URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

Kuna watu hawaelekei kuwa maraisi kabisaa huyu pinda mmoja wapo km sura yake ilivokuwa mbaya na nchi yetu itachukua sura mbaya duniani na hapati hata kwa ligi
 
Hivi wewe umetumwa.Jamani,Pinda, kaa!Ni Pinda mwingine au huyu huyu anayelia na kulalama badala ya kutatua matatizo ya Watanzania.
HABARI ZENU WANAJAMVI:-
KWELI WANYONGE WALISEMA MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPATIENI. KWA SIFA HIZI, MH. KAYANZA MIZENGO PETER PINDA HANA MPINZANI KWA URAIS 2015.
ANAHITAJIWA NA WATANZANIA NA NI MTU MAKINI ANAYEJUA HOMA ZA WATANZANIA. 2015 ATAKAPOWEZESHWA KUINGIA IKULU KWA KUMPIGIA KURA ZETU ZA NDIYO NA KUSHINDA KWA 97% WATANZANIA TUTAONDOKANA NA UMASIKINI.

NANI KAMA PINDA MTOTO WA MKULIMA? HAKUNA

NHC.JPG
pinda.jpg
 
Akiingia ikulu tutapigwa kweli kweli
 
Wazee walishasema ukisha kuwa Waziri Mkuu uwezi kuja kuwa Rais......mtu pekee aliyepata kuwa Waziri Mkuu na akawa Rais ni Mwalimu Julius Nyerere pekee yake......Father Of The Nation.

Usiniulize kwanini tafuta wazee wa jadi waulizie Nchi nayo ina jadi na wazee ndio wanao jua jadi hizo!!!!!!

Ukisema ni upuuzi kwa kuwa unae mpenda alishapata kuwa waziri mkuu ama ni waziri mkuu basi kwa maana hiyo unaumia unaposikia kauri za aina hii, basi waambie wanasiasa wasiwe wanakimbilia kuvalishwa migolole na kama wanapenda kuvaa na kushikilia mikuki na ngao ambazo ndizo siraha za jadi za ulinzi wa Taifa wajue hilo kuwa na Taifa kama Taifa lina Jadi kama walivyokuwa Mababu waliotangulia [Ancestors]!!!!

Alishindana na nani?
 
Kweli wewe ni #team_lowasa . any ways,tuyaache hayo.

Now; kwenye Richmond,Lowasa alitupia vimemo kadhaa kwenye issue hiyo. na viliwekwa mezani na report ya mwakyembe. Kwa Pinda,hakuna popote alipoonekana amechochea pesa kuchukuliwa.

Pili,njoo kwenye #UFANYA_BIASHARA (Kujilimbikizia mali na kujihusisha na biashara/wafanya biawhara). Lowasa ni MROHO na yuko tayari kuwauzia nchi Wafanyabiashara pale anapoona anaweza kutengeneza/kupiga dili. Rejea issue ya NILE & EGYPT miaka ile mpaka Nyerere akamuachia laana yakutoaminiwa na watanzania kwenye nafasi za umma! I believe Pinda hana KALIBA hiyo na amewakwepa wafnyabiashara mno. Ushahidi mmoja nnao mimi mwenyewe.

Nimeshuhudia Mfanyabiashara mmoja mwenye Asili ya Kigoma na mwingine Msomari wakinyimwa "UPATU WA PINDA" kwenye bizness zao "despite" walimchangia pesa nyingi sana kwenye Harusi ya mwanae. Huyu msomari alimchangia zaidi ya Mil.30 kwenye kampeni mwaka 2010 (ingawa alipita bila kupingwa huko jimboni kwao). Jamaa hao wamehaha hadi huruma.

Just to mention the few. Nina mengi sana. Labda Pinda apambanishwe na wengine. sio Lowasa.

NAWASILISHA.

,

Huyu mkuu ndo kasema kweli kabisa, ivi hakuna mtanzania mwingine wa kupewa nchi hii kuongoza hadi tufikirie kumpatia mtu aliyefukuzwa kazi ya PM na bunge la jamhuri ya muungano tanzania tena kwa tuhuma za ufisadi high level.
ivi hata dunia watatucheka na kutuona wapuuzi na wajinga,yule jamaa hasafishiki tena kaoza mno.
Sija m trust sana pinda na ofcourse hana mvuto lakini naona kama hatuoni mwingine basi bora tumpe huyo huyo jamaa wa kulialia.japo naona kuna candidates wengine ccm wapo fit sana kama hili jamaa la barabara.
 
Mkuu;uko vyema & mzalendo kabisa. Wengine tunaamua kumpigia upatu #Pinda humu ndani just kujibu na kupinga hoja za hawa vijana wa Luwasa!!

Mtu ni mchafu hadi inaboa ujue! As for me,nilipumua kidogo(kwa upande wa CCM) baada ya Mizengo kutangaza nia (kimyakimya). Maana wengne walotangulia akiwemo Lowasa, ni #ngedere tu kwenye mashamba ya mahindi. Uozo. Anagalau PINDA unaweza ukamnadi kwa ushahidi kabisa kuwa ni Muadilifu & Mzalendo hakika.

Umeongelea suala la hili libwana la Barabara, sipendi kukupinga. Liko vyema mno. Ila,naamini efficiency yake inaweza kuonekana endapo atakuwa under someone! Magufuli ni mzuri sana. ila,yuko more "" #EMOTIONAL "".

Needs someone above to govern & control his deeds.

Vinginevyo,naomba kukupongeza tu kwa uwazi na utashi wako usiopenda kutangamana na makundi ya ajabuajabu (kama ya akina Lowasa-WEZI).
 
View attachment 210112 Vs View attachment 210113

Lowassa na Pinda ni miongoni mwa wanaCCM waliotangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015. Kila mmoja wa ‘watangaza nia’ hawa ana kundi lake la wanaCCM wanaompigia chapuo na kumpamba kwa kila namna ili chama kimpendekeze kupeperusha bendera ya CCM na, kama akifanikiwa kupenya kwenye mchuano mkali wa UKAWA, awe Rais wa Tanzania 2015-2020.

Kwa mtazamo wangu, kumliganisha Lowasa na Pinda ni sawa na kuulinganisha mlima Kilimanajaro na kichuguu. Pinda anaweza kabisa kulinganishwa na Membe au ‘mtangaza nia’ mwingine lakini sio Lowassa. Lowassa yuko levo nyingine kabisa. Ulinganisho wowote utakaotumia kuwalinganisha wawili hawa, unaonyesha kwamba Pinda hafui dafu mbele ya Lowassa:

KASHFA YA UFISADI
Wote wawili wana kashfa za kifisadi. Wakati Lowassa anakabiliwa na kashafa ya Richmond, Pinda anakabiliwa na kashfa ya ESCROW. Lakini wote ni mashahidi kwamba Lowassa alibambikwa kashfa ya Richmond ili kumuokoa Bwana Mkubwa ambaye alikuwa anahusika moja kwa moja na kashfa hii. Maamuzi yote aliyoyafanya Lowassa kuhusu Richmond yalipata baraka za Bwana Mkubwa. Lilipokuja suala la kutakiwa kujiudhuru, Lowassa alifanya hivyo ili kumlinda Mkubwa huyu asiadhirike mbele ya watanzania. Sote ni mashahidi katika sakata hili na sina haja ya kurudia kusema kilichotokea. Ushahidi wa hili ni pale ambapo Lowassa alimsuta Bwana Mkubwa mbele ya kikao cha CC akabaki hana la kusema…alijua kabisa kwamba Lowassa aliachaia ngazi ili kumlinda yeye (Bwana Mkubwa).

