kutumikia nafasi hii chini ya utaratibu mpya wa ‘mgombea mwenza’ alikuwa ni Dr Omar Ali Juma, chini ya Rais wa tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa. Tangia kipindi hicho, utaratibu huu umeendelea kutoa makamu wa Rais - Dr Ali Mohamed Shein (1998 – 2010); Dr Ghalib Bilal (2010 – 2015), Mama Samia Suluhu Hassan (2015 – 2021) na hatimaye Dr. Phillip Mpango (2021 hadi sasa).

Ipo haja ya kujadili kidogo sababu zilizopelekea tume ya Jaji Bomani ione kwamba mfumo wa Marekani ndio uliotufaa katika mazingira mapya ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania.
 
Sehemu ya Pili - Mfumo wa Mgombea Mwenza na Umakamu wa Rais – Marekani
  • Marekani imekuwa na mfumo wa ‘mgombea mwenza’ kwa zaidi ya miaka 150. Hali hiyo imechangia sana kwa Taifa hilo kuendelea kuwa na mfumo wa Demokrasia wenye mafanikio makubwa kuliko nchi nyingine yoyote duniani. Uamuzi wa Tume ya Jaji Bomani kuazima uzoefu wa Marekani ulifuata ‘mantiki’ hiyo.
  • Ingawa K2atiba ya Marekani haizuii mgombea Urais kuteua mgombea mwenza kutoka chama cha upinzani, utamaduni wa Mgombea uRais na Mgombea mwenza kutoka chama kimoja bado unaendelea kutumika.
  • Kwa Marekani, kigezo kikubwa kinachotumika kuteua mgombea mwenza huwa ni kwa ajili ya kumsaidia mgombea Urais kupata kura nyingi katika majimbo au ‘demographics’ ambazo mgombea urais anaonekana kutokuwa na mvuto wa kutosha kwa wapiga kura. Lakini pia wakati mwingine sababu huwa ni kuteua mtu ambae ana uzoefu zaidi katika maeneo ambayo mgombea urais anaonekana kupwaya – mfano uzoefu katika masuala ya kimataifa, ulinzi na usalama nk.
  • Kikatiba, kazi ya msingi ya Makamu wa Rais nchini marekani ni ile ya Urais wa Bunge. Jukumu lake kubwa ni lile la ‘tie breaker’ pale kura juu ya miswaada au maamuzi mbalimbali bungeni zinapofungana.
  • Inapotokea Rais wa Marekani anashindwa kuendelea kutumikia nafasi hiyo kwa sababu zilizoainishwa Kikatiba, Makamu wa Rais huapishwa ndani ya muda mfupi kuwa Rais wa nchi.
Utaratibu huu unahakikisha uwepo wa ‘smooth transfer of power & political transition’ pale kiti cha Rais kinapokuwa wazi kufuatia kifo au kujiuzulu kwa Rais aliyepo madarkani. Uzoefu wa Marekani unatuonyesha hili, kwa mfano:
  • Marekani ina idadi kubwa ya Makamu wa Rais ambao wamewahi kuapishwa kuwa Marais kufuatia kiti cha Rais kuwa wazi, in a smooth power transfer. Nao ni kama ifuatavyo:
  • Makamu wa Rais John Tyler Mwaka (1841)
  • Makamu wa Rais Millard Fulmore (1850)
  • Makamu wa Rais Andrew Johnson (1865)
  • Makamu wa Rais Chester Arthur (1881)
  • Makamu wa Rais Theodore Roosevelt (1901)
  • Makamu wa Rais Calvin Coolidge (1923)
  • Makamu wa Rais Harry Truman (1945)
  • Makamu wa Rais Lyndon Johson (1964)
 
Sehemu ya Tatu – Ushiriki wa Makamu wa Rais anayetokana na mfumo wa mgombea mwenza, katika maamuzi na shughuli za kila siku chini ya Rais wa nchi

Je:
Makamu wa Rais anayepatikana kwa utaratibu wa ‘mgombea mwenza’ nchini Marekani, anashiriki au nahusika kwa kiwango gani na uendeshaji wa kila siku wa serikali au maamuzi yanayofanywa na Rais aliyepo madarakani?

Pamoja na kwamba utamaduni uliopo nchini Marekani ni kwa mgombea urais na mgombea mwenza kutoka katika chama kimoja, haimaanishi kwamba Makamu wa Rais anashirikishwa katika uendeshaji wa shughuli zote au maamuzi yote yanayofanywa na Rais. Sababu kubwa ni kwamba Makamu wa Rais hana majukumu mengi ya Kikatiba. Badala yake Rais wa nchi ndiye anayeamua yepi yawe majukumu ya makamu wake wa Rais na majukumu hupishana kutegemeana na utashi wa Rais aliyepo madarakani. Kwa mfano:
  • Rais John F Kennedy - yeye alimpa makamu wake – ‘Lyndon Johson’ jukumu la kusimamia zaidi “Space Program”.
  • Rais Bill Clinton - yeye alimwelekeza makamu wake – ‘Al Gore’ kusimamia zaidi sera ya mambo ya nje na sera ya mazingira.
  • Rais George Bush – yeye alimwelekeza makamu wake – ‘Dick Cheney’ kusimamia zaidi sera ya nishati (energy policy) na pia mikakati ya kijeshi (military strategies) kufuatia uvamizi wa magaidi wa Alqaeda katika ardhi ya marekani mwaka 2001 (shambulio la 9/11).
Isitoshe, historia inaonyesha kwamba imetokea mara kadhaa kwa Marais wa Marekani kutoka vyama vyote vya ‘Democrat’ na ‘Republican’, kwa nyakati tofauti kuendesha shughuli zao na pia kufanya maamuzi muhimu na makubwa bila ya kuwafahamisha au kuwashirikisha makamu wao wa Rais. Mfano mkubwa ni ule uliohusu mradi wa ‘Atomic Bomb’ (1939) ambapo Rais Franklin Roosevelt aliuendesha kwa siri na kumficha Harry Truman kwa kipindi chote alichokuwa makamu wake wa Rais. Harry Truman alikuja fahamu kuhusu uwepo wa mradi huo wa ATOMIC baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Marekani kufuatia kifo cha Rais Franklin Roosevelt mwaka 1945.

Hata Tanzania, licha ya Rais na Makamu wa Rais kutokea chama kimoja cha siasa, imetokea mara kadhaa kwa Makamu wa Rais kutokuwa na ufahamu wa maamuzi mengine yanayofanywa na Rais wake. Vile vile ni kawaida kwa Makamu wa Rais kupangiwa majukumu na Rais kwa jinsi Rais anavyoona inafaa. Mfano uliopo ni wa hivi karibuni ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan alimwelekeza Makamu wake wa Rais – Phillip Mpango, ajikite zaidi kwenye ufuatiliaji wa kero za muungano, hasa suala la ‘Fedha za Pamoja”.
 
Sehemu ya Nne - Legacy inayoweza achwa na Rais ambae awali alikuwa ni Makamu wa Rais kupitia mfumo wa mgombea mwenza.

Je:
  • Rais anayepatikana kwa njia ya kurithi nafasi iliyoachwa wazi na Rais aliyefariki akiwa madarakani anaweza kujenga ‘Legacy’ yake tofauti na Rais aliyemtangulia?
Uzoefu wa Taifa la Marekani unaendelea kutupa majibu. Katika sehemu inayofuata tutangalia kwa undani uRais Lyndon B. Johnson.

Lyndon B. Johnson aliteuliwa kuwa mgombea mwenza na mgombea Urais – JF Kennedy katika uchaguzi wa Rais wa mwaka 1960 na hatimaye kuwa makamu wake wa Rais. Sababu kubwa ya JF Kennedy kumteua Lyndon Johnson kuwa mgombea wake mwenza ilikuwa ni kumsaidia JF Kennedy kupata kura za kutosha katika jimbo gumu la Texas. It is such a ‘coincidence’ kwamba miaka mitatu tu baadae (1963), Rais JF Kennedy akauwawa kwa kupigwa risasi akiwa ziarani katika jimbo hilo hilo la Texas.

Lyndon Johnson aliapishwa kuchukua nafasi ya JF Kennedy akiwa angani ndani ya ndege iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu John Kennedy kutoka Texas (jimbo alipouwawa JF Kennedy) kuelekea makao makuu ya taifa hilo, Washington D.C, kwa ajili ya shughuli za mazishi ya kitaifa. Ndege ilipofika Washington DC na mwili wa marehemu JF Kennedy muda mfupi baada ya kuondoka Texas, Rais Lyndon Johnson alishuka ndani ya ndege na kuanza shughuli za mazishi akiwa tayari ameshaapishwa kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Hali hii haina tofauti sana na kilichotokea Tanzania kufuatia kiti cha Urais kuwa wazi baada ya Rais John Magufuli kufariki akiwa bado yupo madarakani.

