URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,725
18,113
View attachment 210112 Vs lowasa.jpg

Lowassa na Pinda ni miongoni mwa wanaCCM waliotangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015. Kila mmoja wa ‘watangaza nia' hawa ana kundi lake la wanaCCM wanaompigia chapuo na kumpamba kwa kila namna ili chama kimpendekeze kupeperusha bendera ya CCM na, kama akifanikiwa kupenya kwenye mchuano mkali wa UKAWA, awe Rais wa Tanzania 2015-2020.

Kwa mtazamo wangu, kumliganisha Lowasa na Pinda ni sawa na kuulinganisha mlima Kilimanajaro na kichuguu. Pinda anaweza kabisa kulinganishwa na Membe au ‘mtangaza nia' mwingine lakini sio Lowassa. Lowassa yuko levo nyingine kabisa. Ulinganisho wowote utakaotumia kuwalinganisha wawili hawa, unaonyesha kwamba Pinda hafui dafu mbele ya Lowassa:

KASHFA YA UFISADI
Wote wawili wana kashfa za kifisadi. Wakati Lowassa anakabiliwa na kashafa ya Richmond, Pinda anakabiliwa na kashfa ya ESCROW. Lakini wote ni mashahidi kwamba Lowassa alibambikwa kashfa ya Richmond ili kumuokoa Bwana Mkubwa ambaye alikuwa anahusika moja kwa moja na kashfa hii. Maamuzi yote aliyoyafanya Lowassa kuhusu Richmond yalipata baraka za Bwana Mkubwa. Lilipokuja suala la kutakiwa kujiudhuru, Lowassa alifanya hivyo ili kumlinda Mkubwa huyu asiadhirike mbele ya watanzania. Sote ni mashahidi katika sakata hili na sina haja ya kurudia kusema kilichotokea. Ushahidi wa hili ni pale ambapo Lowassa alimsuta Bwana Mkubwa mbele ya kikao cha CC akabaki hana la kusema…alijua kabisa kwamba Lowassa aliachaia ngazi ili kumlinda yeye (Bwana Mkubwa).

Tukirejea kwenye ufisadi wa ESCROW, uhusika wa Pinda katika ufisadi huu uko dhahiri 100%. Panda alijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini hakuchukua hatua kuzuia skandali hii isitokee. Matokeo yake, watendaji walio chini yake walitumia udhaifu na ugoigoi wake kufanya madudu yao huku akibariki kila hatua ya ufisadi iliyokuwa ikiendelea. Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW. Na si hilo tu bali amekuwa mara kwa mara akiupotosha umma wa watanzania kwamba fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa fedha za UMMA. Huu ni uongo na unafiki mkubwa!

UTENDAJI KAZI
Wakati wa uongozi wake Waziri Mkuu Mstaafu, Hon Edward Lowassa, alibuni wazo la kuanzishwa kwa shule na hospitali za Kata. Kabla hajaachia ngazi kumpisha Pinda kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu, lengo lake hili lilikuwa limefanikiwa kwa 99.9%. Baada ya Pinda kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya, uendelezaji wa shule za Kata ukaanza kudorora na lile wazo la Lowassa la kuanzishwa Hospitali za Kata likafa kifo cha mende! Mpaka Pinda anamaliza kipindi chake, shule za kata ziko hoi kimiundombinu na kielimu-hakuna maabara, walimu, madarasa, maktaba, vifundishia na mahitaji mengine lukuki. Laiti kama Waziri Laigwanan Lowassa asingeachia madaraka, leo hii nchi hii ingekuwa mbali sana kielimu na katika masuala yote yanayohusu afya ya jamii (kila kata ingekuwa na zahanati yake). Pinda hajafanya lolote la maana kuendeleza ile miradi ya maendeleo aliyoiacha Laigwanan Lowassa.

