Nilikuwepo uwanjani pale lake Tanganyika Kigoma, kilichoandikwa ndicho nilichosikia pia. Videos zitawekwa hapa na zitathibitisha.
Siwezi kuwaandikia mwananchi kwani mimi silalamiki kuhusu habari hiyo. Wenye kuilalamikia habari wameandika.
Mimi ninaamini gazeti la Mwananchi ndio gazeti pekee huru la kiswahili hapa nchini. Ndio gazeti pekee ambalo umiliki wake hauna maslahi na waandishi na wahariri wake ni mahiri, hawana njaa na hawapindishwi. Ndio maana huandika ukweli muda wote na wanapokosea hawasiti kurekebisha. Ndio maana ni gazeti linasomwa kwa wingi kuliko magazeti yote nchini. Hakuna gazeti linalofikia hata nusu ya mwananchi kwa kusomwa. Hivyo Mwananchi linaaminika na umma.
Najua kuna watu wana chuki binafsi na mwananchi kama gazeti na wahariri wa mwananchi kama binaadamu. Hayo wayamalize wenyewe huko walikochukiana.
Subirini video ndio tutajua habari ile imepikwa au ni ya kweli. Kwa tuliokuwepo uwanjani tunajua nani alisema nini.
Mkuu kwa heshima zote, si uiweke hiyo video ili kuondoa utata.
Halafu mkuu, umesema hujamualika mwandishi yeyote wa habari katika tamasha lile. Nani basi kafanya hiyo recording, ni wewe mwenyewe? Kama si wewe utaipataje? Umejuaje nani karekodi matukio ya tamasha?
Kisha umesema tamasha halijaandaliwa na wewe, sasa uliwezaje kuwaalika waheshimiwa wabunge wenzako katika tamasha ambalo hukuliandaa wewe?
Naomba pia ufafanuzi, umejuaje kwamba waandishi wa gazeti la Mwananchi hawana njaa na hawapindishwi!!??