Hata hivyo, Rais Lyndon Johnson aliweza kutumikia nafasi hiyo kwa muhula mmoja tu. Sababu iliyomfanya Lyndon Johnson kuwa Rais wa muhula mmoja haikuwa ni zuio la Kikatiba. Badala yake, kilichomfanya Lyndon B Johnson awe ni Rais wa muhula mmoja ilikuwa ni maaamuzi yake mwenyewe ya kisera akiwa Rais. Ni maamuzi hayo ya kisera ndio yaliyopelekea Rais Johnson apoteze mvuto ndani na nje ya chama chake cha siasa (Chama cha Democrat), hivyo kulazimika kutangaza kutokuwa na nia ya kugombea uchaguzi ili kutumikia awamu ya mbili.

Rais mteule Lyndon Johnson aliapa kuanza kazi kwa kusimamia suala la Haki za Raia – “Civil Rights”. Ikumbukwe kwamba kabla ya kuuwawa kwa risasi, Rais JF Kennedy alijaribu kupeleka muswaada juu ya Haki za Raia bungeni ili uwe sheria lakini alifariki kabla hajafanikiwa. Lakini kufuatia ushawishi na umahiri wake kama Rais, Lyndon Johnson alifanikiwa kuandaa na kupeleka muswada huo bungeni na baadae kupitishwa kuwa sheria – The Civil Rights ACT (1964). Hii lilichangia sana kwa Rais Johnson kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Rais November 1964 dhidi ya mgombea wa chama cha upinzani (Republican Party) – Barry Goldwater.
  • Legacy ya Rais Lyndon Johnson
Kama tulivyogusia awali, mara tu baada ya kuingia madarakani kufuatia kifo cha Rais JF Kennedy, kipaumbele cha kwanza cha Rais Johnson ilikuwa ni maandalizi ya muswada wa HAKI ZA RAIA (Civil Rights) na kuupeleka bungeni ukawe sheria. Tumeona kwamba mtangulizi wake – JF Kennedy alifariki akiwa bado hajafanikiwa katika hilo.

Katika sehemu inayofuata tutaangalia kwa undani sheria ya haki za raia (1964) pamoja na nyinginezo zilizomsaidia Rais Lyndon Johnson kujenga legacy kubwa na tofauti na ya mtangulizi wake, JF Kennedy.

Sheria ya Haki za Raia (1964) zilipiga marufuku ubaguzi wa rangi katika maeneo yafuatayo:
  • ELIMU – Kutoa fursa sawa kielimu kwa raia wote bila ya kujali tofauti za rangi zao.
  • MAJENGO NA MAKAZI – Kutoa fursa sawa kwa raia wote kuingia katika maofisi/majengo yote ya umma bila kujali tofauti za rangi zao. Sambamba na hilo - fursa sawa kwa raia wote kuishi sehemu yoyote ya ardhi ya marekani bila ya kujali tofauti za rangi zao.
  • AJIRA – Kutoa fursa sawa kwa raia wote kuajiriwa bila ya kujali tofauti zao rangi zao.
Kufuatia ushindi wake mkubwa kwenye uchaguzi wa Rais (1964) dhidi ya mgombea wa Republican (Garry Goldwater), Rais Johnson alitoa hotuba ya kusisimua mbele ya Taifa na kutangaza dhamira yake ya kuendelea kuleta mabadiliko makubwa zaidi. Kwa mfano, Rais Johnson alitangaza kuchukua hatua dhidi ya vikwazo vyote vilivyowanyima Wamarekani weusi kupiga kura. Wamarekani weusi walinyimwa haki kupiga kura kupitia mbinu kama vile:
  • Literacy rates tests – yani kuwapa mitihani ya kupima uwezo wao wa kusoma na kuandika kabla ya kuwaruhusu wapige kura. Kwa kipindi kile wengi wao walikuwa bado hawana uwezo wa kusoma na kuandika.
  • Kodi ya Kichwa – Kodi hii ilitumika kama ‘voting fee’ kwa wamarekani weusi kupiga kura, huku raia wengine wakipiga kura bila malipo/bure. Kwa kipindi kile Wamarekani weusi wengi hawakuwa na ajira zenye kuwawezesha kuwa na vipato vya kugharamia kodi husika.
Miswada hii miwili - Muswaada juu ya Kodi ya kichwa na ule wa Literacy Rates Tests, ilikuwa ni the ‘most comprehensive’ katika historia ya marekani, suala ambalo liliimarisha legacy ya Rais Lyndon Johson. Kwa mfano, ni kutokana na Sheria hizi mbili sio tu kwamba wamarekani weusi wameendelea kuwa ni ‘base’ kubwa na muhimu ya wapiga kura nchini Marekani, bali pia Marekani kama taifa lilifanikiwa kupata Rais wa kwanza mwenye asili ya watu weusi- Barrack Obama (2008 - 2016); na hata katika uchaguzi mkuu wa Rais (2020) Marekani ilifanikiwa kupata Makamu wa Rais mwanamke na mwenye asili ya watu weusi kwa mara ya kwanza, Makamu wa Rais Kamala Harris.

Tukiendelea kuangalia Legacy za Rais Lyndon Johnson, tunaangazia sheria zifuatazo:
  • Sheria ya Kutokomeza Umaskini/Fursa Za Kiuchumi (1965)
  • Sheria ya Shule za Msingi na Sekondari (1965)
  • Sheria ya Elimu ya juu (1965).
Sheria ya Kutokomeza Umaskini (1965)
Rais Johnson aliendelea kupeleka miswaada mingi bungeni sambamba na kuanzisha programu mbalimbali zilizolenga kuinua maisha ya wanananchi walio wengi. Moja wapo ulikuwa ni ‘Muswada wa Fursa Za Kiuchumi’ ambao ulikuja kuzaa sheria iliyounda Programu ya ‘Job Corps & Community Action. Pamoja na mengineyo, programu hii ililenga kupunguza umaskini wa wananchi kwa kuzalisha ajira sambamba na matumizi ya fedha (kwa njia ya ruzuku) kusaidia ‘local communities’, ikilenga hasa ‘maendeleo ya watoto’. Jukumu hili lilisimamiwa na ofisi maalum iliyoanzishwa na Rais Johnson – Ofisi ya ‘Fursa Za Kiuchumi’. Ofisi hii pia ilipewa jukumu la kuhakikisha kwamba familia maskini zinapata uhakika wa chakula kupitia sheria iliyojulikana kama – the ‘Food Stamp ACT’ (1964).

Sheria ya Elimu Ya Msingi na Sekondari (1965)
Rais Lyndon Johnson pia alifahamu umuhimu na mchango wa sekta ya Elimu katika mapambano dhidi ya umaskini. Kwa mfano kupitia sheria ya Elimu ya Msingi na Sekondari (1965), serikali yake ilitenga jumla ya Dola za kimarekani Billioni Moja kwa ajili ya kuboresha mfumo wa elimu na kuja na programu maalumu ya elimu kwa ajili ya familia zilizokuwa zinaishi katika maeneo ambayo umaskini ulikuwa umekithiri.

Sheria ya Elimu ya Juu (1965)
Rais Johnson alihakikisha kwamba sekta ya elimu ya juu pia inapatiwa fedha za kutosha. Kwa mfano kupitia sheria ya Elimu ya Juu (1965) serikali yake ilitenga fedha nyingi kwa ajili ya ‘scholarship’ ikilenga zaidi familia maskini ili kutoa fursa za elimu ya juu (vyuo vikuu) kwa vijana ngazi ya vyuo vikuu. Sambamba na hilo, sheria ya Elimu ya Juu (1965) pia ilihakikisha kwamba mikopo ya elimu ya juu inapatikana kwa wingi na kwa riba nafuu.

Sekta ya Afya
Sambamba na Elimu, Rais Johnson pia alilenga kuboresha sekta ya Afya kwa kuanzisha ‘Medicare & Medicaid Programmes’, akilenga zaidi huduma bora za afya kwa wananchi maskini na wazee.

Hatima ya Urais Wa Lyndon Johnson
Pamoja na mafanikio makubwa ya urais wake ambayo hadi leo yameendelea kuacha legacy kubwa, urais wa Lyndon Johson uliishia kuwa ni wa muhula mmoja (1963 – 1969). Kama tulivyogusia awali, hilo halikutokana na zuio la kikatiba bali makosa yake mwenyewe ‘kisera’ akiwa Rais.