UAMUZI MGUMU
Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi ya taifa kuliko Pinda. Wakati nchi ilipokaribia kuingia gizani, Lowassa alichukua uamuzi mgumu wa kutafuta kampuni ya Richmond ili kuzalisha umeme wa kutosha kusaidia maendeleo ya watanzania wote. Aidha, Lowassa alipochomekewa kashfa ya Richmond (ijapokuwa hakuhusika) aliamua kuachia ngazi mara moja ili kuondoa utata uliokuwa umegubika skandali ile. Na alifanya hivyo bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Katika kipindi chake chote, Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote ya maana ya kulisaidia taifa hili. Kama kuna mtu ana kumbukumbu hiyo naomba aiweke hapa. Aidha, Pinda amekumbwa na kashfa ya ESCROW lakini amegoma kuachia madaraka hata baada baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kamati ya PAC iliyochunguza skandali ile na kumkuta na hatia.

UJASIRI WA KIKE/KIUME
Wakati Pinda akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na mauaji sugu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Badala ya kuchukua hatua kukomesha mauaji yale kwa vitendo, alibakia tu analia machozi kama mtoto mdogo! Huu ni ujasiri wa kike na mtu yeyote mwenye roho ya uwoga kama hii hafai kuwa kiongozi wa nchi. Aidha, wakati Pinda alipoelemewa na skandali ya ESCROW bungeni alionekana akilia tena! Mtu wa namna hii hafai kuwa Rais hata kidogo. Kuna hatari nchi ikaja kuvamiwa na maadui badala ya kuamuru majeshi yampige adui yeye akabaki analia machozi kama mamba aliyepaliwa na mawindo. Hon Lowassa hajwahi kulia hata mara moja pindi anapokumbwa na tatizo-badala yake huchukua hatua mara moja kutatua tatizo. Huu ndio ujasiri wa kiume na watu wenye roho kama hii ndio wanaofaa kuliongoza taifa hili na kuliletea mendeleo endelevu.
View attachment 210114 pinda alipobanwa na mbowe.jpg

HITIMISHO
Nimejaribu kutoa ufafanuzi mfupi kwa kuwalinganisha Laigwanan Edward Lowassa na Mtoto wa Mkulima ili kila mtanzania apembue mchele na chuya. Msije mkawa mnashabikia jambo msilolijua kwa kutumia ASHKI badala ya tafakuri yakinifu. Ni bora nchi hii iongozwe na John Komba kuliko kuongozwa na Pinda. Kama CCM wamekosa kabisa mtu wa kumpambanisha na mgombea wa UKAWA ni bora wamteue Komba awe mgombea wao kuliko Pinda

Nawasilisha.
:israel:

CC: FaizaFoxy, MwanaDiwani, MSALANI, East African Eagle, Ritz, mjepo, Mamndenyi, laki si pesa, Agogwe, lusungo, Queen P, gsu, Simiyu Yetu, thatha, et al.
 
Last edited by a moderator:
View attachment 210112 Vs View attachment 210113

Katika kipindi chake chote, Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote ya maana ya kulisaidia taifa hili. Kama kuna mtu ana kumbukumbu hiyo naomba aiweke hapa. Aidha, Pinda amekumbwa na kashfa ya ESCROW lakini amegoma kuachia madaraka hata baada baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kamati ya PAC iliyochunguza skandali ile na kumkuta na hatia.

.

Hakuna maamuzi yoyote magumu aliyowahi kuchukua, but i think that is by design ya mkuu wa nchi. Hataki strong PM ili iwe rahisi ku- deflate weakness za serikali kwa PM.
 
Kazi kwenu wana ccm,kama ni sifa za uwajibika basi leo S.A.Salim angekuwa ndo raisi wa Tz lakini haiko hivyo na sidhani kama ccm watamchagua Pinda eti kisa anauzika dhidi ya Lowassa bali ni kwamba Lowassa ana tabia ya kujisikia,anapenda sana uchifu awe mtemi atembee kama machifu wa kinigeria,na mie kwangu hilo namfananisha na tabia alizonazo Zitto
 
Mimi si mwanaCCM wala si shabiki wa yeyote kati ya Lowasa na Pinda.Huwa najaribu kujiuliza maamuzi magumu yenye faida chanya ambayo Lowasa hutajwa kuyafanya ni yepi hayo?

