Updates: Zoezi la kupiga kura - Arumeru East

Updates: Zoezi la kupiga kura - Arumeru East

Status
Not open for further replies.
tume ya uchaguzi imewaandikia barua chadema wasizunguke katika vituo vya kupigia kula na helkopta
 
Hii imetulia sana mwache kamanda amsaidie dogo. Kwa wasiojua ni kwamba kamanda lema ni best sana wa Nassari hivyo hili zoezi analifanya kiurafiki zaidi
 
Hapo si swala la hela!ni ulinzi wa kura. Kwanza wanajitolea. Au hujui hilo!
Vipi umekasirika mbona unatokwa povu sana?
Tunaangalia mtu ambae haongeki, hatuweki mawakala ili wapate posho, tunaweka watu wenye uwezo wa kulinda kura hata kama hakuna posho!
Navyowajua wachaga hawawezi kufanya kazi isiyo na maslahi....tukubali tu the main motive ya hao wabunge kufanya hivyo ni hela otherwise wangekuwa waangalizi wakuu across vituo vyote na si kustick kwenye kituo kimoja.
 
Hawa jamaa wanapenda hela sana....wanakaba hata hivi vihela vidogo vidogo. Badala wawaachie wanachama wengine uwakala, wanatakufanya hiyo kazi wao ili wapate hizo allowance za uwakala!!

Anatumia nafasi yake kikatiba kuwatumikia wananchi kwa pesa yake, nguvu yake bila allowance. Ila wewe hii allowance ya kwenye keyboard leo inasubiriwa kuweka msosi mezani kwa familia yako.
 
Polisi wamesema, nchemba ndio aliye toa ripoti polis kuwa amevamiwa akiwa anatoka kanisan, polisi ndio wakaja kumnusuru. Sio kwamba amekamatwa na polisi kuwa ametoa rushwa. Lakini polisi bado hawajatoa taharifa kamili, sababu iliyopelekea m.nchemba avamiwe na hilo kundi la watu. Source: mahojiano kati ya kamanda wa polisi na waandishi wa habar- Arumeru
 
Story kamili: Ni kuwa alikuwa kanisani kwa ibada mwisho wa ibada aliombwa na askofu kuwasalimia waumini, nae akawasihi waamini wakitoka kanisani waende wakapige kura kwani hiyo ni haki yao ya msingi!kitu ambacho ni sahihi kabisa lakini baadaye alipotoka nje kwenye gari lake alionekana akiongea na baadhi ya watu huku akigawa baadhi ya bahasha!!! askari wa kanisa alimfuata akamsihi aondoke pale lakini akakaidi ndipo ndipo baadhi ya wamama waliochukizwa na kitendo kile kipiga ukunga(yowe) wa mwiziiii ndipo walipofika viongozi wa cdm na kulibroke gari lake pale alipokuwa anajaribu kuondoka lakini kabla viongozi wa cdm hawajafanya chochote kama vile kulipekua gari kumbe Mwigulu tayari alishakuwa keshawasiliana na Andangenye akiimfahamisha kuwa yuko hatarini hivyo askari walifika pale fasta wakamchukua na kumpeleka usa polisi post. Hivyo kama kawa wameuwa so!!
 
Ina maana watu wasitumie usafiri wao kwa sababu zipi? Wakati mwingine NEC inatumika mpaka wanakuwa kama ndondocha
 
mwigulu atiwa mikononi mwa polisi na kuachiwa.kisa alikuwa akiinadi ccm kanisani na kutaka kuwahonga wapiga kura.
 
kuna hii dhana kwamba watu wengi wakienda kupiga kura ccm hupata wakati mgumu sana, lakini turnup ikiwa mbovu basi ccm hushinda kilaini kabisa.

Sasa Emmanuel Michael wa StarTV anasema idadi ya watu ni ndogo sana, ule umati tuliokua tunauona wakati wa campaign sijui umepotelea wapi. . . hii si habari nzuri hata kidogo kwa CDM
Kama waliuza shahada za kupigia kura kwa vyovyote vile hawawezi kwenda kupiga kura. Watapigia nini? Kama CCM wamefanikiwa kununua Shahada za kutosha basi hapo CHADEMA haina chake. No wonder CCM walikuwa wanajiamini kwamba watashinda kwa kishindo.
 
vijana wanafanya jitihada kubwa bila malipo yoyote.mungu awabariki wote!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom