URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

URAIS 2015: Pinda Vs Lowassa

Mtakoma wana ccmajambaz maana nyie mmetuchosha na uongozi wenu wa kukumbatiana kama kuku hamfai kabsa...UKAWA tunaunda jeshi imara la uongozi lenye nia ya Watanzania tuwe huru tumechoka na ukoloni mamboleo.....Ukawa tunawika na tunavuma kwa kishindo kila kona ya nchi Yetu
.....
 
lakini hatua tuliyofikia ninzuri katika ukawa.swali lamsingi nikwamba je tutaweza kukubaliana nani agombee nafasi yetu ya juu tukizingatia watu hawa;mbatia,lipumba,Dr slaa
 
View attachment 210112 Vs View attachment 210113

Lowassa na Pinda ni miongoni mwa wanaCCM waliotangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM mwaka 2015. Kila mmoja wa ‘watangaza nia' hawa ana kundi lake la wanaCCM wanaompigia chapuo na kumpamba kwa kila namna ili chama kimpendekeze kupeperusha bendera ya CCM na, kama akifanikiwa kupenya kwenye mchuano mkali wa UKAWA, awe Rais wa Tanzania 2015-2020.

Kwa mtazamo wangu, kumliganisha Lowasa na Pinda ni sawa na kuulinganisha mlima Kilimanajaro na kichuguu. Pinda anaweza kabisa kulinganishwa na Membe au ‘mtangaza nia' mwingine lakini sio Lowassa. Lowassa yuko levo nyingine kabisa. Ulinganisho wowote utakaotumia kuwalinganisha wawili hawa, unaonyesha kwamba Pinda hafui dafu mbele ya Lowassa:

KASHFA YA UFISADI
Wote wawili wana kashfa za kifisadi. Wakati Lowassa anakabiliwa na kashafa ya Richmond, Pinda anakabiliwa na kashfa ya ESCROW. Lakini wote ni mashahidi kwamba Lowassa alibambikwa kashfa ya Richmond ili kumuokoa Bwana Mkubwa ambaye alikuwa anahusika moja kwa moja na kashfa hii. Maamuzi yote aliyoyafanya Lowassa kuhusu Richmond yalipata baraka za Bwana Mkubwa. Lilipokuja suala la kutakiwa kujiudhuru, Lowassa alifanya hivyo ili kumlinda Mkubwa huyu asiadhirike mbele ya watanzania. Sote ni mashahidi katika sakata hili na sina haja ya kurudia kusema kilichotokea. Ushahidi wa hili ni pale ambapo Lowassa alimsuta Bwana Mkubwa mbele ya kikao cha CC akabaki hana la kusema…alijua kabisa kwamba Lowassa aliachaia ngazi ili kumlinda yeye (Bwana Mkubwa).

Tukirejea kwenye ufisadi wa ESCROW, uhusika wa Pinda katika ufisadi huu uko dhahiri 100%. Panda alijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini hakuchukua hatua kuzuia skandali hii isitokee. Matokeo yake, watendaji walio chini yake walitumia udhaifu na ugoigoi wake kufanya madudu yao huku akibariki kila hatua ya ufisadi iliyokuwa ikiendelea. Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW. Na si hilo tu bali amekuwa mara kwa mara akiupotosha umma wa watanzania kwamba fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya ESCROW hazikuwa fedha za UMMA. Huu ni uongo na unafiki mkubwa!

UTENDAJI KAZI
Wakati wa uongozi wake Waziri Mkuu Mstaafu, Hon Edward Lowassa, alibuni wazo la kuanzishwa kwa shule na hospitali za Kata. Kabla hajaachia ngazi kumpisha Pinda kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu, lengo lake hili lilikuwa limefanikiwa kwa 99.9%. Baada ya Pinda kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya, uendelezaji wa shule za Kata ukaanza kudorora na lile wazo la Lowassa la kuanzishwa Hospitali za Kata likafa kifo cha mende! Mpaka Pinda anamaliza kipindi chake, shule za kata ziko hoi kimiundombinu na kielimu-hakuna maabara, walimu, madarasa, maktaba, vifundishia na mahitaji mengine lukuki. Laiti kama Waziri Laigwanan Lowassa asingeachia madaraka, leo hii nchi hii ingekuwa mbali sana kielimu na katika masuala yote yanayohusu afya ya jamii (kila kata ingekuwa na zahanati yake). Pinda hajafanya lolote la maana kuendeleza ile miradi ya maendeleo aliyoiacha Laigwanan Lowassa.

UAMUZI MGUMU
Lowassa ana uwezo mkubwa wa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi ya taifa kuliko Pinda. Wakati nchi ilipokaribia kuingia gizani, Lowassa alichukua uamuzi mgumu wa kutafuta kampuni ya Richmond ili kuzalisha umeme wa kutosha kusaidia maendeleo ya watanzania wote. Aidha, Lowassa alipochomekewa kashfa ya Richmond (ijapokuwa hakuhusika) aliamua kuachia ngazi mara moja ili kuondoa utata uliokuwa umegubika skandali ile. Na alifanya hivyo bila kushurutishwa na mtu yeyote.

Katika kipindi chake chote, Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote ya maana ya kulisaidia taifa hili. Kama kuna mtu ana kumbukumbu hiyo naomba aiweke hapa. Aidha, Pinda amekumbwa na kashfa ya ESCROW lakini amegoma kuachia madaraka hata baada baada ya kushauriwa kufanya hivyo na kamati ya PAC iliyochunguza skandali ile na kumkuta na hatia.

