Serikali iruhusu uraia pacha kati ya miaka 0 hadi 35

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
315
879
Tunajua serikali inahofia kuruhusu uraia pacha kwa sababu za kisiasa kwamba atatokea mtanzania huko mambele mwenye ushawishi na kuchukua nchi. Hilo tuliache.

Tanzania kwa siku za hivi karibuni inajitutumua kwenye nyanja za michezo kimataifa. Mfano hivi karibuni, timu ya Taifa ya mpira wa miguu imefuzu mashindano ya Afrika (AFCON).

Hivyo ni jukumu la Taifa kuhakikisha timu yetu ya taifa inaenda kufanya vizuri huko Ivory coast kwenye mashindano hayo.

Tanzania ina raia wengi wenye vipaji vikubwa huko kwenye nchi za wenzetu sema tu wanashindwa kuja nchini kwa sababu hatujaruhusu uraia pacha.

Serikali tunaomba mruhusu uraia pacha kwa umri huo wa miaka 0 hadi 35. Tutapata vijana wengi wa kitanzania wenye exposure ya kimataifa katika michezo mbalimbali hasa mpira wa miguu.

Baada ya miaka 35, kijana itabidi aamue sasa anakuwa raia wa nchi gani kati ya Tanzania au nchi ya kimataifa aliyoishi hapo kabla.
 
Serikali iruhusu kila mwanadamu mwenye damu ya utanzania aweze pata uraia pacha. Yani kama baba, babu, mama au bibi alikuwa mtanzania basi uraia pacha uwe wazi.
 
Waziri mwenye dhamana wanae ni wamarekani by birth ngoja tuone ukizingatia mtoto pendwa na nyumba kubwa ina-survive kwa ushauri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom