URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

Wahi Monduli ukachukue fedha ya sikukuu ya Xmass na Mwaka Mpya umejitahidi kujikomba
 
Pinda anaweza kuwa Raisi wa nchi hii Lowassa hawezi kuwa Raisi wa nchi hii that's where the difference is

kama macho yako ni makengeza lazima uone hivyo. lowassa ni mtendaji na mbunifu kuliko pinda. siku pinda akiwa rais wa nchi hii mtatamani bora jk angeongezewa muda. mtakuja kuikumbuka hii kauli yangu.
 
Wahi Monduli ukachukue fedha ya sikukuu ya Xmass na Mwaka Mpya umejitahidi kujikomba

mkuu, mimi sijikombi kama wewe na wala sina maslahi na yeyote kati ya hawa wawili bali najaribu kuonyesha uhalisia ili watanzania mpembue pumba na mchele wenyewe.
 
Mimi si mwanaCCM wala si shabiki wa yeyote kati ya Lowasa na Pinda.Huwa najaribu kujiuliza maamuzi magumu yenye faida chanya ambayo Lowasa hutajwa kuyafanya ni yepi hayo?

Utendaji uliotukuka wa Lowasa ni upi huo?

Ninachoweza kukiona kwa Lowasa ni kuwa ni Mzee mwenye uzoefu Mkubwa wa kiutawala hasa utawala wa kutaka kutukuzwa.Lakini pia Lowasa amejaaliwa sauti yenye nguvu na msisitizo.Sauti pekee kuwa ya msisitizo hakumfanyi kiongozi kuwa makini au mchapakazi.

Pia ieleweke kuwa Kiongozi kutokuwa na sauti yenye nguvu haina maana kuwa kiomgozi hawezi kutoa maamuzi magumu.

Kiongozi bora si yule anayekuwa na tabia ya "ukasuku".Ukasuku ni tabia ya kufanya maamuzi kutokana na mihemko ya umma au sauti zinazovuma sana dhidi ya jambo fulani na kiongozi huyo anachukua maamuzi kutokana na mvumo wa sauti hizo bila kujali maslahi ya Taifa.

Pinda ni kiongozi asiye na ukasuku,ni mtulivu na hakurupuki kutoa maamuzi.

Pinda ni kiongozi mchapakazi na mfuatiliaji lakini maneno kidogo.

Pinda ni mbunifu,ndiye aliyependekeza sera ya kilimo kwanza,sera iliyopelekea ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya kilimo.Japokuwa sera hiyo ina mapungufu na changamoto nyingi; ambazo ni ukosefu wa masoko ya uhakika, ukosefu wa viwanda vya kuchakata na kupandisha thamani ya mazao hayo.Sera hiyo imepelekea Boss wake apewe u-profesa huko China.Na pia sera hiyo kukubalika sana na secretariet ya AU.

kwa mizania yangu Pinda ni bora kuliko Lowasa,japokuwa wote hao wawili hawafikii uwezo wa Dr.W. Slaa.

Najaribu kukumbusha moja ya Maamuzi Magumu,Suala la Kudondoka kwa Jengo kule Temeke,Mh Lowasa hakusubiri tume Iundwe aliwaajibisha Woote walio husika on the spot tena wakiwa hawapo eneo la tukio na alifika eneo la Tukio dakika chache baada ya kutokea.

Suala la Uanzishwaji wa chuo cha uma,Udom,pamoja na kutokuwa ajenda ya ccm na kupingwa na baraza la mawiziri wake lakini aliona umuhimu wa kuanzishwa chuo kikuu kingine chenye kutoa wahimu wengi wa Ualimu ili kuendana na sera ya shule kwa kila kata.

Ufunguaji wa Matumizi ya Mto nile,ni yeye tena aliyepigania na kubishana na wakubwa huko sudani na kuamuru Maji ya ziwa victoria yatumike,Mwanza,Shinyanga na Mara sasa wana enjoy uamuzi huu.

Kukubali kuachia Ngazi/nafasi ya Uaziri mkuu ni Moja ya Maamuzi magumu,1. Moja kulinda serikali yake otherwise angeendelea kukomaa yangetokea kama haya ya Escrow.

