Upuuzi wa Joyce Kiria kuhusu Mbasha

Upuuzi wa Joyce Kiria kuhusu Mbasha

Status
Not open for further replies.
Bola hata mm nisiyejua wanawake live ni nn,mengne katuachie wenye upeo tuyapambanue ee
 
Nakiri kwamba Joyce Kiria nae amepitiliza mipaka... na yeye ni kama amehukumu tayari! Hata hivyo, hivi wale wanaopinga KATAKATA kwamba Mbasha hakubaka wanaweza kuniambia wanatumia vigezo gani hasa? What's so special alichonacho Mbasha kinachomfanya asiweze kubaka lakini wabakaji wengine hawana? Kwavile ana sura mzuri kama dada zetu wanavyosema kwahiyo ndo hawezi kubaka? Wengine wanadai eti Mbasha ana fedha ya kuweza kupata mwanamke amtakaye... kwani ni wapi panaonesha wabakaji ni wale wenzangu mimi tusio na fedha ya kuhonga? Hivi si mwakajuzi tu hapa Rais wa IMF (or World Bank kama sikosei) alipata kashfa ya kumtomasa muhudumu wa hotel... hivi mnafikiri nini kingefuata kama sio kupigwa rungu endapo yule mwanamke asingegangamala?! Ni watu maarufu wangapi duniani tena wenye fedha kuliko Mbasha ambao wamewahi kukutwa na tuhuma za ubakaji? Nyie wanaume mliooa hapa jamvini semeni ukweli wenu hapa... wangapi miongoni mnapiga ma-house girl wenu? Mnataka kuniambia mnapiga wakati wenyewe wameridhika kwa 100%? Hata nyinyi ma-brother men mnaoishi kwa wazazi wenu.... ni wangapi miongoni mwenu mmetungua ma-house girl wenu au ndugu za shemeji zenu? Mnataka kuniambia wote mliotungua waliridhia wenyewe?? Kuna wehu wengine utasikia msichana mwenyewe alicheza mkanda wa ngono na Ngasa... ebo! Ina maana mwanamke aliyecheza mkanda wa ngono ndo hawezi kubakwa? Kwani tuhuma zilizopo ni za utoaji bikira au ubakaji? Do I need to remind you kwamba hata mkeo ukipiga bila ridhaa yake nao ni ubakaji? Ajabu ya maswahibu haya hata wanawake wanamshambulia Flora kwavile tu wamesikia hili na lile!!! Hivi yule Emmanuel Mbasha angekuwa na sura kama ya Mpoki nyie wanawake mngeendelea kusema uongo, Mpoki hakubaka?!

Emmanuel Mbasha kama mwanadamu mwingine yeyote yule nae ana mapungufu yake! Kukataa katakataka kwamba hakubaka is like you guys mnakuwa na Mbasha masaa yote bila kumwachia japo kwa sekunde moja!!! Yaani mnaokataa katakata wala hamna tofauti na huku Uswahilini kwetu... mama anapelekewa kesi kwamba mwanae ni mwizi lakini mama anakuja juu kama moto wa kifuu kwamba mwanae hawezi kuwa mwizi wakati hashindi nae!!!
 
Huu ndo upumbavu ulioandikwa na Joyce Kiria facebook saa 1 lililopita;-


FRORA MBASHA POLE SANA...
NIJUAVYO MIMI NI KWAMBA, WAANDISHI WA
HABARI NA VYOMBO VYA HABARI TUNAONGOZWA
NA KANUNI NA SHERIA! NA KAZI KUBWA NI
KUIELIMISHA JAMII BADALA YA KUKANDAMIZA NA
KUPOTOSHA JAMII. KWA
JINSI HIYO NI LAZIMA IFIKE MAHALI TUONE
KWAMBA KUMDHALILISHA MTU ,PAMOJA NA
KUINGILIA UHURU WA MTU BINAFSI NI MAKOSA!
Kinachoe delea sasa ivi juu ya Flora&Mbasa ni
kwamba tunaingilia maisha binafsi ya mbasha na
mbaya zaidi tunamdhalilisha ''MWANAMKE''
Flora..kwa sasa tunauza sana magazeti na tunapata
trafiki kubwa kwenye blogs zetu ili kujiingizia
kipato..kwa Kumdhalilisha Flora ndicho
kinachoendelea...
Kama tumeamua kuchukua jukumu la Mahakama
sawa. Maana ndicho tunachokifanya kila kona
kujaribu kutoa hukumu ya kesi hii! Mbaya zaidi 99%
tunamuhukumu Flora eti kwa misemo kwamba
MWANAMKE -------- hubomoa nyumba yake
mwenyewe!
Ni lini huu mfumo dume ndani yetu utaondoka?
Kosa linalomkabili mume wa Flora liko wazi wazi, na
vitendo hivyo vinafanyika sana sana ndani ya
nyumba zetu. Ni vitendo vya kumdhalilisha
Mwanamke sana na vinatuumiza sana kina mama
wengi. Hakuna mwanamke atakaependa kusikia
mumewe kamdhalilisha kwa kulala na mwanamke
mwingine. Tena mdogo wake??! Tena kwa kubaka!
Hakunaaaaa! Hayupo huyo mwanamke...
Nikijaribu kuvaa viatu vya Flora ni vizito sana. Wala
sijui ningefanya nini kwa maumivu ninayohisi....
Kinachoniumiza ni kwamba jamii imeacha HOJA ya
msingi ambayo ni kitendo alichofanya Mbasha na
ndicho kimempandisha kizimbani Mbasha!! na
badala yake jamii kuanza kumuona Flora ni mkosefu
kuliko aliyebaka..
Kwa maneno mengine ni kwamba tunabariki
alichokifanya mbasha, na kwamba Mwanamke
yeyote asichukue hatua yeyote endapo Mume
atabaka au kutoka nje ya Ndoa yake.
Yaani mnatuambia wanawake wa nchi hii kwamba,
ukimfumania mumeo au akibaka we umsamehe
kimya kimya na maisha yaendelee! Mpaka sasa
jamii haioni kwamba Mbasha amefanya kosa kabisa!
Kana kwamba kama Mbasha hatakiwi kukemewa bali
asifiwe mwanzo mwisho na zawadi apewe kwa
kitendo hicho kama atakutwa na hatia kwamba
amefanya...
yaan kwenye jamii yetu inaonekana mwanaume kua
na mahusiano nje ya nyumba yake ni Sifa tena
anapewa majina mazuri ya urijali! lakini kwa
mwanamke ni umalaya na Ukahaba...
Hapo ndo napataga wazimu wa kichaga aiseee...
Inaniumiza sana na kuna siku nilikaa nikaamua
kuvunja ukimya juu ya hili jambo la michepuko tena
nikawataja wazi wazi watu tunaowategemea wawe
mifano bora lakini wao ndo waharibifu wakubwa! Cha
ajabu jamii iliinuka juu yangu ila ukweli ulisimama
na unabaki palepale kwamba mtu anapotoka nje ya
Ndoa yake au nyumba yake ni MZINZI na anatakiwa
akemewe bila kuangalia Hadhi yake.
kinachofanyika sasa kwenye jamii ni UNYANYASAJI
DHIDI YA MWANAMKE NA UKATILI WA KIJINSIA pale
tunapowaona wanaume WAzinzi ni marijali na
Wanawake ndo Malaya na makahaba...
mbaya zaidi kuna baadhi ya wanawake wenzetu
wanaushadadia huu MFUMO DUME kiasi kwamba
wanakua mstari wa mbele kumnyooshea Flora vidole
huku wakisahau kua mwenzio akinyolewa na ww
zako tia maji..WANAWAKE TUSIMAME IMARA
KUTOKOMEZA UKATILI NA MFUMO DUME kwenye
jamii yetu...Kama kuna mwanamke atakaeshereheke
a mume wake akimbaka mdogo wake basi huyo
amnyooshee kidole Flora...
Nasisitiza! ni kwa nn mwanaume husifiwa kwa uzinzi
Na jamii inatetea???! HUU NI MFUMO DUME na ni
Ukatili dhidi ya Wanawake...
MIMI JOYCE KIRIA NASEMA, MAADILI YAZINGATIWE
NA WATU WOTE BILA KUJALI WADHIFA WA MTU. NA
ENDAPO MTU AKIKENGEUKA BASI JAMII IMKEMEE
VIKALI. BADALA YA KUTUKUZA UZINZI KWA
KUANGALIA STATUS ZA WATU NA KUKANDAMIZA
WANAWAKE....
kwa pamoja tunaweza kutokomeza ukatili huu.....
NOTE: WAKINA MAMA TUPIGE MAGOTI TUMLILIE
MUNGU ASEME NA HAWA WATU WANAOTAWALIWA
NA PEPO MCHAFU WA UZINZI..IN THE MIGHT NAME
JESUS I PRAY....

umeangalia upande wa mbasha tu mbona flora anagongwa na Gwajima na hiyo nayo ipo wazi hujasema chochote? Pia una uhakika gani kama kweli mbasha alibaka na si hila na fitina za flora na Gwajima? Laana na iwe juu flora
 
Alichokipinga ni nini na aalichokipigia chapuo ni nini, mbona yeye tayari ameshamuhukumu Mbasha?
 
