Lubebenamawe
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 2,001
- 2,329
Jaji Mkuu mstaafu kuwa rais wa nchi Hainingii akilini kabisa kwani kufanya hivyo tunaua uhuru wa muhimili wa mahakama. Jaji mkuu hata anapostaafu bado huwa anainfluence sana upande wa mahakama mana hukumu zake alizotoa akiwa kazini (jaji mkuu) zitaendelea kuwa kama sheria/kanuni mpaka atakapoibuka jaji mkuu mwingine na kuamua kuhama(to abandon/disregard the previous position established). Hali hii itaifanya mahakama iwe na kigugumizi kutamka hukumu dhidi ya serikali ambayo kiongozi wake aliwahi kuwa kiongozi wa mahakama. Hapo ndipo waswahili wanaposema kesi ya tumbili na fisi uinaipeleka kwa nyani aiamue!!