Utendaji uliotukuka wa Lowasa ni upi huo?

Ninachoweza kukiona kwa Lowasa ni kuwa ni Mzee mwenye uzoefu Mkubwa wa kiutawala hasa utawala wa kutaka kutukuzwa.Lakini pia Lowasa amejaaliwa sauti yenye nguvu na msisitizo.Sauti pekee kuwa ya msisitizo hakumfanyi kiongozi kuwa makini au mchapakazi.

Pia ieleweke kuwa Kiongozi kutokuwa na sauti yenye nguvu haina maana kuwa kiomgozi hawezi kutoa maamuzi magumu.

Kiongozi bora si yule anayekuwa na tabia ya "ukasuku".Ukasuku ni tabia ya kufanya maamuzi kutokana na mihemko ya umma au sauti zinazovuma sana dhidi ya jambo fulani na kiongozi huyo anachukua maamuzi kutokana na mvumo wa sauti hizo bila kujali maslahi ya Taifa.

Pinda ni kiongozi asiye na ukasuku,ni mtulivu na hakurupuki kutoa maamuzi.

Pinda ni kiongozi mchapakazi na mfuatiliaji lakini maneno kidogo.

Pinda ni mbunifu,ndiye aliyependekeza sera ya kilimo kwanza,sera iliyopelekea ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya kilimo.Japokuwa sera hiyo ina mapungufu na changamoto nyingi; ambazo ni ukosefu wa masoko ya uhakika, ukosefu wa viwanda vya kuchakata na kupandisha thamani ya mazao hayo.Sera hiyo imepelekea Boss wake apewe u-profesa huko China.Na pia sera hiyo kukubalika sana na secretariet ya AU.

kwa mizania yangu Pinda ni bora kuliko Lowasa,japokuwa wote hao wawili hawafikii uwezo wa Dr.W. Slaa.
 
Kuishi Nchi ya mazuzu ni shida sana.E.Lowassa alimuokoa bwana mkubwa maana yake ni kwamba aribariki uovu ambao ulitesa watu wengi kiuchumi,hivyo hivyo kwa M.pinda na sakata la escrow.alafu bado humu ndani tunajiona werevu sana na tunaojitambua kwa kuwapigia chapuo kushika nyazifa kubwa zaidi.ule msemo wa kuwa wasomi wa Tanzania ni wajinga zaidi kuliko ambao hawajasoma unaweza kuwa ni ukweli mtupu.mungu atusaidi ipo siku tutabadirika.
 
View attachment 210112 Vs View attachment 210113

Lowassa na Pinda ni miongoni mwa wanaCCM waliotangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015. Kila mmoja wa ‘watangaza nia’ hawa ana kundi lake la wanaCCM wanaompigia chapuo na kumpamba kwa kila namna ili chama kimpendekeze kupeperusha bendera ya CCM na, kama akifanikiwa kupenya kwenye mchuano mkali wa UKAWA, awe Rais wa Tanzania 2015-2020.

Kwa mtazamo wangu, kumliganisha Lowasa na Pinda ni sawa na kuulinganisha mlima Kilimanajaro na kichuguu. Pinda anaweza kabisa kulinganishwa na Membe au ‘mtangaza nia’ mwingine lakini sio Lowassa. Lowassa yuko levo nyingine kabisa. Ulinganisho wowote utakaotumia kuwalinganisha wawili hawa, unaonyesha kwamba Pinda hafui dafu mbele ya Lowassa:

KASHFA YA UFISADI
Wote wawili wana kashfa za kifisadi. Wakati Lowassa anakabiliwa na kashafa ya Richmond, Pinda anakabiliwa na kashfa ya ESCROW. Lakini wote ni mashahidi kwamba Lowassa alibambikwa kashfa ya Richmond ili kumuokoa Bwana Mkubwa ambaye alikuwa anahusika moja kwa moja na kashfa hii. Maamuzi yote aliyoyafanya Lowassa kuhusu Richmond yalipata baraka za Bwana Mkubwa. Lilipokuja suala la kutakiwa kujiudhuru, Lowassa alifanya hivyo ili kumlinda Mkubwa huyu asiadhirike mbele ya watanzania. Sote ni mashahidi katika sakata hili na sina haja ya kurudia kusema kilichotokea. Ushahidi wa hili ni pale ambapo Lowassa alimsuta Bwana Mkubwa mbele ya kikao cha CC akabaki hana la kusema…alijua kabisa kwamba Lowassa aliachaia ngazi ili kumlinda yeye (Bwana Mkubwa).

Tukirejea kwenye ufisadi wa ESCROW, uhusika wa Pinda katika ufisadi huu uko dhahiri 100%. Panda alijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini hakuchukua hatua kuzuia skandali hii isitokee. Matokeo yake, watendaji walio chini yake walitumia udhaifu na ugoigoi wake kufanya madudu yao huku akibariki kila hatua ya ufisadi iliyokuwa ikiendelea. Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW. Na si hilo tu bali amekuwa mara kwa mara akiupotosha umma wa watanzania kwamba fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa fedha za UMMA. Huu ni uongo na unafiki mkubwa!

UTENDAJI KAZI
Wakati wa uongozi wake Waziri Mkuu Mstaafu, Hon Edward Lowassa, alibuni wazo la kuanzishwa kwa shule na hospitali za Kata. Kabla hajaachia ngazi kumpisha Pinda kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu, lengo lake hili lilikuwa limefanikiwa kwa 99.9%. Baada ya Pinda kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya, uendelezaji wa shule za Kata ukaanza kudorora na lile wazo la Lowassa la kuanzishwa Hospitali za Kata likafa kifo cha mende! Mpaka Pinda anamaliza kipindi chake, shule za kata ziko hoi kimiundombinu na kielimu—hakuna maabara, walimu, madarasa, maktaba, vifundishia na mahitaji mengine lukuki. Laiti kama Waziri Laigwanan Lowassa asingeachia madaraka, leo hii nchi hii ingekuwa mbali sana kielimu na katika masuala yote yanayohusu afya ya jamii (kila kata ingekuwa na zahanati yake). Pinda hajafanya lolote la maana kuendeleza ile miradi ya maendeleo aliyoiacha Laigwanan Lowassa.

UAMUZI MGUMU
Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi ya taifa kuliko Pinda. Wakati nchi ilipokaribia kuingia gizani, Lowassa alichukua uamuzi mgumu wa kutafuta kampuni ya Richmond ili kuzalisha umeme wa kutosha kusaidia maendeleo ya watanzania wote. Aidha, Lowassa alipochomekewa kashfa ya Richmond (ijapokuwa hakuhusika) aliamua kuachia ngazi mara moja ili kuondoa utata uliokuwa umegubika skandali ile. Na alifanya hivyo bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Katika kipindi chake chote, Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote ya maana ya kulisaidia taifa hili. Kama kuna mtu ana kumbukumbu hiyo naomba aiweke hapa. Aidha, Pinda amekumbwa na kashfa ya ESCROW lakini amegoma kuachia madaraka hata baada baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kamati ya PAC iliyochunguza skandali ile na kumkuta na hatia.

UJASIRI WA KIKE/KIUME
Wakati Pinda akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na mauaji sugu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Badala ya kuchukua hatua kukomesha mauaji yale kwa vitendo, alibakia tu analia machozi kama mtoto mdogo! Huu ni ujasiri wa kike na mtu yeyote mwenye roho ya uwoga kama hii hafai kuwa kiongozi wa nchi. Aidha, wakati Pinda alipoelemewa na skandali ya ESCROW bungeni alionekana akilia tena! Mtu wa namna hii hafai kuwa Rais hata kidogo. Kuna hatari nchi ikaja kuvamiwa na maadui badala ya kuamuru majeshi yampige adui yeye akabaki analia machozi kama mamba aliyepaliwa na mawindo. Hon Lowassa hajwahi kulia hata mara moja pindi anapokumbwa na tatizo—badala yake huchukua hatua mara moja kutatua tatizo. Huu ndio ujasiri wa kiume na watu wenye roho kama hii ndio wanaofaa kuliongoza taifa hili na kuliletea mendeleo endelevu.
View attachment 210114 View attachment 210115

