URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

Wakuu, Pinda akiwa rais wa nchi hii, naihama. Huwezi kuwa na rais kikaragosi kama Pinda halafu useme nchi ina rais. Thubutuuuuu!
 
Wakuu, Pinda akiwa rais wa nchi hii, naihama. Huwezi kuwa na rais kikaragosi kama Pinda halafu useme nchi ina rais. Thubutuuuuu!

Hehehehehehehehehehehe apo vp?
 

Attachments

  • 1418445936134.jpg
    1418445936134.jpg
    12.9 KB · Views: 262
tpaul safi sana kumbe mnajua rais anatoka chama cha mapinduzi ndio maana mnakata mauno sana kwenye huu uzi vipi kule UKAWA nani atasimama kuisindikiza CCM ikulu? :becky:
 
Last edited by a moderator:
"Bando kitita" ya Pinda imeexpire

Thats why your interest ni kwa mabinti na sio siasa hivo hujui chochote kuhusu siasa waachie wenyewe we endelea na vibinti vyako ndio interest yako
 
Wakuu, Pinda akiwa rais wa nchi hii, naihama. Huwezi kuwa na rais kikaragosi kama Pinda halafu useme nchi ina rais. Thubutuuuuu!

Mh mkuu unapiga debe, au upo kwenye mgao wa EL? maana uzi huu uliouweka unaupigia debe kweli kweli hata huwapi wenzio fursa ya kusema yao
 
Wahi Monduli ukachukue fedha ya sikukuu ya Xmass na Mwaka Mpya umejitahidi kujikomba

Ni kweli mkuu huyu mleta mada kaitoa wakati muafaka maana kipindi cha mgao kimefika, si unajua tena akishafika Monduli, utasikia "MH. UNAJUA NAFIGHT SANA HADI KULE JF NIMEFANIKIWA KUWA-CONVINCE WATU NA SASA UPO JUU" then anapewa bahasha ya X-mas
 
Wapigwe tu atang'oa watu miguu, maana ana hasira ya kufa mtu. Lowassa ni mtetezi wa watu hivyo anafaa kuwa Rais wa nchi hii. CCM tufanye uamuzi makini 2015.
 
Wote waliotajwa hawafai ebu nipeni ulinganisho na pombe magufuli kama shida sio njaa ktk wadau hawa.wanaowatetea
 
Wote waliotajwa hawafai ebu nipeni ulinganisho na pombe magufuli kama shida sio njaa ktk wadau hawa.wanaowatetea

Aka Pombe, ya aina gani hiyo? Gongo, chimpumu, kangara, uyoga, mbege, mtama, chibuku, ni ipi hiyo?
 
lowasa ni moja kat ya mawzir wakuu wajasir waliowah kutokea katk nchi hii,binafs najivunia yeye kwa uamuz wake na usimamiz uliotukuka katka shule za kata japo naamin kuwa lait angekuwa wazir mkuu had leo shule za kata zingekuwa mbali pia uwepo wa chuo cha udom alifanya maamuz magum hadi kfikia pale,kiukwel siwez kumlinganisha na mtu yeyote na anafaa kupeperusha bendera ya chama chetu tukufu@kila la kher katka nia yako sis tuko nyuma yako kuhakikisha ndoto yako inatimia
 
Mh mkuu unapiga debe, au upo kwenye mgao wa EL? maana uzi huu uliouweka unaupigia debe kweli kweli hata huwapi wenzio fursa ya kusema yao

mkuu mimi sina mgao kutoka popote bali nausema ukweli bila kumumunya maneno. kama CCM mtateua Pinda, UKAWA tutashinda misa ya kwanza.
 
Wakati hawa wanapimwa, kigezo cha ''ufisadi'' au ''wizi'' kisiangaliwe. Pinda ni fisadi au mwizi mkubwa kuliko Lowassa. Kitendo cha watu kuiba kwa bidii kuu huku ukiangalia tuu bila kusema wala kuchukua hatua, kina maana moja tu - Unafaidika na wizi huo. Ofisi ya Pinda inaongoza kwa ufisadi wa kutisha.

Inaonekana anawatikisa
 
mimi ni team UKAWA ila najaribu kuwaonyesha maCCM udhaifu wa Pinda maana naona baadhi yao wanahemka sana. wote wawili ni dhaifu lakini pinda ni dhaifu mara dufu. nawaomba waje watuletee mgombea mwenye unafuu ili mgombea wa UKAWA atakapomtimulia vumbi mgombea wao wasije wakasingizia kwamba walikosea kuteua--kama ilivyo kawaida yao.

Pinda ni Rais 2015 piga ua hapatoshi.
 
View attachment 210112 Vs View attachment 210113

Lowassa na Pinda ni miongoni mwa wanaCCM waliotangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015. Kila mmoja wa ‘watangaza nia’ hawa ana kundi lake la wanaCCM wanaompigia chapuo na kumpamba kwa kila namna ili chama kimpendekeze kupeperusha bendera ya CCM na, kama akifanikiwa kupenya kwenye mchuano mkali wa UKAWA, awe Rais wa Tanzania 2015-2020.

