Urafiki wa Mkapa na Magufuli ulianzia Kagera ukafia Lushoto

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,093
36,030
1995
Benjamin William Mkapa anachukua fomu ya kugombea Urais, gazeti moja kwa kebehi likaandika "Mkapa naye achukua fomu."

Hili neno "Naye" kwa sisi wana fasihi tuliona ni dongo, maana kipindi hicho habari ya mjini ilikuwa Boyz II Men, Lowassa na Jakaya Kikwete, wakiwa vijana kabisa hakuna hata aliyekuwa na miaka 45 ila mwisho wa siku Mkapa "naye" akawa Rais.

Mkapa hakuwa na makundi, Mkapa hakuwa na mtandao, Mkapa hakuwa maarufu kivile, Nyerere alipata shida sana kumnadi.

Mkapa hakuipenda Dar, Mkapa hakupapenda kwao Masasi, alipanga akistaafu akaishi mkoani Kagera.

Kule kuna rafiki yake Balozi Ferdinand Ruhinda ,walifanya kazi pamoja tangu ujanani,ndiye aliyemshauri kuishi mkoani Kagera,kipindi Mkapa anasoma Makerere alikuwa na marafiki wengi mkoani kagera maana ilikuwa ndio njia ya kuelekea chuoni.

Sasa hiyo 1995 Mkapa anashinda na Hayati Magufuli na Wilson Masilingi wanashinda ubunge majimboni kwao.
Wanatengeneza bond moja nzuri ila taratibu wanagundua Masilingi hawamatch tabia, Mkaoa hakuwa mtu wa starehe sana zaidi ya konyagi zake, suti zake akishonea Sky Tailoring Mart Mnazi Mmoja, Magufuli yeye suti zake akishonea Mwenge kwa wasambaa, Masilingi yeye aliagiza ulaya suti zake.

Wakamtenga kiaina, Masilingi msomi bishoo, mtoto wa mjini, kampani yake akina Fred Rwegasira, Mutta, Michael Njumba, madon wa enzi hizo.

Wazo la Mkapa kuishi mkoani kagera bado lipo, lakini je Kagera kubwa akaishi wapi? Miaka ikaenda miaka ikarudi, kuna shirika likiitwa PSRC, hili kazi yake ilikuwa kuuza mashirika ya umma kipindi cha Mkapa, wakawa wanauza ranchi za shirika na NARCO, shirika la ranch za Taifa.

Ranchi ya Kitengule mkoani Kagera ikauzwa wanunuzi hawakuanikwa hadharani, hii ni Ranch kubwa sana tena sana unahitaji kuwa na mafuta full tank kuizunguka kwa gari ila inasemekana ni wakubwa wawili.

Baadae Mkapa akabadili mawazo ya kuishi mkoani Kagera sababu ya umbali kutoka Dsm, hii ni kutokana na umri kusonga mbele magonjwa nyemelezi kwa wazee hayakosi, hutakiwi kuishi mbali na Muhimbili, akachagua kuishi Lushoto, mkoani Tanga.

Akapoteza interest za kwenda mkoani Kagera, akienda ni kumsalimia rafiki yake balozi Ruhinda.

2015
Magufuli anakuwa Rais wa JMT akiwa Bukoba kwenye mkutano wa hadhara anadai yeye ni myango mzirankende na kaburi la babu yake lipo Bukoba na akistaafu ataishi Karagwe.

Ranch ya kitengule kukaibuka ujenzi usiku na mchana tukaambiwa ni makazi ya mstaafu mmoja.

Waliojiuzia Ranch sasa wajulikana rasmi.
 
Back
Top Bottom