DOKEZO Taarifa kwa Serikali na Sekta za Elimu Tanzania kuhusu Katavi Institute and Development Studies (KISDES)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

carister benson

New Member
Oct 9, 2023
2
0
kwa yeyote anaye weza saidia kufikisha ujumbe huu
==
Taarifa kwa Serikali na Sekta za Elimu Tanzania

Nikiwa kama mhanga na mdau wa elimu, napenda kueleza mambo machache juu ya mwenendo mzima wa Chuo cha Katavi Institute and Development Studies (KISDES) kilichopo Mpanda, Katavi, kata ya Misunkumilo, kijiji cha Milala chenye usajili wa BTP 094. Lengo la taarifa hii ni kusaidia Serikali kuwa na wasomi wenye tija na pia kuokoa upotevu wa fedha za wazazi zinazoharibiwa na chuo hiki.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo:

1. Ukosefu wa Maktaba na Maabara (Famasi):

Chuo hiki kimepewa ithibati ya ubora, lakini hakina hata kozi moja yenye vitabu wala chumba cha maktaba. Mbaya zaidi, kuna wanafunzi wa famasi ambao wanatakiwa kutoa huduma za afya lakini hawana maabara yenye vifaa wala kemikali. Hali hii inaleta wasiwasi kuhusu ubora wa wasomi wanaotolewa na chuo hiki na athari kwa fedha za wazazi.

2. Uwepo wa Kozi Isiyosajiliwa kwa Miaka 5 na Wanafunzi Wanahitimu (ECE):
Kwa miaka minne sasa, chuo hicho kimekuwa kikitoa kozi ya Ualimu wa Chekechea ambayo haijasajiliwa rasmi. Wanafunzi wanapewa vyeti feki, na hii inasababisha matatizo kwa wahitimu wanapoomba kazi. Kozi hii isiyo sajiliwa inahitaji kuchunguzwa kwa maslahi ya taifa na wazazi, na wanafunzi wanaoendelea kusoma wanapaswa kupewa msaada ili kuongeza ubora wa elimu yao.

3. Wanafunzi Ambao Kwa Miaka 3 Hawapo Kwenye Mfumo:
Kuendelea kuwa na wanafunzi ambao hawapo kwenye mfumo wa NACTE ni kinyume cha sheria. Chuo kinapaswa kuchukua hatua za haraka kumaliza tatizo hili na kuwasikiliza wanafunzi hao ili kutatua kero zao.

4. Unyanyasaji wa Wafanyakazi na Kufukuza Bila Mpangilio:
Kuna unyanyasaji wa wafanyakazi kwenye chuo hicho, ikiwa ni pamoja na kutofuata sheria za kazi kuhusu masaa ya kazi, likizo, malipo ya ziada, na mishahara. Wafanyakazi wamekuwa wakiachishwa kazi bila kupewa stahiki zao. Hii inahitaji uchunguzi na hatua za kisheria.

5. Chuo Kuendeshwa Bila Bodi:
Chuo kinapaswa kuwa na bodi inayosimamia shughuli zake. Hali ya chuo kuendeshwa bila bodi na kutokuwa na vikao vya kawaida inaleta wasiwasi.

6. Chuo Kutolipa Stahiki za Wafanyakazi kama vile Loan Board, NSSF, WCF, PAYEE:
Chuo kinapaswa kuzingatia taratibu za kisheria za kulipa kodi, PAYEE, WCF, na mkopo wa masomo. Kukata fedha kwenye mishahara ya watumishi bila kulipa taasisi hizo ni kinyume cha sheria na inaathiri uchumi wa serikali.

7. Wanafunzi Waliomaliza Lakini Wapo Level 5:
Kuna wanafunzi ambao wameshahitimu lakini mfumo unasema bado wapo Level 5. Hii inaashiria udanganyifu kwenye matokeo na inapaswa kuchunguzwa.

8. Mkuu wa Chuo Asiye na Vigezo Kama Ilivyo Elekezwa na NACTE Standard:
Mkuu wa chuo anapaswa kuwa na vigezo kama ilivyoelekezwa na NACTE Standard. Uongozi wa chuo unapaswa kuzingatia miongozo na viwango vinavyotolewa na NACTE.

9. Chuo Kutawaliwa na Rushwa:
Inasikitisha kuona chuo kimeathiriwa na rushwa, na baadhi ya watumishi wanashiriki katika vitendo hivyo. Hii inahitaji kuchunguzwa na hatua stahiki kuchukuliwa.

Ninatoa mapendekezo kwa mamlaka husika kuchunguza kila kipengele kilichoelezwa hapo juu na kuchukua hatua kwa kuzingatia maslahi ya elimu na jamii kwa ujumla. Taarifa hii imepelekwa kwa:

  • Mkuu wa Mkoa
  • Mkuu wa Wilaya
  • Afisa Elimu Mkoa
  • TAKUKURU Mkoa
  • NACTE Makao Makuu
  • NACTE Zonal
  • Waziri wa Elimu

Asante.
 
NAOMBENI MSHARE MNAVO WEZA TAARIFA HII IWFIKIE WAHUSIKA
 

Attachments

  • TAARIFA KWA SERIKALI NA SECTOR ZA ELIMU TANZANIA.pdf
    124.4 KB · Views: 10
Back
Top Bottom