Kwa mtazamo wangu, kumliganisha Lowasa na Pinda ni sawa na kuulinganisha mlima Kilimanajaro na kichuguu. Pinda anaweza kabisa kulinganishwa na Membe au ‘mtangaza nia’ mwingine lakini sio Lowassa. Lowassa yuko levo nyingine kabisa. Ulinganisho wowote utakaotumia kuwalinganisha wawili hawa, unaonyesha kwamba Pinda hafui dafu mbele ya Lowassa:

KASHFA YA UFISADI
Wote wawili wana kashfa za kifisadi. Wakati Lowassa anakabiliwa na kashafa ya Richmond, Pinda anakabiliwa na kashfa ya ESCROW. Lakini wote ni mashahidi kwamba Lowassa alibambikwa kashfa ya Richmond ili kumuokoa Bwana Mkubwa ambaye alikuwa anahusika moja kwa moja na kashfa hii. Maamuzi yote aliyoyafanya Lowassa kuhusu Richmond yalipata baraka za Bwana Mkubwa. Lilipokuja suala la kutakiwa kujiudhuru, Lowassa alifanya hivyo ili kumlinda Mkubwa huyu asiadhirike mbele ya watanzania. Sote ni mashahidi katika sakata hili na sina haja ya kurudia kusema kilichotokea. Ushahidi wa hili ni pale ambapo Lowassa alimsuta Bwana Mkubwa mbele ya kikao cha CC akabaki hana la kusema…alijua kabisa kwamba Lowassa aliachaia ngazi ili kumlinda yeye (Bwana Mkubwa).

Tukirejea kwenye ufisadi wa ESCROW, uhusika wa Pinda katika ufisadi huu uko dhahiri 100%. Panda alijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini hakuchukua hatua kuzuia skandali hii isitokee. Matokeo yake, watendaji walio chini yake walitumia udhaifu na ugoigoi wake kufanya madudu yao huku akibariki kila hatua ya ufisadi iliyokuwa ikiendelea. Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW. Na si hilo tu bali amekuwa mara kwa mara akiupotosha umma wa watanzania kwamba fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa fedha za UMMA. Huu ni uongo na unafiki mkubwa!

UTENDAJI KAZI
Wakati wa uongozi wake Waziri Mkuu Mstaafu, Hon Edward Lowassa, alibuni wazo la kuanzishwa kwa shule na hospitali za Kata. Kabla hajaachia ngazi kumpisha Pinda kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu, lengo lake hili lilikuwa limefanikiwa kwa 99.9%. Baada ya Pinda kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya, uendelezaji wa shule za Kata ukaanza kudorora na lile wazo la Lowassa la kuanzishwa Hospitali za Kata likafa kifo cha mende! Mpaka Pinda anamaliza kipindi chake, shule za kata ziko hoi kimiundombinu na kielimu—hakuna maabara, walimu, madarasa, maktaba, vifundishia na mahitaji mengine lukuki. Laiti kama Waziri Laigwanan Lowassa asingeachia madaraka, leo hii nchi hii ingekuwa mbali sana kielimu na katika masuala yote yanayohusu afya ya jamii (kila kata ingekuwa na zahanati yake). Pinda hajafanya lolote la maana kuendeleza ile miradi ya maendeleo aliyoiacha Laigwanan Lowassa.

UAMUZI MGUMU
Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi ya taifa kuliko Pinda. Wakati nchi ilipokaribia kuingia gizani, Lowassa alichukua uamuzi mgumu wa kutafuta kampuni ya Richmond ili kuzalisha umeme wa kutosha kusaidia maendeleo ya watanzania wote. Aidha, Lowassa alipochomekewa kashfa ya Richmond (ijapokuwa hakuhusika) aliamua kuachia ngazi mara moja ili kuondoa utata uliokuwa umegubika skandali ile. Na alifanya hivyo bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Katika kipindi chake chote, Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote ya maana ya kulisaidia taifa hili. Kama kuna mtu ana kumbukumbu hiyo naomba aiweke hapa. Aidha, Pinda amekumbwa na kashfa ya ESCROW lakini amegoma kuachia madaraka hata baada baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kamati ya PAC iliyochunguza skandali ile na kumkuta na hatia.

UJASIRI WA KIKE/KIUME
Wakati Pinda akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na mauaji sugu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Badala ya kuchukua hatua kukomesha mauaji yale kwa vitendo, alibakia tu analia machozi kama mtoto mdogo! Huu ni ujasiri wa kike na mtu yeyote mwenye roho ya uwoga kama hii hafai kuwa kiongozi wa nchi. Aidha, wakati Pinda alipoelemewa na skandali ya ESCROW bungeni alionekana akilia tena! Mtu wa namna hii hafai kuwa Rais hata kidogo. Kuna hatari nchi ikaja kuvamiwa na maadui badala ya kuamuru majeshi yampige adui yeye akabaki analia machozi kama mamba aliyepaliwa na mawindo. Hon Lowassa hajwahi kulia hata mara moja pindi anapokumbwa na tatizo—badala yake huchukua hatua mara moja kutatua tatizo. Huu ndio ujasiri wa kiume na watu wenye roho kama hii ndio wanaofaa kuliongoza taifa hili na kuliletea mendeleo endelevu.
View attachment 210114 View attachment 210115

HITIMISHO
Nimejaribu kutoa ufafanuzi mfupi kwa kuwalinganisha Laigwanan Edward Lowassa na Mtoto wa Mkulima ili kila mtanzania apembue mchele na chuya. Msije mkawa mnashabikia jambo msilolijua kwa kutumia ASHKI badala ya tafakuri yakinifu. Ni bora nchi hii iongozwe na John Komba kuliko kuongozwa na Pinda. Kama CCM wamekosa kabisa mtu wa kumpambanisha na mgombea wa UKAWA ni bora wamteue Komba awe mgombea wao kuliko Pinda

Nawasilisha.
:israel:

CC: FaizaFoxy, MwanaDiwani, MSALANI, East African Eagle, Ritz, mjepo, Mamndenyi, laki si pesa, Agogwe, lusungo, Queen P, gsu, Simiyu Yetu, thatha, et al.

Pinda Rais 2015 mtashangazwa sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom