Mohamed Abubakar
JF-Expert Member
- Jun 26, 2014
- 899
- 1,088
Dhana ya Haki na Uhuru wa Kuabudu
JE NI HAKI KWA WATENDAJI WA SERIKALI KULAZIMISHA RAIA AU WATUMISHI WA UMMA KUISHI BILA DINI AU KUZUIA UHURU NA HAKI YA KUABUDU WAKIWA KTK OFISI ZA UMMA?
Kwa ufupi Serikali haina haki ya kuzuia haki na uhuru wa watu kuabudu na kuwang'anya haki yao ya kuwa ndani ya dini.
Lkn lazima tuelewe, kuna serikali na kuna watendaji wa serikali.
Watendaji wa serikali ndio kikwazo ktk taifa letu.
Ndio wanaozuia na kuweka taratibu zinazozuia baadhi ya wenye dini kupractice dini zao.
Haki zinazolibdwa na katiba.
Kuvaa mavazi yenye stara ktk imani ya kiislam ni ibada. Ni kuabudu.
Kuabudu si kuswali, kusali na kusifu tu.
Kuabudu ni kutekeleza kila amri ya Mungu kwa mujibu wa imani yako.
View: https://twitter.com/EduTalkTz/status/1804535133359214893?t=CT9uIeBB6Z2Bz7f2JGoZqg&s=19
Katiba ya nchi kifungu cha 19.
Kifungu cha pili kinatoa uhuru wa kuabudu kwa kila raia.
Na ibara ya 29 - 30:5 inayozuia mtu yyt (watendaji wa serikali) kuwazuia wengine kutekeleza haki zilizoanishwa na katiba.
Kwa muhtadha wa mada hii ni KUABUDU.
19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo
(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari la mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
Masharti ya Jumla (Ib 29-30)
29. Haki na wajibu muhimu
(5) Ili watu wote waweze kufaidi haki na uhuru vilivyotajwa na Katiba hii kila mtu ana wajibu wa kutenda na kuendesha shughuli zake kwa namna ambayo haitaingilia haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
30. Mipaka ya haki na Uhuru na hifadhi kwa haki na wajibu
(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
Mwisho wa kunukuu.
Wiki hii zimetoka nafasi kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mafunzo ya JKT.
Moja ya kitendo cha kudhalili, kinachokosa utu na kinachokiuka utamaduni wetu ni kuwavisha watoto wetu wa kike mavazi ya watoto wa kiume kwa lazima. Nazungumzia vibukta.
Katiba ambayo ndio sheria mama inamlinda kila raia na imani yake kwa kutoa haki na uhuru wa kuabudu.
Kuvaa mavazi yenye stara kwa wanawake/mabinti wa kiislam ni sehemu ya ibada (kuabudu) inaolindwa na katiba.
Ndio maana wanafunzi mashuleni walipewa uhuru huo miaka ya 80 na serikali hii hii baada ya waislam kusimama imara na kudai haki hii.
Huko JKT watoto wetu wa kiislam watavalishwa vibukta kwa jina la serikali isiyo na dini, kwa jina la uzalendo kwanza.
Kumekuwa na dhana kuwa tendo hili linafanywa kwa kwa kuwa tunaongozwa na Serikali ina itikadi ya kutokuwa na dini. Bali tunachojiuliza dhana hii kwa kuwa serikali haina dini ina maana gani kwa sisi wananchi.
Je serikali unalengo la kuwadhibiti wananchi wenye dini au lengo la serikali ni kutulinda bila kubagua yeyote.?
Katika hali halisi yaonyesha Serikali imeamua kudhibiti baadhi ya imani kwa kuwavua baadhi ya Watanzania imani za dini zao na kuwalazimisha kufata imani ya kipagani.
Kazi ya serikali yyt duniani ni kuwalinda raia wake. Kulinda ardhi zao, mila na tamaduni zao. Na inapotokea jamii fulani ina mila potofu serikali hufanya kampeni za kuwashawishi raia waondokane na mila hizo.
Tunaomba serikali au watendaji wa serikali watufafanunue je ibada hii kwa wasichana wa kiislam kuvaa unifomu yenye stara ni mila potofu kwa serikali isiyo na dini (kipagani).
Kinyume chake sisi kama sehemu ya jamii inayounda Tanzania tunaamini Serikali imekuwa kuvunja katiba kwa kutowaruhusu mabinti wa kiislam kuvaa uniform zinazikidhi uhitaji wao wa kuabudu.