Makosa ya Kisera yaliyopelekea ndoto ya Lyndon Johnson kuwa Rais wa mihula miwili kuyeyuka yalitokana zaidi na maamuzi aliyochukua wakati wa Vita Vya Marekani nchini Vietnam (1964). Rais Johnson alifanya ‘controversial decisions’ nyingi ambazo zilipelekea taifa la Marekani kuingia kwenye vita ngumu na ndefu, iliyogharimu taifa la marekani maisha mengi na fedha nyingi za walipa kodi. Mbaya zaidi, ilikuja kufahamika kwamba Rais Johnson alidanganya taifa umma kuhusu “uhalisia na ukweli” wa vita vya Vietnam. Hii ndio iliyopelekea ‘approval ratings’ zake kama Rais kushuka kwa kasi, hivyo kupoteza mvuto wake kisiasa ndani na nje ya chama chake cha Democrat.

Kufuatia changamoto hizi, hatimaye Rais Lyndon Johnson akafikia uamuzi wa kutangazia chama chake na umma kwa ujumla kwamba hakuwa na nia ya kugombea kwa muhula wa pili. Ulipofika msimu mwingine wa uchaguzi mkuu wa Rais (1968), chama chake cha Democrat kikamchagua Hubert Humphrey kuwa mgombea urais. Ni chama cha upinzani cha Republican ndicho kilichoibuka mshindi kwa nafasi hiyo ya urais kupitia mgombea wake - Richard Nixon. Hata hivyo Rais Richard Nixxon nae aliishia kutawala kwa muhula mmoja baada ya kujiuzulu kufuatia kashfa ya ‘Watergate’. Kashfa hii ilihusisha wasaidizi wake ndani ya ikulu na pia chama chake cha Republican ambao walishutumiwa kuvamia ofisi za chama cha upinzani – chama cha Democrat, pamoja na kuhujumu viongozi wa chama hicho.

Kufikia hapa tumejifunza mambo makuu menne:

Kwanza tumejifunza kwamba asili ya urais wa Mama Samia Suluhu Hassan ni mfumo wa mgombea mwenza wa Marekani. Hii ni kutokana na mabadiliko ya kumi na moja ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kufuatia kazi ya tume ya Jaji Bomani miaka ya tisini. Tumejifunza mambo makuu matatu:

Pili tumejifunza kwamba Makamu wa Rais anaye rithi kiti cha uRais kufuatia kifo cha Rais aliyepo madarakani ana uwezo mkubwa wa kutengeneza legacy yake tofauti na yenye maslahi mapana kwa nchi na wananchi kwa ujumla. Tuliona hilo kwa kujadili urais wa Lyndon Johnson kufuatia kifo cha Rais JF Kennedy.

Tatu tumejifunza kwamba chini ya mfumo wa mgombea mwenza, makamu wa Rais hausiki moja kwa moja na maamuzi yote yanayofanywa na Rais wa nchi. Tuliona hilo kupitia mjadala wetu wa utawala wa Rais Franklin Roosevelt na Makamu wake Harry Truman.

Nne tumejifunza kwamba - Makamu wa rais anaporithi kiti kilichoachwa wazi na rais aliyefariki dunia ana nafasi ya kuendelea na kumaliza mihula yake miwili Kikatiba. Anaweza pia kukwama katika hilo, sio kutokana na zuio la Kikatiba bali maamuzi mabaya ya “kisera”, suala ambalo linaweza pelekea apoteze mvuto wake kisiasa na kuishia kuwa rais wa muhula mmoja. Tuliona hilo katika mjadala wetu juu ya urais wa Lyndon Johnson.

Katika sehemu inayofuata, tutajaribu kujadili uzoefu wa Marekani katika muktadha wa nchi yetu ya Tanzania. Tutaangazia zaidi utawala wa sasa wa Rais Samia Suluhu Hassan, hasa kwa kuangalia fursa na changamoto zinazomkabili.
 
Sehemu ya Tano - Fursa alizonazo Rais Samia Suluhu Hassan kujenga legacy yake.

Rais Samia Suluhu Hassan ana fursa ya kujenga legacy yake yenye masalahi mapana kwa taifa kwa njia nyingi. Hapa chini tutajaribu kuangaza machache:

  • Haki za Raia – Kiuchumi na Kisiasa.
  • Haki hizi zinapaswa kuwepo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi.
  • Ujenzi na Usimamizi wa Fursa za kiuchumi - Uchumi wa WATU/WANANCHI.
  • Hasa kwa vijana na wanawake, na ziwepo kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.
  • Nchi yetu ina rasilimali nyingi ambazo zikisimamiwa vyema zinaweza kufanikisha hili. Sambamba na hili ni kuwekeza juhudi kubwa za serikali kwenye ‘Mobilization of Tax Revenues’, lakini kwa kuhakikisha kinachofanyika ni - ‘increasing the TAX BASE’, kuliko ‘increasing the TAX RATE’.
  • Sambamba na hilo ni kujenga mazingira rafiki ya kibiashara na kiuwekezaji kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutokna ndani na nje ya nchi.
  • Uboreshwaji ‘Social Infrastructure’ - MiundoMbinu ya Kijamii:
  • Elimu ya Msingi, Sekondari na Elimu ya Juu.
  • Ubora unaozungumziwa hapa ni ule wa ‘Quality improvement’, sambamba na ‘Quantity Improvement’ inayoendana na mahitaji katika soko la ajira.
  • Muhimu pia ni kushughulikia suala la mikopo ya elimu ya juu kwa kuhakikisha kwamba – kwanza vijana wengi zaidi wenye sifa wanapatiwa mikopo kwa wakati; na pia kupunguza riba za mikopo pamoja na maboresho on ‘payback period & schedule’.
  • Uboreshwaji wa mifumo ya Afya nchini – pia katika hili, ‘quality improvement’ sambamba na ‘quantity improvement’.
  • Ujenzi na Uboreshwaji wa ‘Economic Infrastructure’ - Miundombinu ya Kiuchumi
Barabara, bandari, anga, reli, maji na umeme.
 
Sehemu ya Sita na ya Mwisho - Changamoto zinazomkabili Rais Samia Suluhu Hassan

Zipo changamoto nyingi lakini hapa tutajadili kwa uchache:
  1. Changamoto ya kwanza ipo katika - ‘balancing’ mahitaji ya Miundombinu ya Kiuchumi (Economic Infrastructure) na Miundombinu ya Kijamii (Social Infrastructure).
Miundombinu ya kiuchumi
Hii ni miundombinu inayosaidia au wezesha uchumi wa nchi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Mifano ni pamoja na miundombinu ya barabara, reli, anga, bandari, maji, umeme na telecommunications.

Tafiki za kiuchumi zinaonyesha kwamba - umuhimu wa miundombinu ya kiuchumi katika taifa upo kwenye mchango na uwezo na wake to ‘boost productivity’ ya local firms/Small and Medium Entreprises (SMEs).

Miundombinu ya Kijamii
Hii ni ‘capital’ ambayo inatumika kuzalisha huduma za kijamii, hasa shule za msingi na sekondari, vyuo vikuu na mahospitali.

Tafiti za kiuchumi zinaonyesha kwamba - umuhimu wa miundombinu ya kijamii katika taifa upo kwenye mchango au uwezo wake to ‘boost productivity’ ya wafanyakazi (workers) au nguvu kazi katika taifa (hasa watu wenye umri kati ya miaka 15 na 35).

Swali linalofuata hapa ni je:
Kati ya Miundombinu ya Kichumi na Miundombinu ya Kijamii, Uwekezaji upi ni bora kwa Taifa?

Watafiti wa masuala ya uchumi na maendeleo wametafuta majibu kwa swali hili kwa kujenga economic models zinazotumia “ujenzi wa BARABARA” kuwakilisha uwekezaji wa miundombinu ya kiuchumi na “ujenzi wa SHULE” kuwakilisha uwekezaji wa miundombinu ya Kijamii. Katika sehemu inayofuata tunajadili matokeo ya tafiti hizi kwa kifupi:
  • Uwekezaji wa kudumu kwenye SHULE badala ya BARABARA hupelekea pato kubwa zaidi kwa taifa kiuchumi (national output/GDP) tofauti na uwekezaji huo kufanywa kwenye BARABARA badala ya SHULE.
  • Faida au matokeo ya uwekezaji kwenye miundombinu ya kiuchumi (barabara) huonekana ndani ya kipindi kifupi (short term);
  • Faida au matokeo ya uwekezaji kwenye miundombinu ya kijamii (shule) huonekana baada ya kipindi kirefu (long term).

Lakini pia:
  • Kwa kipindi kirefu (takribani miaka 15) nchi inafaidika na kasi kubwa ya ukuaji uchumi kwa kuwekeza kwenye barabara badala ya shule, na inachukua karibia miaka 24 kwa ‘output’ iliyotokana na uwekezaji kwenye shule ‘to overtake’ output iliyotokana na uwekezaji katika barabara.
  • Lakini hili linakuja na fiscal impplications:
  • Uwekezaji katika shule unapelekea ongezeko la deni la taifa kiasi cha mara tatu zaidi ya uwekezaji kwenye barabara.
  • Nchi ikiongeza uwekezaji kwenye SHULE kwa kutumia fedha zisizotokana na kodi za wananchi (mfano mapato ya fedha za kigeni kutokana uuzwaji wa madini, mazao ya Kilimo na pia mapato ya Utalii), unaletea nchi faida ya kasi kubwa zaidi ya ukuaji uchumi ikifananishwa na ongezeko la uwekezaji wa fedha zisizotokana na kodi za wananchi (mfano mapato ya fedha za kigeni kutokana uuzwaji wa madini, mazao ya Kilimo na pia mapato ya Utalii) kwenye sekta ya BARABARA.
Kwa hali hii, tofauti ya kasi ambayo shule na barabara zinachangia kwa ukuaji wa uchumi wa nchi becomes of central importance to policymaker’s optimal allocation decision. Kwa upande mmoja - uboreshaji wa miundombinu ya kiuchumi (barabara) unaongeza ‘productivity’ ya sekta binafsi (SMEs) kwa haraka zaidi; Kwa upande meingine uwekezaji wa miundombinu ya kijamii (shule) unaongeza ‘productivity’ ya wafanyakazi/nguvu kazi, hasa kwa muda mrefu ujao (long run) huku zikitumika gharama kubwa, upfront costs. Vile vile uwekezaji wa miundombinu ya kijamii (shule) unahusisha matumizi makubwa sana ya ‘current expenditures’ (matumizi ya kawaida ya KIBAJETI), ikiwa ni pamoja na yale yanayohusu “operations & maintenance” – mishahara na posho za walimu; vitabu na vitendea kazi vya mahabara; umeme nk.
  • Ukosefu wa Ajira kwa Vijana.
  • Changamoto ya pili ipo katika kugeuza - ‘demographic bomb’ kuwa ‘demographic dividend’
  • Demographic dividend
Dhana hii ina maana ya – uwezekano (potentials) wa nchi kukua uchumi kwa kasi kubwa kwa kutumia faida zinazokuja na mabadiliko in ‘population’s age structure’, hasa pale ambapo nchi inakuwa na idadi kubwa ya ‘working age population’ (watu wenye umri kati ya miaka 15 na 60) ni kuliko idadi ya ‘non – working population’ (watoto chini ya umri wa miaka 15 na wazee umri zaidi ya miaka 60).
  • Demographic bomb -
Dhana hii maana yake ni kwamba – iwapo inatokea kwamba sehemu kubwa ya idadi ya watu katika taifa ni ile yenye nguvu za kufanya kazi (hasa umri wa miaka 15 hadi 35) lakini uchumi wa nchi unashindwa kukidhi mahitaji yao ya ajira (hivyo vipato), hali hii inaweza kuchangia kutokea kwa vurugu na uvunjaji wa amani katika taifa.

Tanzania imepiga hatua kubwa katika kupunguza ‘mortality rates’ na kuongeza ‘fertility rates’ suala ambalo limepelekea nchi kuwa na idai kubwa sana ya vijana. Lakini mafanikio haya yanakuja na changamoto kubwa:

Katika hali ya kawaida, taifa lenye uwezo wa kutengeneza ajira za maana kwa vijana (hasa umri kati ya miaka 15 – 35) linafaidika na GDP Per Capita ya juu. Hali hii hufanya nchi husika kuvuna faida za ‘Demographic Dividend’ (rejea mjadala hapo juu). Lakini iwapo inatokea kwamba Taifa linashindwa kuzalisha ajira za maana kwa vijana, aidha GDP Per Capita huporomoka au haikui kwa kiwango cha kuridhisha. Hali hii hupelekea taifa husika kukabiliwa na tishio la ‘Demographic Bomb’ (rejea mjadala hapo juu). Hoja hii iliwahi pia kujadiliwa siku za nyuma na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa pale aliposema kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana Tanzania ni - ‘TIME BOMB’.

Mantiki ya ‘Demographic bomb’ ni kwamba makundi makubwa ya vijana yanapokuwa frustrated kutokana na kukosa ajira zenye kuwapatia vipato vya kuweza kumudu mahitaji yao ya msingi, hali hii inakuwa ni - potential source of ‘social and political instability’ in the country.

Changamoto kubwa kwa utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan ni kugeuza ‘youth bulge’ kuwa ‘Demographic dividend’ kupitia ajira in productive activities.
  • Changamoto ya tatu ni magaidi, hasa kwenye mipaka ya nchi yetu.
  • Changamoto ya nne ni mahitaji ya Katiba Mpya.
  • Siasa za makundi ndani ya Chama cha mapinduzi.
  • Changamoto ya Mwisho ni kwamba sehemu kubwa ya wananchi wanaishi katika umaskini. Sambamba na hilo, taifa lina idadi kubwa ya makabila, na itikadi mbali mbali za kisiasa na kidini. Inahitajika mikakati na sera nzuri za kusaidia taifa to experience ‘Unity’ in ‘Diversity’.
 
Mkuu Mchambuzi natumaini utaendelea na mjadala wako kama ulivyoahidi

Kilichotokea katika Taifa kimedhihirisha madai ya siku nyingi kuhusu ubovu wa mfumo wetu wa utawala

Tumeshuhudia katiba (muongozo wa sheria) ukitumika kuweka viongozi halafu wanakuwa wakuu kuliko katiba

Tumeshuhudia udhaifu wa katiba yetu na jinsi udhaifu huo unavyoweza kutumiwa vibaya kuua Taasisi za nchi

Pili, tumeona udhaifu wa katiba katika nafasi kama ya makamu wa Rais.

Kwamba, makamu anapewa majukumu na Rais. Hili linafungua mwanya wa matumizi mabaya ya madaraka. Kwamba, Rais atataka agenda zake zitimizwe na Makamu na si katiba.

Rais Samia kalionyesha hili kwa kumpa jukumu la kero za Muungano.
Kero za muungano si jukumu la mtu bali la taasisi na hilo limeonyesha 'Nepotism'.

Katiba ya 1964 ilikuwa sahihi kwa kugawa majukumu kwa Makamu wa Rais.

Tatu, fursa aliyo nayo Rais ni kujenga umoja wa Taifa. Kazi hii imefanywa na Marais Wanne waliotanguliwa na kuharibiwa na Rais wa tano. Tumeshuhudia nepotism , ukanda na hata chuki dhidi ya maeneo ya Tanzania.

Rais Samia anaweza kutekeleza yote kama walivyofanya watangulizi lakini umoja wa Taifa ni muhimu

Fursa nyingine ni kurekebisha madhaifu ya katiba na hivyo katiba mpya ni suala muhimu sana kwakwe.

Hili litampa legacy ya karne. Katiba mpya ina maana moja, kujitathmini pale tulipo na kama tunahitaji mwelekeo mpya, kutengeneza taasisi imara na si watu imara.
Kutoa haki za msingi za Raia wa nchi na kuwapa fursa ndani na nje ya nchi yao.

Katika changamoto, kubwa inayomkabili ni suala la Muungano. Katika hili kuangalia kauli ni muhimu

Ni mara mbili ametamka kauli zinazowatia shaka 'Tanganyika' kama ni Rais aliyekuja si kuimarisha muungano bali kutekeleza kero za Wazanzibar. Kuungwa mkono na pande mbili ni muhimu kwake

Changamoto ya pili ni kuondoa 'mfumo wa nepotism' uliojengwa na mtangulizi wake ili kuweka mazingira ya kuaminiana miongoni mwa Watendaji.

Changamoto ya tatu ni kuvunja mfumo wa kihifadhina na kibabe ndani ya chama chake.
Kama kuna eneo litalomkwamisha kutekeleza sera zake ni mtifuano, kuchimbana na kutoaminiana miongoni mwa wanachama wa chama chake.

Tutaendelea kujadili
 
Mkuu Mchambuzi natumaini utaendelea na mjadala wako kama ulivyoahidi

Kilichotokea katika Taifa kimedhihirisha madai ya siku nyingi kuhusu ubovu wa mfumo wetu wa utawala

Tumeshuhudia katiba (muongozo wa sheria) ukitumika kuweka viongozi halafu wanakuwa wakuu kuliko katiba

Tumeshuhudia udhaifu wa katiba yetu na jinsi udhaifu huo unavyoweza kutumiwa vibaya kuua Taasisi za nchi

Pili, tumeona udhaifu wa katiba katika nafasi kama ya makamu wa Rais.