Tukirejea kwenye ufisadi wa ESCROW, uhusika wa Pinda katika ufisadi huu uko dhahiri 100%. Panda alijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini hakuchukua hatua kuzuia skandali hii isitokee. Matokeo yake, watendaji walio chini yake walitumia udhaifu na ugoigoi wake kufanya madudu yao huku akibariki kila hatua ya ufisadi iliyokuwa ikiendelea. Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW. Na si hilo tu bali amekuwa mara kwa mara akiupotosha umma wa watanzania kwamba fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa fedha za UMMA. Huu ni uongo na unafiki mkubwa!

UTENDAJI KAZI
Wakati wa uongozi wake Waziri Mkuu Mstaafu, Hon Edward Lowassa, alibuni wazo la kuanzishwa kwa shule na hospitali za Kata. Kabla hajaachia ngazi kumpisha Pinda kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu, lengo lake hili lilikuwa limefanikiwa kwa 99.9%. Baada ya Pinda kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya, uendelezaji wa shule za Kata ukaanza kudorora na lile wazo la Lowassa la kuanzishwa Hospitali za Kata likafa kifo cha mende! Mpaka Pinda anamaliza kipindi chake, shule za kata ziko hoi kimiundombinu na kielimu—hakuna maabara, walimu, madarasa, maktaba, vifundishia na mahitaji mengine lukuki. Laiti kama Waziri Laigwanan Lowassa asingeachia madaraka, leo hii nchi hii ingekuwa mbali sana kielimu na katika masuala yote yanayohusu afya ya jamii (kila kata ingekuwa na zahanati yake). Pinda hajafanya lolote la maana kuendeleza ile miradi ya maendeleo aliyoiacha Laigwanan Lowassa.

UAMUZI MGUMU
Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi ya taifa kuliko Pinda. Wakati nchi ilipokaribia kuingia gizani, Lowassa alichukua uamuzi mgumu wa kutafuta kampuni ya Richmond ili kuzalisha umeme wa kutosha kusaidia maendeleo ya watanzania wote. Aidha, Lowassa alipochomekewa kashfa ya Richmond (ijapokuwa hakuhusika) aliamua kuachia ngazi mara moja ili kuondoa utata uliokuwa umegubika skandali ile. Na alifanya hivyo bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Katika kipindi chake chote, Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote ya maana ya kulisaidia taifa hili. Kama kuna mtu ana kumbukumbu hiyo naomba aiweke hapa. Aidha, Pinda amekumbwa na kashfa ya ESCROW lakini amegoma kuachia madaraka hata baada baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kamati ya PAC iliyochunguza skandali ile na kumkuta na hatia.

UJASIRI WA KIKE/KIUME
Wakati Pinda akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na mauaji sugu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Badala ya kuchukua hatua kukomesha mauaji yale kwa vitendo, alibakia tu analia machozi kama mtoto mdogo! Huu ni ujasiri wa kike na mtu yeyote mwenye roho ya uwoga kama hii hafai kuwa kiongozi wa nchi. Aidha, wakati Pinda alipoelemewa na skandali ya ESCROW bungeni alionekana akilia tena! Mtu wa namna hii hafai kuwa Rais hata kidogo. Kuna hatari nchi ikaja kuvamiwa na maadui badala ya kuamuru majeshi yampige adui yeye akabaki analia machozi kama mamba aliyepaliwa na mawindo. Hon Lowassa hajwahi kulia hata mara moja pindi anapokumbwa na tatizo—badala yake huchukua hatua mara moja kutatua tatizo. Huu ndio ujasiri wa kiume na watu wenye roho kama hii ndio wanaofaa kuliongoza taifa hili na kuliletea mendeleo endelevu.
View attachment 210114 View attachment 210115

HITIMISHO
Nimejaribu kutoa ufafanuzi mfupi kwa kuwalinganisha Laigwanan Edward Lowassa na Mtoto wa Mkulima ili kila mtanzania apembue mchele na chuya. Msije mkawa mnashabikia jambo msilolijua kwa kutumia ASHKI badala ya tafakuri yakinifu. Ni bora nchi hii iongozwe na John Komba kuliko kuongozwa na Pinda. Kama CCM wamekosa kabisa mtu wa kumpambanisha na mgombea wa UKAWA ni bora wamteue Komba awe mgombea wao kuliko Pinda

Nawasilisha.
:israel:

CC: FaizaFoxy, MwanaDiwani, MSALANI, East African Eagle, Ritz, mjepo, Mamndenyi, laki si pesa, Agogwe, lusungo, Queen P, gsu, Simiyu Yetu, thatha, et al.

