Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,893
- 3,121
Mfumo dume ni mfumo wa Kihistoria unaoelezewa kwa upande mmoja (Mbaya) hivi leo, kwenye kizazi chenye kulea na kuendekeza huruma kimatukio, kuna upande wa Mfumo huu haukusimuliwa ndio maana leo kuna majanga tunayoyaona.
Mfumo dume ulitengeneza HALI YA UMILIKI kwa Wanaume, kuwaweka wao kuwa Watunzaji, Wahudumu na Watoaji wa Familia zao. Hali hii ilifanya kuwe na dhana kwamba MTOTO NI WA BABA, hivyo kwa hali yoyote ni udhaifu mkubwa kwa Mwanamume kutelekeza familia au watoto wake (DAMU HAILALI NJE); hivyo, story za Single Mothers zilibaki kwa Wajane au Wanawake ambao Wanaume wao wamekimbia mbali zaidi kiasi cha kushindwa kuwawajibisha.
Hakuna baba mdogo, Mkubwa au shangazi atakayekubali uzae na Mwanamke kisha umtelekeze mtoto, ni wa KWAO. Hivyo kwa namna yoyote utamlea TU, ndizo zama ambazo Wanaume walioshindwa majukumu walilelewa watoto na mama zao, yaani bibi za watoto; ila UPANDE WA BABA.
Leo maisha marahisi sana kwa Wanaume wahuni, wenye hela. Anaweza akachezea Wanawake atakavyo, akazalisha atakavyo, ILA hakuna atakayejali kwa sababu moja tu "ANATUNZA WATOTO WAKE" tukisahau kwamba watoto wanakuzwa na MALEZI sio MATUNZO. Leo tunashangaa watoto wengi wa Kiume kutojua namna ya kuwa Mwanamume.
Upande mwengine wa MFUMO DUME ambao Wanawake wengi leo hawataki kuusema ni kwamba; mfumo huo huo uliwafundisha Wanaume kutokuwa Walalamikaji hata kama kuna changamoto wanapitia kwenye familia zao. Tunakubaliana kuwa; hata Wanawake, ambao kimsingi wao ndio WAHANGA wa mfumo dume, wao wenyewe wanakubali kwamba, Wanaume wanafariki kwa maradhi ya muda mrefu yanayojengeka ndani yao na kukusanya sumu zinazotokana na dhana ya KUVUMILIA kila kitu.
Babu zetu wameishi na Wanawake wenye kila aina ya uchafu, uchawi, wazinzi, wafitini na wasengenyaji; ila kilichokuja kusikika ni kibao, ngumi au teke ambalo bibi alipigwa na babu, au mama alipigwa na baba. Na si walichokuwa wanabebeshwa babu zetu, ukiangalia tamaduni kama za Ukeketaji kwenye jamii; Mangariba walikuwa Wanawake, ila wanavyotoka kupiga kelele humu nje utadhani walikuwa wanakeketwa na babu zao.
Anyway, MFUMO DUME ulikuwa umelenga ku "Maintain order" yaani hatuwezi wote kulalamika lalamika kama tumechanganyikiwa. Ili jamii iendelee kuna jinsia moja, ambayo ni ya kiume haipaswi kutia tia huruma kama wenzao ambao kucha kutwa kulalamika kunyanyaswa, halafu mwenzao akionyesha unyanyasaji wanaanza kutafuta "SABABU".
LEO ni haya tu; siku nyingine nitarudi na suala la Wanawake kunyimwa elimu, hii ni moja kati ya story yenye uongo mwingi kuwahi kuzungumzwa. Hakuna Mwanamke au Msichana aliyewahi kunyimwa elimu chini ya Mila na Desturi zetu.