UJASIRI WA KIKE/KIUME
Wakati Pinda akiwa Waziri Mkuu kulikuwa na mauaji sugu ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Badala ya kuchukua hatua kukomesha mauaji yale kwa vitendo, alibakia tu analia machozi kama mtoto mdogo! Huu ni ujasiri wa kike na mtu yeyote mwenye roho ya uwoga kama hii hafai kuwa kiongozi wa nchi. Aidha, wakati Pinda alipoelemewa na skandali ya ESCROW bungeni alionekana akilia tena! Mtu wa namna hii hafai kuwa Rais hata kidogo. Kuna hatari nchi ikaja kuvamiwa na maadui badala ya kuamuru majeshi yampige adui yeye akabaki analia machozi kama mamba aliyepaliwa na mawindo. Hon Lowassa hajwahi kulia hata mara moja pindi anapokumbwa na tatizo-badala yake huchukua hatua mara moja kutatua tatizo. Huu ndio ujasiri wa kiume na watu wenye roho kama hii ndio wanaofaa kuliongoza taifa hili na kuliletea mendeleo endelevu.
View attachment 210114 View attachment 210115

HITIMISHO
Nimejaribu kutoa ufafanuzi mfupi kwa kuwalinganisha Laigwanan Edward Lowassa na Mtoto wa Mkulima ili kila mtanzania apembue mchele na chuya. Msije mkawa mnashabikia jambo msilolijua kwa kutumia ASHKI badala ya tafakuri yakinifu. Ni bora nchi hii iongozwe na John Komba kuliko kuongozwa na Pinda. Kama CCM wamekosa kabisa mtu wa kumpambanisha na mgombea wa UKAWA ni bora wamteue Komba awe mgombea wao kuliko Pinda

Nawasilisha.
:israel:

CC: FaizaFoxy, MwanaDiwani, MSALANI, East African Eagle, Ritz, mjepo, Mamndenyi, laki si pesa, Agogwe, lusungo, Queen P, gsu, Simiyu Yetu, thatha, et al.

wewe mtoa mada na hao uliowajadili ni majizi watupu. nimeisoma taarifa yako na kutafakari nkagundua kuwa wewe ni mwana ccm ambao ndo majizi . pia uko upande wa Lowasa, nahisi amekutuma au najipendekeza kwake. unawezaje kusema hakuhusika Richmond huyo? tumewachoka wote...Kuku ni kuku tu, jogoo jina
 
Mh.Edward Lowassa ni rais 2015 upende usipende,kama hutaki kakoroge juice ya sumu ya panya kanywe ili asikuongoze,watanzania tumechoka na umaskini na kuwafuga wez
 
HABARI ZENU WANAJAMVI:-
KWELI WANYONGE WALISEMA MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPATIENI. KWA SIFA HIZI, MH. KAYANZA MIZENGO PETER PINDA HANA MPINZANI KWA URAIS 2015.
ANAHITAJIWA NA WATANZANIA NA NI MTU MAKINI ANAYEJUA HOMA ZA WATANZANIA. 2015 ATAKAPOWEZESHWA KUINGIA IKULU KWA KUMPIGIA KURA ZETU ZA NDIYO NA KUSHINDA KWA 97% WATANZANIA TUTAONDOKANA NA UMASIKINI.

NANI KAMA PINDA MTOTO WA MKULIMA? HAKUNA

NHC.JPG
pinda.jpg
 
Haa haa yaani pinda awe rais? Kupitia chama gani? Kama ni ccm hakunaga kama lowasa. Hakuna wa kumng'oa lowasa ndani ya ccm kamwe.
 
okay wale wa team Pinda mnahitajiwa huku.
Team lowasa kaeni pembeni kwa sasa, Team Nchemba
msilete majungu, Team Muhongo muda wenu bado..
Team...........

CCM kuna mabaka si utani.
 
Haa haa yaani pinda awe rais? Kupitia chama gani? Kama ni ccm hakunaga kama lowasa. Hakuna wa kumng'oa lowasa ndani ya ccm kamwe.



Mmeisha waona watanzania wajinga kiasi hicho acha zenu hizo, Lazima tumpime yoyote anayataka urais amefanyia nini watanzania. Huyu jamaa hafai ni mpole kupindukia hasimamii chochote, mwoga na yupo mfumo mbovu wa ccm. hakuna kitu hapo jifurahisheni tu.
 
haa haa yaani pinda awe rais? Kupitia chama gani? Kama ni ccm hakunaga kama lowasa. Hakuna wa kumng'oa lowasa ndani ya ccm kamwe.

lowasa ni fisadi alaf makonda alishaga mchafu kwenye media .atatupa kazi kumnad ccm maana ile clip ipo hadi u tube wengine wameshatoa cd zake kibao bado kusambaza tu
 
mmeisha waona watanzania wajinga kiasi hicho acha zenu hizo, lazima tumpime yoyote anayataka urais amefanyia nini watanzania. Huyu jamaa hafai ni mpole kupindukia hasimamii chochote, mwoga na yupo mfumo mbovu wa ccm. Hakuna kitu hapo jifurahisheni tu.

unataka auwe watu kama idd amin dadaaa>
 
lowasa ni fisadi alaf makonda alishaga mchafu kwenye media .atatupa kazi kumnad ccm maana ile clip ipo hadi u tube wengine wameshatoa cd zake kibao bado kusambaza tu



Watanzania hatudanganyiki kwa sasa. Lowasa fisadi mkuu na yupo mfumo wa kifisadi. amekuwa serikalini miaka mingi kipi hasa kikubwa cha kiuchumi amekisimamia tunaweza kukiona . Hamna kitu ccm mwaka huu tunapiga chini wote.
 
Back
Top Bottom