Upimaji holela DNA udhibitiwe

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Baada ya mkemia kutoa takwimu ile kuna watu wengi watataka kwenda kupima ili kujua kama watoto ni wao.

Naomba serikali iwe makini hapa wakiruhusu kila mtu kupima itapelekea watoto wengi wa mitaani na kuvunjika ndoa nyingi kwani hali mbaya sana wanaume wengi sana wanalea watoto ambao sio wao ili hali wao wakijua ni damu yao.
 
Sasa mkuu huu ni ushauri gani,kwa hyo waendelee kulea damu zisizokuwa zao kwa sababu hyo???,mi naona kipimo kikiwa rahisi ndio fresh kwani madada zetu ndo watatuzalia watoto wetu halisi na si wa kubambikiziwa kama hv sasa
 
Mkuu hichi kipimo kikiwa rahisi ndoa nyingi zitavunjika na kupelekea watoto wengi wa mitaani tuendelee kulea tu hamna namna.
 
Namuonea huruma jamaa yng mmoja daah inauma sana analea mtoto ambaye sio wake alafu mkeo anatamba kabsaa na kumkebihi jamaa
 
Watoto wang lazima nipime.unakuta dem katiwa mimba na mwanaume ambaye hajajiweza bado,anasingizia mwingine.
Kweli tusiikwpeshe bcs itatuweka huru.
 
DNA sio malaria haipimwi hovyo hadi document za mahakamani zinahitajika kwa kifupi ni process hadi Kuja kufanya hicho kipimo
 
Acha watu wapime.

Kama mtu yeye hataki na asiende.

Lakini sio kuwapangia wengine ambao wana mashaka na watoto wao na wanataka kwenda kuthibitisha.

Asiyetaka na asiende na anayetaka na aende.
 
watanzania tumejaribu uongo unaoponya na umetufanya kiwa watu wa ajabu sasa ni bora kuugeukia ukweli unaouma! Wapime
 
DNA kwa Tz ipo kwa mkemia mkuu wa serikali tuuu,na inatumika kutambua vinasaba mbalimbali hata vya wahalifu pia ,lakini kufikia maamuzi ya kupima ni lazima muwe mmeanza mbali na mzazi mwenzio i mean kuwe na mgogoro mahakamani ambao mahakama kwa busara zake itaona kuwa ili kutatua mgogoro huo ni lazima utambuzi wa vinasaba vya wazazi uwepo,na wanaopimwa husindikizwa na majibu hawapewi wao huwa yanarudishwa mahakamani kisha mahakama inaamua kifuatacho.
 
Mkuu hiyo taarifa ya mkemia ni ya lini?..Mbona kama upo nyuma ya muda
 
Baada ya mkemia kutoa takwimu ile kuna watu wengi watataka kwenda kupima ili kujua kama watoto ni wao. Naomba serikali iwe makini hapa wakiruhusu kila mtu kupima itapelekea watoto wengi wa mitaani na kuvunjika ndoa nyingi kwani hali mbaya sana wanaume wengi sana wanalea watoto ambao sio wao ili hali wao wakijua ni damu yao.
Bado sijaelewa madhumuni ya Mkemia Mkuu kuwasilisha taarifa potoshi namna ile! Taarifa imewakilishwa kama matokeo ya utafiti rasmi wakati yalikuwa ni matokeo ya sampuli za watu waliokwenda kupimwa wakiwa katika ubishi wa kisheria.
Upimaji na utoaji holela matokeo ya DNA unakwenda kinyume cha maadili ya kisayansi na naishangaa wizara ya kina Kigwangala "kupotezea" upotoshaji huu na kuhangaika na waganga wa asili ambao baadhi matibabu yao yameleta matumaini na wameonyesha uwezo wa kufahamu wanachofanya hata zaidi ya hao Vigwangala!
 
Unaogopa watoto wako kuambiwa si wako
 
DNA sio malaria haipimwi hovyo hadi document za mahakamani zinahitajika kwa kifupi ni process hadi Kuja kufanya hicho kipimo

Nikiwa na ndugu office ya mkemia mkuu nampelekea blood sample tu ya mtoto.Me naona wangeweka njia rahisi zisizo na mlolongo mrefu kuipata hii huduma itarudisha heshima sana majumba yenye wanawake wahuni.
 
Bado sijaelewa madhumuni ya Mkemia Mkuu kuwasilisha taarifa potoshi namna ile! Taarifa imewakilishwa kama matokeo ya utafiti rasmi wakati yalikuwa ni matokeo ya sampuli za watu waliokwenda kupimwa wakiwa katika ubishi wa kisheria.
Upimaji na utoaji holela matokeo ya DNA unakwenda kinyume cha maadili ya kisayansi na naishangaa wizara ya kina Kigwangala "kupotezea" upotoshaji huu na kuhangaika na waganga wa asili ambao baadhi matibabu yao yameleta matumaini na wameonyesha uwezo wa kufahamu wanachofanya hata zaidi ya hao Vigwangala!

Pole. Watu wengi hawaelewi taarifa ya mkemia mkuu. Lakini nafikiri vyombo vya habari pia viliitoa kishabi zaidi na hivyo kuonyesha kama ulikuwa ni utafiti ambao sampo yake ilichukuliwa random.

Alichotoa mkemi mkuu ni takwimu za watu waliolazimika kupima baada ya kuwa na mgogoro. So hawa na kina baba ambao walisha onyesha au kushtukia kwamba watoto siyo wao, kwa mfano mtu anaona kabisa kwa mazingira fulani huyu mtoto si wangu, ana kataa kupeleka matunzo, then anaenda kushtakiwa. Akifika ustawi wa jamaa ana sema ipimwe DNA. Sasa 49% ya watu wenye mazingira haya ilithibitishwa kweli watoto siyo wa kwao.
 
siku hizi wanaume wakiulizwa mtoto huyu wako huwa wanajibu " mama yake anasema wangu " .
 
Mahakama, Police na Hospital ndio mamlaka zinawoweza kuomba vipimo vya DNA sio kila anaejisikia kufanya hivo, wananchi wangeruhusiwa kupima hovyo hovyo wanawake wengi wangepigwa mapanga kwa usaliti.
 
DNA itapelekea watoto weng wa mtaani na ndoa nyingi kuvunjika but madada au wanawake wakileo sio wakweli kwakwel unakuta mtoto haelewek ananywele tofauti na wewe sababu tu umeambiwa wako huwezi kukata sababu hamjapima damu upande mwaingine DNA ipitishwe ili watu walee damu zao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom