Updates: Maandamano ya CHADEMA Arusha, Hai, Mwanga na Same

Updates: Maandamano ya CHADEMA Arusha, Hai, Mwanga na Same

Ikiwa arab springs unaowasema, waliandamana pamoja na kwamba walikuwa na maisha mazuri, huoni kama unajenga hoja nzuri na ya msingi kwa Watanzania wasiokuwa na mavazi, malazi, chakula, wala kesho yao hawaifahamu kama ipo wanahaki zaidi ya kuandamana ili wajikomboe? Kumbuka hawakupenda kuwa maskini kama walivyo. Ni serikali lya ccm ndiyo ime breed Tanzania hiyo unayoidhihaki. Bahati nzuri umesema hadharani tumekusikia. Sasa tunaandamana hata sisi tusio wana CHADEMA, ili kuunga mkono harakati za ukombozi.

Ni dhahiri kabisa ninyi mnashangilia matabaka ya watu duni wanaoishi katika maisha yasiyostahiki kwa binadamu na ambayo mmeyategnezza kwa utawala wenu wa miaka 50. Sasa hao unaowafanya si binadamu, ndio wenye nchi. Wazazi wao walilipa kodi za maendeleo ya nchi, ninyi mmebinafsisha maendeleo na kuwaacha vijana wakiishi kama nguchiro pori. Mmetumia raslimali za taifa kujinufaisha ninyi na watoto wenu. Mnatengeneza utawala wa kifalme kinyume na democrasia. mnatumia ubabe kuzidi kuwadidimiza na sasa mnawazomea hadharani. Elimu bora mmewanyima. Huduma za afya ni zenu tu, wao wanateketea kwa maradhi yanayozuilika na kutibika kwa sababu hamjali maisha yao.

Wanadai haki zao, unaasema bila haya, eti kwa kuwa ni maskini sana, hawana hata haki ya kudai kitu. Afadhali wangekuwa na maisha isha kama angalau Arab springs, wangekuwa hata na hadhi ya kusikilizwa.
Hata mwehu kuna siku huwa anajitambau. Fahamu zinamrudia anaanza kutaja majina ya rafiki zake walikuwa wanacheza wote.

Sasa Watanzania maskini, wajinga, wafu watarajiwa, waliotolewa muhanga kwa ufisasi na umangi meza wenu, wameamka. Wanajua kufa watakufa wakati wowote. Hata msipowapiga risasi, watakufa kwa kukosa huduma za afya, watauawa kwa uharibifu wamiundo mbinu mibovu, watakufa kwakukosa makazi bora, watakufa kwa kukosa elimu sahihi ya maisha, watakufa kwa uharifu unaoongezeka kila mara, kama si leo ni kesho. Hata msipowapiga risasi, wanajua watakufa kwa madawa fake na vyakula vyenye sumu vinavyoingizwa kifisadi.

Wanajua seriakli ingekuwa makini, maisha yao yasingekuwa yalivyo na wangeona mwanga na mwelekeo wa njia ya kupita. Sasa hawana cha kupoteza. Wameamua ni afadhali wauae na mkono wa serikali inayowadharau, kuwanyonya na kuwaona hawafai kama uliyvosema hapa, wakidai haki zao, kulilko kukaa wasubiri kufa kwa umaskini uliokithiri bila jitihada.

Sasa waueni. Lakini pia mtafute mahali ya kujificha maana bila shaka vituo vya polisi si vingi kiasi cha kuwaweka polisi na koo zao zote, pamoja na watu kama wewe mnaojitangaza hadhari kuwa ni adui wa Watanzania.


Bora hata arabs spring movement waandamanaji walikuwa na vyakula na maji ya kutosha ya kuweza kuandamana hata kwa mwezi mzima bila kuchoka wla kuhisi njaa maana wana food, shelter, na pia clothes, ila nyie wahuni, vibaka, wanywa viroba, wavuta unga wa arusha hamna hata mia mnataka muandame ili mkakwapue vitu vya raia wapenda amani...hamwezi andamana hata kwa masaa manne!

Nnavyowatamani mkijichanganya ntawachakaza huko frontline!!
 
