Pendael laizer
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 958
- 105
Kama ni Arusha hii lazima tuitafute haki ya mbuge wetu lema kwa njia yeyote ile na hawa ccm wanazidi kujichimbia kaburi hapa A. City kiukweli na si propaganda.
MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini, (Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma tatau.
"Hatuwezi kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili"alisema Sabas.
Wakati Kamanda huyo akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi huku akitakiwa kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo.
Lema alikamatwa usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa ndani ya nyumba hiyo kufanyika.
Mbune huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.
My Out Look:
Nazidi kuyasadiki Maneno ya Rafiki yangu SSP Chuwa kuwa Tatizo sio Mulongo.
Yeye ana execute to Matakwa ya Mkulu Dhidi ya Lema.
Ile Issue ya Lema kumpa Live Mkulu kuwa analea Udini imemchoma sana Mkulu.
Rafiki Yangu SSP Chuwa Akaongeza, "CCM ni Wepesi Mno na Weupe Suala linapofika Mahakani"
Wao wana Mamlaka na Fedha, Lema ana Mungu
===================
Kinachojiri Mahabusu
===================
Hujui kuwa kama system ikiwa nzuri hata hauitaji kutoa jasho ili kufanikiwa? . Jiunge na wenzako uboreshe maisha yako na ya kizazi chako.Hii ni kama uko sincere na wewe siyo imposter!
Kwa sababu kuna watu walioko CCM na serikalini wanapitia huku,nadhani ni muda muafaka wa kumweleza Rais wetu wa Jamhuri ya Tanzania kuwa kinachoendelea chini ya himaya yake kinamatokea hasi,basi awawajibishe watu wake watende haki ,vinginevyo kwanye shimo la panya hata nyoka huwa wanaingia,wasitegemee vurugu itakapoaanza ni watu maskini na wanyonge tu ndio wataadhirika hata wenye pesa zao pia.
Kwani lupango ni watu wa namna gani wanaokaa humo siyo watanzania? je hakuna wapiga kura wake humo? je huoni kama wanahitaji kupata mawazo yake?...Mhe Lema alishaenda magereza mwenyewe baada ya kukataa mdhamana hivyo kwa Lema kumtishia Lokapu ni upumbavu mtupu..ngoja zamu yenu ikifika...Mkuu wahenga walisema kipenda roho hula nyama mbichi,kwako wewe Lema ni malaika.
Kama waona Lema ana ubavu wa kupimana na Mkuu wa Mkoa basi sisi tutabaki kuwa watazamaji.
Picha inaendelea, Lema yuko lupango na Mkuu anapeta.
Haihitaji akili nyingi kuelewa nani anaumia.
Mkuu naamini wewe ni mtu mwenye akili timamu.Kwani lupango ni watu wa namna gani wanaokaa humo siyo watanzania? je hakuna wapiga kura wake humo? je huoni kama wanahitaji kupata mawazo yake?...Mhe Lema alishaenda magereza mwenyewe baada ya kukataa mdhamana hivyo kwa Lema kumtishia Lokapu ni upumbavu mtupu..ngoja zamu yenu ikifika...
Hawawezi kumpa kesi ya mauaji. Sana watasema alichochea wanachuo kumfanyia vurugu mulongo. Prosecutors wamweke mulongo kama mmoja wa mashahidi akatoe ushahidi.Hapa wakimpa kesi ya mauaji Mji hautakalika.
Hivi kwanini watanzania tusifuate mfano wa wananchi wa Misri,Tunisia na Libya?
Kuna haja gani ya kuendelea kuwavumilia hawa watawala wanaofanana na madikteta?
jamani naomba msaada kujuwa hatima ya lema ya kusumbua jeshi la taifa na kuchochea vurugu atapona kweli pamoja na vijana wa arusha kutaka kumtetea......chama ambacho kinaangaliwa sasa hivi kuwa kiinaweza leta mabadiliko baadae member wake wanafanya mambo ya namna hiyo