ivi mavazi ndio yanayovuta ngono ama ni mentality za wanaotazama,mbona zaman watu waliishi kw kujifunika na ngoz sehem ya mbele tu,matiti yalikua wazi na walikaa pamoja bila kuwepo hizo tabia za ngono?tatizo lipo akilini hata uvae hijabu bdo mentality kama umeitune kingono utawaza na kuchukua hatua. .mimi nalaumu SAUTI wamekurupuka sana,na ni uhuru wa mtu kuchagua avaaje,pale kila mtu katokea mkoa wake au nchi yke labda ndo mavazi yake aliyozoea. ?..hebu tuheshimu uhuru wa wav,mavaz pekee sio kipimo cha maadil..maadili ni atitude,ni imani.Taarifa zilizopo ni kuwa mavazi hayo yamepigwa marufuka katika chuo hiki kilichopo mwanza. na imekuwa ni amri kwa yeyote kuyavaa.
duh! Poleni sanaNi kweli jamani hiyo sheria imepitishwa hapa SAUT. Yaan hawa wadada walikuwa wanatutia nye-,g,e sana kwa vinguo vyao wanavyovaa. Ni full kuacha matamanio na maungo nje. Kdume uktoka lecture lazma ukapunye.. Well done uongozi wa SAUT.
Miaka kenda mkazo umekuwa ni kwa wanawake wasivae hivi wasionekane vile. Kama kweli tunataka kuondoa hiki kinachoitwa ngono zembe, ukahaba etc ni lazima tuangalie pande mbili za coin. Kwa nini mwanaume anabaka? Ni kwa sababu wanawake/wasichana wanavaa nguo fupi au suruali au ni kwa sababu mbakaji hajieshimu? Kwa nini kama mwanamke amevaa nguo fupi na unaona unashawishika usifumbe macho? why should one human being be subjected to some sort restrictions in order to accommodate weakeness of the other? Statistically nani anaweza kutupa data kwamba ngono zembe zinatokea pale msichana anapovaa nguo fupi au suruali? Saudi Arabia wanakojifunika bado kuna ubakaji tena wao una laana maana watoto wa kiume wanabaka mama zao! (nimesema watoto wa kiume wanabaka mama zao). Na skendo za mapadre na masista je? tuseme masista wanavaa vimini au suruali?
Kama kweli nguo fupi ndio chanzo hebu tuangalie kwa mfano Sweden, wasichana/wanawake tena wengi sana wanavaa vimini -vimini kweli sio hizi maxi za hapa tunazoziita vimini. mwanaume hasogei maana akimgusa anajua kiama kinafuata. Kinachonifurahisha ni kwamba hata mwanaume Mtanzania akienda huko anakuwa na mtazamo tofauti anaheshimu uhuru wa mwanamke kuvaa anachotaka, na hutamuona mtanzania huyo akibweka kama mbwa anapomwona mwana dada amevaa kimini. Lakini mtu huyo huyo akifika hapa Bongo anakuwa kama katoka kizuizini, ni miluzi kwa kila sketi inayopita mbele yake. This tells us something kwamba ukimkingia mtoto kifua huku watu wanakuambia kuwa mtoto wako anafanya makosa, na mtoto akajua kuwa unamkingia kifua kwa vijisababu unavyojua mwenyewe, basi subiri janga litokee. Sasa hivi wasichana wadogo hasa wa vyuo wanajiuza kwa sababu soko lipo, whether wanavaa vimini au mabaibui haijalishi chochote. Unless wanaume nao wabanwe mwishoni tutaishia kusema wanawake wote wavae kama telebani na bado tatizo likajitokeza!
Ni hatua nzuri, natarajia vyuo vyote vitaiga kwani ni jambo zuri, na wanaharakati wanaojiita wanatetea haki za mwanamke basi hili wanatakiwa kuliunga mkono kwa nguvu zao zote katika kumjulisha mwanamke hadhi yake. kila kukicha mwanamke hasa anayeishi mjini anazidi kupoteza aibu ya yeye kukaa uchi, imefikia hali ambayo wanajiona kama kwa wao ni kawaida kukaa na kutembea uchi.
NI mwanzo mzuri...niliwahi kufika CHUO CHA DIPLOMASIA pale kurasini....waoooooh nilifurahi kuona wababa kwa wamama wamevaa mavazi yasiyotoa maswali kwa kundi lingine la kijamii......VYUO VINGINE VINAVYOJALI UTU WA MTU MWINGINE KWENYE MAVAZI NI VYUO VYA UALIMU......Huwezi kuta U-WESTERN katika mavazi...kitu ambacho kwetu ni udhalilishaji....!
Enyi mnaotetea u-nusu uchi.....nendeni NIGHT CLUBS...ama mkasome huko nje ambako kuna uhuru wa MWANAUME KUWA SHOGA NA BINTI KUWA MSAGAJI
Tuachiane TANZANIA YETU...WENGINE TUNA WATOTO....Tunawafundisha kupitia watiu wengine pia