Update: Lema kufikishwa Mahakamani Jumatatu

Update: Lema kufikishwa Mahakamani Jumatatu

Natamani na mimi ningekuwa Arusha nijumuike na mapambano dhidi ya haki. Nchi imefika pabaya sana kwa mkuu wa mkoa aliyechaguliwa na watu wawili tu (Riziwani na Jakaya) kuamuru mbunge aliyechaguliwa na watu zaidi ya 50,000 akamatwe kirahisi tu, tena bila staha wala heshima. Hiki kiburi cha maCCM kitawaghalimu. Kama wanatenda hivyo kwa mbunge, je inakuwaje kwa mlalahoi wa kawaida.

Nawaunga mkono wana Arusha na mikoa ya jirani kwa uamuzi wenu wenye kuakisi upeo wa hali ya juu na ukomavu katika kudai haki
 
Safi sana.....Ngoja tuone mambo yatakayojiri mahakamani...
 
lema is mandela of our generation,mk.we.re atamhamisha magessa mda si mrefu,anachafua hali ya hewa ndani ya chama.
 
Kesho tutapiga kura za kuondolewa huyu mkuu wa mkoa wa arusha kwanza haendani na jiji.pili hajui mipaka ya kazi yake na haujui mkoa huu kiundani,sasa mkuu wa mkoa hapajui hata njiro je?pembeni ya mkoa atapajua?huyu nisawa na shati liko golini wanajidai wako na golikipa matata hahahaha,kesho itakua kesho eiza lema atafutiwe jimbo jinginea au mkuu wa mkoa afanyiwe mpango huko mbali na tz.so watachagua moja ntakua front zaidi
 
Mh. Lema anaudhalilisha ukoo wa Lema. Sijawahi kukutana na Lema kilaza kama huyu ndugu yangu Mh. Lema.

Afungwe kwa maslahi ya taifa.
 
Kimsingi nawaombea sana muwe na moyo wa uzalendo na umoja wa aina hiyo,maana vita hivi dhidi ya dhuluma ya haki,ukombozi wa taifa,ubabe wa maccm unahitaji ujasiri na umoja kwa wapenda mabadiliko na wapigania haki kokote duniani.nawaomba muendelee kuhamasishana mjitokeze kwa wingi sana,sisi tuko mbali lakini nawaombea Mungu awatangulie,japo na hisi kutakuwa na mbinu za kukwamisha watu wasitokeze lakini msikate tamaa.
Ikumbukwe,DHAMBI MBAYA KULIKO ZOTE DUNIANI NI UWOGA by G LEMA.
 
Jiji la Arusha kesho litarindima pale mbunge wa Arusha mjini na kipenzi cha wakaazi wa mkoa huo Godbless Lema atakapopandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya uchochezi aliyofunguliwa kwa amri ya mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo.

Tayari jijini hapa kuna hekaheka kubwa ambapo maelfu ya wafuasi wa Chadema na wananchi wengine wa kawaida wameapa kufurika kesho mahakamani kama ishara ya kumuunga mkono mbunge wao na pia kumuonyesha mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo kwamba vita anayopigana na Lema kamwe hatafanikiwa.

Tayari kuna taarifa pia kuwa wafuasi wa Chadema kutoka mikoa ya jirani hasa Kilimanjaro na Manyara watawasili jijini Arusha alfajiri ya Jumatatu kumsindikiza Lema mahakamani.

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari na Mbunge wa Kawe Halima Mdee wako njiani sasa wakitokea Dodoma kuja Arusha kuungana na maelfu ya wananchi kumsindikiza Lema mahakamani.

Inasemekana pia tayari kuna malumbano makali kwa makada wa CCM hapa Mkoani ambapo wamemlaumu mkuu wa mkoa kwa kuzidi kumpa umaarufu Lema hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa madiwani wa kata zipatazo nne hali inayoipa Chadema ushindi mkubwa kwenye chaguzi hizo.

Hapo kwenye red!

Watajuta kuijua CDM!
 
Natamani na mimi ningekuwa Arusha nijumuike na mapambano dhidi ya haki. Nchi imefika pabaya sana kwa mkuu wa mkoa aliyechaguliwa na watu wawili tu (Riziwani na Jakaya) kuamuru mbunge aliyechaguliwa na watu zaidi ya 50,000 akamatwe kirahisi tu, tena bila staha wala heshima. Hiki kiburi cha maCCM kitawaghalimu. Kama wanatenda hivyo kwa mbunge, je inakuwaje kwa mlalahoi wa kawaida.

Nawaunga mkono wana Arusha na mikoa ya jirani kwa uamuzi wenu wenye kuakisi upeo wa hali ya juu na ukomavu katika kudai haki
Hizi kazi za wakuu wa mikoa wangekua wanazitangaza kama hawawajui watu wenye akili. Watu wenye akili wangeweza kuomba sio hawa vilaza kazi kujipendekeza hadi kulamba miguu. Sasa hii ndio kitu gani amefanya? cdm inakuja juu chama kilichokua cha ujamaa na kujitegemea sasa kitabakia cha wanyonyaji.
 
mkuu wa mkoa anapigana na LEMA au wakaazi wa Arusha ?
 
Huyu mkuu wa mkoa na mamluki wa chadema, na ndio maana anaipromote chadema kiasi icho...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
raha tupu!yaani wanampa promotion na ujasiri zaidi.
bye bye magesa.
 
Mh. Lema anaudhalilisha ukoo wa Lema. Sijawahi kukutana na Lema kilaza kama huyu ndugu yangu Mh. Lema.

Afungwe kwa maslahi ya taifa.

una mimba ya wana ukoo wa Lema??
 
Nipo safarini ngorongoro,ngoja niwawahisha hawa wazungu jioni kesho Nijumuike na makamanda.
 
A
Mh. Lema anaudhalilisha ukoo wa Lema. Sijawahi kukutana na Lema kilaza kama huyu ndugu yangu Mh. Lema.

Afungwe kwa maslahi ya taifa.

kweli wewe ni SUMU maana sumu inadhuru chochote kile chenye UHAI
 
Hivi kesho watu hawana shughuli zozote za kuingiza pesa ?? Watu wafanye kazi waache uvivu na kukaa kijuweni .

NB
Nina shamba la maindi nahitaji vibarua kwa ajili ya kupalilia , kwa wale wasio na kazi za kufanya wanaweza kutumia hii fursa kujipatia kipato kwa ajili ya kujikumu badala ya kukaa vijiweni na kuandamana kusiko na msingi huku wakilalamika maisha magumu.
 
Back
Top Bottom