Naendelea kufunua Makabrasha yangu Nitaendelea kukuletea ila nitakueletea Mana Halmashauri enzi yake ya uwaziri mkuu waulize wafanyakazi waliokuwa chini yake watakwambia Lowasa ni mtu wa namna gani lonapokuja suala la utendaji na uwajibikaji.

Amekaa ofisini kwa kipindi kifupi lakini kazi yake na sifa yake imemzidi Pinda na Sumaye waliokaa vipindi virefu.

Wakati wanaingia Madarakani yeye na Mh Jk walikuwa na vision na mawazo makubwa yalikuwa kwake baada ya kuondoka umeona jinsi serikali ya Mh Jk inavyoyumba kwa mambo mengi mana hamna wa mfano wake,Pinda yupo pale kwa ajili ya stamp tu,kila kitu hadi raisi sasa yeye ana umuhimu gani wa kuwa Waziri mkuu kama Mhongo na Maswi au mawaziri Wabovu wapo chini yake.

Ni hayo tu kwa sasa ila Guys Lowasa ndio anaweza kurudisha matumaini yaliyopotea Membe,Pinda na Wengine sioni mwenye vision na akaweza kuisimamia.

cc Pasco,Ritz,John Okello et.all
 
Mh E. L kujitoa kafara kuwahadaa Watanzania ndio uamuzi mgumu!!?? Wote wawili wanadhambi ya mizani sawa kwa kusappoti uhujumu uchumi wa Wa Tz.
 
pamoja na sifa zote ulizozitoa kwa Luwasa sikubaliani na sifa uliyosema eti alijiuzulu kwa sababu ya kumuokoa Rais kwenye kashfa ya Richmod,hapo ilitakiwa amwachie mzigo wake lakini alichofanya ni kualalisha wizi dhidi ya wananchi
 
Najaribu kukumbusha moja ya Maamuzi Magumu,Suala la Kudondoka kwa Jengo kule Temeke,Mh Lowasa hakusubiri tume Iundwe aliwaajibisha Woote walio husika on the spot tena wakiwa hawapo eneo la tukio na alifika eneo la Tukio dakika chache baada ya kutokea.

Suala la Uanzishwaji wa chuo cha uma,Udom,pamoja na kutokuwa ajenda ya ccm na kupingwa na baraza la mawiziri wake lakini aliona umuhimu wa kuanzishwa chuo kikuu kingine chenye kutoa wahimu wengi wa Ualimu ili kuendana na sera ya shule kwa kila kata.

Ufunguaji wa Matumizi ya Mto nile,ni yeye tena aliyepigania na kubishana na wakubwa huko sudani na kuamuru Maji ya ziwa victoria yatumike,Mwanza,Shinyanga na Mara sasa wana enjoy uamuzi huu.

Kukubali kuachia Ngazi/nafasi ya Uaziri mkuu ni Moja ya Maamuzi magumu,1. Moja kulinda serikali yake otherwise angeendelea kukomaa yangetokea kama haya ya Escrow.

Naendelea kufunua Makabrasha yangu Nitaendelea kukuletea ila nitakueletea Mana Halmashauri enzi yake ya uwaziri mkuu waulize wafanyakazi waliokuwa chini yake watakwambia Lowasa ni mtu wa namna gani lonapokuja suala la utendaji na uwajibikaji.

Amekaa ofisini kwa kipindi kifupi lakini kazi yake na sifa yake imemzidi Pinda na Sumaye waliokaa vipindi virefu.

Wakati wanaingia Madarakani yeye na Mh Jk walikuwa na vision na mawazo makubwa yalikuwa kwake baada ya kuondoka umeona jinsi serikali ya Mh Jk inavyoyumba kwa mambo mengi mana hamna wa mfano wake,Pinda yupo pale kwa ajili ya stamp tu,kila kitu hadi raisi sasa yeye ana umuhimu gani wa kuwa Waziri mkuu kama Mhongo na Maswi au mawaziri Wabovu wapo chini yake.

Ni hayo tu kwa sasa ila Guys Lowasa ndio anaweza kurudisha matumaini yaliyopotea Membe,Pinda na Wengine sioni mwenye vision na akaweza kuisimamia.

cc Pasco,Ritz,John Okello et.all

Tunatofautiana sana namna ya kufikiri,sikujua kama kufukuza kazi wato hovyo ni moja ya sifa za kuchaguliwa kuwa rais.Lowasa ni kiongozi wa Media na si mchapakazi kama unavyodhani.

Sifa za Udom na maji ya Victoria zimuendee JK.
 
Labda niseme tu kuwa,Urais ni taasisi kubwa sana,na anaeingia pale magogoni haongozi tu mwenyewe kwa utashi wake,Tulishuhudia mbwembwe nyingi sana za JK alivyoingia Ikulu,alitembelea mawizara,mahospitali,taasisi za umma,semina elekezi za ngurduto,mabilioni ya JK,nk.Mambo yalikuwa mengi sana na wananchi walikuwa na imani kubwa sana na uongozi wa nchi wakati ule,wengine walisena JK ni chaguo la mungu,sasa hivi tunazungumzaje?ari ile iko wapi?uongozi ule uko wapi?wamechoka na kutuacha watanzania hoi tukiwa hatuna tumaini tena?Kwangu mimi ndani ya chama tawala hakuna mwenye uwezo wa kutuvusha watanzania,hata kama kuna MALAIKA atakeotoka ccm kuja kutuongozea nchi hii,ibilisi na mashetani waliopo ccm ni wengi mno watammeza huyu malaika mmoja,ni vyema tukawapumzisha tu wawe wapinzani labda wataweza kuwasimamia UKAWA.Huu ni mtazamo wangu.
 
kama macho yako ni makengeza lazima uone hivyo. lowassa ni mtendaji na mbunifu kuliko pinda. siku pinda akiwa rais wa nchi hii mtatamani bora jk angeongezewa muda. mtakuja kuikumbuka hii kauli yangu.

I stand to my kauli hawezi "Lowassa hawezi kuwa Rais wa nchi hii" rudi 2015 tufanye majumuisho.....
 
wote hawafai. ila mtoa mada wewe ni team lowassa
Wewe unayo akili, tunahitaji mtu tofauti na hawa kwani wana watu wengi wakuwatetea na hatimaye watabidi kuja kulipa fadhila na hapo ndipo mtasikia mikoa inaongezeka kila kukicha ilimradi watu wapewe ulaji.Hivyo Lowasa hatufai na Pinda kadhalika.
 
Wakati hawa wanapimwa, kigezo cha ''ufisadi'' au ''wizi'' kisiangaliwe. Pinda ni fisadi au mwizi mkubwa kuliko Lowassa. Kitendo cha watu kuiba kwa bidii kuu huku ukiangalia tuu bila kusema wala kuchukua hatua, kina maana moja tu - Unafaidika na wizi huo. Ofisi ya Pinda inaongoza kwa ufisadi wa kutisha.
 
View attachment 210112 Vs View attachment 210113

Lowassa na Pinda ni miongoni mwa wanaCCM waliotangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015. Kila mmoja wa ‘watangaza nia’ hawa ana kundi lake la wanaCCM wanaompigia chapuo na kumpamba kwa kila namna ili chama kimpendekeze kupeperusha bendera ya CCM na, kama akifanikiwa kupenya kwenye mchuano mkali wa UKAWA, awe Rais wa Tanzania 2015-2020.

Kwa mtazamo wangu, kumliganisha Lowasa na Pinda ni sawa na kuulinganisha mlima Kilimanajaro na kichuguu. Pinda anaweza kabisa kulinganishwa na Membe au ‘mtangaza nia’ mwingine lakini sio Lowassa. Lowassa yuko levo nyingine kabisa. Ulinganisho wowote utakaotumia kuwalinganisha wawili hawa, unaonyesha kwamba Pinda hafui dafu mbele ya Lowassa:

KASHFA YA UFISADI
Wote wawili wana kashfa za kifisadi. Wakati Lowassa anakabiliwa na kashafa ya Richmond, Pinda anakabiliwa na kashfa ya ESCROW. Lakini wote ni mashahidi kwamba Lowassa alibambikwa kashfa ya Richmond ili kumuokoa Bwana Mkubwa ambaye alikuwa anahusika moja kwa moja na kashfa hii. Maamuzi yote aliyoyafanya Lowassa kuhusu Richmond yalipata baraka za Bwana Mkubwa. Lilipokuja suala la kutakiwa kujiudhuru, Lowassa alifanya hivyo ili kumlinda Mkubwa huyu asiadhirike mbele ya watanzania. Sote ni mashahidi katika sakata hili na sina haja ya kurudia kusema kilichotokea. Ushahidi wa hili ni pale ambapo Lowassa alimsuta Bwana Mkubwa mbele ya kikao cha CC akabaki hana la kusema…alijua kabisa kwamba Lowassa aliachaia ngazi ili kumlinda yeye (Bwana Mkubwa).

Tukirejea kwenye ufisadi wa ESCROW, uhusika wa Pinda katika ufisadi huu uko dhahiri 100%. Panda alijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini hakuchukua hatua kuzuia skandali hii isitokee. Matokeo yake, watendaji walio chini yake walitumia udhaifu na ugoigoi wake kufanya madudu yao huku akibariki kila hatua ya ufisadi iliyokuwa ikiendelea. Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW. Na si hilo tu bali amekuwa mara kwa mara akiupotosha umma wa watanzania kwamba fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa fedha za UMMA. Huu ni uongo na unafiki mkubwa!

UTENDAJI KAZI
Wakati wa uongozi wake Waziri Mkuu Mstaafu, Hon Edward Lowassa, alibuni wazo la kuanzishwa kwa shule na hospitali za Kata. Kabla hajaachia ngazi kumpisha Pinda kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu, lengo lake hili lilikuwa limefanikiwa kwa 99.9%. Baada ya Pinda kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya, uendelezaji wa shule za Kata ukaanza kudorora na lile wazo la Lowassa la kuanzishwa Hospitali za Kata likafa kifo cha mende! Mpaka Pinda anamaliza kipindi chake, shule za kata ziko hoi kimiundombinu na kielimu—hakuna maabara, walimu, madarasa, maktaba, vifundishia na mahitaji mengine lukuki. Laiti kama Waziri Laigwanan Lowassa asingeachia madaraka, leo hii nchi hii ingekuwa mbali sana kielimu na katika masuala yote yanayohusu afya ya jamii (kila kata ingekuwa na zahanati yake). Pinda hajafanya lolote la maana kuendeleza ile miradi ya maendeleo aliyoiacha Laigwanan Lowassa.

UAMUZI MGUMU
Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi ya taifa kuliko Pinda. Wakati nchi ilipokaribia kuingia gizani, Lowassa alichukua uamuzi mgumu wa kutafuta kampuni ya Richmond ili kuzalisha umeme wa kutosha kusaidia maendeleo ya watanzania wote. Aidha, Lowassa alipochomekewa kashfa ya Richmond (ijapokuwa hakuhusika) aliamua kuachia ngazi mara moja ili kuondoa utata uliokuwa umegubika skandali ile. Na alifanya hivyo bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Katika kipindi chake chote, Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote ya maana ya kulisaidia taifa hili. Kama kuna mtu ana kumbukumbu hiyo naomba aiweke hapa. Aidha, Pinda amekumbwa na kashfa ya ESCROW lakini amegoma kuachia madaraka hata baada baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kamati ya PAC iliyochunguza skandali ile na kumkuta na hatia.

UJASIRI WA KIKE/KIUME
Wakati Pinda akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na mauaji sugu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Badala ya kuchukua hatua kukomesha mauaji yale kwa vitendo, alibakia tu analia machozi kama mtoto mdogo! Huu ni ujasiri wa kike na mtu yeyote mwenye roho ya uwoga kama hii hafai kuwa kiongozi wa nchi. Aidha, wakati Pinda alipoelemewa na skandali ya ESCROW bungeni alionekana akilia tena! Mtu wa namna hii hafai kuwa Rais hata kidogo. Kuna hatari nchi ikaja kuvamiwa na maadui badala ya kuamuru majeshi yampige adui yeye akabaki analia machozi kama mamba aliyepaliwa na mawindo. Hon Lowassa hajwahi kulia hata mara moja pindi anapokumbwa na tatizo—badala yake huchukua hatua mara moja kutatua tatizo. Huu ndio ujasiri wa kiume na watu wenye roho kama hii ndio wanaofaa kuliongoza taifa hili na kuliletea mendeleo endelevu.
View attachment 210114 View attachment 210115

