Sijui kama ni utashi wangu ama ndivyo ilivyo au laa,maana nguvu nyingi inatumika kumkamata mbunge Godbless Lema eti kwa kusema watu wasiwe waoga,hawa ndiyo viongozi wetu nk,jambo linaloonekana kama ni kubwa utadhani ni kesi ya uhaini.Maswali yangu ni haya:
1.Je,mbona nguvu hiyo haijatumika kumsaka mwuaji wa yule kijana mwanachuo?
2.Je,kwanini nguvu hiyo haikutumika kumkamata yule waziri aliye sema wanachi wa mtwara ni wahuni,mpaka wapanda jazba na kuleta fujo.Je,ule haukuwa uchochezi?
3.Kwanini lema akamatwe usiku wa manane na siyo wakati ule ule wakati akitoa hotuba na hali askari walikwepo?
4.Kwanini nguvu hii haikutumika kuwasaka watu walio mtesa na kumwumiza kibanda?
5.Kwanini nguvu hii haijatumika kumsaka mtu aliye mtumia Lema ujumbe wa vitisho na hali namba ilitolewa?
Binafsi yangu naona ni upuuzi kuhangaika na mtu mmoja kana kwamba yeye anamiliki jeshi ambalo litaweza kuipindua nchi,hali kuna matatizo kibao ambayo viongozi wetu wanatakiwa kuyashughulikia.
Kwani Magesa Mulongo ni nani katika nchi hii ambaye hatakiwi kukosolewa wala kuambiwa ukweli,kama sembuse Mheshimiwa Rais huwa anakosolewa mambo makubwa na anaubali na haishii kutumia nguvu za dola kuwadhibiti wakosoaji wake?.
Lengo langu si kwamba nataka watumie lugha kali,kuudhi,kejeli nk katika kushauri jambo au kushughulikia matatizo yaliyopo mbele yetu,lahasha,ila ningependa kuona ile"fairness" katika kushughulikia matatizo katika nchi yetu kuliko kuliko kutumia nguvu nyingi kunyamazisha watu kutoa maoni yao jambo ambalo si tu linaiharibia sifa serikali iliyoko madarakani,bali pia inachochea hasira na chuki miongoni mwa watanzania jambo ambalo ni hatari zaidi.
Haina maana kuona kila siku mtu huyo huyo anapelekwa mahakamani kwa kesi za kijinga jinga huku kesi kubwa tena zenye maslahi kwa taifa zikiachwa.
Kwa mtu anayeweza kuchambua mambo,anaweza kuungana na mimi kuwa katika historia ya nchi hii,wanachi wa LIWALE hawa kuwahi kusikika wakifanya fujo mpaka kuchoma moto ofisi na mali nyingine za serikali na viongozi wake,lakini kwa sasa wenyewe mmejionea kilichotokea.Hali kama hiyo pia ya weza ikatokea pia mjini Arusha pale watu watakapochoka nakudhani kuwa kesi zote ambazo mh.Lema anazipata zinatokana na hila ya serikali pengine siyo kweli,ila tu ni namna mambo yanavyochukuliwa na baadhi ya viongozi wachache na vyombo vya dola.Ushauri wangu nikuwa wavumilivu nakukubali kukosolewa au kupokea maneno na mawazo ya watu wengine pasipo kujali maneno/mawazo hayo ni ya kukera au kufurahisha,ilimradi taswira ya nchi iendelee kuonekana kuwa ni ile yenye kutenda haki na usawa kwa watu wake na si kupambana na watu wanaojaribu kuikosoa.
Aksante!