Kwamba, makamu anapewa majukumu na Rais. Hili linafungua mwanya wa matumizi mabaya ya madaraka. Kwamba, Rais atataka agenda zake zitimizwe na Makamu na si katiba.

Rais Samia kalionyesha hili kwa kumpa jukumu la kero za Muungano.
Kero za muungano si jukumu la mtu bali la taasisi na hilo limeonyesha 'Nepotism'.

Katiba ya 1964 ilikuwa sahihi kwa kugawa majukumu kwa Makamu wa Rais.

Tatu, fursa aliyo nayo Rais ni kujenga umoja wa Taifa. Kazi hii imefanywa na Marais Wanne waliotanguliwa na kuharibiwa na Rais wa tano. Tumeshuhudia nepotism , ukanda na hata chuki dhidi ya maeneo ya Tanzania.

Rais Samia anaweza kutekeleza yote kama walivyofanya watangulizi lakini umoja wa Taifa ni muhimu

Fursa nyingine ni kurekebisha madhaifu ya katiba na hivyo katiba mpya ni suala muhimu sana kwakwe.

Hili litampa legacy ya karne. Katiba mpya ina maana moja, kujitathmini pale tulipo na kama tunahitaji mwelekeo mpya, kutengeneza taasisi imara na si watu imara.
Kutoa haki za msingi za Raia wa nchi na kuwapa fursa ndani na nje ya nchi yao.

Katika changamoto, kubwa inayomkabili ni suala la Muungano. Katika hili kuangalia kauli ni muhimu

Ni mara mbili ametamka kauli zinazowatia shaka 'Tanganyika' kama ni Rais aliyekuja si kuimarisha muungano bali kutekeleza kero za Wazanzibar. Kuungwa mkono na pande mbili ni muhimu kwake

Changamoto ya pili ni kuondoa 'mfumo wa nepotism' uliojengwa na mtangulizi wake ili kuweka mazingira ya kuaminiana miongoni mwa Watendaji.

Changamoto ya tatu ni kuvunja mfumo wa kihifadhina na kibabe ndani ya chama chake.
Kama kuna eneo litalomkwamisha kutekeleza sera zake ni mtifuano, kuchimbana na kutoaminiana miongoni mwa wanachama wa chama chake.

Tutaendelea kujadili
Naomba nijadili kidogo suala la kinachoitwa "Kero za Muungano".

Iwapo tunakubaliana kwamba:

1. Muungano ulikuwa na washirika wawili: Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

2. Mkataba wa muungano (1964) ndio "legal basis: ya muungano.

3. Chanzo cha kero za muungano ni kukiukwa kwa makubaliano ya muungano (1964),

Basi nadhani pia tutakubaliana kwamba Wahanga wa kero za muungano ni washirika wote wawili, yani - Tanganyika na Zanzibar.

Kiini macho kilichopo sio tu kwamba Tanganyika imefunikwa isionekane kwa kuvalishwa Koti la muungano, bali pia koti hili ndio linamponza Tanganyika na kumbebesha lawama juu ya kero zote za muungano. Mbaya zaidi, Koti hili vile vile linamkosesha haki zake kama Mshirika wa muungano, haki ambazo Mshirika mwenzake - yani Zanzibar angalau anafaidika nazo hasa kwa kutambuliwa kama nchi kamili kwa Mujibu wa katiba yake ya mwaka 2010.

Kumekuwa na muendelezo wa both - imani, kauli na maamuzi kwamba:

1. Utatuzi wa kero za Zanzibar is synonymous to utatuzi wa kero za muungano.

2. Kutatua Kero za muungano maana yake ni kuimarisha Muungano wa Serikali mbili.

This is very illogical hasa ikizingatiwa kwamba:

Kwanza, tofauti na Tanganyika kama Mshirika mwenza wa muungano, Zanzibar inaendelea kutambulika kisheria na Kikatiba (rejea katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010).

Pili Tanganyika ilifutwa rasmi kupitia decree, hivyo haina katiba yake na utambulisho wake kama Mshirika mwenza wa muungano.

Tatu, Tanganyika ambayo imefichwa chini ya koti la muungano ilipaswa kugharamia masuala ya muungano tu lakini inaendelea kugharamia masuala ambayo hayahusiani na Muungano.

Katika mazingira haya, hoja kwamba Tanganyika kama
Mshirika anafaidika zaidi hazina mashiko.

Kero za muungano zitapungua na pengine kuisha iwapo tu wahusika kwanza watakubaliana kwamba chanzo cha kero za muungano ni ukiukwaji wa mkataba wa muungano (1964) ambao haukutendea haki washirika wote - Zanzibar na Tanganyika.

Hivi Karibuni (mwaka 2020) serikali ilitangaza kuondoa masuala Sita ya muungano ambayo iliamini kuwa na mchango mkubwa wa kero husika kwa imani kwamba kuondoa masuala haya kutaimarisha Muungano. Lakini ukitazama yaliyoorodheshwa kufutwa unaona kwa uwazi kabisa hayo ni kero za Zanzibar zaidi, hazistahili kuitwa kero za muungano kwa sababu kero za Mshirika mwenza zimefichwa chini ya zulia. Masuala yaliyotajwa kupatiwa ufumbuzi ni pamoja na:

- Makubaliano juu ya utafiti na matumizi kuhusu rasilimali za mafuta na gesi.

- Gharama za importation ya mizigo kutokea Zanzibar kwenda Bandari ya Dar es salaam (Tanganyika).

- Ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika mashariki.

- Ushiriki wa Zanzibar katika masuala ya kikanda na kimataifa.

Tangazo la Serikali juu ya utatuzi wa kero hizi ulienda sambamba na maelekezo kwa wanasheria wakuu wa Serikali ya JMT (kwa upande wa Tanganyika?) na Mwanasheria mkuu wa Serikali wa Zanzibar kuharakisha legal provisions kisheria ili kutatua kero zilizobakia. Nayo ukiyatazama yanahusu Mshirika mmoja tu wa muungano (Zanzibar):

* Importation ya Maziwa ya Zanzibar kuingia Tanganyika (ukipenda Tanzania bara).

* Uteuzi wa mzanzibari kwenye bodi ya Tanzania revenue tribunal.

* Uteuzi wa mzanzibari kwenye bodi ya Tanzania insurance deposits.

* Usimamizi wa huduma za simu na makusanyo ya kodi kupitia Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB).

*Mgawanyo wa mapato/fedha kwa pande zote mbili.

* Uundwaji/uboreshwaji wa kamati ya fedha za pamoja; na

* Usajili wa vyombo vya moto;

Kama Nguruvi3 ulivyogusia, yale yote yanayokubaliwa na pande zote kuwa ni kero yanapaswa kushughulikiwa "kitaasisi". Lakini muhimu pia ni kwamba ni imani potofu kwamba utatuzi wa kero za Mshirika mmoja wa muungano (Zanzibar) utaimarisha muungano wa Serikali mbili.
 
Naomba nijadili kidogo suala la kinachoitwa "Kero za Muungano".
Mkuu ninatambua ulileta mada yako kwa mtazamo mpana. Nimeongelea muungano kwasababu kuu mbili
1. Ni changamoto iliyowasumbua viongozi wote waliopita
2. Kauli za Mh Rais ambazo kimuonekano zimeegemea na kuchagizwa pengine na 'reservations''

Changamoto ya muungano ni ngumu kuliko ya demographic bom au economic injustice etc.
Hizo mbili zinawaunganisha watu kutafuta common ground, hoja ya muungano inawagawa watu

Tatizo la muungano ni la kihistoria kama ulivyoanisha lakini kuna makosa yalifanyika kulishughulikia.
Viongozi waliopita waliamini kutazama 'hoja za upande mmoja' kutatua tatizo.

Kwa wenye umri watakumbuka, Wazanzibar walikuwa na kauli yao '' kama hamtaki tunavunja muungano'' . Mtakumbuka Komandoo alipokwenda Dodoma na kusema atarudi Zanzibar na ASP.
Mtakumbuka kauli ya muungano ni kama koti likikubana unalivua.

Jeuri hiyo iliwalazimisha viongozi kukubaliana na hoja za Wazanzibar hata pale ilipokuwa si sahihi.

Miaka ya 90 kwa kutambua wanasikilizwa, Zanzibar wakaamua kujiunga na OIC bila kushirikisha JMT

Sababu kubwa ya kufanya hivyo, Rais wa JMT alikuwa Mzee Mwinyi na hivyo walikuwa na uwezo wa kufanya lolote. Makosa hayo ndiyo aliyoanza nayo Rais Samia na haionekani kama historia ilitoa funzo

Kilichofuata ni Tanganyika kuchoshwa na ndipo kundi la G55 chini ya Marehemu Njelu Kasaka , Jenerali na wengine wakajiunga kutaka uwepo wa serikali ya Tanganyika.

