Update: Mashtaka dhidi ya makampuni manne ya simu

Pambana kiongozi .... Nikiwakumbuka Airtel walichonufanyia 2015 napata hasira Sana.... MPAKA Leo Sina line yao KABISA na niliwashawishi watu wengine wawili ambao Mimi ndio nilifanya wawe na line zao wajitoe...

Ilikuwa hivi...Mimi nilikuwa napata 140,000# per month Kama communication allowance lakini inarushwa kwa mfumo wa Airtel aitime...

Kwasababu ya matumizi madogo na asante kwa vifurushi basi mara nyingine simu inakuwa hata na 400,000#ila airtime tu...

Sasa siku moja nikajiloga, usingizi umekata saa Tisa nikawaza nijiunge na bandle la internet niangalie movie...ilikuwa kuamkia jumamosi, nikajiunga bwana Bwana.....movie zikanoga nikaangalia Hadi saa nne asubuhi....

Nacheki salio ili nijiunge Tena nakuta Nina elfu 48 na chenchi kadhaa Kama salio .... Aisee nililaani Airtel, nikajilaani kea kuamka usiku....hi kitu iliniuma Sana mno .... Unaingiliaje airtime ya mtu bila kumjulisha......

Hao kwanza wapigwe faini za kutosha, Kama kuwagaia wananchi logistically Ni ngumu the pesa iende serikali I ifanye kitu Cha kumbukumbu....

Umefanya Jambo la kishujaa Sana, ingekuwa nchi yet inaweka historian ungewekwa kwenye upande wa mawasiliano.
 
ningependa uwashitaki wao na tcra walioshuhudia wizi huu kwamiakawakaunyamazia.
 
Tabutupu,

Please revisit your skewed comments, vije, au na wewe ni stake holder wa moja ya makampuni tajwa.
 
Kindly revisits you law books!
 
Hongera sana mkuu,una moyo wa kusaidia wanyonge kweli,maana hizo kampuni za simu ni wezi wa mchana
 
Hongera sana kwa kutulinda walaji wa huduma hii,kwani tumeumizwa mno,na sasa inatosha.
->Isajili kabisa "communications consumer protections against"
 
kwahyo ni sahihi nikinunua zege muuzaji anipangia muda wa kulila?
 
wakimuhurumia sana watamwekea mlungula mezani aachane na kesi
 
Tunahitaji consumer protection groups na activists kama huyu zaidi.
 
Wewe unit zako za umeme unazonunua unapewa expire date?,naomba jibu tafadhali.
 
Mkuu, ukimalizana na makampuni ya simu naomba ushughulikie issue ya mahoteli yanayohudumia wasafiri wa mabasi. Yaani chips kavu tunauziwa 3000 kweli? Mkuu tunaomba utusaidie katika hili pia
 
  • TCRA hawakuliona hilo kabla?
  • Kitu gani kimewafanya wakuite wakati suala lilikuwa baina yako na makampuni ya simu?
  • Je TCRA wana maslahi gani binafsi toka kwa makampuni hayo?
  • Nini kiliwafanya wakusubiri uanzishe mchakato na wao wadandie kwa mbele?
  • TCRA wakuajiri kwakuwa nimeona una uchungu na wananchi masikini kuliko wao.
 
kwahyo ni sahihi nikinunua zege muuzaji anipangia muda wa kulila?
Wewe unit zako za umeme unazonunua unapewa expire date?,naomba jibu tafadhali.
Nimeelezea post # 84 not all sales agreements are equal

It depends on the offer, muuza chips biashara yake aina masharti ya kula na wala TANESCO awauzi vifurushi isipokuwa independent units.

Tumuombe huyu brother afike mahakamani, atatupa mrejesho.
 
Hivi mnalazimishwa kujiunga vifurushi? Mbona haya ni masuala yaliyo wazi sana kibiashara? Vifurushi ni mkataba wa hiari wenye vigezo na masharti yake unayoyakubali kuyazingatia!!!
Huwezi mnyanganya sahani kisa muda wa lunch umeisha, halafu sio contract Law Ni "Law of Contract"
B
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…