Upi mtazamo wako kuhusu idadi ya watoto wa kuzaa kwa maisha ya sasa?

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Jul 3, 2015
608
1,263
Kumekuwa na hoja maoni na mitazamo tofauti sana kwa baadhi ya watu kuhusu idadi sahihi ya watoto wanaozaliwa zama hizi kulinganisha na zamani.

Dada mmoja mtu mzima kazini ana watoto watatu na wote wapo shule anasema
"Najilaumu sana kuzaa watoto wachache sasa hivi tumebaki wawili ndani, vijana ambao bado mnazaaa msifanye makosa yangu."

Nikiziangalia familia zilizofanikiwa kiuchumi wengi wana watoto wawili, mmoja au watatu tu, while familia za kipato cha chini zikiwa na watoto 4-7 waliowengi.

Kwa kizazi cha sasa, mfumo mzima wa maisha kuanzia malezi, uchumi, teknolojia unafikiri ni faida kuwa na watoto wengi/au je ni hasara kuwa na watoto wachache?

Ainisha sababu kwa jibu utakalotoa.
 
Hata ukizaa watoto 7 lazima utafika muda mtabaki na mwenzi wako tu. Ni swala la muda tu. Muombe Mungu akulinde wewe na mwenzi wako mzeeke pamoja.

Vinginevyo anaweza akabaki mmoja vile vile. Kwetu tulizaliwa 6. Wote tupo mikoa ya mbali. Mama ametangulia mbele za haki amebaki mzee tu saa hizi. Huzuni sana
 
Mimi nasema kuzaa kuwe na uwiano na kipato chako, kama una pesa basi utazaa watoto utakaoweza hata 13 mradi unaweza kuwatimizia mahitaji muhimu ikiwemo malezi bora.
Ila kama ni kapuku mchumia tumbo basi utazaa watoto wachache kuendana na kipato chako au kama unashidia andazi basi ni bora usizae kabisa.

Watoto 5 ndio minimum kwangu.
 
Binafsi naona kila mtu afanye vile anavyoona inampendeza au kufaa.Tukisema suala la kipato kuna watu wana maisha ya chini muda mwingine hata kula tu ni mtihani na bado wanaongeza watoto hivo mtu kama huyo sio kwamba haioni hali yake ila anataka familia kubwa na wengine hela ipo ila anaishia wawili tu na wala haoni umuhimu wa kuwa na familia kubwa.
Mimi binafsi yangu wawili nikizidi sana watatu wanatosha.
Ila likija nani azae kiasi gani na kwasababu gani kila mtu ana mtizamo wake na malengo yake.
 
Upande wangu huwa naona kuzaa watoto wachache ni nzuri sana kwasababu sinaga Ile mentality ya kuzaa watoto wengi ili waje kunisaidia au ule mtazano nikizaa wachache wanaweza kufa. Mimi naamini familia ya watoto wachache itanisaidia kuwapa mahitaji yao yote ya kimwili, kiimani na kisaikolojia kwa wakati na nitaweza kuwapenda vizuri kwa upendo wa hali ya juu.
 
Hili suala nadhani Kila mtu aangalie jinsi atakavyoweza kuwalea na kuwahudumia hadi pale watakapoanza kujitambua, siyo unafyatua then matunzo hujajipanga, usiwatese watoto bure. Mimi napenda nije kuwa na watoto 4 au 5. Ntajitahidi na baba yao kuwapambania kadri ya uwezo wetu kuwapa basic needs.
 
Hili suala nadhani Kila mtu aangalie jinsi atakavyoweza kuwalea na kuwahudumia hadi pale watakapoanza kujitambua, siyo unafyatua then matunzo hujajipanga, usiwatese watoto bure. Mimi napenda nije kuwa na watoto 4 au 5. Ntajitahidi na baba yao kuwapambania kadri ya uwezo wetu kuwapa basic needs.
Utaweza lakini round zote tano za leba
 
Back
Top Bottom