Hoja kubwa ilikuwa kuirudisha Tanganyika ifanye maamuzi kwa faida yake kwavile tu Zanzibar ilidekezwa kiasi cha kuonekana ni kubwa na muhimu sana

Hoja ya G55 ilitisha Urais wa Mzee Mwinyi na tunakumbuka aliyeizima ni Mwalimu Nyerere

Marais waliofuata walipita kule kule bila kuwa na suluhisho.
Wote walidhani kero ni kwa Wazanzibar na si Tanganyika

Hali hiyo imewazindua sana Watanganyika ambao sasa wanasema wazi kwamba Zanzibar inafaidika na muungano na kwamba ipo katika mbeleko.

Hoja inashadidiwa na rasimu ya katiba ya Warioba ambayo Watanganyika wanaipenda sana.

Sababu ni moja, inatoa fursa kwa Tanganyika kuwa na maamuzi yake na kupunguza utegemezi wa Zanzibar.

Kwanini kauli za Rais Samia zina matatizo ? Tutajadili





 
Ni ngumu kwa watawala kujadili kikamilifu masuala ya muungano wakati maeneo mengine yamewekwa kuwa ni off limits hata kuyataja mojawapo ni suala la Tanganyika.
 
Wakati akiapisha mawaziri na Manaibu Rais Samia aliwaagiza ''wizara ya mambo ya nje kuwa na sura ya muungano na si hiyo tu na wizara zote''. Hii ni moja ya malalamiko ya Wazanzibar hawateuliwi katika balozi
Swali, ni kiasi gani SMZ inachangia katika kuendesha balozi hizo? Mbona hilo halisemwi?

Pili, Rais anapoagiza Wizara zote si sahihi. Hivi Tamisemi wanahusiana vipi na Zanzibar?
Wizara ya afya, Elimu, Mifugo na Kilimo , mawasiliano n.k. zinahusiana vipi na kero za Zanzibar kiasi cha kuagiza ziwe na sura ya muungano ili hali si sehemu ya muungano?

Tatu, Rais akamuagiza Makamu ashughulikie kero. Hili ni kosa Marais waliopita walifanya hivyo na matokeo yake maamuzi yanakuwa kama memorandum of understanding or non legal binding.
Kwa kukosa nguvu za kisheria Rais ajaye anaweza kuyafuta bila tatizo.

Matatizo ya muungano na si kero yatatuliwa kwa taasisi kukaa chini na kujadili.
Hili kosa wamelifanya viongozi waliotangulia na Rais Samia anaonekana kupita huko huko.
Muungano ni maridhiano ya umma si watu au kikundi cha watu.

Kumekuwa na muendelezo wa both - imani, kauli na maamuzi kwamba:
1. Utatuzi wa kero za Zanzibar is synonymous to utatuzi wa kero za muungano.
2. Kutatua Kero za muungano maana yake ni kuimarisha Muungano wa Serikali mbili.

This is very illogical hasa ikizingatiwa kwamba:

Kwanza, tofauti na Tanganyika kama Mshirika mwenza wa muungano, Zanzibar inaendelea kutambulika kisheria na Kikatiba (rejea katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010).

Pili Tanganyika ilifutwa rasmi kupitia decree, hivyo haina katiba yake na utambulisho wake kama Mshirika mwenza wa muungano.

Tatu, Tanganyika ambayo imefichwa chini ya koti la muungano ilipaswa kugharamia masuala ya muungano tu lakini inaendelea kugharamia masuala ambayo hayahusiani na Muungano.

Katika mazingira haya, hoja kwamba Tanganyika kama Mshirika anafaidika zaidi hazina mashiko.
Na kwasasa Watanganyika wamelielewa hili vizuri sana ndiyo maana wanathubutu hata kusema kama hamtaki muungano ondokeni. Kauli hii ina maana kubwa sana kutokana na hoja hapo juu.
Kero za muungano zitapungua na pengine kuisha iwapo tu wahusika kwanza watakubaliana kwamba chanzo cha kero za muungano ni ukiukwaji wa mkataba wa muungano (1964) ambao haukutendea haki washirika wote - Zanzibar na Tanganyika.
Na kukubali ukweli kuwa muungano uangaliwe kwa pande zote mbili na si kero za upande mmoja
Hivi Karibuni (mwaka 2020) serikali ilitangaza kuondoa masuala Sita ya muungano ambayo iliamini kuwa na mchango mkubwa wa kero husika kwa imani kwamba kuondoa masuala haya kutaimarisha Muungano. Lakini ukitazama yaliyoorodheshwa kufutwa unaona kwa uwazi kabisa hayo ni kero za Zanzibar zaidi, hazistahili kuitwa kero za muungano kwa sababu kero za Mshirika mwenza zimefichwa chini ya zulia. Masuala yaliyotajwa kupatiwa ufumbuzi ni pamoja na:

- Makubaliano juu ya utafiti na matumizi kuhusu rasilimali za mafuta na gesi.
Kuna tatizo hapa. Zanzibar wameondoa mafuta na gesi katika muungano. Gesi inayopatikana Tanganyika inalipa 4% Zanzibar. Pato la madini ya Tanganyika linatoa 4% anayoagiza Rais iende Zanzibar
- Gharama za importation ya mizigo kutokea Zanzibar kwenda Bandari ya Dar es salaam (Tanganyika).
Bandari waliondoa si suala la muungano. Vipi basi uendeshaji wa Bandari za Tanganyika uwe wa muungano.

Importation ya mizigo kutoka Zanzibar ina maana moja , kutengeneza uchochoro wa kukwepa kodi.
Madhara ya bidhaa kupitia Zanzibar ni kutolipiwa kodi na zile chache zinabaki Zanzibar.
Hili linamtwisha Mtanganyika mzigo kwa kukosa mapato.
- Ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika mashariki.
Ikiwa tunaamini kuwa importation inahusu nchi moja kwanini Rais wa JMT asiwakilishe nchi hiyo?
I mean kwanini tunaamini ni nchi moja katika nyakati fulani na nyingine hatuamini hilo?
- Ushiriki wa Zanzibar katika masuala ya kikanda na kimataifa.

Tangazo la Serikali juu ya utatuzi wa kero hizi ulienda sambamba na maelekezo kwa wanasheria wakuu wa Serikali ya JMT (kwa upande wa Tanganyika?) na Mwanasheria mkuu wa Serikali wa Zanzibar kuharakisha legal provisions kisheria ili kutatua kero zilizobakia. Nayo ukiyatazama yanahusu Mshirika mmoja tu wa muungano (Zanzibar):

* Importation ya Maziwa ya Zanzibar kuingia Tanganyika (ukipenda Tanzania bara).

* Uteuzi wa mzanzibari kwenye bodi ya Tanzania revenue tribunal.

* Uteuzi wa mzanzibari kwenye bodi ya Tanzania insurance deposits.

* Usimamizi wa huduma za simu na makusanyo ya kodi kupitia Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB).

*Mgawanyo wa mapato/fedha kwa pande zote mbili.

* Uundwaji/uboreshwaji wa kamati ya fedha za pamoja; na

* Usajili wa vyombo vya moto;
Tukiyatazama hayo yote yamelenga jambo moja kutengeneza ajira kwa Wazanzibar na kutengeneza kipato kupitia mapato ya JMT.

Ikiwa tunaongelea rasilimali, ni lazima tuangalie assets and liabilities.
Swali, nini mchango wa Zanzibar katika muungano?
Ni nini mchango wa Zanzibar katika madeni yanayotokana na muungano?

Na swali muhimu zaidi, ikiwa Rais Samia atawaongelea Wazanzibar nani atawaongelea Watanganyika?

Katika hili naliona tatizo kubwa sana. Siku Utanganyika utakapowaunganisha Watanganyika historia inaweza kujirudia na kwasasa hatuna Nyerere , hili ni tatizo na sijui kama ameliona Mh Rais

Fursa aliyo nayo Rais Samia si kuchagua ''cherry pick' aliyoanza nayo. Rais ni wa JMT ambayo Tanganyika ni sehemu kubwa na muhimu iliyobeba muungano.
 
Ni ngumu kwa watawala kujadili kikamilifu masuala ya muungano wakati maeneo mengine yamewekwa kuwa ni off limits hata kuyataja mojawapo ni suala la Tanganyika.
Mkuu kuna tatizo kwa viongozi kuliona suala la Zanzibar kama 'taboo' . Kumekuwa na suluhu za kuziba vidonda na si kuponya ''bandage' . Suala la muungano ni la kitaasisi zaidi ya maamuzi ya chama au kiongozi aliyeko madarakani.

