Urais 2015: Jina la Augustino Ramadhan lajitokeza

Urais 2015: Jina la Augustino Ramadhan lajitokeza

Kuna jaji mmoja alijaribu kugombea huko nyuma nasikia aliambiwa kuwa ukshakuwa jaji Uraisi utausikia kwenye bomba. Sasa sijui kama ipo kikatiba ma la maana nasikia hata Warioba anapigiwa chapuo na UKAWA ingawa yeye kasema wazi HATAKI

Hiyo mkuu inaweza kuwa kweli labda magamba kwa vile sasa hivi yanatapatapa kupata mtu wa kuyaokoa yanaweza kupindisha na hilo. Ukisoma ibara inayohusu uchaguzi wa Rais wa JMT katika katiba ya zamani (ambayo bila shaka tutaendelea nayo kwenye uchaguzi ujao) kuna kipengere kinasema mtu anayestahili kuchaguliwa kuwa Rais ni yule anayetimiza masharti ya kuweza kuchaguliwa kuwa Mbunge.

Sasa ukisoma hizo sifa za mtu kuwa Mbunge, kuna hii moja kwenye Ibara ya 67 (2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge: -

(g)
ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;

Sasa hapo sijui na huyu mzee itamgusa? Au kwa vile alishatoka hiyo sifa ilishajifuta? Yaani kwamba inawahusu tu wale ambao bado wako kwenye utumishi wa serikali? Wanasheria watusaidie hapo!! Kwa maana ya hiyo ibara (kama mimi nilivyoielewa) Jaji atakuwa amepoteza sifa ya kuwa Mbunge, hivyo moja kwa moja hata ile sifa ya kuchaguliwa kuwa Rais atakuwa ameikosa!!

Magamba kwishneyyyyyyyy!!!!
 
Kama hivyo ndivyo kwanza itabidi katiba ya Zanzibar iandikwe upya kwani hatuwezi kukubali kuongozwa na raia wa nchi nyingine. Sisi wenyewe tunatosha.

Kwelim kabisa huku ni Tanganyika na Zanzibar ni nchi za Nje.Vilevile mzanzibar hawezi kutawala huku tena wananchi yao ...
 
DSC08497.jpg


Jamani huyu Jaji, Brigedia, Mchungaji Augustino Ramadhan anatokea Zanzibar; vipi wakubwa anafaa kuvaa viatu vya rais Kikwete?

Na aliyesoma hilo gazeti anaweza kuweka habari yake nipo shamba sijafanikiwa kulisoma

Mtu kesha staafu utumishi wa umma na kwa hesabu za kawaida alistaafu akiwa na 60yrs unategemea leo awe rais? Si ndio mambo ya mugabe hayo ta kuanguka anguka hovyo.
 
Kama hivyo ndivyo kwanza itabidi katiba ya Zanzibar iandikwe upya kwani hatuwezi kukubali kuongozwa na raia wa nchi nyingine. Sisi wenyewe tunatosha.

Labda apatiwe uraia kwanza
 
Taarifa za ndani wanasema huyu ndiye chaguo la magamba ila sasa wale wa lowassa sijui itakuwaje kwa sababu jamaa anatafuta urais kwa udi na uvumba.

Lowasa ndiye chaguo la watanzania wapenda maendeleo
 
DSC08497.jpg


Jamani huyu Jaji, Brigedia, Mchungaji Augustino Ramadhan anatokea Zanzibar; vipi wakubwa anafaa kuvaa viatu vya rais Kikwete?

Na aliyesoma hilo gazeti anaweza kuweka habari yake nipo shamba sijafanikiwa kulisoma

Kulingana na katiba ya Zanzibat ya 2010 Zanzibar ni nchi na kwa sababu hiyo sisi Watanganyika hatuwezi kuongozwa na Wazanzibari. Akagombee kule kwao kama anautaka urais.
 
Huyu angalau kitaeleweka. Hata Mkapa alianza mbio zake mdogo mdogo. Alipochukua fomu, kuna magezeti yaliandika: Mkapa naye achukua fomu! Yaliyobaki ni historia.

Huyu naona anakidhi mambo mengi. Hajautafuta urais kwa kutumia pesa. Wanaomfahamu wanasema ni muadilifu. Mkristo atayempokea muislamu na mzanzibar atayempokea mtanganyika.

Ila siyo mtanzania kwani zanzibar ni taifa kamili na si sehemu ya tanzania
 
Wakuu
Nchi kwa sasa hivi inamtaka mtu mwenye vigezo vya jaji Warioba. Kama watanzania wakimwomba na akakubali Warioba tu ndo kiongozi aliyebakia.

Mkuu warioba anafaa sana kuwa rais, ila kwa hali ilivyo ndani ya ccm siyo rahisi ccm wakampatia nafasi hiyo jaji warioba.
 
Reviews ya utumishi wake inaweza kutueleza iwapo anafaa kuongoza. Si ukristo wala uzanzibara/i? wake.
 
Kwa jinsi nchi ilivyokwisha kuharibiwa na Magamba, huyu bwana hafai, ni mpole mno hatawashghulikia vyema mafisadi
 
Huyu jaji anatoka nchi gani.?! Mbona mwinyi mpeku mzaramo ngingo katutawala.? Na katugaragaza...

By then Zanzibar haikuwa nchi bali sehemu ya muungano. Sasa ni nchi kamili ina kila utambulisho. Hatutaki kutawaliwa na raia wa nchi nyingine. Vinginevyo katiba ya Zenj ibadilishwe. Hiyo ndiyo habari.
 
Katiba ya Zanzibar untouchable , ni ya Wazanzibar si lazima Mtanganyika kuikubaliii... rufisheni Tanganyika yenu

Safi sana ndo maana sisi Watanganyika hatutakubali kutawaliwa na Wazenji
 
huyu jamaa ni mchungaji wa kanisa na kiongozi mkubwa kabisa..... Hafai kabisa hatuwezi tukachagua mchungaji awe kiongozi wa nchi. Kwenye public anaweza kuwa yupo neutral lakini inside ataendesha mfumo kristo hatari sana. Nchi hii mtaibomoa.... Mnataka kuanzisha muslim brotherhood kwa hili swala.

mkuu embu punguza jazba zako za kidini. Mbona kikwete hakuendesha nchi kiislamu? Acheni chuki binafsi...sasa ni zamu ya mkristo, bila kujali anatokea upande upi wa muungano. Umenielewa?
 
Salaam Wana JF, Kuna Tetesi Kuwa CCM Wanapanga Kumuomba Jaji Ramadhani Agombee Urais.Nia Ni Kuvunja Makumdi CCM,kuwafurahisha/kuwarubuniZ'bar Kuhusu Kura Ya Maoni Kat. Mpya,kuondoa Sumu Ya Udini Waliyoipanda,kumkomoa EL Au Kuitikia Ramli Ya Mtoto Wa Sheikh Yahya Kuhusu Mgombea Mwenye Dini Mchanganyiko?

Kama anataka kubaki nanheshima yake akatae ombi lao aendelee na uchungaji wake.
 
Back
Top Bottom