Sawa nakubaliana na wewe ila mimi ninachopata shida hapa ni kwamba kama amebaka mabint wawili Consecutively, najifunza kuna uwezekano jamaa alikuwa na ngunga ya kufa mtu. Halafu halafu hadi jamaa anabaka inaonesha katika akili yangu ndogo huduma kuna. uwezeiano zilikuwa adimu au ratiba imepungua au imesitishwa kwa muda. Sijui haya mambo yote anayafahamu mbasha na mkewe. Ila mwisho namalizia kwa kusema NJIA PANDA NOMA NA NDIYO INAYOLETA YOTE HAYA.
 
Nadhani hana uelewa wa kutosho, anachojua yy ni haki za wanawake tu, bora aendelee kumsapoti mmewe kwny siasa n c anachokifany ss
 
Sasa upuuzi wake huko wapi? Sasa Joyce Kiria hana haki ya kutoa mawazo yake bali ni ninyi tuu?

Muda mwingine baadhi ya wana jf mnanishangaza sana,yani mna mtuhumu mtu kutoa hukumu wakati hata ninyi mmekuwa mkitoa hukumu?

Kama Joyce Kiria hana haki ya kutoa kwa Mbasha? hukumu ninyi mliipata wapi hiyo haki ya kumhukumu Frola? Alicho kifanya Joyce kiria hakina tofauti na ambacho kimekuwa kikifanyika humu?

Hivi ni nani kati yenu amethibitisha pasi shaka kuwa Mbasha kabaka au hakubaka?

Ni nani kati yenu kathibitisha pasi
Shaka kuwa Frola anasema uongo au lah?
Kama ni kweli tunajua kazi ya kutoa hukumu ni ya Mahakama kwanini sisi kujivika kofia za mahakama ni sawa hila wengine
Wakijivika ni kosa?

Alaf kusema kwakuwa mtu ni standard 7 haiwezi kuwa hoja ya msingi kabisa maana kama tunaye muona ni Standard 7 mahakama ikifika hitimisho kama lake atakuwa ametushinda kufikiri na kutafiti sisi tunao jiita wasomi ambao tunajipa haki ya kuhumu! Mimi nafikiri swala hapa
ni wote kusubiri ukweli na kuacha kila mtu awe na haki ya kuongea na mwisho wa siku mahakama hitatoa maamuzi.

Kama sisi tume amua kutoa hukumu upande fulani basi tusi wazuie wengine kutoa hukumu upande fulani wanao ona wao.

Kama tunakubaliana na maneno ya title ya mtoa mada kuwa Joyce kiria ni mpuuzi kwa kusema hayo na tukijua hakuna kati yetu aliye mahakama basi na sisi ambao kila leo tumekuwa tuKiwanyooshea vidole watu fulani katika hili sakata wote ni wapuuzi maana sote bila shaka tumetumia mechanism mmoja kufikia hitimisho.

Maandishi ya Joyce Kiria, waandishi na wana jf yatabaki kuwa ya uongo mpaka hapo mahakama itakapo toa hukumu!


NB: Kama tunafikiri tuna haki ya kutoa hukumu basi tusimnyime Joyce Kiria haki ya kutoa hukumu maana hata hivyo kwenye hili swala sote tu third party!
 
Last edited by a moderator:
Uckute uwanaharakati wa joyce anauleta mpka kwa henry kilewo, mana c mda magazeti ya udaku yatamwandika yy
 
Nadhani hana uelewa wa kutosho, anachojua yy ni haki za wanawake tu, bora aendelee kumsapoti mmewe kwny siasa n c anachokifany ss
Hebu nipe tofauti mbili kati ya kilichofanywa na joyce kiria na kinachofanywa na baadhi ya wana jf!
 
Siku zote Wanawake Wana akili za kuvukia Barabara tu..

Kama Elimu ameikosa basi kukaa mjini kungemfanya walau ajitambue..

Nimeamini wanawake akili zao ni Shake Well before Use...

NB;
Hakuna harakati kwenye ndoa.

Mungu akusamehe maana unamtukana mpk aliyekuketa dunian,lau mama ako angejua anazaaa mtt atake mtukana kua hana akili angekutolea mbali,tukambunguza dharau duniani,think b4 u say co unakurupuka
 
usilazimishe unachoamini wewe kila mwanamke afuate. usituharibie wake zetu kama umezoea kubadili wanaume kila mara kutokana na kujifanya unajua sana haki za wanawake ni wewe. kaa kimya kama huna la kuongea.

Ivi wameshatemana na Kileo?
MABIG!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom