Upepo mkali watokea jijini Arusha, anga lajaa vumbi...

Upepo mkali watokea jijini Arusha, anga lajaa vumbi...

Hili ni jambo la kawaida sana Wilaya ya Hanang nilikozaliwa na maeneo mengine ya Mkoa wa Manyara nimeshuhudia sana haya matukio tangu nikiwa mtoto. Huko kwetu huwa wanahusisha sana hiyo hali na uwepo wa mvua kubwa msimu unaofuatia lakini utafiti huo si wa TMA bali wa jadi.
 
Hiyo hali ni ya kawaida sana kule kwenye bonde la ufa.
Pale Mto wa Mbu hiyo hali ni ya kawaida sana. Nadhani upepo umebadili mwelekeo kutoka kufuatisha binde la ufa na sasa umekuja mjini na vumbi lake.
Ni kweli ni hali ya kawaida. Lakini hilo vumbi limetokea maeneo ya KIA, Boma na maeneo ya Mbuguni yenye vumbi jingi sana kama la Mto wa mbu.
 
Ka video ka ushaidi .....
Kiujumla hali ya hewa ilikuwa mbaya sanaa
 
Mkuu nikweli niko bar moja hapa sanawari Osaka bar nyama tayar imeisha nimekosa.


Hyo ilkua lazima iwe hvyo kale mvua kalizidisha hamu ya nyama ya motoo alafu unshushia kitu suuza roho usiku unafika unaenda kulala
 
Mi mpaka nikaanza kutubu dhambi na kuomba toba... Inatisha ndo kwa mara ya kwanza naona hivi
Mimi padre niambie dhambi zako nikupe malipizi!!!! Hahaha natania hiyo itakuwa tornado imepita ila ilibidi watu wa hali ya hewa waone mapema.
 
Back
Top Bottom