By
Mungi
Wakuu,
Kwa taarifa za maandalizi ya kufanyika kwa maandamano ya amani yatakayofanyika kesho tarehe 20/9/2014 yatakayofanyika kesho nchi nzima kupinga bunge la katiba linaloendelea mjini Dodoma, ambalo halina uhalali wa kuendelea, kwa upande wa Arusha kesho kutakuwa na njia sita tofauti kuanza maandamano yasiyo na kikomo.
Kwa taarifa hizo maandamano yataanzia Phillips-Mount Meru Hotel kupitia AICC, Central Police hadi Kilombero, Mengine yataanzia maeneo ya Sakina Machinjioni kuelekea mianzini, yatashuka na Kaloleni, Mwenge hadi Kilombero, Mengine yataanzia Majengo, Mbauda hadi Kilombero, Mengine yataanzia Kwa Morombo-Olasiti kuelekea Ngusero, Sonbetini, Corner Nairobi hadi Kilombero, Mengine yataanzia Kijenge, Uzunguni, Clock Tower hadi Kilombero.......
Kwa upande wa Arumeru maandamano yataongozwa na Dogo Janja, tutawajuza kila kitakachokuwa kikijiri, na upande wa Arumeru Magharibi maandalizi ni makubwa, wananchi wanatamani yaanze leo kama ilivyo kwa Arusha mjini.....
Tutaendelea kuwajuza kadiri tutakapokuwa tunapokea taarifa
Wao wamebeba bunduki, mabomu, marungu na pingu kuwaziba midomo wanaodai haki kwa amani,..... sisi tumebeba vitambaa vyeupe mikononi kuashiria tunadai haki kwa amani..... Dunia itashuhudia maandamano haya ya amani kesho..