Katiba ya nchi ndio sheria kuu na hivyo kama kuna Sheria za JKT zinazowataka wasichana kuvaa vibukta, ieleweke ya kuwa sheria na amri hiyo ni batili. Kwa kuwa inakwenda kinyume na katiba ya nchi inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu.
Hoja ya uzalendo au serikali isiyo na dini naamini ni tafsiri ya tabaka la sasa la watendaji chini ya Chama Cha Mapinduzi tuliowaamini watekeleza mahitaji na matakwa yetu sisi wananchi tuliowachagua. Kinyume chake wameamua kutafsiri dhana hizi kwa matakwa na imani walizonazo ambazo zinatuathiri sisi na haziathiri imani zao binafsi.
Kwa miaka mingi sasa JKT imeamua kuminya wenye dini wasipractice uhuru wao wa kuabudu unalindwa na katiba.
Kwani JKT ni moja ya taasisi za umma inayoendeshwa kwa maamuzi binafsi ya wafanya maamuzi. Jambo hili halikubaliki.
Tunaitaja jamii, vyama vya siasa, kijamii na taasisi za dini kupaza sauti na kuwatetea mabinti hawa ambao hawana wa kuwasemea kutokana na sababu za kihistoria ambapo waislam ni asilimia isiyozidi 10 ya wafanya maamuzi.
Kama ambavyo vijana wa kike wana uhuru wa kuvaa nguo zenye stara mashuleni kwanini katika mafunzo ya JKT wasiwe na uhuru huo.
Ni katiba,
Ni serikali au sheria za chuo inayolazimisha mabinti wanaohitaji mafunzo ya jkt na wakati huo huo kuhitaji stara lkn huvuliwa stara zao kwa amri binafsi ya viongozi.
Iwapo ni masharti ya serikali (JKT) hawaoni wanaisigina Katiba inayotoa uhuru wa kuabudu na kwamba kuvaa uniform maalum vitakazolinda stara zao ni haki ya kimsingi kama ambavyo nchi zenye kufata demokrasia na serikali isiyo na dini tena zenye waislam wachache wanavyowaruhusu kutekeleza ibada hii ya mavazi kwa kuweka dressing code kwa wanaotaka kuvaa hivyo.
Tukitafakari tutagundua kuwalazimisha mabinti kuvaa vibukta si matakwa ya kisheria bali ni matamanio tu ya watendaji wa serikali wanavyotafsiri mambo sawa na imani zao binafsi.
Kuwavua mavazi ya stara mabinti zetu si sehemu ya Uzalendo? Hakuna manufaa yeyote zaidi ya matamanio ya nafsi.
Na huenda ni takwa na tamani la mtendaji mmoja mvuta bangi anatumia nafasi hiyo kutafuta hamu ya kuwafanya wake zao mabinti hao.
Tunawataka Watanzania waelewe hili, uhuru wa kuabudu ni misingi ya haki za binadamu.
Kwanini watz tuko wa ajabu sana linapokuja suala la kuvumiliana values zetu.
Kwanini kama watz wenye imani tofauti tulazimishwe kufata imani na values za kipagani (Ujamaa).
Kwani maandiko wanasema ujamaa ni imani.
Na kwamba Ujamaa ni upagani.
Kwanini serikali iwe na imani ambayo iwe ni lazima kwa wenye imani nyingine kuifata.
Mataifa ya kidemokrasia yanayojipambanua kusimamia haki za binadamu na uhuru wa kuabudu wameweka
Mwongozo kama huu kwa askari na walioko mafunzoni kufata ili waendelee kuwa na dini zao, wapate kuabudu na wakati huo huo wanaitumikia serikali
Hatutaki jeshi la kidini, tunataka jeshi lenye kufata katiba na kuzingatia haki na uhuru wa kuabudu huko makambini.
Kuvaa uniform zenye stara ni kuabudu kwa mabinti wa kiislam.
Nchi zinazojipambanua ni za kidemokrasia zenye serikali isiyo na dini wanalinda wenye dini. Mf Marekani, UK, SA na hata majirani zetu Malawi. Tz wenye waislam wengi kwanini wanadhibitiwa na kubaguliwa.
Kama ni kwa kutokujua basi tunaweza kujifunza kupitia waraka huu.
View: https://youtu.be/WYAUNij6meo?si=KF6MURiFhUFat7Xx