HITIMISHO
Nimejaribu kutoa ufafanuzi mfupi kwa kuwalinganisha Laigwanan Edward Lowassa na Mtoto wa Mkulima ili kila mtanzania apembue mchele na chuya. Msije mkawa mnashabikia jambo msilolijua kwa kutumia ASHKI badala ya tafakuri yakinifu. Ni bora nchi hii iongozwe na John Komba kuliko kuongozwa na Pinda. Kama CCM wamekosa kabisa mtu wa kumpambanisha na mgombea wa UKAWA ni bora wamteue Komba awe mgombea wao kuliko Pinda

Nawasilisha.
:israel:

CC: FaizaFoxy, MwanaDiwani, MSALANI, East African Eagle, Ritz, mjepo, Mamndenyi, laki si pesa, Agogwe, lusungo, Queen P, gsu, Simiyu Yetu, thatha, et al.

Vizuri Sana Mwana JF. Umenifurahisha Sana Hebu Nitumie Namba Yako Ya Tigopesa au MPesa Nami Nikugawie Chenji Zilizobaki Kutoka Kwa VIP, IPTL na ESCROW! Anayemkataa Lowassa Asiwe Rais Huyo Ana PEPO. Yaani Nina Hamu Hata Leo Lowassa Atangazwe Kuwa Rais MTEULE Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.....Tanzania Ya Sasa Tunahitaji Kiongozi Msimamo, Mbabe, Anayejiamini, Asiyeogopa Na Mchapakazi Kwa Vitendo Na Siyo kwa Blah Blah. Edward Ngoyai Lowassa ANATUFAA Watanzania!
 
mkuu, Econometrician, hata kama wote ni viwete mbele ya mgombea wa UKAWA, sio dhambi kuwapambanisha peke yao. ndio maana nimeonyesha udhaifu wao wote na uafadhali wa Lowassa.

mkuu KBOSCO, hata kama Lowassa ni mpiga deal lakini sehemu ya deal hiyo akaitumia kunufaisha wananchi ni bora kuliko mtu asiyeweza lolote na anayelia ovyo kama mtoto badala ya kutatua matatizo. kama pinda angekuwa PM kipindi kile nchi inaelekea gizani asingefanya maamuzi yote magumu zaidi ya kulia machozi ya kike!

Too biased you are.

Hatari sana watu wa aina yenu. Hiyo inaitwa "Mahaba Niue" sio Mapenzi ya dhati. Na hasara yake inafahamika.
 
Last edited by a moderator:
mkuu naona sasa umeanza kutupigia RAMLI badala ya kutueleza FACTS.

Naona tpain ahaha sorry tpaul hivi nyumbani kwenu kuna wazee kwa misingi ya baba yako na ndugu zake wadogo kwa wakubwa na pia baba yako ana baba yake...baba yake baba yako wewe ni kaka yako na mkewe wake huyo kaka yako ni shemeji yako wewe. Sasa ukitaka kujua ninachokizungumzia kikoje japo simaanishi matamshi yako YA RAMLI [Japo kwa Mila na Jadi ya kiafrika kipo hicho ukisemacho ipo] namaanisha kuwa kakae na hao kaka zako kwa muda kidogo watakusaidia kukujenga kujua JADI YA KWENU IKOJE...na kupitia jadi hiyo utajua baadhi ya mambo ambayo pamoja na kuwa modern bado yatakusaidia wewe na kizazi chako.

Ndio maana Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika moja ya hotuba [Speech ] yake kuhusu matumizi ya kipengere watu kuulizwa dini zao kwenye karatasi za kiserikali cha DINI YA MTU anasema hawakuitaji kujua DINI ya MTU.Kwani wanataka KUTAMBIKA.Manake anasema kama yeye anataka kutambika uenda kwa WATYAMA[Akimaanisha Jamii Ya Watu Wa Kabila Lake La Wazanaki] wenzie wakajiunga huko KUTAMBIKA kwa MUNGU wa WATYAMA.

Jadi ni nguzo za asilia ambazo jamii husika au Wananchi kwa umoja wao wanakubaliana kuwa jambo husika kwa misingi yake ni Sawa na kuwa hivyo na kwa uamuzi huo jamii utazifuata kwa vizazi na vizazi kwa kuzingatia nyakati na mafunuo weredi.