HITIMISHO
Nimejaribu kutoa ufafanuzi mfupi kwa kuwalinganisha Laigwanan Edward Lowassa na Mtoto wa Mkulima ili kila mtanzania apembue mchele na chuya. Msije mkawa mnashabikia jambo msilolijua kwa kutumia ASHKI badala ya tafakuri yakinifu. Ni bora nchi hii iongozwe na John Komba kuliko kuongozwa na Pinda. Kama CCM wamekosa kabisa mtu wa kumpambanisha na mgombea wa UKAWA ni bora wamteue Komba awe mgombea wao kuliko Pinda

Nawasilisha.
:israel:

CC: FaizaFoxy, MwanaDiwani, MSALANI, East African Eagle, Ritz, mjepo, Mamndenyi, laki si pesa, Agogwe, lusungo, Queen P, gsu, Simiyu Yetu, thatha, et al.

Kweli wewe ni #team_lowasa . any ways,tuyaache hayo.

Now; kwenye Richmond,Lowasa alitupia vimemo kadhaa kwenye issue hiyo. na viliwekwa mezani na report ya mwakyembe. Kwa Pinda,hakuna popote alipoonekana amechochea pesa kuchukuliwa.

Pili,njoo kwenye #UFANYA_BIASHARA (Kujilimbikizia mali na kujihusisha na biashara/wafanya biawhara). Lowasa ni MROHO na yuko tayari kuwauzia nchi Wafanyabiashara pale anapoona anaweza kutengeneza/kupiga dili. Rejea issue ya NILE & EGYPT miaka ile mpaka Nyerere akamuachia laana yakutoaminiwa na watanzania kwenye nafasi za umma! I believe Pinda hana KALIBA hiyo na amewakwepa wafnyabiashara mno. Ushahidi mmoja nnao mimi mwenyewe.

Nimeshuhudia Mfanyabiashara mmoja mwenye Asili ya Kigoma na mwingine Msomari wakinyimwa "UPATU WA PINDA" kwenye bizness zao "despite" walimchangia pesa nyingi sana kwenye Harusi ya mwanae. Huyu msomari alimchangia zaidi ya Mil.30 kwenye kampeni mwaka 2010 (ingawa alipita bila kupingwa huko jimboni kwao). Jamaa hao wamehaha hadi huruma.

Just to mention the few. Nina mengi sana. Labda Pinda apambanishwe na wengine. sio Lowasa.

NAWASILISHA.

,
 
Last edited by a moderator:
Wazee walishasema ukisha kuwa Waziri Mkuu uwezi kuja kuwa Rais......mtu pekee aliyepata kuwa Waziri Mkuu na akawa Rais ni Mwalimu Julius Nyerere pekee yake......Father Of The Nation.

Usiniulize kwanini tafuta wazee wa jadi waulizie Nchi nayo ina jadi na wazee ndio wanao jua jadi hizo!!!!!!

Ukisema ni upuuzi kwa kuwa unae mpenda alishapata kuwa waziri mkuu ama ni waziri mkuu basi kwa maana hiyo unaumia unaposikia kauri za aina hii, basi waambie wanasiasa wasiwe wanakimbilia kuvalishwa migolole na kama wanapenda kuvaa na kushikilia mikuki na ngao ambazo ndizo siraha za jadi za ulinzi wa Taifa wajue hilo kuwa na Taifa kama Taifa lina Jadi kama walivyokuwa Mababu waliotangulia [Ancestors]!!!!
 
Mkuu tpaul nakubaliana nawewe....

EL anampenda JK kuliko JK anavyompenda EL...

