Miezi ya nyuma nilileta hii mada hapa jukwaani lakini kwa bahati mbaya MODs waliinyofoa dakika 20 baada ya kuiweka. Sina budi kurudisha hii mada baada ya sakata la Zitto Kabwe, Nassari, Alima Mdee pamoja na gazeti la Mwananchi. Kwa muda wa miaka kadhaa sasa, nimekuwa katika tasnia ya habari na lazima nikiri kwamba mengine yanayofanyika katika hii tasnia ni ya kukatiza moyo hasa kazi za wanahabari zinapoingiliwa na wanasiasa. Kwetu sisi wanawake inakuwa ni vigumu sana kukataa kutii haya maagizo ambayo mengine unaona kabisa ni za vitisho
Zitto Kabwe, January Makamba, Bernard Membe na hata Ngeleja kwa siku za nyuma alishiriki sana katika kuingilia kazi za waandishi. Kinara wao akiwa Zitto January na Membe. Hawa viongozi hasa Zitto wamezoea sana kujiandikia makala na hata habari kisha kumlazimisha mwandishi kuzichapisha ukurasa wa mbele kwa gharama yoyote ile. Wanatoa hela nyingi sana kwa waandishi na wahariri. Mbaya zaidi ni kwamba hawa viongozi wanajitengenezea kashfa au kutoka ndani ya vyama vyao.
Matokeo yake kesho wanaitisha waandishi tena kukanusha (kashfa) zao za kujipikia wakati ni wao ndio chanzo cha hizo habari. Lengo lao kubwa ni kutafuta huruma kutoka kwa umma wa kitanzania kwa vitu ambavyo havipo.
Kinachonishangaza ni kwa nini mtu ajichafue kwa kujitengenezea kashfa maadui feki ndani ya chama chake heti ndio wanaomchafua kumbe ni yeye mwenyewe alafu kesho yake akane hizo taarifa? Nadhani tunaelekea kubaya hawa watu wakiendelea nah ii tabia. Moja ya habari hizi ni zile zinazomlaumu Mbowe kam mtazikumbuka..
nawakilisha
Katika utawala na siasa za nchi, kila mwanasiasa anatakiwa kuwa na ushirikiano mzuri sana na waandishi wa habari. Na maadam nchji yetu ni ya mkono uendao kinywani nawapongeza sana Zitto, Makamba, Na Membe kwa kuelea kwamba mwanasiasa unatakiwa ku control media. Mtachukia na kuwasema kwa mabaya lakini ndivyo Rostam alivyoweza kutukamata.. Huwezi kutumia UTU na Uzalendo wakati wote hata kama unashambuliwa na huna pa kushtaki..
Labda tatizo ya swala hili zima ni kama Makamba, Zitto na Membe wanaifanya kazi hii wao wenyewe bila kutumia mtandao lakini kisiasa hakuna uharamu kabisa unless kwa kutumia media unajaribu kuzuia habari za makosa ya ubadhilifu iwe ufisadi, wizi, na kadhalika. Siasa ni mchezo mchafu sana na ukiingia ni sawa na kuingia nyumba ya anasa - Casino. Kipimo cha uzalendo ni wewe mwandishi if you can be bought..Na ikijulikana mhariri au mwandishi unaweza kununuliwa basi unatakiwa kufukuzwa kazi wewe sio swala wala makosa ya mwanasiasa kujipamba gazetini..
Mwisho, binafsi yangu nilidhani kweli Zitto amepania kugombea mwaka 2015, maana kutangaza nia ya kugombea sidhani kama ni makosa isipokuwa makosa ni kufanya kampeni na maandalizi kabla ya wakati wake (binafsi yangu hili nalo sii kosa)... Nina hakika kabisa mtu yeyote anayetaka kugombea urais mwaka 2015 by now na kisha weka nia yake. Kama kweli hakuna mtu aloweka dhamira na nia kugombea mwaka 2015 basi hizi ndizo sababu hatupati viongozi bora maana watu wanakurupushwa tu na kupewa usukani.
Vyama havina maandalizi yoyote kama rais ila wana maandalizi ya kugombea urais kazi ya miezi mitatu inakuwa muhimu zaidi ya kazi ya miaka mitano. For that, Katiba lazima ibadilishwe ili tuwaandae marais wetu kwa miaka na watuonyeshe uwezo wao ktk mamlaka walokabidhiwa kabla ya kugombea..
Hivyo maadam Zitto naye anakanusha yaliyoandikwa ktk gazeti la mwananchi, basi sioni sababu hata ya kuweka hizo video..Habari hii ni ya Uongo nani anapenda kuuujua Uongo? Kama ingelikuwa kweli na Zitto kweli amepania kugombea urais hapo mjadala ungependeza zaidi na hizo video zingeleta starehe. Maadam ndivyo sivyo, am not interested tuwaachie wenyewe watu wa GP.