Mkuu Ritz, kwa kawaida kwenye vita ukiona Mkuu wa Platoon anakimbia kwenye eneo la mapambano, basi ujue mambo yameharibika. Ndivyo alivyofanya Mbowe
Mkuu Lizaboni

Hawa makamanda wa kihindi wana kauli yao moja wanasema hakuna dhambi kama uoga lakini cha kushangaza viongozi wao ndiyo wamekuwa wa kwanza kuyakimbia maandamano.
 
Last edited by a moderator:
attachment.php

Mbwembwe tu hamna kitu,mbeya mtiti wake wanaujua siku 3 hakuna kulala mpaka Rais wa mbeya alivyokuja kusuluhisha,makombati hayo,virungu,risasi havijawahi shinda nguvu ya umma.

Kaandamane Kamanda na uache umbea humu Jukwani kwani time hizi sio za JF ni time za maandamano
 
Makamanda mnaogopa polisi? Dhambi mbaya kuliko zote ni uoga.
 
Kamanda unaomba kwa nani tena unatakiwa wewe mwenyewe uende kwenye maandamano utuletee update au unaogopa risasi za moto.

Ha ha ha ha ha we Ritz, usinivunje mbavu, labda anaomba updates za trip ya Mbowe huko south alikoenda na small house yake!
 
Last edited by a moderator:
Kamshahara ako ndo kamemsomesha mdogo wangu mpaka amegraduates na kuwa mkaguzi wa hesabu za serikali.
Don't ignore!!
Kama ni kweli wewe ni polisi kwa mshahara huo umeweza kumsomesha mdogo wako, basi nyinyi ndio mapolisi wala rushwa na hapo ulipo utakuwa huna uzalendo na nchi yako bali unahakikisha unausaidia mfumo huu mbovu usiondolewe ili uendelee kufaidika nao. Ni aibu kujivunia kupiga watz wenzako wanaoandama kwa amani wakijaribu kuonyesha hisia zao na kujaribu kuzuia upotevu wa hela za walipa kodi. Wewe ni mmoja wapo wanaounga mkono kwamba bunge la katiba lipo kisheria bila kujali sheria hiyo imetungwaje.
Kumbuka ndugu zako wanakutegemea wewe badala ya wao kuwezeshwa na serekali kimfumo ili wajimudu wenyewe. Viwanda vingi vya nchi hii viliuzwa kisheria na sera mbovu zilizotungwa na watawala matokeo yake ndio hayo mdogo wa mke wako, mtoto wa mjomba wako, mdogo wako wote wamejazana nyumbani kwako wakikutegemea wewe mwenye kipato kizuri cha rushwa. Jitambue acha kujivunia ujinga ndugu yangu.
 
Ukamanda wa kwenye mitandao tu, nendeni uwanja wa mapambano tuone nani mwanaume, mliokuwa mnasema mnaenda mbona bado mko ktk mitandao tu mkiuliza kinachoendelea?
 
Kwa hesabu yako raia na police ni wapi wengi raia tukiamua kuwasambaratisha hao police wako Tz nzima nusu saa ni kubwa mno hakutakuwa na police hata mmoja Tz achana kabisa na nguvu ya uma dogo hata hivyo raia wa Tz ni wapole sana!! Nchi nyingine rais yupo marekani anaambiwa baki hukohuko nchi imeshakombolewa na wapenda haki!!

Tatizo mnasahau kuwa raia wengi hawafungamani na sera zenu za fujo na vurugu,
 
nanyaroEphata tupe updates kamanda, saa tano hiyo!
Huyo Kamanda atakuwa yupo nyumba ya wageni anaandamana. Kamanda wao Mbowe ameenda kuandamana huko South Afrika. Nasikia Wenje kaenda kuandamana huko Kenya
 
Ukamanda wa kwenye mitandao tu, nendeni uwanja wa mapambano tuone nani mwanaume, mliokuwa mnasema mnaenda mbona bado mko ktk mitandao tu mkiuliza kinachoendelea?
Mkuu, hata humu kwenye mitandao hawapo. Sijui wanaandamana wapi
 
Back
Top Bottom