Lowassa hajatangaza nia
 
Last edited by a moderator:
Kabla ya taswira ya kumchagua rais kutoka ccm haijaota mizizi:inatupasa kusoma nyakati watanzania wanazopita kwa sasa.Wengi sasa wanaamini wamekuwa masikini kwa sababu ya ufisadi Wa serkali ya sisiem.Na bahati mbaya ushahidi Wa escrow umetokea sawia na kuvikataa vipengele mhimu vya katiba ya time ya jaji warioba.katika Hali hii nyuso za wabongo wengi zinaonyesha kukatishwa tamaa na serial I hii.Tuombe Mungu isitokee kashifa nyingine kabla ya octoba
 
Mkuu;uko vyema & mzalendo kabisa. Wengine tunaamua kumpigia upatu #Pinda humu ndani just kujibu na kupinga hoja za hawa vijana wa Luwasa!!

Mtu ni mchafu hadi inaboa ujue! As for me,nilipumua kidogo(kwa upande wa CCM) baada ya Mizengo kutangaza nia (kimyakimya). Maana wengne walotangulia akiwemo Lowasa, ni #ngedere tu kwenye mashamba ya mahindi. Uozo. Anagalau PINDA unaweza ukamnadi kwa ushahidi kabisa kuwa ni Muadilifu & Mzalendo hakika.

Umeongelea suala la hili libwana la Barabara, sipendi kukupinga. Liko vyema mno. Ila,naamini efficiency yake inaweza kuonekana endapo atakuwa under someone! Magufuli ni mzuri sana. ila,yuko more "" #EMOTIONAL "".

Needs someone above to govern & control his deeds.

Vinginevyo,naomba kukupongeza tu kwa uwazi na utashi wako usiopenda kutangamana na makundi ya ajabuajabu (kama ya akina Lowasa-WEZI).

Mkuu, watanzania hawahitaji rais MPOLE na MNYENYEKEVU bali wanahitaji rais MTENDAJI na MWENYE UWEZO. Kama sifa ya urais ni upole, unyenyekevu, ukarimu na uzuri, basi hata mimi nafaa kuwa rais wa Tanzania (ijapokuwa sijawahi kushika wadhifa wowote hata wa uMONITA wa darasa)....nitatangaza nia basi kama vigezo vya uraisi wa nchi hii ni rahisi kiasi hicho. Ikiwa Pinda amelia mara mbili yangu awe PM, je akiwa rais atalia mara ngapi? Mwacheni mzee wa watu akalime na kufuga nyuki huku akila pensheni yake ya uwaziri mkuu. Ni afadhli Chenge awe rais wa nchi hii kuliko Pinda.
 
Alishindana na nani?
Haya HG ndio mambo gani unauliza ama ni issue zako za How are You kiswahili cha Mombasa Hawa si yule na mambo ya Ghasia mtu unauliza nini sasa hiki?...........Mwinisita mzima...aibu pole sanaaa na hakika historia haitajiludia.Ndio maana kumbe kauri ya nshazoea...kwa swali hili ningekuwa nunda ningemwaga ...saa ukiwa GT basi staha jambo la muhimu.
 
Jibu swali:

quote_icon.png
By FaizaFoxy
Alishindana na nani?

Kama ni kivuli, sema tu usione haya.
 
Kwa CCM Ni zamu ya Zanzibar sasa.
Tumempata mwadilifu wa waadilifu.Augustino Ramadhani anatosha ndani ya CCM.
 
Rais anayesema hata hajui kwa nini wananchi wake ni maskini?rais gani huyo?pinda amepinda kama jina lake
 
Back
Top Bottom