EL amemkingia kifua JK ktk mengi Sana kuelekea magogoni na anajua mengi Sana juu ya huyu bwanamkubwa....

Nakubaliana nawe Richmond EL alibebeshwa mzigo usiomhusu maana aliyemleta nchini Naem Gire Wa Richmond anajulikana na watu wanamstahi tu kuepusha machafuko....

Wakati husema na kutenda ngoja tusubiri....
 
Last edited by a moderator:
Pinda anaweza kuwa Raisi wa nchi hii Lowassa hawezi kuwa Raisi wa nchi hii that's where the difference is
 
Hakuna maamuzi yoyote magumu aliyowahi kuchukua, but i think that is by design ya mkuu wa nchi. Hataki strong PM ili iwe rahisi ku- deflate weakness za serikali kwa PM.
Sawa mkubwa hataki PM strong! Lakini Kama wewe ni viongozi anayependa uwajibikaji unaachia ngazi kuliko kufanya kazi na mtu anayependa kuwa underrate others.
 
wote hawafai. ila mtoa mada wewe ni team lowassa

mimi ni team UKAWA ila najaribu kuwaonyesha maCCM udhaifu wa Pinda maana naona baadhi yao wanahemka sana. wote wawili ni dhaifu lakini pinda ni dhaifu mara dufu. nawaomba waje watuletee mgombea mwenye unafuu ili mgombea wa UKAWA atakapomtimulia vumbi mgombea wao wasije wakasingizia kwamba walikosea kuteua--kama ilivyo kawaida yao.
 
mkuu, Econometrician, hata kama wote ni viwete mbele ya mgombea wa UKAWA, sio dhambi kuwapambanisha peke yao. ndio maana nimeonyesha udhaifu wao wote na uafadhali wa Lowassa.

mkuu KBOSCO, hata kama Lowassa ni mpiga deal lakini sehemu ya deal hiyo akaitumia kunufaisha wananchi ni bora kuliko mtu asiyeweza lolote na anayelia ovyo kama mtoto badala ya kutatua matatizo. kama pinda angekuwa PM kipindi kile nchi inaelekea gizani asingefanya maamuzi yote magumu zaidi ya kulia machozi ya kike!
 
Last edited by a moderator:
Wazee walishasema ukisha kuwa Waziri Mkuu uwezi kuja kuwa Rais......mtu pekee aliyepata kuwa Waziri Mkuu na akawa Rais ni Mwalimu Julius Nyerere pekee yake......Father Of The Nation.

Usiniulize kwanini tafuta wazee wa jadi waulizie Nchi nayo ina jadi na wazee ndio wanao jua jadi hizo!!!!!!

Ukisema ni upuuzi kwa kuwa unae mpenda alishapata kuwa waziri mkuu ama ni waziri mkuu basi kwa maana hiyo unaumia unaposikia kauri za aina hii, basi waambie wanasiasa wasiwe wanakimbilia kuvalishwa migolole na kama wanapenda kuvaa na kushikilia mikuki na ngao ambazo ndizo siraha za jadi za ulinzi wa Taifa wajue hilo kuwa na Taifa kama Taifa lina Jadi kama walivyokuwa Mababu waliotangulia [Ancestors]!!!!

mkuu naona sasa umeanza kutupigia RAMLI badala ya kutueleza FACTS.
 
Asante kwa kazi nzuri, ila naomba utusaidie wengine, hivi Lowassa aliitangaza lini hii nia?!.

Pasco.

Lowassa alitangaza nia siku alipowaita mashabiki wake nyumbani na kuwatangazia kwamba wameanza SAFARI YA MATUMAINI (safari ya kuelekea ikulu). najua nawe ulikuwepo kwenye msafara ule lakini leo hii unajifanya hujui. mlilia pamoja na mtafurahi pamoja.
 
tulifedheheshwa sana,tulihuzunika sana,tulidhalilishwa sana,tulilia sana...kwa pamoja tutafurahi sana na yote tutasahau 2015,chagua lowassa kwa maendeleo ya taifa
 
Back
Top Bottom