Mfano Mdogo Wa Vitu Vya Jadi ambavyo ujenga mazoea na kuwa ni JADI AU UTAMADUNI.
Kwa Watanzania ni UTAMADUNI AU JADI kuona TAUSI [Peacock] wanapatikana kwenye majengo muhimu yenye heshima ya upekee kwenye TAIFA kama IKULU na Nyumba za kuu za USALAMA wa TAIFA hili.Sasa tpaul nenda katafute Tausi ufuge nyumbani kwako, ata kama ni Tajiri Mkubwa kiasi gani Watanzania Watakukata Mapemba Ya Utajiri huo na Wamchukue TAUSI huyo haraka sana na watakuadhibu kwa kumilki nembo hiyo muhimu ambayo ni ishara ya UKUU WA TAIFA ambayo Watanzania waliipewa kama zawadi toka kwa Utawala wa TAIFA la INDIA.

Kwa kuonyesha tunavyoishi na Jadi hata NENO IKULU si neno kutoka kwenye kutohoa majina ya ya kigeni kisasa [Modern] bali imetokana na neno lenye ASILI YA WATEMI toka mkoa wa TABORA.Watemi enzi ya MTEMI MIRAMBO ngome zao kuu ziliitwa IKULU yani UKUU.hivyo usione neno ikulu ukajua Dunia nzima inalitumia bali ni neno la ASILI TOKA TANZANIA likiwa ni neno la KIJADI toka moja ya Makabila yenye asili ya Kishujaa Ya Tanzania.

Wananyamwezi wana nyimbo zao zenye uswahiba na neno ilo IKULU kama huu!!
''Mwafuma mwikulu Mwangaruka Ngw'naa Ontemi'' Maaana yake umetoka kwenye nyumba ya Ukuu Habari Yako Mtoto Wa Mfalme.Hizo ni nyimbo za salamu za mapokezi kwa viongozi na sherehe zingine za kijamiii kama HARUSI nk.


MFANO WA BATA MZINGA NA IKULU YA MAREKANI NA KISA CHA BATA MZINGA
[h=3]Origins[/h] Each year since 1947, the National Turkey Federation and the Poultry and Egg National Board have given a turkey to the President of the United States at a White House ceremony. Since then, presidents have been more likely to eat the turkey rather than give it a reprieve. A notable exception occurred in 1963, when President Kennedy, referring to the turkey given to him, said, "Let's just keep him." It wasn't until the first Thanksgiving of President George H.W. Bush, in 1989, that a turkey was officially pardoned for the first time.
[h=3]Confusing the Practice[/h] Presidents Bill Clinton, George W. Bush, and Barack Obama continued the pardons begun under the first Bush. Some confusion about the true origin of this practice has crept into recent presidential speeches though. One story claims that Harry Truman pardoned the turkey given to him in 1947, but the Truman Library has been unable to find any evidence of this. Another story claims the tradition dates back to Abraham Lincoln pardoning his son Tad's pet turkey.
 
Mtu akishakuwa fisadi hafai kuwa kiongoz hata wa familia
 
Vizuri Sana Mwana JF. Umenifurahisha Sana Hebu Nitumie Namba Yako Ya Tigopesa au MPesa Nami Nikugawie Chenji Zilizobaki Kutoka Kwa VIP, IPTL na ESCROW! Anayemkataa Lowassa Asiwe Rais Huyo Ana PEPO. Yaani Nina Hamu Hata Leo Lowassa Atangazwe Kuwa Rais MTEULE Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.....Tanzania Ya Sasa Tunahitaji Kiongozi Msimamo, Mbabe, Anayejiamini, Asiyeogopa Na Mchapakazi Kwa Vitendo Na Siyo kwa Blah Blah. Edward Ngoyai Lowassa ANATUFAA Watanzania!

Kumbe una akili hvo??? Ntaongea na baba yako ukasome Marekani walai
 
Usinywe kwanza kiroba ndo uje kucomment hapa bhana!!!

Narudia tena...kiongozi yeyote ambaye ni fisadi hafai kuwa kiongozi wa nchi achilia mbali wa familia...hizi buku 2 mnalipwa zitaja warudia nyie...sawa???
 
Back
Top Bottom