Kumeundwa kamati zaidi ya 12 za kero na maagizo yasiyo na idadi lakini bado hakuna suluhisho

Kwa hali ilivyo sasa, rasimu ya Mzee Warioba ingesaidia sana kutatatua matatizo. Ingawa watu hawakubali ukweli, lakini ni dhahiri kilichomo ndani ya rasimu ya Wariona ndicho kinachoendelea kwa njiazisizo rasmi.

Mathalani, ukiacha wizara ya mambo ya ndani, ulinzi, mambo ya nje, usajili wa vyama mengine katika wizara na taasisi yapo sehemu mbili ambazo ni Zanzibar na Zanzibar ndani ya Tanganyika a.k.a JMT

Ukiondoa Wizara tajwa hapo juu zingine zote zipo pande mbili, yaani JMT na SMZ.
Taasisi nazo ni vivyo hivyo, zipo za JMT na Zanzibar

Hizi za JMT ndizo za Tanganyika ambazo Mchambuzi anasema ni koti la JMT ambalo Tanganyika inabeba mzigo

Kwa maneno mengine, Wizara na Taasisi ambazo zipo Zanzibar, za upande wa JMT ni za Tanganyika.

Kama ni hivyo basi, kwanini Wazanzibar washiriki katika taasisi zisizowahusu?
Kwanini waajiriwe katika wizara na taasisi zisizo za muungano?

Rais Samia anaposema Taasisi na Wizara ziwe na sura ya muungano kuna tatizo hapa.
Hivi Mzanzibar anahitajikaje kuwa mtumishi wa TAMISEMI? au TBS , TMDA(TFDA), Bandari, Baraza a Mitihani n.k.

Zanzibar wanaondoaje gesi na Mafuta kutoka JMT wakati huo huo wanadai 4% ya gesi na madini kutoka JMT!

Utaona wazi kwamba kinachoitwa kero za Zanzibar ni fursa za Wazanzibar katika Tanganyika!
Watanganyika a.k.a JMT hawana fursa SMZ wala Zanzibar.

Hili ndilo lilichagiza uwepo wa G55 wakidai Tanganyika
Kama kuna wakati wa G55 kurudi ni sasa hivi kwasababu Tanganyika haina mtetezi katika JMT

Turejee katika rasimu ya Warioba tutekeleze yale 7 tu mengine kila nchi itafute njia zake
 
Hatari kubwa kwa muungano haipo katika kuruhusu Tanganyika kuchukua nafasi yake ya Kikatiba katika muungano bali hatari ipo katika kuendelea kulazimisha kuinyima nafasi hiyo.

Mwalimu Nyerere alinukuliwa nje ya nchi Miaka ya 1960s akisema kwamba:

"Itokeapo nchi yoyote shiriki itaamua kujitoa basi muungano huo hautakuwepo".

Kinyume na mkataba wa muungano (1964), Miaka mitatu baadae (1967) ilipitishwa sheria namba 24 iliyompa mamlaka Rais wa JMT kubadilisha neno la Mshirika Mshirika wa muungano kutoka Tanganyika na kuwa Tanzania bara. Suala la kubadilisha jina la Mshirika wa muungano haijawahi kuwa ni suala la muungano. Haki hiyo ilipaswa kubakia Mikononi mwa nchi washirika na mabunge yao. Hivyo basi ni Tanganyika ndio ilikuwa na mamlaka ya kuamua jina gani wanataka Tanganyika yao itumie.

Ikumbukwe kwamba hata Zanzibar iliwahi badilishwa Jina kiholela kama Tanganyika kwa kuitwa "Tanzania Visiwani" kabla ya Mshirika huyu wa muungano kupigania na kusimamia haki yake na kufanikiwa kurudisha jina lake per articles of the union (1964).

Miaka 57 baada ya muungano, Mshirika mwenza na halali wa muungano (Tanganyika) anaendelea kunyimwa haki yake ya kujidai kwa nafasi yake halali kama Mshirika wa muungano kwenye masuala yasiyohusika na yale ya muungano, akinyimwa hata haki ya kuwepo. Hapo juu umegusia sakata la G55 na madai ya Tanganyika. Suala hilo halikupatiwa ufumbuzi badala yake lilisokomezwa chini ya zulia. Tukirejea maneno ya Mwalimu miaka ya 1960s alipokuwa ziarani nje ya nchi kwamba:

"Itokeapo nchi yoyote shiriki itaamua kujitoa basi muungano huo hautakuwepo",

itafika mahali Tanganyika itaamua kujiondoa.

Suala la Mzigo wa Kifedha
Ikumbukwe kwamba siku ya muungano (1964), Tanganyika tayari ilikuwa na taasisi kamili, wafanyakazi na fedha zake kuiwezesha kuendesha na kusimamia mambo yake yote nje ya yale yaliyokubaliwa kwamba yawe ya muungano. Isitoshe haya yote bado yapo hadi Leo, kinachokosekana ni haki ya Tanganyika kusimamiwa kama Mshirika mwenza wa Muungano na kulivua Koti la muungano alilovishwa Tanganyika.

Koti hili inabidi livuliwe ili haya yote yarejeshwe kwa Tanganyika ili muungano uachwe usimamie mambo yake kwa Mujibu wa mkataba wa muungano, masuala ambayo yaliboreshwa na Rasimu Ya Katiba ya Jaji Warioba. Hii pia itasaidia maamuzi juu ya kupunguza ukubwa wa Bunge la JMT huku Tanganyika ikibakia na "bunge lake kamili" huku kila Mshirika akishughulika na mambo yake kikamilifu huku washirika wakiunganishwa na mambo machache ya muungano.

Wakati akiapisha mawaziri na Manaibu Rais Samia aliwaagiza ''wizara ya mambo ya nje kuwa na sura ya muungano na si hiyo tu na wizara zote''. Hii ni moja ya malalamiko ya Wazanzibar hawateuliwi katika balozi
Swali, ni kiasi gani SMZ inachangia katika kuendesha balozi hizo? Mbona hilo halisemwi?

Pili, Rais anapoagiza Wizara zote si sahihi. Hivi Tamisemi wanahusiana vipi na Zanzibar?
Wizara ya afya, Elimu, Mifugo na Kilimo , mawasiliano n.k. zinahusiana vipi na kero za Zanzibar kiasi cha kuagiza ziwe na sura ya muungano ili hali si sehemu ya muungano?

Tatu, Rais akamuagiza Makamu ashughulikie kero. Hili ni kosa Marais waliopita walifanya hivyo na matokeo yake maamuzi yanakuwa kama memorandum of understanding or non legal binding.
Kwa kukosa nguvu za kisheria Rais ajaye anaweza kuyafuta bila tatizo.

Matatizo ya muungano na si kero yatatuliwa kwa taasisi kukaa chini na kujadili.
Hili kosa wamelifanya viongozi waliotangulia na Rais Samia anaonekana kupita huko huko.
Muungano ni maridhiano ya umma si watu au kikundi cha watu.


Na kwasasa Watanganyika wamelielewa hili vizuri sana ndiyo maana wanathubutu hata kusema kama hamtaki muungano ondokeni. Kauli hii ina maana kubwa sana kutokana na hoja hapo juu.

Na kukubali ukweli kuwa muungano uangaliwe kwa pande zote mbili na si kero za upande mmoja

Kuna tatizo hapa. Zanzibar wameondoa mafuta na gesi katika muungano. Gesi inayopatikana Tanganyika inalipa 4% Zanzibar. Pato la madini ya Tanganyika linatoa 4% anayoagiza Rais iende Zanzibar

Bandari waliondoa si suala la muungano. Vipi basi uendeshaji wa Bandari za Tanganyika uwe wa muungano.

Importation ya mizigo kutoka Zanzibar ina maana moja , kutengeneza uchochoro wa kukwepa kodi.
Madhara ya bidhaa kupitia Zanzibar ni kutolipiwa kodi na zile chache zinabaki Zanzibar.
Hili linamtwisha Mtanganyika mzigo kwa kukosa mapato.

Ikiwa tunaamini kuwa importation inahusu nchi moja kwanini Rais wa JMT asiwakilishe nchi hiyo?
I mean kwanini tunaamini ni nchi moja katika nyakati fulani na nyingine hatuamini hilo?

Tukiyatazama hayo yote yamelenga jambo moja kutengeneza ajira kwa Wazanzibar na kutengeneza kipato kupitia mapato ya JMT.

Ikiwa tunaongelea rasilimali, ni lazima tuangalie assets and liabilities.
Swali, nini mchango wa Zanzibar katika muungano?
Ni nini mchango wa Zanzibar katika madeni yanayotokana na muungano?

Na swali muhimu zaidi, ikiwa Rais Samia atawaongelea Wazanzibar nani atawaongelea Watanganyika?

Katika hili naliona tatizo kubwa sana. Siku Utanganyika utakapowaunganisha Watanganyika historia inaweza kujirudia na kwasasa hatuna Nyerere , hili ni tatizo na sijui kama ameliona Mh Rais

Fursa aliyo nayo Rais Samia si kuchagua ''cherry pick' aliyoanza nayo. Rais ni wa JMT ambayo Tanganyika ni sehemu kubwa na muhimu iliyobeba muungano.
 
Hatari kubwa kwa muungano haipo katika kuruhusu Tanganyika kuchukua nafasi yake ya Kikatiba katika muungano bali hatari ipo katika kuendelea kulazimisha kuinyima nafasi hiyo.
Kuntu! neno zito sana na linabeba maana yangu ya kujadili changamoto inayomkabili Rais Samia

Kwamba anapotoa kauli zinazoashiria kusimamia masilahi ya Zanzibar zaidi ya kuwa msuluhishi( Rais wa JMT) anapeleka ujumbe huo unaosema '' kulazimisha kuinyima Tanganyika nafasi hiyo''
 
Kwa kila namna inaonekana kwamba Iwapo kutatokea mabadiliko yoyote ya katiba kwa ajili ya kukidhi matakwa ya sasa, sehemu kubwa ya mabadiliko hayo itahusisha mapendekezo ya chama tawala juu ni mfumo utakaofaa. Turejee kidogo yaliyojiri kipindi kile cha mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Kufuatia mchakato wa katiba mpya, aliyekuwa Rais wa JMT wakati ule alitamka kwamba:

"Serikali tatu ni mfumo legevu utakaongezea wananchi mzigo".

Hoja kubwa ya CCM wakati ule ikawa kwamba badala ya mfumo wa Serikali tatu, mfumo wa Serikali mbili “utaboreshwa”, huku chama cha mapinduzi kikipendekeza kwamba – katika katiba ijayo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano anyang’anywe mamlaka aliyokuwa nayo ya kuwa msaidizi mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, na badala yake, mamlaka hayo yahamie kwa Rais wa “Zanzibar”. Kwa maana nyingine, chini ya serikali mbili “zilizoboreshwa”, Rais wa “Zanzibar” atakuwa ndiye msaidizi mkuu wa Rais wa Muungano kwa masuala ya Zanzibar, lakini pia atakuwa ni mmoja wa viongozi wakuu wa nchi yani - Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CCM haikusema lolote kuhusu kiongozi atakayekuwa msaidizi wa Rais wa Muungano katika masuala ya Tanganyika (ukipenda, sema - Tanzania Bara).

Mkataba wa Muungano (1964) uliweka utaratibu ambao – Rais wa Muungano wa NCHI Moja, alikuwa na wasaidi wake wakuu wawili – Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Zanzibar (Marehemu Karume), na Makamu wa Pili wa Rais ambaye alikuwa anawajibika na masuala yote yasiyo ya muungano kwa upande wa Tanganyika (Marehemu Rashid Mfaume Kawawa).

Chini ya Katiba Mpya, CCM ikapendekeza kwamba – Rais wa Zanzibar afanywe kuwa Makamu wa Rais wa Muungano bila ya kujalisha Rais wa Muungano anatokea upande upi wa Muungano. Kwa kufanya hivyo, CCM ikadai kwamba – hali hii itamwongezea Rais wa Zanzibar - “madaraka na hadhi” ndani ya serikali ya Muungano na pia nje ya nchi.

Chini ya mfumo huu wa serikali mbili ambazo CCM ililenga “kuziboresha”, CCM haikusema iwapo Rais ni mmoja - yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano, ni kiongozi gani ndiye atakayesimamia Mawaziri watakaokuwa wanasimamia mambo ya Tanganyika (au Tanzania Bara) katika mfumo huu wa serikali mbili “ulioboreshwa”. Pamoja na kuendelea kupigia debe serikali mbili “zitakazoboreshwa”, CCM bado ikaendelea kukaa kimya juu ya ufafanuzi wa masuala muhimu (kiutekelezaji), kwa mfano, - katika mazingira ya Zanzibar kuwa ni “nchi” kamili, yenye “mamlaka” kamili - kwa Mujibu wa katiba ya Zanzibar(2010), ikitokea kwamba Rais wa Muungano anatokea upande wa pili wa muungano (Zanzibar), JE:

· Rais huyu kutoka “Zanzibar” atasimamia masuala yasiyo ya muungano - ya upande unaoitwa Tanganyika (“Tanzania Bara”), ndani ya Jamhuri ya Muungano, kwa mamlaka yepi?

Leo ndio tupo katika hali hiyo. Rais mpya wa JMT anatokea upande wa Zanzibar. Inaonekana kwamba kwa wakati ule hapakuonekana umuhimu wa kujibu maswali haya muhimu. Kutokana na hali hii, serikali mbili ambazo CCM ilijenga hoja kwamba “zitaboreshwa”, kiuhalisia hazitaboresha muungano bali zitajenga mazingira ya kuvunja muungano. Hii ni kwa sababu:

Iwapo Rais wa Muungano anatokea upande wa “Zanzibar” (hali iliyopo sasa), ambaye chini ya mfumo wa serikali mbili ambao CCM ilidai utakuwa “umeboreshwa”, Rais wa Zanzibar pia atakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano. CCM ikapendekeza kuwa iwe hivyo bila ya kujali Rais wa Muungano atatokea upande upi wa Muungano. Chini ya mapendekezo haya, kilichotarajiwa (kwa kusudia au kutokusudia) ni kwamba - siku moja, Rais wa Muungano na Makamu Wa Rais Wa Muungano, wote watakuwa wametokea upande wa “Zanzibar”. Kwa maana hii, kupitia Katiba iliyopendekezwa na CCM wakati ule, ilichokifanya CCM, aidha kwa makusudi au bahati mbaya, CCM iliweka mazingira ambayo Zanzibar wasingeweza tena kutoa Rais wa Muungano nje ya utaratibu wa hali ya dharura.

Hii ni kwa sababu:

Kama tulivyoona, chini ya serikali mbili ziliziboreshwa na CCM, Rais wa Zanzibar “automatically”, angekuwa pia ni Makamu wa Rais wa Muungano. Katika mazingira haya, CCM ikimsimamisha mgombea Urais wa Muungano kutokea “Zanzibar”, mshirika wa muungano ambayo pia automatically atatoa makamu wa Rais wa Muungano, chini ya mazingira ya sasa ya mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, wapiga kura kutoka upande wa inayoitwa “Tanzania Bara”, upande ambao una wapiga kura zaidi ya 90% ya wapiga kura wote wa Jamhuri ya Muungano, wengi ya wapiga kura hawa kutoka “Tanzania Bara”, hawatakubali kumchagua mgombea wa urais (CCM) kutokea Zanzibar huku wakijua kwamba makamu wake pia anatokea huko huko Zanzibar.

Iwapo Rais wa sasa ambae anatokea Zanzibar atakuwa na nia ya kutumia haki yake kikatiba kuongoza kwa mihula miwili, haya ni miongoni mwa masuala muhimu ambayo yeye na wasaidizi wake wanapaswa kutatazama kwa ukaribu sana.
Kuntu! neno zito sana na linabeba maana yangu ya kujadili changamoto inayomkabili Rais Samia

Kwamba anapotoa kauli zinazoashiria kusimamia masilahi ya Zanzibar zaidi ya kuwa msuluhishi( Rais wa JMT) anapeleka ujumbe huo unaosema '' kulazimisha kuinyima Tanganyika nafasi hiyo''
 
Hivi Karibuni (mwaka 2020) serikali ilitangaza kuondoa masuala Sita ya muungano ambayo iliamini kuwa na mchango mkubwa wa kero husika kwa imani kwamba kuondoa masuala haya kutaimarisha Muungano. Lakini ukitazama yaliyoorodheshwa kufutwa unaona kwa uwazi kabisa hayo ni kero za Zanzibar zaidi, hazistahili kuitwa kero za muungano kwa sababu kero za Mshirika mwenza zimefichwa chini ya zulia. Masuala yaliyotajwa kupatiwa ufumbuzi ni pamoja na:

- Makubaliano juu ya utafiti na matumizi kuhusu rasilimali za mafuta na gesi.

- Gharama za importation ya mizigo kutokea Zanzibar kwenda Bandari ya Dar es salaam (Tanganyika).

- Ushiriki wa Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika mashariki.

- Ushiriki wa Zanzibar katika masuala ya kikanda na kimataifa.

Wapi dokumenti inapatikana kwa umma inayoelezea haya?
 
Back
Top Bottom